Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed,
Na wale wafuasi wa ANC waliokuwa na kambi zao Morogoro si raia wa Afrika kusini?

Jasusi,

Kuna post nimesema nilipokuwa nazungumzia kuhusu hili nilikusudia ''the standard of the reasonable man.''
Hii alizungumza Lord Denning.

Hebu mpitie ukiwa na wasaa.
Inasaidia na inapunguza mambo kama haya.

Inasaidia kwa kuwa wala hutakuwa na haja ya kusoma katikati ya mistari.

Vinginevyo tutazungushana kwa jambo dogo.
 
Hapana. Hii si kweli kabisa. Kama wewe ni mtafiri mahiri ungejua kwamba Nyerere hakutaka Biafra ijitenge kwa madai ya kunyanyaswa na waislamu. Nyerere alichukua muda kuleta upatanishi kati ya Gowon na Ojuku na Gowon akawa mkaidi. Wakati huo Waibo wakiendelea kuuawa kama wanyama na Wahausa. There was a pogrom against the Ibos in Nigeria. Ila kwenu ninyi kama Muislamu anaua Wakristo siyo nongwa, inaonekana. Kuna thread humu aliianzisha William Malecela kuhusu Biafra. Itafute. Tulimpa somo kule. Kwa hiyo usidanganye watu kwamba Nyerere alitaka Biafra ijitenge kwa sababu hizo alizotaja mfumo.

Jasusi,

Nimekusoma.
Sidanganyi natoa fikra zangu.

Mimi si mtu wa kusema uongo.
Sina sababu za kufanya hivyo.
 
Ndugu, Mimi nimezaliwa kabla ya uhuru. Mama yangu Mkiristo na baba yangu Muislam. Nimefuatilia mnakasha huu, lakini nazidi kuchanganyikiwa. Naomba wachangiaji hapa ambao wengi mmedhihirisha uwezo wenu kwa hoja mtueleze kila mmoja kwa wakati wake suluisho la tatizo hili kati ya jamii yetu (Waislam na Waksrito). La sivyo mtaendelea na huu mtanange ambao hautakuwa na mwisho.

Mpaka sasa pande hizi mbili ni 2 parallel sides which will never meet.
For the sake of harmony in our up to now peaceful nation we need to reach a compromise.
Let us concentrate on the future and our well being.

Waislam msimamo mkali, hawataki kusikia harmony for the sake of our nation, wao wanataka kusikia harmony for the sake of ARABS traditions, building Islamic state to a country of mixed cultures and traditions. Labda wanaweza kukusikia hawa vibaraka wa al qaeda, al shabab na boko haram
 
Ndugu, Mimi nimezaliwa kabla ya uhuru. Mama yangu Mkiristo na baba yangu Muislam. Nimefuatilia mnakasha huu, lakini nazidi kuchanganyikiwa. Naomba wachangiaji hapa ambao wengi mmedhihirisha uwezo wenu kwa hoja mtueleze kila mmoja kwa wakati wake suluisho la tatizo hili kati ya jamii yetu (Waislam na Waksrito). La sivyo mtaendelea na huu mtanange ambao hautakuwa na mwisho.

Mpaka sasa pande hizi mbili ni 2 parallel sides which will never meet.
For the sake of harmony in our up to now peaceful nation we need to reach a compromise.
Let us concentrate on the future and our well being.

Nkungu,

Mnakasha huu ulianza na kauli ya maaskofu kufuatia vurugu za kidini.
Alituwekea Yericko Nyerere.

Maaskofu wao wakisema neno serikali inatimiza.

Safari hii nikaona ngoja niingie niwakumbushe hawa maaskofu historia
ya uhuru wa Tanganyika.

Nia ni kuwaeleza kuwa uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa kwa nafasi pana
sana na Waislam ambao hadi leo hawajanufaika na uhuru huo.

Mtanange ndipo ulipoanza hapo.

Nchi yetu ina matatizo Waislam tunabaguliwa na hii haikuanza leo ni historia
iliyoanza baada ya uhuru kupatikana1961 lakini serikali bado haijakubali hili.

