Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nguruvi,

Tawi la jani la mpapai.
Akili yangu inashughulika sana.

Angalia nimeandika maneno mangapi katika paper ngapi katika vyuo vingapi nimeandika vitabu vingapi.
Ukiwa unaona kosa, kosa, kosa, kosa, kosa...

Shylock na kilo ya nyama.
Sina la kusema zaidi.

Mkitaka tunaweza tukabaki hapa katika kosa, kosa, kosa...
Au tukaendelea na mjadala.

Data ya Daily News nimesingizia UDSM!
Hakika ni jambo la kuchekesha.

Ndugu yangu ushaandika chochote tukisome?

Mzee Said, tuliache hilo la 'kosa' la Kawawa na tuseme ulipitiwa na halikuwa lengo lako kutumia cheo cha Umakamu wa Rais to sensationalize hoja yako. Lakini tuzungumzie utafiti wenu wa Warsha:

a. Ulifanyika vipi
b. Kwanini matokeo yasiyohusisha vitengo muhimu yachukuliwe ni ya chuo kizima?
c. Kwanini matokeo (tukiamini kuwa ni ya kweli) yachukuliwe ni ya nchi nzima na taasisi zote za elimu ya Juu nchini? Je hali ilikuwa vipi kwenye vyuo vingine, mgawanyo wa Waislamu naWakristu ulikuwaje?
d. HOja ya kuwa "Dar-es-Salaam ina Waislamu wengi" kwanini haikutumika kuelezea Tanga, Mtwara, Lindi au Kigoma ambako kote ni sehemu zenye Waislamu wengi? Kwanini Dar iwe kigezo cha Waislamu wote Tanzania?
 
Sheikh MS tuendelee na darsa,
Kwa heshima, Mzee wangu naomba unisaisie jibu ya hili swali langu, niliwahi kusikia ya kwamba Bwana “Mtakatifu” mtarajiwa aliwahi kutaka BIAFRA (Wakristo) ijitenge kwa madai wakinyanyaswa na Waislamu na wakati huo huo Bwana huyu akiushupalia kwa nguvu zake zote Muungano wa Zanzibar na Tanganyika hivi kuna ukweli wowote wa hili?

Juu ya BIAFRA na Mwalimu,

Hili linahitaji upembuzi yakinifu, ukikurupuka kutafakari kauli/maoni Mwalimu kama alivyokujibu Shekhe Mohamed Said utaona wazi kuwa kulikuwa na mtazamo hasi kwa mwalimu.

Zingatia huyuhuyu Mwalimu alipinga utawala wa kizayuni kuikoloni Palestine, vuta picha kisha tafakari ya Biafra.
 
Ami, Mohamed ni mwanadamu kama wengine. Kama umeona kuna mapungufu je, bado unampa benefit of doubt ya kutumia mapungufu hayo katika kuelezea dhulma? Hayo mapungufu si bahati mbaya ni makusudi sasa wewe unataka Mohamed aelezee dhulma kwa kutumia dhulma! tena akimtanguliza mwenyezi mungu kwa kusema anasimamia dini. Huoni dhulma yake imefika mahali pa kumdhulum mwenyezi munguUlitaka Nyerere awafanyaje? Hebu fafanua kuwapiga teke ni kwa namna ipi?
Mohamed ameshindwa kuonyesha labda wewe unaweza. Hairi inshallah tupe ilm, kama huna ufunge mdomo!Tunaweza kumsadia mtu asiwe mpuuzi lakini hatuwezi kumzuia awaye asiwe mpuuzi. Wewe umekiri kuwa kuna mapungufu katika hicho kitu kinachofanana na utafiti. Tumekuonyesha umeelewa, sasa kama utarudi kuamini alichosema Mohamed tena ukijua alikudanganya sisi tukusadieje! wewe endelea kutafuna ngano una khiariKama Mohamed atasema alichokifanya ni mazingaombwe au mdumange wala hatutakuwa na tatizo naye. Akishasema ni research hapo ametualika bila kupenda. Sisi tunaamini katika utaalam.
Mwalimu ni mtaalam wa elim na si daktari na injia ni mtaalam wa jambo lingine wala si daktari.

Umesema kifaa cha ndege! unajua dreamliner wamesimamisha ndege zao zote na kuingia hasara ya mabilioni kwasababu tu betri inaonekana kuwa na matatizo.

