Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!

Jasusi,

Nadhani nilipata kukugusia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyoandika mapendekezo ya
katiba kwa Gavana Edward Twining.

Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Mapendekezo ya kamati hii yalizungumzwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.

Yaliyokuwa katika mapendekezo yale ya Political Subcommittee hayana tofauti na yale TANU iliwasilisha
UNO 1955.

Na mengine mengi nikakueleza nikiamini utanielewa.

Kuna mengine sijayasema lakini kuhusu document hiyo nadhani unajua kuwa ilipotea na haionekani
popote.

Hiyo ''kunakili'' unasema wewe.
Mimi sijasema neno hilo.

Mimi sijasema uongo na ndiyo maana husema siku zote.
Nanyi andikeni huo ukweli tuusome.

Hivi unajua kama katika ile Political Subcommittee alikuwapo mwanasheria Earle Seaton kama mshauri
wa TAA toka 1950?

Unaijua style ya uandishi wa Seaton?
Unajua kuwa Seaton na Abdu walikuwa marafiki wakubwa?

Nadhani unatambua kwa nini nakudokeza haya.
 
Sasa hivi mmekuja na mtindo mpya mtu akikosea kuandika basi kosa la jinai...ha haa ha.

kuna makosa ya uandishi; lakini kuna makosa ya facts; makosa ya uandisi si ya msingi sana tena wala si ya kujali; makosa ya facts (factual errors) ni makosa ya hhoja nzima. Ukikosea kwenye facts hoja yako haiwezi kusimama. Kama unasema utafiti uliofanywa na Warsha ni wa kisomi na tukaonesha kuwa si wa kisomi hahpo si makosa ya uandishi...
 
Huijui Kariakoo wewe bora ungekaa kimya unadhani karikoo kama Kibosho.
Kariakoo sehemu kubwa inamilikiwa na wazawa, waarabu, wapemba, wachaga na wakinga nyumba zao zinahesabika.
Misheni kota ilikuwa sehemu maalumu kwa Wakirsto saizi yote inanunuliwa na waarabu "Wamaara"
Ungetueleza habari za Kibosho au Marungu hatupafahamu lakini siyo kariakoo.
Unaijua historia ya Kariakoo wewe? Unajua kuwa wakati wa Mjerumani Kariakoo haikuwepo? Unajua Kariakoo ilikuwa ni shamba tu la Mjerumani alilolinunua kutoka kwa Sultani? Kwa ufupi ni kuwa baada ya vita vya kwanza vya dunia Kariakoo ilikuja kuwa kituo cha kijeshi na baadaye makazi ya kwanza ya African Carrier Cops (kariakoo). Unajua baada ya Uingereza kuiasisi Tanganyika kwa nini iliitwa nchi ya Rangi Tatu? Unajua ni mwaka gani iliamuliwa na serikali ya wakati huo kuligawanya hilo shamba kuwa viwanja na kuwapa "natives"? Unajua "natives" wa kwanza Kariakoo walikuwa ni wa jamii ipi? Usichokijua ni kama usiku wa giza, pole sana.
 
Ami, Mohamed ni mwanadamu kama wengine. Kama umeona kuna mapungufu je, bado unampa benefit of doubt ya kutumia mapungufu hayo katika kuelezea dhulma? Hayo mapungufu si bahati mbaya ni makusudi sasa wewe unataka Mohamed aelezee dhulma kwa kutumia dhulma! tena akimtanguliza mwenyezi mungu kwa kusema anasimamia dini. Huoni dhulma yake imefika mahali pa kumdhulum mwenyezi munguUlitaka Nyerere awafanyaje? Hebu fafanua kuwapiga teke ni kwa namna ipi?
Mohamed ameshindwa kuonyesha labda wewe unaweza. Hairi inshallah tupe ilm, kama huna ufunge mdomo!Tunaweza kumsadia mtu asiwe mpuuzi lakini hatuwezi kumzuia awaye asiwe mpuuzi. Wewe umekiri kuwa kuna mapungufu katika hicho kitu kinachofanana na utafiti. Tumekuonyesha umeelewa, sasa kama utarudi kuamini alichosema Mohamed tena ukijua alikudanganya sisi tukusadieje! wewe endelea kutafuna ngano una khiariKama Mohamed atasema alichokifanya ni mazingaombwe au mdumange wala hatutakuwa na tatizo naye. Akishasema ni research hapo ametualika bila kupenda. Sisi tunaamini katika utaalam.
Mwalimu ni mtaalam wa elim na si daktari na injia ni mtaalam wa jambo lingine wala si daktari.