Hapa ndipo tulipokwama.

Inachofanya serikali ni kukwepa na kutoa picha kuwa Waislam wana ugomvi
na Wakristo wakati si kweli.

Hivi sasa kuna makamati yanaundwa ya masheikh kukutana na Wakristo kudumisha
amani.

Kubwa ni kuwa hao masheikh wanaounda hizo kamati wengi wao ni kutoka BAKWATA.

Waislam hatuitambui BAKWATA na hao BAKWATA hawana yoyote anaewasikiza ila
serikali.

Umma mkubwa wa Waislam uko nje ya BAKWATA.
Hii ni kwa mukhtasari.
 
kutoa fikra zinazohusiana na historia halafu kwa makusudi ukapindisha historia hiyo, si ndo uongo mwenyewe?

Ntamaholo,

Uongo ni neno zito kumtuhumu mtu.
Ikiwa lipo la uongo katika nilosema tafadhali nifahamishe.

Insha Allah tutalijadili.
Nimeileleza historia ya uhuru kama ninavyoifahamu.
 
Waislam msimamo mkali, hawataki kusikia harmony for the sake of our nation, wao wanataka kusikia harmony for the sake of ARABS traditions, building Islamic state to a country of mixed cultures and traditions. Labda wanaweza kukusikia hawa vibaraka wa al qaeda, al shabab na boko haram

Ntamahalo,

Kwa lugha kama hiyo yako inakuwa tabu kwangu mimi kufanya majadala na wewe.
Nawaachia wengine.
 