Sayansi ndiyo iliwaongoza kufanya hivyo na wame ground ndege zao zote. Mfano wako ni mzuri kuwa Mohamed anatakiwa afanye grounding ya vitabu vyake na paper zake maana ni hatari kama ilivyo hatari kuruhusu dreamliner angani bila kujua chanzo.

Kanuni za utafiti ndizo zinamuongoza mtu kama daktari atambue tofauti ya jipu na korodani. Kama una daktari asiyeweza kujua korodani zinafafananaje basi kila siku watu wataondolewa korodani kwa operesheni. Sijui huyo utampa benefit of doubt. Sasa Mohamed anayeeneza uzushi na uongo bado unampa benefit of doubt huoni hatari hiyoKwahiyo Mohamed asamehewe ili aendelee kulivuruga taifa kwasababu kuna watu wanafanya makosa duniani. No thank you sir !
Sisi wenye akili hatukubali hilo hata kidogo.

Nguruvi,

Sasa tutabaki hapa hapa kwenye kosa langu au utapenda tuendelee na habari za Sheikh Malik?
Nakusikiliza.
 
No uliahidi audio ukasema itamuumbua Mohamed.
Sie wengine twaisubiri kwa hamu ili umuumbue.

Mpaka leo huna ulichoprovide bali kumpaisha Mohamed angani.
Kama nilivyosema mwanzo nilikua simjui huyu mzee wala vitabu vyake ila umeniweka mdadisi nijue vitabu vyake zaidi.
Yaliyopo yametosha kuueleza ulimwengu juu ya udharimu wa Mohamed Said,

Ni vigumu kwako kuamini kuwa yatosha kwakuwa usehemu ya maasi.
 
Mzee MS,
Naamini wewe ni msomi, Tena MwanaHistoria na Muandishi Mahiri..

nadhani utakuwa ume come across kitu kinaitwa Credibility

Credibility refers to the objective and subjective components of the believability of a source or message

the quality of being believable or worthy of trust

Mzee MS umeweka nondo hapa, nondo nzito, na kwakweli umekuja na kuleta kitu ambacho nimekuja kukifahamu kwenye uzi huu kwa mara ya kwanza. Kuna watu wengi ambao nimeawasikia hapa kwa mara ya kwanza.

na nimejifunza kuwa it is a pity watanzania wengi hatuijui vizuri historia yetu (hata ile ya juu juu tu).

Lakini katika nondo zako ume highlight madai ya dhulma dhidi ya Waislamu, na katika madai hayo, kuna takwimu zilizotumika kama reference.

Sasa kuna watu (Nguruvi3 to be exact) wamekuja na kuchambua na kuonesha makosa(in accuracy) kwenye takwimu zile, sasa watu wanao ziamini hizo data nao wangekuja kudespute wakina nguruvi3 kuwa hizi stats ziko accurate.

Pia kuna sehemu ummesema

na watu wakaja wakasema kwamba umekosea, sijui kama umekubali kama umekosea.

Hapa ndo lile neno Credibility linapokuja....

Makosa kama haya unaweza kuyaona madogo na yakibinadamu lakini ndo yanayo anza kuquestion credibilty ya infomation ya author, hence credibility ya Madai ya author..

Makosa yasiwe excused na kufunika kombe kwasababu kuna dai kuu zaidi... Tunaliheshimu dai (Dhulma) lakini makosa makubwa kama haya yanaweza kutumika kuanza kuuliza je content nzima ya kitabu inaweza kutumika kama reference ya madai ya ''dhulma''.

Ndo nasema hata MM,Nguruvi,Mag3 wakileta info zenye utata lazima waulizwe, na kama wameshindwa kudhibitisha watu watajionea na kuwadiscredit. mfano nimeweka hilo swala la Vice President 1981 and 1982 ni nani kati ya Aboud jumbe na Msuya lina maana sana..

kwasababu ikijulikana kama Mzee MM ndiyo kakosea(intentionally) then tutaanza kudoubt ngano zake, hapa..

vivyo hivyo ikijulikana wewe pia ndo umekosea (intentionaly) pia tutaanza kudoubt ngano zako...

fair treatment kwa wote....