Umesema kifaa cha ndege! unajua dreamliner wamesimamisha ndege zao zote na kuingia hasara ya mabilioni kwasababu tu betri inaonekana kuwa na matatizo.

Sayansi ndiyo iliwaongoza kufanya hivyo na wame ground ndege zao zote. Mfano wako ni mzuri kuwa Mohamed anatakiwa afanye grounding ya vitabu vyake na paper zake maana ni hatari kama ilivyo hatari kuruhusu dreamliner angani bila kujua chanzo.

Kanuni za utafiti ndizo zinamuongoza mtu kama daktari atambue tofauti ya jipu na korodani. Kama una daktari asiyeweza kujua korodani zinafafananaje basi kila siku watu wataondolewa korodani kwa operesheni. Sijui huyo utampa benefit of doubt. Sasa Mohamed anayeeneza uzushi na uongo bado unampa benefit of doubt huoni hatari hiyoKwahiyo Mohamed asamehewe ili aendelee kulivuruga taifa kwasababu kuna watu wanafanya makosa duniani. No thank you sir !
Sisi wenye akili hatukubali hilo hata kidogo.

Ami, Mohamed ni mwanadamu kama wengine. Kama umeona kuna mapungufu je, bado unampa benefit of doubt ya kutumia mapungufu hayo katika kuelezea dhulma?.
Wacha kushangilia kasoro ndogo kati ya rundo la ukweli usiokanushika
Hayo mapungufu si bahati mbaya ni makusudi sasa wewe unataka Mohamed aelezee dhulma kwa kutumia dhulma! tena akimtanguliza mwenyezi mungu kwa kusema anasimamia dini. Huoni dhulma yake imefika mahali pa kumdhulum mwenyezi munguUlitaka Nyerere awafanyaje? Hebu fafanua kuwapiga teke ni kwa namna ipi? .
Wewe ni nani hata ujue kuwa mapungufu ni ya makusudi?.Wapi amesema anasimamia dini?.Usiwe unasingizia wenzio uwongo.
Unauliza ulitaka Nyerere awafanyeje?.Hilo swali limejibiwa mara nyingi na mantiki iko wazi.Hao wazee wala hawakudai kufanyiwa lolote.Kilichowauma na sisi kutuuma ni kufanyiwa vibaya kwa kutukanwa juhudi zao.

Mohamed ameshindwa kuonyesha labda wewe unaweza. Hairi inshallah tupe ilm, kama huna ufunge mdomo!Tunaweza kumsadia mtu asiwe mpuuzi lakini hatuwezi kumzuia awaye asiwe mpuuzi. Wewe umekiri kuwa kuna mapungufu katika hicho kitu kinachofanana na utafiti. Tumekuonyesha umeelewa, sasa kama utarudi kuamini alichosema Mohamed tena ukijua alikudanganya sisi tukusadieje! wewe endelea kutafuna ngano una khiariKama Mohamed atasema alichokifanya ni mazingaombwe au mdumange wala hatutakuwa na tatizo naye. Akishasema ni research hapo ametualika bila kupenda. Sisi tunaamini katika utaalam..
Kwa hili nakuona umehemkwa bure.Kukubali kosa na kukiri kosa ni tabia ya kiungwana.Kwa Mohammed kitu kidogo kama hicho ni sadaka ambayo wala haitopunguza uzito wa ukweli alioufukua ambao mmejipinda kutaka kuurudisha nyuma.
Kama ni kujibu basi tukianza kuorodhesha sehemu ambazo mmeshindwa kujibu basi huu mjadala utakuwa mrefu mara kadhaa kuliko ulipofikia.
Mwalimu ni mtaalam wa elim na si daktari na injia ni mtaalam wa jambo lingine wala si daktari.