Hali tete inayotikisa taifa sasa katika masuala ya kidini imewafanya baadhi ya wasomaji wa safu hii kuomba mwandishi airudie kwa madhumuni ya kuweka msisitizo. Kwa mara ya kwanza uchambuzi huu ulichapishwa na gazeti hili tarehe 21/11/201. Endelea:
NILIMSIKIA Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 10. Kuna jambo lilinigusa. Nadhani anataka kutuletea matatizo kwa kujadili – kwa staili aliyochagua – suala la udini.
Alisema katika kampeni za mwaka huu kumeibuka nyufa za udini na kwamba yuko tayari kuchukua hatua za haraka kuziba nyufa hizi. Ni hoja nzito, lakini inazua maswali.
Alipoingia yeye hakukuwa na kelele za udini. Ni kitu gani kinamfanya yeye aone udini katika siasa baada ya miaka yake mitano Ikulu? Kama kweli kuna udini, anawezaje kujivua lawama za serikali yake kujenga mazingira ya kuasisi udini huo?
Mwaka 2005, wakati chati yake kisiasa ikiwa juu, aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Dk. Methodius Kilaini, alitamka kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu.
Wengi tunajua kuwa Askofu Kilaini ni rafiki binafsi wa Rais Kikwete kwa muda mrefu. Tunajua pia kwamba urafiki huo ulijengwa na Kikwete kimkakati, na askofu akajikuta ameingizwa katika mtandao wa Kikwete bila kujua na bila kutaka.
Kwanini, kwa kauli hiyo, iliyotolewa na askofu Mkatoliki, Watanzania hawakumtuhumu Kikwete wala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendekeza udini, wala hawakumtuhumu Askofu Kilaini kwa kuingiza dini katika siasa?
Ikumbukwe kuwa Rais Kikwete alitumia vema kauli hiyo na nyingine, na hata baadhi ya makada na wapiga debe wake walitumia mazingira hayo kujinasibu na ‘misingi na malezi mazuri aliyopewa na Wakatoliki.' Mbona hakuna aliyenyoosha mkono kusema hapa kuna harufu ya udini?
Nasema hivi nikijua kwa dhati kuwa timu ya mtandao wa kampeni ilitumia nguvu nyingi sana kushawishi maaskofu wa madhehebu kadhaa ya dini yamuunge mkono. Namjua hata aliyetumwa kujenga mazingira mazuri kwa baadhi ya maaskofu Wakatoliki ‘wasimpige mawe' Kikwete kabla hata hajajitokeza kugombea.
Walifanya hivyo wakitambua kuwa nguvu ya kanisa ni kubwa na kwamba kama ingetumika dhidi yao wasingepata watakacho. Bahati nzuri, kwa nguvu ya ushawishi waliotumia, kanisa halikumpiga vita. Kwanini hakuna aliyezuka kuzungumzia udini katika siasa za Kikwete?
Ikumbukwe pia, Kikwete ndiye aliyenadi sera za CCM, ikiwamo ya kuwaahidi Waislamu kuwapatia ufumbuzi wa suala la Kadhi Mkuu, ambalo limeleta sokomoko kwa miaka mitano yote. Mbona Watanzania hawakusema Kikwete anaendekeza udini katika siasa?
Ninachokumbuka haraka haraka, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Rais Kikwete, yupo Mtanzania mmoja, Nathaniel Limu, aliandika kuhoji uteuzi wa viongozi waandamizi ndani ya serikali ya Kikwete, ambao wengi walikuwa Waislamu.
Kutokana na ukali wa mwandishi Limu, timu ya Rais Kikwete, kupitia kwa swahiba wake, Rostam Azizi, ilimuomba aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Salva Rweyemamu kujibu hoja za Limu.
Makala zote mbili, ya Limu na ya Rweyemamu ziliandikwa katika gazeti hili; moja ikikosoa uteuzi wa Rais Kikwete na kuuita wa kidini, na nyingine ikijibu na kutetea uteuzi huo kwamba ulizingatia sifa za walioteuliwa, na hata kuorodhesha majina na nafasi za vigogo Wakristo serikalini. Kwanini Kikwete hakujitokeza kukemea udini?
Yapo magazeti pia ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiandika habari na makala za udini, na yakihusisha dini za watu na uongozi wa vyama kadhaa vya siasa, hata kwa kuvitaja majina. Serikali iliyosajili magazeti hayo haijawahi kuvichukulia hatua kwa miaka mitano.
Na hata katika kampeni za mwaka huu, magazeti hayo yaliendelea kuandika habari zinazowataja baadhi ya wagombea kuwa ni makafiri, na kwamba wasichaguliwe. Kwanini serikali imekaa kimya hadi baada ya uchaguzi?
Si hilo tu. Hata katika baadhi ya nyumba za ibada, wamesikika viongozi wa kidini wakiwaomba wafuasi wa madhehebu yao wasiwachague makafiri. Na wengine walidiriki kumpigia debe Rais Kikwete katika nyumba hizo hizo za ibada. Kwanini hakujitokeza kukemea kauli hizo wakati ule?
Inafahamika pia kwamba miongoni mwa mbinu chafu za kampeni za chama chake mwaka huu, ni matumizi ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi, dhidi ya mgombea urais kupitia CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kwa misingi kwamba ni kafiri.