MF,

Kosa lolote katika kazi zangu ni kosa la kibinadamu wala sikudhamiria.
Umeniuliza swali zuri na mimi nimekupa jibu hilo hapo juu.

Ungesimama kwenye swali nami ungenitia moyo wa kukuuliza swali zuri
vilevile kwa yote ambayo nimeandika hapa na wewe nadhani umesoma.

Bahati mbaya hukuishia hapa ''bug'' ya Mohamed Said ''bashing'' imekushinda
nguvu.

Umezungumza kuhusu ''ngano.''

Kwa kuwa tokea mwanzo hukuniamini nami sina sababu ya kukuuliza hilo swali
langu.
 
Mzee Said, tuliache hilo la 'kosa' la Kawawa na tuseme ulipitiwa na halikuwa lengo lako kutumia cheo cha Umakamu wa Rais to sensationalize hoja yako. Lakini tuzungumzie utafiti wenu wa Warsha:

a. Ulifanyika vipi
b. Kwanini matokeo yasiyohusisha vitengo muhimu yachukuliwe ni ya chuo kizima?
c. Kwanini matokeo (tukiamini kuwa ni ya kweli) yachukuliwe ni ya nchi nzima na taasisi zote za elimu ya Juu nchini? Je hali ilikuwa vipi kwenye vyuo vingine, mgawanyo wa Waislamu naWakristu ulikuwaje?
d. HOja ya kuwa "Dar-es-Salaam ina Waislamu wengi" kwanini haikutumika kuelezea Tanga, Mtwara, Lindi au Kigoma ambako kote ni sehemu zenye Waislamu wengi? Kwanini Dar iwe kigezo cha Waislamu wote Tanzania?
Maswali mazuri sana, majibu ya Shekhe wetu Mohamed Said yatatoa mwangaza zaidi wakuuelewa utafiti wao hawa Warsha.
 
Nimeishi Muheza,Agley,Udowe na Sikukuu. Hata hivyo hapo nimeuliza watu wawili tofauti na wewe umenipa jibu la mmoja tu.
Na je unajua ni kwanini aliwekwa kizuizini? Alikuwa Bakwata au swarsun?

Sikukuu na Udowe nyumba ipi? hapo kuna ya Alamarhum Sheikh Hashim bin Abdallah, usoni kwake kwa kina Moshi (nyumba imebomolewa siku nyingi sana), upande wa pili kwa kina Mwita (wapo) usoni pembeni yake kwa Sharrif. Hiyo ndiyo udoe na Sikukuu. Lete habari zako.
 
Julius Kambarage Nyerere
1922 to 1999
Roman Catholic Church
Tanzania

[SIZE=-1] Julius Kambarage Burito Nyerere was born in 1922 at Butiama village, Musoma, Tanzania. He was a Zanaki by tribe. His father was Chief Burito Nyerere and his mother was Mgaya Wanyang'ombe. His father died while Kambarage was still young. His mother who raised him died in 1997 at the ripe old age of almost 100. Kambarage, the name he was given at birth, means "the spirit which gives rain" in Zanaki because the day he was born a very heavy rain fell.

In 1934 he was admitted to Mwetenge Primary School in Musoma, Tanzania, a school that was about forty-two kilometers from his home. Nyerere was a brilliant and hard working student. He regularly scored the highest marks in the class and was the leading pupil in all examinations. He received the highest score in the country on the standard four examination. After that he undertook studies at Tabora Government School in 1937, graduating in 1942.[/SIZE]
Ile shule ni Mwisenge, siyo Mwetenge.
 
MMM unaposema ume discredit ''utafiti'' naona wapo wanaoweza kutoa benefit of doubt ku-sooth nafsi zao.
Mimi nasema ni NULL AND VOID.

Tumejifanya mazumbu kuku na kukubali kuzijadili kama zilivyo, hata katika uzumbu kuku wetu wa kujifanya, Mohamed ameshindwa, nasema failed to stand and defend a single line. failure! Mo failed misereably to defend his own research methodology and findings scientifically.

Halafu bado anatumia neno research. Please tumia neno jingine ili researchers wasipate nausea.
Miaka 15 analisha vijana wetu ngano hii! Jamanani jamani ! eh mola.

Hilo la Kawawa linachekesha kweli. Hivi 1982 Kawawa alikuwa VP!
Alichokifanya ni kitu kinaitwa ''sensational news'' kwamba watu washtuke kuwa aliyekuwepo alikuwa VP.