Umesema kifaa cha ndege! unajua dreamliner wamesimamisha ndege zao zote na kuingia hasara ya mabilioni kwasababu tu betri inaonekana kuwa na matatizo.

Sayansi ndiyo iliwaongoza kufanya hivyo na wame ground ndege zao zote. Mfano wako ni mzuri kuwa Mohamed anatakiwa afanye grounding ya vitabu vyake na paper zake maana ni hatari kama ilivyo hatari kuruhusu dreamliner angani bila kujua chanzo..
Madhumuni ya mfano huo ilikuwa ni kuonesha kuwa hakujawa na tishio la aina hiyo.Hata dreamliner huwa zinapata mikwaruzo ya aina tofauti lakini haikuwa sababu ya kusitishwa kuruka.
Nimetoa mfano wa Biblia lakini mmekaa kimya.Hapa ndipo mnapomshinda Mohammed katika ujanja wa kutokujibu vitu vigumu.

Kanuni za utafiti ndizo zinamuongoza mtu kama daktari atambue tofauti ya jipu na korodani. Kama una daktari asiyeweza kujua korodani zinafafananaje basi kila siku watu wataondolewa korodani kwa operesheni. Sijui huyo utampa benefit of doubt. Sasa Mohamed anayeeneza uzushi na uongo bado unampa benefit of doubt huoni hatari hiyoKwahiyo Mohamed asamehewe ili aendelee kulivuruga taifa kwasababu kuna watu wanafanya makosa duniani. No thank you sir !
Sisi wenye akili hatukubali hilo hata kidogo..
Huko ndiko kuhemkwa kwa kutamani sifa.Narudia kusema wanaojiamini kuita historia iliyoandikwa na Mohammed ni uzushi na uongo basi ni watu wa kutumwa na mfumo kuzima mafanikio yake kama mtaweza.
 
Mohamed,
Nina swali jingine la ziada. Usichoke na maswali yangu, tafadhali. Mara kadhaa umezungumzia Christian lobby, sasa sijui hii Christian lobby ni akina nani. Niliwahi kufanya kazi katika bunge la Marekani na malobbyist wote wakifahamika pale wanapokuja kukutana na wabunge. Utasikia huyu ni lobbyist wa farmers union, lobbyist wa jews, etc. etc. But you could identify them. Sasa wewe unazungumzia Christian lobby in Tanzania in the abstract. Can you at least put a name or a face on them? Kama ni akina Peter Kisumo, John Malecela, at least tujue hawa akina Christian lobby ni akina nani. Ni hilo tu.
 
Unaijua historia ya Kariakoo wewe? Unajua kuwa wakati wa Mjerumani Kariakoo haikuwepo? Unajua Kariakoo ilikuwa ni shamba tu la Mjerumani alilolinunua kutoka kwa Sultani? Kwa ufupi ni kuwa baada ya vita vya kwanza vya dunia Kariakoo ilikuja kuwa kituo cha kijeshi na baadaye makazi ya kwanza ya African Carrier Cops (kariakoo). Unajua baada ya Uingereza kuiasisi Tanganyika kwa nini iliitwa nchi ya Rangi Tatu? Unajua ni mwaka gani iliamuliwa na serikali ya wakati huo kuligawanya hilo shamba kuwa viwanja na kuwapa "natives"? Unajua "natives" wa kwanza Kariakoo walikuwa ni wa jamii ipi? Usichokijua ni kama usiku wa giza, pole sana.

