Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!
Jasusi,
Nadhani nilipata kukugusia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyoandika mapendekezo ya
katiba kwa Gavana Edward Twining.
Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Mapendekezo ya kamati hii yalizungumzwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.
Yaliyokuwa katika mapendekezo yale ya Political Subcommittee hayana tofauti na yale TANU iliwasilisha
UNO 1955.
Na mengine mengi nikakueleza nikiamini utanielewa.
Kuna mengine sijayasema lakini kuhusu document hiyo nadhani unajua kuwa ilipotea na haionekani
popote.
Hiyo ''kunakili'' unasema wewe.
Mimi sijasema neno hilo.
Mimi sijasema uongo na ndiyo maana husema siku zote.
Nanyi andikeni huo ukweli tuusome.
Hivi unajua kama katika ile Political Subcommittee alikuwapo mwanasheria Earle Seaton kama mshauri
wa TAA toka 1950?
Unaijua style ya uandishi wa Seaton?
Unajua kuwa Seaton na Abdu walikuwa marafiki wakubwa?
Nadhani unatambua kwa nini nakudokeza haya.