Ni kile kile cha kuonyesha namba 18 Vs 82 huku akibadili maudhui ya ''reseach'' kila uchao.
Mara 18: 82 Muslim vs Christian, mara 18:82 Muslims vs Non Muslims. Ilimradi kuamsha hisia tu.

Ni kile kile cha hotuba ya karne ya Rehani Waikela ambayo nakala yake haipo duniani lakini tunaambiwa alisimama na kutaka kumbaraza Nyerere kwa bakora. Ushabiki ni kitu kibaya sana hasa kwenye intellectual discourse.

Mkuu Nguruvi3, wewe acha tu...huyu Mohamed Said yawezekana alifanya utafiti kweli lakini utafiti wenyewe ulijikita katika kuwatambua aina ya watu ambao angeweza kuelekeza ngano zake kwao na wao wakazimeza nzima nzima bila kufikiri, kuuliza wala kutafakari. Kuna wakati tulimpa fursa ya kujinasua mapema asije akaumbuka na kuhadhirika...nakumbuka sana nilivyomsihi achutame kwani anazidi kuanika utupu katika simulizi zake lakini hakunisikiliza.

Hatukukata tamaa na hivyo tukazidi kumuuliza hivi, je Mohamed kama ungepewa nafasi ya kuiandika kitabu chako upya, kuna marekebisho ungekuwa tayari kuyafanya? Kwa kibri isiyo kifani akatamba hawezi kufanya hivyo...kuwa yote aliyoandika ndiyo ukweli na UKWELI MTUPU, DUH!

  • Nakumbuka alivyodai, eti kulingana na maandishi ya John Iliffe, Kleist Sykes ndiye aliasisi AA mwaka 1929, tukamwambia hapana huyo alikuwa katibu tu, Raisi muasisi alikuwa Cecil Mtola, Myao, msomi na Mwalimu.
  • Nakumbuka alivyodai kulingana na utafiti wake kuwa mikutano ya kwanza wa AA ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Sykes nikamwambia, hapana wewe muongo, mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola kabla ya Gavana Cameron kutoa kiwanja na Headquarter ya AA kuhamia New Street mwaka 1931.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa mwaka 1950, Tanganyika ilikuwa Mandate Territory, akaambiwa acha uongo, mwaka 1950 Tangayika ilikuwa bado Trust Territory.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere aliingizwa kwenye siasa mwaka 1953 alipotambulishwa kwa wazee wake Mohamed Said mjini Dar es Salaam, akaambiwa la hasha toka mwaka 1946 Mwalimu Nyerere tayari alikuwa kiongozi wa AA Tabora.
  • Nakumbuka alivyolalama baada ya kufanya utafiti wa miaka 15 na kudai kuwa kuwa kiongozi wa kwanza wa TAA alikuwa Abdulwahid Sykes, tukamwambia, no way, Raisi wa kwanza wa TAA alikuwa msomi wa Makerere Dr. Vedasto Kyaruzi.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Waislaam walisahaulika katika uongozi baada ya uhuru na idadi yao kuwa ndogo kwenye baraza la mawaziri wa kwanza Tanzania, nikamwita muongo mkubwa na kumpa si majina tu bali picha ya baraza hilo idadi kubwa ikiwa ni ya Waislaam.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa EAMWS ilikataliwa kujenga chuo na baadaye kupigwa marufuku, nikamweleza jinsi EAMWS ya Ismailia ilivyovamiwa na viongozi wa AMNUT baada ya kutoungwa mkono na Waislaam wenyewe na kuigeuza kuwa kama chama cha upinzani.
  • Nakumbuka alivyodai Darul Iman ilikatazwa kujenga chuo cha ufundi Kibaha na serikali, akapewa kweli kuwa sababu ya Darul Iman kufungasha virago ilikuwa ni kukosa imani baada ya mafisadi kutafuna hadi hela za kujenga misikiti na kuamua kusitisha mipango yake Tanzania.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere hakuweza kumkumbuka Abdulwahid Sykes kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, akaumbuka pale alipowekewa hotuba ya Mwalimu lakini bila aibu akaanza na kudai mkanda wa sauti na video.
  • Nakumbuka alivyodai ni Profesa Kigoma Malima ndiye aliyeanzisha mpango wa kutumia namba kwenye mitihani, akaumbuka pale alipoambiwa mpango huo ulianzishwa miaka mingi kabla ya Malima ila kitu alichotaka ni upendeleo maalum kwa wanafunzi wa Kiislaam, mpango ulioungwa mkono na Meya Kitwana Kondo.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa fujo za Mwembe Chai zilianza mwaka 1998 wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, tukamwambia, hapana, huo ulikuwa ni mwendelezo tu wa fujo zilizoanza wakati wa Hasan Ali Mwinyi ambapo bucha za kuuza nyama zilishambuliwa na watu waliotoka Misikitini.
  • Nakumbuka alivyodai...I could gon on and on!
Yaani kama unavyosema Nguruvi3, kwa mtu yeyote mwenye uelewa mpana, madai Mohamed Said ni upuuzi na kama unavyosema ni NULL AND VOID. Hata hivyo yana lengo na kwa kiasi fulani kafanikiwa kwa sababu hatuna serikali, this man should be behind bars pamoja na wanafunzi wake Ponda, Ilunga, Uamsho and the rest of the gang...nawakumbuka kwa mbali Mzige, Shaaban na Hashim Saiboko.