Sasa umeandika nini hapo bado haijafuta uongo wako kuwa Msikiti wa Manyema upo nyuma ya ofisi za CCM ungekuwa unaijua kariakoo usingeandika pumba hizo.

Wewe Dar es Salaam umekuja umefikia Kimara mie Dar es Salaam, Kariakoo nimezaliwa halafu wewe wa kuja unipe mie historia ya Kariakoo si vichekesho.

Kwa kukusaidia tafuta kitabu cha Mohamed Said kaelezea historia ya Kariakoo.
 
Jasusi,

Nadhani nilipata kukugusia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyoandika mapendekezo ya
katiba kwa Gavana Edward Twining.

Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Mapendekezo ya kamati hii yalizungumzwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.

Yaliyokuwa katika mapendekezo yale ya Political Subcommittee hayana tofauti na yale TANU iliwasilisha
UNO 1955.

Na mengine mengi nikakueleza nikiamini utanielewa.

Kuna mengine sijayasema lakini kuhusu document hiyo nadhani unajua kuwa ilipotea na haionekani
popote.

Hiyo ''kunakili'' unasema wewe.
Mimi sijasema neno hilo.

Mimi sijasema uongo na ndiyo maana husema siku zote.
Nanyi andikeni huo ukweli tuusome.

Hivi unajua kama katika ile Political Subcommittee alikuwapo mwanasheria Earle Seaton kama mshauri
wa TAA toka 1950?

Unaijua style ya uandishi wa Seaton?
Unajua kuwa Seaton na Abdu walikuwa marafiki wakubwa?

Nadhani unatambua kwa nini nakudokeza haya.

Lakini bado kuna wingu kuhusu hiyo hotuba ya UNO. Ukisoma kitabu cha Nyerere utaona kwa hakika kaiandika mwenyewe kwa sababu kaiweka in the first person. Na kama ali-plagiarize hotuba ya wengine pia tunapaswa kujua kwa faida ya historia. Na wewe, kama mwandishi ambaye umearifu kuwa hotuba ya UNO iliandikwa na wengine mbali na Nyerere, unalo jukumu la kuthibitisha hilo kwetu wasomaji.
 
Sasa umeandika nini hapo bado haijafuta uongo wako kuwa Msikiti wa Manyema upo nyuma ya ofisi za CCM ungekuwa unaijua kariakoo usingeandika pumba hizo.

Wewe Dar es Salaam umekuja umefikia Kimara mie Dar es Salaam, Kariakoo nimezaliwa halafu wewe wa kuja unipe mie historia ya Kariakoo si vichekesho.

Kwa kukusaidia tafuta kitabu cha Mohamed Said kaelezea historia ya Kariakoo.

Ritz,
Ulizaliwa Dar-es-salaam, Mwanza au Mkendo Musoma?
 
Kibaya zaidi kwa Mzee M.Saidi ni kuwa now days kariakoo yote inanunuliwa na inaendelea kununuliwa na watu wakuja wa makabila tafauti kutoka Mikoa ya Bara,wapemba na kidogo waarabu. Watu wananunua hayo magofu yenu ya zamani na wanapandisha magorofa. Yaani ukiona kuna gorofa jipya linajengwa ujue hapo rafiki yake au mfia dini wake Mohamedi Saidi
ndiyo keshanunuliwa na anaelekea kuanza maisha mapya maeneo ya Chanika kwa mgao wa pesa hiyo ya mirathi ya watoto 6 au 10....so day by day watu kama dizain ya mzee M.Saidi wanazidi kupungua kariakoo kwa kuuza magofu yao na kwenda kuishi nje ya mji huko!. Maana kwa mzee M.Saidi kwake yeye eneo la Kariakoo ndiyo Tanganyika mzima. Pole sana mzee wetu!
Hii mbinu tumeishtukia zamani.Hata makaburi pia mnataka kuchimbua mifupa muipeleke huko Mbagala.
Tatizo ni umaskini wetu kwa kutokufaidika na ajira serikalini ambazo hutolewa kwa mtindo wa kimfumo.Hata hivyo huko tuendako mtaona tutabanana hapa hapa.
 
