Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mzee Said, tuliache hilo la 'kosa' la Kawawa na tuseme ulipitiwa na halikuwa lengo lako kutumia cheo cha Umakamu wa Rais to sensationalize hoja yako. Lakini tuzungumzie utafiti wenu wa Warsha:

a. Ulifanyika vipi
b. Kwanini matokeo yasiyohusisha vitengo muhimu yachukuliwe ni ya chuo kizima?
c. Kwanini matokeo (tukiamini kuwa ni ya kweli) yachukuliwe ni ya nchi nzima na taasisi zote za elimu ya Juu nchini? Je hali ilikuwa vipi kwenye vyuo vingine, mgawanyo wa Waislamu naWakristu ulikuwaje?
d. HOja ya kuwa "Dar-es-Salaam ina Waislamu wengi" kwanini haikutumika kuelezea Tanga, Mtwara, Lindi au Kigoma ambako kote ni sehemu zenye Waislamu wengi? Kwanini Dar iwe kigezo cha Waislamu wote Tanzania?
 

Juu ya BIAFRA na Mwalimu,

Hili linahitaji upembuzi yakinifu, ukikurupuka kutafakari kauli/maoni Mwalimu kama alivyokujibu Shekhe Mohamed Said utaona wazi kuwa kulikuwa na mtazamo hasi kwa mwalimu.

Zingatia huyuhuyu Mwalimu alipinga utawala wa kizayuni kuikoloni Palestine, vuta picha kisha tafakari ya Biafra.
 


Nguruvi,

Sasa tutabaki hapa hapa kwenye kosa langu au utapenda tuendelee na habari za Sheikh Malik?
Nakusikiliza.
 
Yaliyopo yametosha kuueleza ulimwengu juu ya udharimu wa Mohamed Said,

Ni vigumu kwako kuamini kuwa yatosha kwakuwa usehemu ya maasi.
 

MF,

Kosa lolote katika kazi zangu ni kosa la kibinadamu wala sikudhamiria.
Umeniuliza swali zuri na mimi nimekupa jibu hilo hapo juu.

Ungesimama kwenye swali nami ungenitia moyo wa kukuuliza swali zuri
vilevile kwa yote ambayo nimeandika hapa na wewe nadhani umesoma.

Bahati mbaya hukuishia hapa ''bug'' ya Mohamed Said ''bashing'' imekushinda
nguvu.

Umezungumza kuhusu ''ngano.''

Kwa kuwa tokea mwanzo hukuniamini nami sina sababu ya kukuuliza hilo swali
langu.
 
Maswali mazuri sana, majibu ya Shekhe wetu Mohamed Said yatatoa mwangaza zaidi wakuuelewa utafiti wao hawa Warsha.
 
Nimeishi Muheza,Agley,Udowe na Sikukuu. Hata hivyo hapo nimeuliza watu wawili tofauti na wewe umenipa jibu la mmoja tu.
Na je unajua ni kwanini aliwekwa kizuizini? Alikuwa Bakwata au swarsun?

Sikukuu na Udowe nyumba ipi? hapo kuna ya Alamarhum Sheikh Hashim bin Abdallah, usoni kwake kwa kina Moshi (nyumba imebomolewa siku nyingi sana), upande wa pili kwa kina Mwita (wapo) usoni pembeni yake kwa Sharrif. Hiyo ndiyo udoe na Sikukuu. Lete habari zako.
 
Ile shule ni Mwisenge, siyo Mwetenge.
 

Mkuu Nguruvi3, wewe acha tu...huyu Mohamed Said yawezekana alifanya utafiti kweli lakini utafiti wenyewe ulijikita katika kuwatambua aina ya watu ambao angeweza kuelekeza ngano zake kwao na wao wakazimeza nzima nzima bila kufikiri, kuuliza wala kutafakari. Kuna wakati tulimpa fursa ya kujinasua mapema asije akaumbuka na kuhadhirika...nakumbuka sana nilivyomsihi achutame kwani anazidi kuanika utupu katika simulizi zake lakini hakunisikiliza.