Nakumbuka WARSHA iliyokuwa inaandika makala katika gazeti la Annur lililokuwa linafadhiliwa na bwana Kileo...wao ndio walikuja na mkakati wa kuwa na Ubungo Islamic Centre na kuanzishwa kwa redio Kheri. Kituo kikubwa cha kazi za Mohamed Said ni msikiti wa Manyema pale nyuma ya CCM Lumumba. Msikiti ule unamtafaruku kwasababu wamanyema walitaka kupewa jina na uongozi na in fact ndio wanaoongoza akina Jongo. Mohamed Said pia ndiye mentor wa Basaleh pamoja na kuwa kamzidi kiumri.
 
Mandown,
Angalia na hii:

Marehemu Prof. Haroun Othman si mtu mjinga.

Alipokisoma kitabu changu na kugundua mengi ambayo kwake yalikuwa mapya
aliathirika sana. Khasa kuwa harakati za kuwakusanya wananchi kuwa kitu kimoja
chini ya African Association ilianzwa na baba yake Abdulwahid Sykes Mzee Kleist
mwaka wa 1929.

Pili aliposoma kwa ushahidi wa nyaraka kuwa Abdu Sykes alikichukua chama
alichoasisi baba yake na kuanza mipango ya kuuunda TANU mwaka 1950.

Tatu kuwa hata ile hotuba iliyosomwa na Nyerere UNO 1955 chanzo chake
kilikuwa TAA Political Sub Committee katibu akiwa Abdu Sykes. TAA Political
Sub Commiittee ndiyo iliyoandika hotuba ile waandishi wakiwa Sheikh Hassan
bin Amir, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando, Dr Vedasto
Kyaruzi na Said Chaurembo.

Lakini zito kwake Prof. Haroub ni pale aliposoma njama za Nyerere katika kupiga
vita historia hii na kuhujumu juhudi za Waislam katika kujenga taasisi za elimu.

Prof. Haroub alipitia ushahidi wote nilioweka katika kitabu na kama haitoshi
alikwenda kuzungumza na Ahmed Rashad Ali rafiki yake Abdulwahid Sykes toka
1939 kutafuta ukweli wa maneno yangu. Huko nako alishibishwa.

Siku nilipokutananae uso kwa uso Prof. Haroub alikuwa kapwelewa kwani kwake
yeye Nyerere alikuwa kila kitu.

Kiongozi muadilifu atoae haki kwa raia wake wote bila ubaguzi, hana udini nk. na nk.

Aliniuliza mengi na mimi nilimjibu kila swali lake alilouliza.

Kwa mara ya kwanza mimi ambaye nilikuwa mwanafunzi wake Mlimani akinisomesha
"Theories of Development" sasa nikawa namsomesha prof. wangu historia ya kweli ya
Tanganyika.

Prof. Haroub alikuwa kama wengi walivyokuwa - hawakumjua Nyerere wala historia ya
kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nilikuwa nimemfungulia mlango ambao hakuwahi kupita hata siku moja.

Sishangai hapa JF ninaposoma kejeli na matusi.