Rais Kikwete alishindwa kuwazuia wanachama wake kufanya kampeni hizo. Na walipogundua kwamba kampeni ya kidini dhidi ya Dk. Slaa ingeweza kuwafanya waamini wa upande mwingine nao wajihami, wakaanza propaganda za kumshutumu kwamba anatumia makanisa kufanya kampeni!
Kilichomzuia kuwazuia wafuasi wake kufanya kampeni za kidini kwa kutumia sms ni kitu gani? Mbona hakujitokeza kukemea baadhi ya misikiti na makanisa wakati wa kampeni? Anapata wapi leo nguvu ya kukemea matawi wakati amepalilia mizizi ya tatizo hilo hilo?
Lakini pia anaposema kwamba uchaguzi huu umefanyika kwa misingi ya udini, anataka kusema kwamba hizo kura milioni tano alizotangazwa kupata ni za watu wa imani moja (Waislamu) pekee? Anataka kusema kwamba kama Wakristo wangepiga kura za udini Dk. Slaa angepata kura milioni mbili zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)?
Au anataka kusema kwamba anajua zaidi, kwamba Wakristo walimchagua Mkristo, na Waislamu walimchagua Mwislamu, lakini kura zilizopigwa sizo zilizotangazwa?
Ipo pia hoja iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship. Mwaka 2000 alimpigia debe mgombea urais kupitia TLP, akimpinga rais aliyekuwa madarakani, Benjamin Mkapa.
Mbona hakuna aliyehoji udini katika siasa? Ni kitu gani kinawafanya watawala wafikirie kwamba kwa kuwa mwaka huu Askofu Kakobe ameendelea kuwapinga, alipinga dini zao si udhaifu wao wa uongozi?
Kama ambavyo baadhi ya watu wamejadili, watawala wamekuwa na tabia ya kuchomeka hoja za ajabu ajabu kama nia ya kuwaondoa Watanzania katika mijadala mizito ya kitaifa.
Na sote tumeshuhudia mbinu yao hii katika kampeni za uchaguzi mwaka huu. Hata baadhi ya vyombo vya habari vilivyomuunga mkono Rais Kikwete na CCM, jambo ambalo si kosa kisera vilishindwa kumjenga mtu wao, vikaishia kutafuta namna ya kubomoa washindani wake, hasa Dk. Slaa.
Lakini havikujua kwamba udhahifu wa kiuongozi wa Rais Kikwete wa miaka mitano iliyopita, usingeweza kuboreshwa au kutetewa kwa mashabulizi dhidi ya washindani wake.
Na tayari baadhi yetu tunajua mikakati yao ya kipropaganda ya kutumia mashambulizi dhidi ya kina Dk. Slaa na wenzao kuelekea 2015. Tunasubiri kuona ufundi utakaozitengeneza!
Lakini mwandishi mmoja, Richard Mgamba, amehoji: "Tanzania kuna udini upi? Nani mdini? Ukiomba Mahakama ya Kadhi kosa, ukiomba OIC dhambi; askofu akikosoa serikali tayari kuna udini. Hivi kweli nchi hii kuna udini au ni uoga wa viongozi wetu? Huko mtaani mbona tunaishi salama Wapagani, Waislamu na Wakristo? Huo udini wanauona watu wa usalama tu na bwana mkubwa? Jamani tusiingie kwenye mitego ya kipuuzi.
Udini kama ungekuwepo hapa, leo hii huko mitaani kwetu kungekuwa hakukaliki. Kama kuna Mkristo fulani mwendawazimu haina maana Wakristo wote wanafikiria hivyo, na pia kama kuna Mwislamu mmoja kichaa, haina maana Waislamu wote wako hivyo.
"CCM inadai ina wanachama milioni 5 nchi nzima. Imepata kura milioni 5.8 mwaka huu. Ina maana imepigiwa kura na wasio na vyama laki nane. Mwaka 2005 ilipata kura milioni 8.9, sasa ina maana hizo kura zilizopotea milioni 3.1 ni za Wakristo?
"Hivi mbona hatujiulizi uhalali wa watu milioni 19.5 kujiandikisha kupiga kura, kisha wanaojitokeza ni milioni 8.5 tu, hao milioni kumi na moja wako wapi? Hawa wote walikufa, au walisafiri au waliamua kutokupiga kura ghafla?"
Sasa Rais Kikwete atuambie. Amechaguliwa na Waislamu milioni tano? Au amechaguliwa na wana CCM milioni tano? Au amechaguliwa na Watanzania milioni tano?
Na huu ndio uongo wa takwimu za watawala. Kama wana CCM ni milioni tano, na rais anachaguliwa na watu milioni tano, basi amekosa uhalali wa kutawala Watanzania takriban milioni 45.
Na kama amechaguliwa na Waislamu milioni tano, basi maana yake CCM ni chama cha watu wa imani moja tu, jambo ambalo si kweli. Na kama miongoni mwa waliompigia kura Kikwete wamo Wakristo, basi hoja yake ni potofu.
Maana natambua kuwa idadi ya Wakristo nchini inazidi milioni tano. Vile vile idadi ya Waislamu ni kubwa kuliko milioni tano. Kwa mujibu wa ensaiklopidia ya Wikipedia, hadi mwaka 2007, idadi ya Waislamu na Wakristo nchini inazidiana kidogo, na wote wako kati ya asilimia 30 na 40 ya Watanzania wote.
Kama Waislamu wote wangehamasishwa rasmi kumchagua Mwislamu mwenzao, na kama wangekubali wote, Kikwete na Profesa Lipumba wangegawana kura.
Na kama Wakristo wangekuwa wamehamasishwa rasmi kumchagua Mkristo mwenzao na wakakubali, kura za Dk. Slaa zingekuwa nyingi kuliko milioni tano alizopata Kikwete.
Lakini suala la msingi analopaswa kujiuliza Kikwete ni hili. Hoja hii ya udini aliirithi kutoka kwa Rais Mkapa au imeota mizizi katika miaka mitano ya utawala wake?