Hatukukata tamaa na hivyo tukazidi kumuuliza hivi, je Mohamed kama ungepewa nafasi ya kuiandika kitabu chako upya, kuna marekebisho ungekuwa tayari kuyafanya? Kwa kibri isiyo kifani akatamba hawezi kufanya hivyo...kuwa yote aliyoandika ndiyo ukweli na UKWELI MTUPU, DUH!

  • Nakumbuka alivyodai, eti kulingana na maandishi ya John Iliffe, Kleist Sykes ndiye aliasisi AA mwaka 1929, tukamwambia hapana huyo alikuwa katibu tu, Raisi muasisi alikuwa Cecil Mtola, Myao, msomi na Mwalimu.
  • Nakumbuka alivyodai kulingana na utafiti wake kuwa mikutano ya kwanza wa AA ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Sykes nikamwambia, hapana wewe muongo, mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola kabla ya Gavana Cameron kutoa kiwanja na Headquarter ya AA kuhamia New Street mwaka 1931.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa mwaka 1950, Tanganyika ilikuwa Mandate Territory, akaambiwa acha uongo, mwaka 1950 Tangayika ilikuwa bado Trust Territory.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere aliingizwa kwenye siasa mwaka 1953 alipotambulishwa kwa wazee wake Mohamed Said mjini Dar es Salaam, akaambiwa la hasha toka mwaka 1946 Mwalimu Nyerere tayari alikuwa kiongozi wa AA Tabora.
  • Nakumbuka alivyolalama baada ya kufanya utafiti wa miaka 15 na kudai kuwa kuwa kiongozi wa kwanza wa TAA alikuwa Abdulwahid Sykes, tukamwambia, no way, Raisi wa kwanza wa TAA alikuwa msomi wa Makerere Dr. Vedasto Kyaruzi.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Waislaam walisahaulika katika uongozi baada ya uhuru na idadi yao kuwa ndogo kwenye baraza la mawaziri wa kwanza Tanzania, nikamwita muongo mkubwa na kumpa si majina tu bali picha ya baraza hilo idadi kubwa ikiwa ni ya Waislaam.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa EAMWS ilikataliwa kujenga chuo na baadaye kupigwa marufuku, nikamweleza jinsi EAMWS ya Ismailia ilivyovamiwa na viongozi wa AMNUT baada ya kutoungwa mkono na Waislaam wenyewe na kuigeuza kuwa kama chama cha upinzani.
  • Nakumbuka alivyodai Darul Iman ilikatazwa kujenga chuo cha ufundi Kibaha na serikali, akapewa kweli kuwa sababu ya Darul Iman kufungasha virago ilikuwa ni kukosa imani baada ya mafisadi kutafuna hadi hela za kujenga misikiti na kuamua kusitisha mipango yake Tanzania.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa Mwalimu Nyerere hakuweza kumkumbuka Abdulwahid Sykes kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam, akaumbuka pale alipowekewa hotuba ya Mwalimu lakini bila aibu akaanza na kudai mkanda wa sauti na video.
  • Nakumbuka alivyodai ni Profesa Kigoma Malima ndiye aliyeanzisha mpango wa kutumia namba kwenye mitihani, akaumbuka pale alipoambiwa mpango huo ulianzishwa miaka mingi kabla ya Malima ila kitu alichotaka ni upendeleo maalum kwa wanafunzi wa Kiislaam, mpango ulioungwa mkono na Meya Kitwana Kondo.
  • Nakumbuka alivyodai kuwa fujo za Mwembe Chai zilianza mwaka 1998 wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, tukamwambia, hapana, huo ulikuwa ni mwendelezo tu wa fujo zilizoanza wakati wa Hasan Ali Mwinyi ambapo bucha za kuuza nyama zilishambuliwa na watu waliotoka Misikitini.
  • Nakumbuka alivyodai...I could gon on and on!
Yaani kama unavyosema Nguruvi3, kwa mtu yeyote mwenye uelewa mpana, madai Mohamed Said ni upuuzi na kama unavyosema ni NULL AND VOID. Hata hivyo yana lengo na kwa kiasi fulani kafanikiwa kwa sababu hatuna serikali, this man should be behind bars pamoja na wanafunzi wake Ponda, Ilunga, Uamsho and the rest of the gang...nawakumbuka kwa mbali Mzige, Shaaban na Hashim Saiboko.