MMM unaposema ume discredit ''utafiti'' naona wapo wanaoweza kutoa benefit of doubt ku-sooth nafsi zao.
Mimi nasema ni NULL AND VOID.

Tumejifanya mazumbu kuku na kukubali kuzijadili kama zilivyo, hata katika uzumbu kuku wetu wa kujifanya, Mohamed ameshindwa, nasema failed to stand and defend a single line. failure! Mo failed misereably to defend his own research methodology and findings scientifically.

Halafu bado anatumia neno research. Please tumia neno jingine ili researchers wasipate nausea.
Miaka 15 analisha vijana wetu ngano hii! Jamanani jamani ! eh mola.

Hilo la Kawawa linachekesha kweli. Hivi 1982 Kawawa alikuwa VP!
Alichokifanya ni kitu kinaitwa ''sensational news'' kwamba watu washtuke kuwa aliyekuwepo alikuwa VP.

Ni kile kile cha kuonyesha namba 18 Vs 82 huku akibadili maudhui ya ''reseach'' kila uchao.
Mara 18: 82 Muslim vs Christian, mara 18:82 Muslims vs Non Muslims. Ilimradi kuamsha hisia tu.

Ni kile kile cha hotuba ya karne ya Rehani Waikela ambayo nakala yake haipo duniani lakini tunaambiwa alisimama na kutaka kumbaraza Nyerere kwa bakora. Ushabiki ni kitu kibaya sana hasa kwenye intellectual discourse.
Nakuahidi kwa uwezo wa Allah nitakuletea alipodefend chapters za uongo wenu.Nitakapokuletea uwe tayari kuchagua tusi la kujitukana mwenyewe.Naona Nguruvi utaalamu kidogo wa statistics unataka kukupa kiburi na kufru.
 
Hata kama upo kazini kuifanyia uadui historia halisi ya Tanzania na mchango wa waislamu kutafuta uhuru lakini unapoita si ngano bali ni porojo unajitangaza ujinga na upuuzi wako.Kwa kauli hii inakutoa kwenye mchangiaji wa mjadala na kukuingia kwenye mpayukaji ambayo ni sifa ya wendawazimu na walevi wa gongo.
Mapovu ya nini?
 
Ritz,
Ulizaliwa Dar-es-salaam, Mwanza au Mkendo Musoma?

Jasusi,

Mimi nimezaliwa karibia na Ikulu, karibia na uwanja wa golf, karibia na bahari.

Mwanza, Musoma, Shinyanga, Tanga, Bukoba, na kwingineko ni kuangaika tu na maisha.
 
Lakini bado kuna wingu kuhusu hiyo hotuba ya UNO. Ukisoma kitabu cha Nyerere utaona kwa hakika kaiandika mwenyewe kwa sababu kaiweka in the first person. Na kama ali-plagiarize hotuba ya wengine pia tunapaswa kujua kwa faida ya historia. Na wewe, kama mwandishi ambaye umearifu kuwa hotuba ya UNO iliandikwa na wengine mbali na Nyerere, unalo jukumu la kuthibitisha hilo kwetu wasomaji.

Jasusi,

Kalamu nimeshanyanyua na wino umekauka.
Sasa ni zamu yenu kuandika.

Hivi nyinyi hamchoki huku JF kuwa wauliza maswali na mimi muindikaji wenu?
 
MF,

Unakifahamu kisa cha Shylock?
Ukiwa hukijui soma ''Merchant of Venice.''
William Shakespeare.

