Mkuu
Nguruvi3, wewe acha tu...huyu
Mohamed Said yawezekana alifanya utafiti kweli lakini utafiti wenyewe ulijikita katika kuwatambua aina ya watu ambao angeweza kuelekeza ngano zake kwao na wao wakazimeza nzima nzima bila kufikiri, kuuliza wala kutafakari. Kuna wakati tulimpa fursa ya kujinasua mapema asije akaumbuka na kuhadhirika...nakumbuka sana nilivyomsihi achutame kwani anazidi kuanika utupu katika simulizi zake lakini hakunisikiliza.
Hatukukata tamaa na hivyo tukazidi kumuuliza hivi, je Mohamed kama ungepewa nafasi ya kuiandika kitabu chako upya, kuna marekebisho ungekuwa tayari kuyafanya? Kwa kibri isiyo kifani akatamba hawezi kufanya hivyo...kuwa yote aliyoandika ndiyo ukweli na UKWELI MTUPU, DUH!
- Nakumbuka alivyodai, eti kulingana na maandishi ya John Iliffe, Kleist Sykes ndiye aliasisi AA mwaka 1929, tukamwambia hapana huyo alikuwa katibu tu, Raisi muasisi alikuwa Cecil Mtola, Myao, msomi na Mwalimu.
- Nakumbuka alivyodai kulingana na utafiti wake kuwa mikutano ya kwanza wa AA ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Sykes nikamwambia, hapana wewe muongo, mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola kabla ya Gavana Cameron kutoa kiwanja na Headquarter ya AA kuhamia New Street mwaka 1931.
- Nakumbuka alivyodai kuwa mwaka 1950, Tanganyika ilikuwa Mandate Territory, akaambiwa acha uongo, mwaka 1950 Tangayika ilikuwa bado Trust Territory.
- Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere aliingizwa kwenye siasa mwaka 1953 alipotambulishwa kwa wazee wake Mohamed Said mjini Dar es Salaam, akaambiwa la hasha toka mwaka 1946 Mwalimu Nyerere tayari alikuwa kiongozi wa AA Tabora.
- Nakumbuka alivyolalama baada ya kufanya utafiti wa miaka 15 na kudai kuwa kuwa kiongozi wa kwanza wa TAA alikuwa Abdulwahid Sykes, tukamwambia, no way, Raisi wa kwanza wa TAA alikuwa msomi wa Makerere Dr. Vedasto Kyaruzi.
- Nakumbuka alivyodai kuwa Waislaam walisahaulika katika uongozi baada ya uhuru na idadi yao kuwa ndogo kwenye baraza la mawaziri wa kwanza Tanzania, nikamwita muongo mkubwa na kumpa si majina tu bali picha ya baraza hilo idadi kubwa ikiwa ni ya Waislaam.
- Nakumbuka alivyodai kuwa EAMWS ilikataliwa kujenga chuo na baadaye kupigwa marufuku, nikamweleza jinsi EAMWS ya Ismailia ilivyovamiwa na viongozi wa AMNUT baada ya kutoungwa mkono na Waislaam wenyewe na kuigeuza kuwa kama chama cha upinzani.
- Nakumbuka alivyodai Darul Iman ilikatazwa kujenga chuo cha ufundi Kibaha na serikali, akapewa kweli kuwa sababu ya Darul Iman kufungasha virago ilikuwa ni kukosa imani baada ya mafisadi kutafuna hadi hela za kujenga misikiti na kuamua kusitisha mipango yake Tanzania.
- Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere hakuweza kumkumbuka Abdulwahid Sykes kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, akaumbuka pale alipowekewa hotuba ya Mwalimu lakini bila aibu akaanza na kudai mkanda wa sauti na video.
- Nakumbuka alivyodai ni Profesa Kigoma Malima ndiye aliyeanzisha mpango wa kutumia namba kwenye mitihani, akaumbuka pale alipoambiwa mpango huo ulianzishwa miaka mingi kabla ya Malima ila kitu alichotaka ni upendeleo maalum kwa wanafunzi wa Kiislaam, mpango ulioungwa mkono na Meya Kitwana Kondo.
- Nakumbuka alivyodai kuwa fujo za Mwembe Chai zilianza mwaka 1998 wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, tukamwambia, hapana, huo ulikuwa ni mwendelezo tu wa fujo zilizoanza wakati wa Hasan Ali Mwinyi ambapo bucha za kuuza nyama zilishambuliwa na watu waliotoka Misikitini.
- Nakumbuka alivyodai...I could gon on and on!
Yaani kama unavyosema
Nguruvi3, kwa mtu yeyote mwenye uelewa mpana, madai
Mohamed Said ni upuuzi na kama unavyosema ni NULL AND VOID. Hata hivyo yana lengo na kwa kiasi fulani kafanikiwa kwa sababu hatuna serikali, this man should be behind bars pamoja na wanafunzi wake Ponda, Ilunga, Uamsho and the rest of the gang...nawakumbuka kwa mbali Mzige, Shaaban na Hashim Saiboko.
Nakumbuka WARSHA iliyokuwa inaandika makala katika gazeti la Annur lililokuwa linafadhiliwa na bwana Kileo...wao ndio walikuja na mkakati wa kuwa na Ubungo Islamic Centre na kuanzishwa kwa redio Kheri. Kituo kikubwa cha kazi za
Mohamed Said ni msikiti wa Manyema pale nyuma ya CCM Lumumba. Msikiti ule unamtafaruku kwasababu wamanyema walitaka kupewa jina na uongozi na in fact ndio wanaoongoza akina Jongo. Mohamed Said pia ndiye mentor wa Basaleh pamoja na kuwa kamzidi kiumri.