Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Jasusi,

Nadhani nilipata kukugusia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyoandika mapendekezo ya
katiba kwa Gavana Edward Twining.

Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Mapendekezo ya kamati hii yalizungumzwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.

Yaliyokuwa katika mapendekezo yale ya Political Subcommittee hayana tofauti na yale TANU iliwasilisha
UNO 1955.

Na mengine mengi nikakueleza nikiamini utanielewa.

Kuna mengine sijayasema lakini kuhusu document hiyo nadhani unajua kuwa ilipotea na haionekani
popote.

Hiyo ''kunakili'' unasema wewe.
Mimi sijasema neno hilo.

Mimi sijasema uongo na ndiyo maana husema siku zote.
Nanyi andikeni huo ukweli tuusome.

Hivi unajua kama katika ile Political Subcommittee alikuwapo mwanasheria Earle Seaton kama mshauri
wa TAA toka 1950?

Unaijua style ya uandishi wa Seaton?
Unajua kuwa Seaton na Abdu walikuwa marafiki wakubwa?

Nadhani unatambua kwa nini nakudokeza haya.
 
Sasa hivi mmekuja na mtindo mpya mtu akikosea kuandika basi kosa la jinai...ha haa ha.

kuna makosa ya uandishi; lakini kuna makosa ya facts; makosa ya uandisi si ya msingi sana tena wala si ya kujali; makosa ya facts (factual errors) ni makosa ya hhoja nzima. Ukikosea kwenye facts hoja yako haiwezi kusimama. Kama unasema utafiti uliofanywa na Warsha ni wa kisomi na tukaonesha kuwa si wa kisomi hahpo si makosa ya uandishi...
 
Unaijua historia ya Kariakoo wewe? Unajua kuwa wakati wa Mjerumani Kariakoo haikuwepo? Unajua Kariakoo ilikuwa ni shamba tu la Mjerumani alilolinunua kutoka kwa Sultani? Kwa ufupi ni kuwa baada ya vita vya kwanza vya dunia Kariakoo ilikuja kuwa kituo cha kijeshi na baadaye makazi ya kwanza ya African Carrier Cops (kariakoo). Unajua baada ya Uingereza kuiasisi Tanganyika kwa nini iliitwa nchi ya Rangi Tatu? Unajua ni mwaka gani iliamuliwa na serikali ya wakati huo kuligawanya hilo shamba kuwa viwanja na kuwapa "natives"? Unajua "natives" wa kwanza Kariakoo walikuwa ni wa jamii ipi? Usichokijua ni kama usiku wa giza, pole sana.
 

Ami, Mohamed ni mwanadamu kama wengine. Kama umeona kuna mapungufu je, bado unampa benefit of doubt ya kutumia mapungufu hayo katika kuelezea dhulma?.
Wacha kushangilia kasoro ndogo kati ya rundo la ukweli usiokanushika
Wewe ni nani hata ujue kuwa mapungufu ni ya makusudi?.Wapi amesema anasimamia dini?.Usiwe unasingizia wenzio uwongo.
Unauliza ulitaka Nyerere awafanyeje?.Hilo swali limejibiwa mara nyingi na mantiki iko wazi.Hao wazee wala hawakudai kufanyiwa lolote.Kilichowauma na sisi kutuuma ni kufanyiwa vibaya kwa kutukanwa juhudi zao.

Kwa hili nakuona umehemkwa bure.Kukubali kosa na kukiri kosa ni tabia ya kiungwana.Kwa Mohammed kitu kidogo kama hicho ni sadaka ambayo wala haitopunguza uzito wa ukweli alioufukua ambao mmejipinda kutaka kuurudisha nyuma.
Kama ni kujibu basi tukianza kuorodhesha sehemu ambazo mmeshindwa kujibu basi huu mjadala utakuwa mrefu mara kadhaa kuliko ulipofikia.
Madhumuni ya mfano huo ilikuwa ni kuonesha kuwa hakujawa na tishio la aina hiyo.Hata dreamliner huwa zinapata mikwaruzo ya aina tofauti lakini haikuwa sababu ya kusitishwa kuruka.
Nimetoa mfano wa Biblia lakini mmekaa kimya.Hapa ndipo mnapomshinda Mohammed katika ujanja wa kutokujibu vitu vigumu.

Huko ndiko kuhemkwa kwa kutamani sifa.Narudia kusema wanaojiamini kuita historia iliyoandikwa na Mohammed ni uzushi na uongo basi ni watu wa kutumwa na mfumo kuzima mafanikio yake kama mtaweza.
 
Mohamed,
Nina swali jingine la ziada. Usichoke na maswali yangu, tafadhali. Mara kadhaa umezungumzia Christian lobby, sasa sijui hii Christian lobby ni akina nani. Niliwahi kufanya kazi katika bunge la Marekani na malobbyist wote wakifahamika pale wanapokuja kukutana na wabunge. Utasikia huyu ni lobbyist wa farmers union, lobbyist wa jews, etc. etc. But you could identify them. Sasa wewe unazungumzia Christian lobby in Tanzania in the abstract. Can you at least put a name or a face on them? Kama ni akina Peter Kisumo, John Malecela, at least tujue hawa akina Christian lobby ni akina nani. Ni hilo tu.
 

Sasa umeandika nini hapo bado haijafuta uongo wako kuwa Msikiti wa Manyema upo nyuma ya ofisi za CCM ungekuwa unaijua kariakoo usingeandika pumba hizo.