Humo utamkuta Shylock ambae alipompata
adui yake hakumwachia akidai kilo yake moja
ya nyama sharti aipate.

Huyu Mohamed Said kafanya kosa basi ndiyo
hapa hapa sisi hatutaki kusikia chochote.

Ni kosa, kosa, kosa, kosa, kosa dunia lazima
isimame hadi kosa, kosa, lifikie mwisho.

Yote hayana maana hadi tupate hatima ya kosa hili.
Kosa, kosa, kosa, kosa, kosa...
Unakubali umekosea?
 
Nakuahidi kwa uwezo wa Allah nitakuletea alipodefend chapters za uongo wenu.Nitakapokuletea uwe tayari kuchagua tusi la kujitukana mwenyewe.Naona Nguruvi utaalamu kidogo wa statistics unataka kukupa kiburi na kufru.
Yaani wewe Ami kwa uwezo wa Allah unaahidi kuleta ngano za mohamed akidefend chapters za hizo hizo ngano alizoziandika! Nilidhani kwa akili yako utajitahidi kuleta kitu kipya tofauti na ngano ulizolishwa na sasa zinapata upinzani mkali kutoka kwa watu wenye uelewa mpana zaidi yake!...nakulilia shule...!
 
Last edited by a moderator:

Mag,

Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Wewe Dar es Salaam umekuja umefikia Kimara mie Dar es Salaam, Kariakoo nimezaliwa halafu wewe wa kuja unipe mie historia ya Kariakoo si vichekesho.
Duh, siwezi kushindana na jini, mimi ni binadamu...naweza nikazaliwa sehemu moja tu, si kila sehemu Tanzania!
Kwa kukusaidia tafuta kitabu cha Mohamed Said kaelezea historia ya Kariakoo.
Ha ha haaaa...! Acha utani.
Mag,
Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
Mohamed Said, kwenye kundi la vipofu, mwenye chongo ni mfalme!
 
Last edited by a moderator:
Duh, siwezi kushindana na jini, mimi ni binadamu...naweza nikazaliwa sehemu moja tu, si kila sehemu Tanzania!

Ha ha haaaa...! Acha utani.

Siyo kushindana onyesha wapi nilipokuambia nimezaliwa kwingine unaleta porojo tena.

Leo unakesha JF.
 
Yaani wewe Ami kwa uwezo wa Allah unaahidi kuleta ngano za mohamed akidefend chapters za hizo hizo ngano alizoziandika! Nilidhani kwa akili yako utajitahidi kuleta kitu kipya tofauti na ngano ulizolishwa na sasa zinapata upinzani mkali kutoka kwa watu wenye uelewa mpana zaidi yake!...nakulilia shule...!
Yote yanawezekana kwa uwezo wa Allah.Lakini ikiwa unatamani kitu kipya ni HIKI.usisite kuleta jibu kumsaidi Mundungus ambaye bado hajarudi.
Sidhani kama hiyo mpya imeandikwa na Mohammed Said.Ikiwa ni yeye basi natanguliza kuomba samahani.
 
Mag,

Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
Kumbuka vitabu vya historia vilivyofanikiwa ni vile vilivyoaandikwa na watu wahusika au wa karibu na wahusika.Mmoja alijaribu kuandika kule Zanzibar kujaza uongo wake wazanzibari wakakichoma moto.
Hadithi za Mtume S.A.W.sahih au karibu yake ni zile zilizotokana na maswahaba wake.
Tanzania nijuavyo kuna vitabu vitatu vikubwa vya historia,mojawapo ni hii ya Maisha ya Abdulwahid Sykes.Hizi zote zimeandikwa na watu ambao ni wahusika wa karibu.
Yerico na Mwanakijiji mkiandika historia kwanza mtapata tabu kubwa kukamilisha na kufikia malengo yenu ya kutaka kupuuzwa waislamu katika historia hiyo.
 
Back
Top Bottom