usisite kuleta jibu kumsaidi Mundungus ambaye bado hajarudi.
.
Mwandishi aliyeandika makala uliyo iweka
ni personal opinion yake. Alichoandika si facts.
Sawa sawa na makala aliyoleta jasusi hapa ya nani kama nyerere iliyoandikwa kwenye same newspaper.
History ya Nyerere ipo, story za nyerere zipo, video zake zipo, audio za hotuba zake zipo, facts kuhusu yeye pia zipo. So ni swala la msomaji na mtu mwenyewe kufanya upembuzi yakinifu, kumchambua na hatimae kujiridhisha yeye mwenyewe Nyerere anamchukiliaje.
Ila kwa kusoma makala moja, na kumsikiliza mtu moja kukuambia kuhusu nyerere na hapo hapo ukafikia tamati na Kumlabel nyerere unavyotaka wewe (kama ni shujaa au mdhulmati) basi utakuwa humtendei haki.
Mimi sio mtaalamu wa Historia, mimi pia sina upande katika mjadala huu, kwasababu sio mtaalamu wa historia, hivyo kuwa na upande itakuwa nasukumwa na hisia zaidi. Kwasababu Mzee Saidi akinipa nondo zake ntajuaje kama hizi ni za ukweli au za uongo.. Sina utalaamu.
Vivyo hivyo Mzee MM, nguruvi3 na mg3 bila ya kumsahau Jasusi wakitoa nondo zao mimi ntajuaje kama hizi ni za ukweli au za uongo.
Ila mimi na tatizo na ukweli wa swala linalo itwa "dhulma" kwa waislamu.
Ingawa si mtaalaamu na sijabobea katika historia, lakini najua kutambua kama sehemu ina makosa. Hasa linapokuwa linahusu vitu vinavyoweza kuwa prove bila ya kutumia historia.
Huu mnakasha ni mrefu sana, vivyo nina uhakika ni watu wachache sana ambao wameufutalia neno kwa neno kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Ila katika fuatilia yangu mimi, mwanzoni Mzee Said, alionekana kuwakimbiza sana wanao mpinga, na hasa walionekana wanampinga tu kutokana na hisia zao binafsi na walikuwa hawana facts na hawaijui historia vizuri.
Kama umefuatilia vizuri hata wale Pro Mzee Said arguments,(zomba,Ritz, etc) walikuwa wapo kasi sana mwanzoni lakini sasa hivi wamepunguza spidi hata wao wenywe wamepungua (inawezekana pia majuku yamewashika)..
Vivyo hivyo kwa Anti-mzee Said au Pro -Yericko arguments, walikuwa hawana nguvu kabisa mwanzoni lakini sasa naona wameshika kwenye makali, na wako full force.
Kwanini
Na kuna sehemu moja ambayo pamekuwa moto ambapo Anti-Mzee Said, wamepashikilia.
WARSHA's Research
Hizi data zilitumiwa sana humu kwenye mnakasha, na hata kwenye mijadala mengine humu JF na kwenye mitandao mengine, data zilitumiwa kama scientific proof au Tangible truth dhidi ya "dhulma" kwa waislamu. Hizi data zilishika makali na zikakata kata.
Wakaja watu humu Anti-Mzee Said argument wakaleta na wao tangible proof kuonesha highly inaccuracy ya ile Research, the whole methodology wameonesha ina uwalakin, wameelezea kwa kirefu sihiitaji kuingia kiundani.
Hapo is where i come in. Mimi nikaja kumuuliza Mzee Said apinge na adispute (KITAALAMU) claims za kambi pinzani na kudhibitisha ile Research haiko inaccurate na haiwezi kutumiwa kama ushahidi wa kitaalamu wa dhulma dhidi ya waislamu.
Hakuna aliyekuja mpaka sasa hivi, sio Mzee Said wala Ritz, wala wewe Ami wala mtu yoyote.
Sasa wewe ukaja na kuanza kutoa sababu zakitoto kwnye maswala ya kitaalamu. Ukaanza kusema makosa ni ubinadamu, Mzee Said ni binadamu. Inawezekana this, inawezekana that.... Maelezo mengi ya kuexcuse kitu kilichofanyika hapa.
Watu wengi wakaja wakaeleza ni vipi tofauti ya makosa ya kiuandishi na factual errors. Na kwanini wanasema hii ni factual error na hivyo hii Research iko null and void, haiwezi kutumika tena kama kigezo na kielezo cha dhulma dhidi ya waislamu.
Nakama mtu anajua ukweli huu na bado anataka kuitumia Research hii kuaminisha watu wengi ambao anajua kabisa hawajui au hawezi kujua kama i
Zile data sio sawa huyo ni MCHOCHEZI period.
Na mimi naongeze kusema, Mzee Said, ni msomi tena msomi sana, wasifu wake wenyewe mmeuona hapa.
Yeye na watu waliofanya hii Research inaonekana ni watu waliokuwa wanajua kabisa kitu walichokuwa wanafanya. Inawezekana kweli wana VALID madai, au Madai Halal, lakini kutumia njia zisizo halal kudhibitisha madai yako si uungwana. Huku hakuna tofauti na uchakachuaji.
Ni sawa wakristu nao wachukue data za chuo Huko Zanzibar na kuzitumia kama kielezo cha kusema kuwa kweli waislamu hawadhulumiwi Tanzania.
Na hapo ndo lile swala la credibility nililolisema linapokuja...
Kama Research tu ina uwalakin? Kitu ambacho can be proven wrong... Vipi kuhusu reference nyingine ambazo haziwezi kudhibitishwa????
So nadhani hapo mimi ndo naposimamia. Sitaki kusema tuache kuzungumzuia Dai kuu, ila lipo na tunataka kulidhibitisha tulete ushahidi wa kihalali ma hata vijana wadogo wakislamu wajiridhishe kweli tunaonewa na kudhulumiwa au kuna tatizo somewhere...