h.sep3.gif



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Kikwete kachaguliwa kwa udini au siasa?
ban.maswali.jpg


Ansbert Ngurumo​
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Ritz,
Umezaliwa mwaka gani? Nipe shikamoo!

Jasusi,

Hospital ya Ocean road imefunguliwa mwaka 1897 ilikuwa inaitwa European hospital, mwaka 1960 ikabadilishwa jina ndiyo ikaitwa Ocean road hospital mwaka 1996 ikawa hospital ya kansa.

Sasa nikupe shikamoo vipi wakati kila siku nakuita Bro haitoshi. Jususi, umri wako ni kama Mohamed Said wote ni kaka zangu.
 
Waislam msimamo mkali, hawataki kusikia harmony for the sake of our nation, wao wanataka kusikia harmony for the sake of ARABS traditions, building Islamic state to a country of mixed cultures and traditions. Labda wanaweza kukusikia hawa vibaraka wa al qaeda, al shabab na boko haram

ntamaholo hivi unaujua uislam au ushabiki unakusumbu kwa taarifa yako uislamu sio uarabu na ndio maana kwenye QURAN utakuta kuna aya zinasema ole wao waarabu haina maana kwamba Quran kuandikwa kwa lugha ya kiarabu ndio uarabu na ktk QURAN kuna aya inasema hakuna kulazimishana katika dini wala wewe hujalazimishwa kuingia kwenye uislamu nenda uingereza na ufaransa ndio utajua uislamu unavyokuwa kwa kasi na wao unataka kuniambia wamelazimishwa?
 
Sawa, hiyo iliandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema na anayejitambulisha kama Mwandishi Wetu, huyu anaweza akawa mtu yeyote yule, je umesoma na hii Nani kama Mwalimu Julius Nyerere? iliyoandikwa kwenye gazeti hilo hilo?
Katika hiyo Nani imeandikwa hivi:
Wakati huo huo, Serikali inapoteza dola milioni 20 (karibu bilioni 290) kwa mwaka kwa njia ya msamaha wa kodi (kwa mujibu wa TRA), kiasi kinachotosha kugharamia elimu yenye sifa kwa miaka mitano chini ya “Mpango wa Elimu kwa Wote” – (UPE). Tanzania inahitaji dola milioni 45 kwa mwaka kuboresha mfumo wake wa elimu.
Hao wanaong'ang'ania kubaki na misamaha ya kodi ni nani kama si wale waliozoea better chance aliowaacha Nyerere.Wamezoea kudekezwa.Wenzao waislamu wakifanya vitu vyao hawaachi wivu na kutaka kudekezwa kwa kutoa matamko na mashinikizo kwa serikali wawashughulikie waislamu.Hili ni zao gani alilotuwachia watanzania.Katuwachia zahma tu badala ya neema.
Nyengine ni hii
...Hajatokea kiongozi Mtanzania mashuhuri kama Mwalimu Nyerere, ambaye ameweza kuheshimiwa na kila mtu katika Taifa, Afrika ikamtukuza, mataifa makubwa yakamheshimu na kumtetemekea hata kama hakuwa na umbo kubwa, jeshi kubwa wala utajiri binafsi au wa nchi....