Hakika hawa wenzetu wana haki ya kupata mshtuko.

Kuja kujua ukweli baada ya miaka 50 si jambo dogo.

Inahitaji wapewe muda wasafishe bongo zao ili ziwe tayari kupokea elimu mpya.

Baada ya miaka 50 Rais Kikwete anatoa nishani kwa Abdulwahid Sykes na Ally Sykes.

Kwanini hakutoa nishani kwa baba yao Kleist Sykes au kwa Hamza Mwapachu, Stephen
Mhando, Zubeir Mtemvu, Sheikh Hassan bin Amir na wengine hili ni swali linalohitaji
majibu.

Historia hii bado inahitaji utafiti zaidi na iandikwe.
Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!
 
Wanajamvi hawa ndio wanafunzi wa Mohamed.
Tafadhali asitokee mtu akawa na hasira nao, haya ndyo mapungufu ya wanadamu.
Muhimu ni kuwasaidia kujitambua maana tatizo lao si hoja tatizo ni kujitambua.

Eee Mwenyezi mungu wasaidiae waja wako wenye dhiki na wanaohitaji msaada kama hawa.
Dhiki si njaa tu bali yaweza kuwa mateso yatokanayo dhulma ya fikra.
Waongoe wale wanaowatia maumivu wenzao wakurejee na kukuomba mswamaha. Amin

mnakasha uendelee

Amina Amina
 
Mkuu Nguruvi3, wewe acha tu...huyu Mohamed Said yawezekana alifanya utafiti kweli lakini utafiti wenyewe ulijikita katika kuwatambua aina ya watu ambao angeweza kuelekeza ngano zake kwao na wao wakazimeza nzima nzima bila kufikiri, kuuliza wala kutafakari. Kuna wakati tulimpa fursa ya kujinasua mapema asije akaumbuka na kuhadhirika...nakumbuka sana nilivyomsihi achutame kwani anazidi kuanika utupu katika simulizi zake lakini hakunisikiliza.

Hatukukata tamaa na hivyo tukazidi kumuuliza hivi, je Mohamed kama ungepewa nafasi ya kuiandika kitabu chako upya, kuna marekebisho ungekuwa tayari kuyafanya? Kwa kibri isiyo kifani akatamba hawezi kufanya hivyo...kuwa yote aliyoandika ndiyo ukweli na UKWELI MTUPU, DUH!

  • Nakumbuka alivyodai, eti kulingana na maandishi ya John Iliffe, Kleist Sykes ndiye aliasisi AA mwaka 1929, tukamwambia hapana huyo alikuwa katibu tu, Raisi muasisi alikuwa Cecil Mtola, Myao, msomi na Mwalimu.
  • Nakumbuka alivyodai kulingana na utafiti wake kuwa mikutano ya kwanza wa AA ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Sykes nikamwambia, hapana wewe muongo, mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola kabla ya Gavana Cameron kutoa kiwanja na Headquarter ya AA kuhamia New Street mwaka 1931.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa mwaka 1950, Tanganyika ilikuwa Mandate Territory, akaambiwa acha uongo, mwaka 1950 Tangayika ilikuwa bado Trust Territory.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere aliingizwa kwenye siasa mwaka 1953 alipotambulishwa kwa wazee wake Mohamed Said mjini Dar es Salaam, akaambiwa la hasha toka mwaka 1946 Mwalimu Nyerere tayari alikuwa kiongozi wa AA Tabora.
  • Nakumbuka alivyolalama baada ya kufanya utafiti wa miaka 15 na kudai kuwa kuwa kiongozi wa kwanza wa TAA alikuwa Abdulwahid Sykes, tukamwambia, no way, Raisi wa kwanza wa TAA alikuwa msomi wa Makerere Dr. Vedasto Kyaruzi.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Waislaam walisahaulika katika uongozi baada ya uhuru na idadi yao kuwa ndogo kwenye baraza la mawaziri wa kwanza Tanzania, nikamwita muongo mkubwa na kumpa si majina tu bali picha ya baraza hilo idadi kubwa ikiwa ni ya Waislaam.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa EAMWS ilikataliwa kujenga chuo na baadaye kupigwa marufuku, nikamweleza jinsi EAMWS ya Ismailia ilivyovamiwa na viongozi wa AMNUT baada ya kutoungwa mkono na Waislaam wenyewe na kuigeuza kuwa kama chama cha upinzani.
  • Nakumbuka alivyodai Darul Iman ilikatazwa kujenga chuo cha ufundi Kibaha na serikali, akapewa kweli kuwa sababu ya Darul Iman kufungasha virago ilikuwa ni kukosa imani baada ya mafisadi kutafuna hadi hela za kujenga misikiti na kuamua kusitisha mipango yake Tanzania.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere hakuweza kumkumbuka Abdulwahid Sykes kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, akaumbuka pale alipowekewa hotuba ya Mwalimu lakini bila aibu akaanza na kudai mkanda wa sauti na video.
  • Nakumbuka alivyodai ni Profesa Kigoma Malima ndiye aliyeanzisha mpango wa kutumia namba kwenye mitihani, akaumbuka pale alipoambiwa mpango huo ulianzishwa miaka mingi kabla ya Malima ila kitu alichotaka ni upendeleo maalum kwa wanafunzi wa Kiislaam, mpango ulioungwa mkono na Meya Kitwana Kondo.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa fujo za Mwembe Chai zilianza mwaka 1998 wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, tukamwambia, hapana, huo ulikuwa ni mwendelezo tu wa fujo zilizoanza wakati wa Hasan Ali Mwinyi ambapo bucha za kuuza nyama zilishambuliwa na watu waliotoka Misikitini.
  • Nakumbuka alivyodai...I could gon on and on!
Yaani kama unavyosema Nguruvi3, kwa mtu yeyote mwenye uelewa mpana, madai Mohamed Said ni upuuzi na kama unavyosema ni NULL AND VOID. Hata hivyo yana lengo na kwa kiasi fulani kafanikiwa kwa sababu hatuna serikali, this man should be behind bars pamoja na wanafunzi wake Ponda, Ilunga, Uamsho and the rest of the gang...nawakumbuka kwa mbali Mzige, Shaaban na Hashim Saiboko.