Nakumbuka WARSHA iliyokuwa inaandika makala katika gazeti la Annur lililokuwa linafadhiliwa na bwana Kileo...wao ndio walikuja na mkakati wa kuwa na Ubungo Islamic Centre na kuanzishwa kwa redio Kheri. Kituo kikubwa cha kazi za Mohamed Said ni msikiti wa Manyema pale nyuma ya CCM Lumumba. Msikiti ule unamtafaruku kwasababu wamanyema walitaka kupewa jina na uongozi na in fact ndio wanaoongoza akina Jongo. Mohamed Said pia ndiye mentor wa Basaleh pamoja na kuwa kamzidi kiumri.
 
Mohamed,
Nitaendelea kukupinga kuwa hotuba aliyoitoa Nyerere UNO 1955 iliandikwa na akina Sheikh Hassan bin Amir. Huenda kweli walikuwa wameandika hotuba yao lakini ukisoma lugha ya ile hotuba ni typical Nyerere. Na Nyerere asingeiweka kwenye kitabu chake "Freedom and Unity," kama alikuwa ameinakili hotuba ya mtu mwingine. Nilidhani tumeshakubaliana juu ya hili lakini naona mwenzetu ukishashikilia kitu, hata ikithibitika kuwa umekosea, unaendelea kung'ang'ania tu. Sikutaka kurudi hapa kusema hili lakini umelirudia mara hamsha ishirini eti hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na watu wengine. That is a lie!
 

Amina Amina
 


Mag,

Mimi si mtu wa kusutana.

Naona hii ndiyo staili ulokuja nayo ati nilisema kuwa AA ilianzishwa nyumbani kwa Kleist.
Sijapata kusema hili kwa kuwa historia hiyo naijua.

Nimetoa rejea mkasome maisha ya Kleist Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam East
Africana.

Kleist kaeleza kila kitu kuhusu AA.
Hamjakwenda.

Naweka tena reference yake:
A.D. Sykes "The Life of Kleist Sykes," University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15.

Sioni sababu ya kuvutana kwa haya.

Abdulrahman Kileo Allah atamlipa.
Kileo hakuwa anafadhili hiyo si lugha kwa mja anaetoa chake kumpa Allah.

Vipi mja atamfadhili Allah?

Kileo akitoa katika njia ya Allah.

Hayo mengine sina haja ya kuyagusa nakuachia mwenyewe.
 
Jasusi, huyo ndiye Mohamed Said, kurudia rudia uongo kwa matumanini kuwa mwishowe utageuka na kuwa kweli! Kinachosikitisha wako wanaoziamini hizo ngano na wako tayari kujitoa mhanga kuzitetea hata ikibidi kuhamisha vitanda kulala hapa jamvini. Ukisikia kuathirika ndiko huko.
 
Last edited by a moderator:
Mag3,

Chutuma basi na wewe hayo maneno mengine siwezi kuyamalizia kutoka na umri wako.

Acha uongo Msikiti wa Manyema haupo nyuma ya ofisi za CCM upo nyuma ya CRDB mtaa wa Mkunguni...Sheikh Basaleh na Msikiti wa Manyema wapi na wapi? Sheikh Basaleh Msikiti wake ni Idrisa upo Tandamti na Msimbazi.

Chutama basi au unaona aibu.

Hizo ngano zako mlishe Nguruvi3 na Mwanakijiji hujui chochote kuhusu Waislam nyuma ya ofisi za CCM kuna misikiti miwili siyo Manyema huijui hiyo Misikiti halafu unataka kuja kuropoka humu muongo waheed.
 

Inaonesha hujapitia kwa umakini huu uzi, MM kakosea mara nyingi tu "intentionally" na tuka "point out", licha ya makosa ya kibinaadam kama vile ya lugha na sarufi.
 

Hahahaha, kama unao ukweli si uuthibitishe?

=Khamsa wa Ishirin mara, ingeleta raha zaidi.
 

Mohamed Said,

Huyu jamaa ni wakumsamehe tu analazimisha vitu bora umempa huo mpini aangaike nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…