Wacha hiyo ijibiwe na makala mwenzake

...Lakini ni vyema pia kukumbuka kuwa Nyerere mwenyewe alikumbana na zahma adhimu kama miezi miwili kabla Dar es Salaam kutokana na uasi wa kijeshi na yeye kuingia mafichoni kwa siku kadhaa. Akawaomba Waingereza wakaleta manowari na majeshi na kufanikiwa kumrejesha madarakani. Kwa Mwalimu, tukio la yeye kuwaomba wakoloni msaada lilimuaibisha bila kifani. Kwa hiyo haikuwa vigumu ‘kumminya' Nyerere ili afanye kazi yao ya ‘Muungano' baada ya yeye kufaidi fadhila za Waingereza. Waswahili wana msemo, ‘Fadhila huzaa fadhila'. Hata hivyo, Mwalimu katika miaka yote hii, amekuwa akijitetea kuwa Muungano umesababishwa na sababu za udugu baina ya nchi hizi mbili na kuwa hii ni hatua ya mwanzo ya kufikia ‘Muungano wa Afrika' nzima.....

Wanajeshi aliokuwa akiwaongoza nao walitaka kumpindua.Sasa huko kuheshimiwa na kila mtu kuko wapi?.
Kumbe hata muungano ni zao la shinikizo kutoka nje na yeye akatekeleza ili kulipa fadhila.Kwa maana hiyo kumbe kwa mataifa ya nje Nyerere alikuwa kikaragosi tu cha kutekelezea matakwa yake.Huo umaarufu wa kimataifa na heshima iko wapi?.
 
Ha ha haaaaa wafia dini utawajuwa tu. kwa taharifa yako mie nimeishi nyumba ya Sheikh Nurdin(kwa sasa ni marehemu)mtaa wa Udowe na sikukuu barabarani kabisaaa. Je unafahamu Sheikh Nurdin alitokea wapi hapa Tanganyika? Na je unafahamu baba yake ni nani? Musione watu tuko kimya mkaona kama hatujui hizo simulizi zenu za mitaa ya kariakoo...tukimwaga yetu hapa kwa hakika mtakimbia. ANGALIZO: mimi ni kijana ambae niko chini ya miaka 30 ki umri, so usiniulize maswali ya miaka ya 70 au 80 coz itakuwa lugha gongana.
Nenda zako!.Kama una umri wa miaka chini ya 30 kwanini unataka kujibu maswali kuhusiana na sheikh Nurdin ambaye wala hamkucheza pamoja.Si tuwaulize wazee wenzake?.
 
Mzee Saidi nguli wa historia unayekumbuka hata mambo yanayoonwa kuwa yalikuwa insignificant au irrelevant mfano Nyerere alikuwa navaa nini, habari za kina Juma mlevi, Nyerere alilala wapi akiwa Tabora, swali

"Je unawakumbuka kwa majina ni wazee gani waliopewa jukumu la negotiations za uhuru na waingereza na walichaguliwa na nani na kwa nini?''
Huna haja ya kuuliza uliza.Wataje tukuchambulie.
 
Ficha upumbavu wako hujui hata Sheikh Nurdin amefariki lini hujui Sheikh Nurdin alikuwa anakaa wapi halafu una umri wa chini miaka 30 ulingani hata na wajukuu wa Sheikh kwa umri wako huo humjui Sheikh.
Ha ha haaa....sisi wengine tukihadithia stori zetu munatuambia tufiche upumbavu wetu,ila Mohamed Saidi akihadithia stori zake munaona sawa. Sheikh Nurdin amefariki mwaka 2007...matatizo ya afya yake yalianzia Mombasa baada ya kudondoka bafuni. Mbona mwalimu wako S.Mohamedi hajamtaji mpiganaji huyu kwenye histohisia zake? Au kwa vile si mmanyema na mnubi? Pamoja na mchango wake wote katika Taifa hili lakini hakuwa mfia dini...alihishi na kuelewana vizuri na viongozi wote wa kisiasa hadi mauti ilipomfika. Je unajua alitokea wapi na baba yake ni nani?
 