Nakumbuka WARSHA iliyokuwa inaandika makala katika gazeti la Annur lililokuwa linafadhiliwa na bwana Kileo...wao ndio walikuja na mkakati wa kuwa na Ubungo Islamic Centre na kuanzishwa kwa redio Kheri. Kituo kikubwa cha kazi za Mohamed Said ni msikiti wa Manyema pale nyuma ya CCM Lumumba. Msikiti ule unamtafaruku kwasababu wamanyema walitaka kupewa jina na uongozi na in fact ndio wanaoongoza akina Jongo. Mohamed Said pia ndiye mentor wa Basaleh pamoja na kuwa kamzidi kiumri.

Mag,

Mimi si mtu wa kusutana.

Naona hii ndiyo staili ulokuja nayo ati nilisema kuwa AA ilianzishwa nyumbani kwa Kleist.
Sijapata kusema hili kwa kuwa historia hiyo naijua.

Nimetoa rejea mkasome maisha ya Kleist Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam East
Africana.

Kleist kaeleza kila kitu kuhusu AA.
Hamjakwenda.

Naweka tena reference yake:
A.D. Sykes "The Life of Kleist Sykes," University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15.

Sioni sababu ya kuvutana kwa haya.

Abdulrahman Kileo Allah atamlipa.
Kileo hakuwa anafadhili hiyo si lugha kwa mja anaetoa chake kumpa Allah.

Vipi mja atamfadhili Allah?

Kileo akitoa katika njia ya Allah.

Hayo mengine sina haja ya kuyagusa nakuachia mwenyewe.
 
Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!
Jasusi, huyo ndiye Mohamed Said, kurudia rudia uongo kwa matumanini kuwa mwishowe utageuka na kuwa kweli! Kinachosikitisha wako wanaoziamini hizo ngano na wako tayari kujitoa mhanga kuzitetea hata ikibidi kuhamisha vitanda kulala hapa jamvini. Ukisikia kuathirika ndiko huko.
 
Last edited by a moderator:
Mag3,

Chutuma basi na wewe hayo maneno mengine siwezi kuyamalizia kutoka na umri wako.

Acha uongo Msikiti wa Manyema haupo nyuma ya ofisi za CCM upo nyuma ya CRDB mtaa wa Mkunguni...Sheikh Basaleh na Msikiti wa Manyema wapi na wapi? Sheikh Basaleh Msikiti wake ni Idrisa upo Tandamti na Msimbazi.