Wewe Dar es Salaam umekuja umefikia Kimara mie Dar es Salaam, Kariakoo nimezaliwa halafu wewe wa kuja unipe mie historia ya Kariakoo si vichekesho.

Kwa kukusaidia tafuta kitabu cha Mohamed Said kaelezea historia ya Kariakoo.
 

Lakini bado kuna wingu kuhusu hiyo hotuba ya UNO. Ukisoma kitabu cha Nyerere utaona kwa hakika kaiandika mwenyewe kwa sababu kaiweka in the first person. Na kama ali-plagiarize hotuba ya wengine pia tunapaswa kujua kwa faida ya historia. Na wewe, kama mwandishi ambaye umearifu kuwa hotuba ya UNO iliandikwa na wengine mbali na Nyerere, unalo jukumu la kuthibitisha hilo kwetu wasomaji.
 

Ritz,
Ulizaliwa Dar-es-salaam, Mwanza au Mkendo Musoma?
 
Hii mbinu tumeishtukia zamani.Hata makaburi pia mnataka kuchimbua mifupa muipeleke huko Mbagala.
Tatizo ni umaskini wetu kwa kutokufaidika na ajira serikalini ambazo hutolewa kwa mtindo wa kimfumo.Hata hivyo huko tuendako mtaona tutabanana hapa hapa.
 
Nakuahidi kwa uwezo wa Allah nitakuletea alipodefend chapters za uongo wenu.Nitakapokuletea uwe tayari kuchagua tusi la kujitukana mwenyewe.Naona Nguruvi utaalamu kidogo wa statistics unataka kukupa kiburi na kufru.
 
Mapovu ya nini?
 
Ritz,
Ulizaliwa Dar-es-salaam, Mwanza au Mkendo Musoma?

Jasusi,

Mimi nimezaliwa karibia na Ikulu, karibia na uwanja wa golf, karibia na bahari.

Mwanza, Musoma, Shinyanga, Tanga, Bukoba, na kwingineko ni kuangaika tu na maisha.
 

Jasusi,

Kalamu nimeshanyanyua na wino umekauka.
Sasa ni zamu yenu kuandika.

Hivi nyinyi hamchoki huku JF kuwa wauliza maswali na mimi muindikaji wenu?
 
Unakubali umekosea?
 
Nakuahidi kwa uwezo wa Allah nitakuletea alipodefend chapters za uongo wenu.Nitakapokuletea uwe tayari kuchagua tusi la kujitukana mwenyewe.Naona Nguruvi utaalamu kidogo wa statistics unataka kukupa kiburi na kufru.
Yaani wewe Ami kwa uwezo wa Allah unaahidi kuleta ngano za mohamed akidefend chapters za hizo hizo ngano alizoziandika! Nilidhani kwa akili yako utajitahidi kuleta kitu kipya tofauti na ngano ulizolishwa na sasa zinapata upinzani mkali kutoka kwa watu wenye uelewa mpana zaidi yake!...nakulilia shule...!
 
Last edited by a moderator:

Mag,

Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
 
Reactions: Ami
Wewe Dar es Salaam umekuja umefikia Kimara mie Dar es Salaam, Kariakoo nimezaliwa halafu wewe wa kuja unipe mie historia ya Kariakoo si vichekesho.
Duh, siwezi kushindana na jini, mimi ni binadamu...naweza nikazaliwa sehemu moja tu, si kila sehemu Tanzania!
Kwa kukusaidia tafuta kitabu cha Mohamed Said kaelezea historia ya Kariakoo.
Ha ha haaaa...! Acha utani.
Mag,
Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
Mohamed Said, kwenye kundi la vipofu, mwenye chongo ni mfalme!
 
Last edited by a moderator:
Duh, siwezi kushindana na jini, mimi ni binadamu...naweza nikazaliwa sehemu moja tu, si kila sehemu Tanzania!

Ha ha haaaa...! Acha utani.

Siyo kushindana onyesha wapi nilipokuambia nimezaliwa kwingine unaleta porojo tena.

Leo unakesha JF.
 
Yote yanawezekana kwa uwezo wa Allah.Lakini ikiwa unatamani kitu kipya ni HIKI.usisite kuleta jibu kumsaidi Mundungus ambaye bado hajarudi.
Sidhani kama hiyo mpya imeandikwa na Mohammed Said.Ikiwa ni yeye basi natanguliza kuomba samahani.
 
Mag,

Kupinga hapa JF kutasaidia kitu gani bila kuwa na kitabu chenu maktaba
wanafunzi wa historia ya uhuru wakakisoma?
Kumbuka vitabu vya historia vilivyofanikiwa ni vile vilivyoaandikwa na watu wahusika au wa karibu na wahusika.Mmoja alijaribu kuandika kule Zanzibar kujaza uongo wake wazanzibari wakakichoma moto.
Hadithi za Mtume S.A.W.sahih au karibu yake ni zile zilizotokana na maswahaba wake.
Tanzania nijuavyo kuna vitabu vitatu vikubwa vya historia,mojawapo ni hii ya Maisha ya Abdulwahid Sykes.Hizi zote zimeandikwa na watu ambao ni wahusika wa karibu.
Yerico na Mwanakijiji mkiandika historia kwanza mtapata tabu kubwa kukamilisha na kufikia malengo yenu ya kutaka kupuuzwa waislamu katika historia hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…