Chutama basi au unaona aibu.

Hizo ngano zako mlishe Nguruvi3 na Mwanakijiji hujui chochote kuhusu Waislam nyuma ya ofisi za CCM kuna misikiti miwili siyo Manyema huijui hiyo Misikiti halafu unataka kuja kuropoka humu muongo waheed.
 
Mzee MS,
Naamini wewe ni msomi, Tena MwanaHistoria na Muandishi Mahiri..

nadhani utakuwa ume come across kitu kinaitwa Credibility

Credibility refers to the objective and subjective components of the believability of a source or message

the quality of being believable or worthy of trust

Mzee MS umeweka nondo hapa, nondo nzito, na kwakweli umekuja na kuleta kitu ambacho nimekuja kukifahamu kwenye uzi huu kwa mara ya kwanza. Kuna watu wengi ambao nimeawasikia hapa kwa mara ya kwanza.

na nimejifunza kuwa it is a pity watanzania wengi hatuijui vizuri historia yetu (hata ile ya juu juu tu).

Lakini katika nondo zako ume highlight madai ya dhulma dhidi ya Waislamu, na katika madai hayo, kuna takwimu zilizotumika kama reference.

Sasa kuna watu (Nguruvi3 to be exact) wamekuja na kuchambua na kuonesha makosa(in accuracy) kwenye takwimu zile, sasa watu wanao ziamini hizo data nao wangekuja kudespute wakina nguruvi3 kuwa hizi stats ziko accurate.

Pia kuna sehemu ummesema

na watu wakaja wakasema kwamba umekosea, sijui kama umekubali kama umekosea.

Hapa ndo lile neno Credibility linapokuja....

Makosa kama haya unaweza kuyaona madogo na yakibinadamu lakini ndo yanayo anza kuquestion credibilty ya infomation ya author, hence credibility ya Madai ya author..

Makosa yasiwe excused na kufunika kombe kwasababu kuna dai kuu zaidi... Tunaliheshimu dai (Dhulma) lakini makosa makubwa kama haya yanaweza kutumika kuanza kuuliza je content nzima ya kitabu inaweza kutumika kama reference ya madai ya ''dhulma''.

Ndo nasema hata MM,Nguruvi,Mag3 wakileta info zenye utata lazima waulizwe, na kama wameshindwa kudhibitisha watu watajionea na kuwadiscredit. mfano nimeweka hilo swala la Vice President 1981 and 1982 ni nani kati ya Aboud jumbe na Msuya lina maana sana..

kwasababu ikijulikana kama Mzee MM ndiyo kakosea(intentionally) then tutaanza kudoubt ngano zake, hapa..

vivyo hivyo ikijulikana wewe pia ndo umekosea (intentionaly) pia tutaanza kudoubt ngano zako...

fair treatment kwa wote....

Inaonesha hujapitia kwa umakini huu uzi, MM kakosea mara nyingi tu "intentionally" na tuka "point out", licha ya makosa ya kibinaadam kama vile ya lugha na sarufi.
 
Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!

Hahahaha, kama unao ukweli si uuthibitishe?

=Khamsa wa Ishirin mara, ingeleta raha zaidi.
 
Mag,

Mimi si mtu wa kusutana.

Naona hii ndiyo staili ulokuja nayo ati nilisema kuwa AA ilianzishwa nyumbani kwa Kleist.
Sijapata kusema hili kwa kuwa historia hiyo naijua.

Nimetoa rejea mkasome maisha ya Kleist Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam East
Africana.

Kleist kaeleza kila kitu kuhusu AA.
Hamjakwenda.

Naweka tena reference yake:
A.D. Sykes The Life of Kleist Sykes, University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15.

Sioni sababu ya kuvutana kwa haya.

Abdulrahman Kileo Allah atamlipa.
Kileo hakuwa anafadhili hiyo si lugha kwa mja anaetoa chake kumpa Allah.

Vipi mja atamfadhili Allah?

Kileo akitoa katika njia ya Allah.

Hayo mengine sina haja ya kuyagusa nakuachia mwenyewe.

Mohamed Said,

Huyu jamaa ni wakumsamehe tu analazimisha vitu bora umempa huo mpini aangaike nao.
 
Back
Top Bottom