Ha ha haaa....sisi wengine tukihadithia stori zetu munatuambia tufiche upumbavu wetu,ila Mohamed Saidi akihadithia stori zake munaona sawa. Sheikh Nurdin amefariki mwaka 2007...matatizo ya afya yake yalianzia Mombasa baada ya kudondoka bafuni. Mbona mwalimu wako S.Mohamedi hajamtaji mpiganaji huyu kwenye histohisia zake? Au kwa vile si mmanyema na mnubi? Pamoja na mchango wake wote katika Taifa hili lakini hakuwa mfia dini...alihishi na kuelewana vizuri na viongozi wote wa kisiasa hadi mauti ilipomfika. Je unajua alitokea wapi na baba yake ni nani?

Ndiyo maana nakuambia ficha upumbavu wako.

Ungekuwa umesoma kitabu cha Mohamed Said wala usingeandika pumba hizo Mohamed Said kamuelezea kwingi kwenye kitabu chake wewe una miaka 25 halafu unataka kuminyana na historia ya kariakoo.

Hivi wewe kweli ndiyo wakutupa habari za Sheikh Nurdin wakati sisi tulikuwa kwenye darsa lake mpaka tukasafiri kwenda kumzika.

Kuanguka chooni ni jambo la kawaida tu ukikuwa utajua kumbuka hata Dr Slaa alianguka chooni Mwanza akaumia mkono mpaka leo hajapona ni maradhi tu.
 
Ha ha haaa....sisi wengine tukihadithia stori zetu munatuambia tufiche upumbavu wetu,ila Mohamed Saidi akihadithia stori zake munaona sawa. Sheikh Nurdin amefariki mwaka 2007...matatizo ya afya yake yalianzia Mombasa baada ya kudondoka bafuni. Mbona mwalimu wako S.Mohamedi hajamtaji mpiganaji huyu kwenye histohisia zake? Au kwa vile si mmanyema na mnubi? Pamoja na mchango wake wote katika Taifa hili lakini hakuwa mfia dini...alihishi na kuelewana vizuri na viongozi wote wa kisiasa hadi mauti ilipomfika. Je unajua alitokea wapi na baba yake ni nani?

BD,

Sheikh Nurdin Hussein wanae ni marafiki zangu.

Zamani nikenda Mombasa nilikuwa nafika hadi
kwa dada yake Bi Amina kumsalimia.

Nimefika hadi nyumbani kwa sheikh Kilwa...
Niachie hapa au niendelee?
 
usisite kuleta jibu kumsaidi Mundungus ambaye bado hajarudi.
.
Mwandishi aliyeandika makala uliyo iweka
ni personal opinion yake. Alichoandika si facts.

Sawa sawa na makala aliyoleta jasusi hapa ya nani kama nyerere iliyoandikwa kwenye same newspaper.

History ya Nyerere ipo, story za nyerere zipo, video zake zipo, audio za hotuba zake zipo, facts kuhusu yeye pia zipo. So ni swala la msomaji na mtu mwenyewe kufanya upembuzi yakinifu, kumchambua na hatimae kujiridhisha yeye mwenyewe Nyerere anamchukiliaje.

Ila kwa kusoma makala moja, na kumsikiliza mtu moja kukuambia kuhusu nyerere na hapo hapo ukafikia tamati na Kumlabel nyerere unavyotaka wewe (kama ni shujaa au mdhulmati) basi utakuwa humtendei haki.

Mimi sio mtaalamu wa Historia, mimi pia sina upande katika mjadala huu, kwasababu sio mtaalamu wa historia, hivyo kuwa na upande itakuwa nasukumwa na hisia zaidi. Kwasababu Mzee Saidi akinipa nondo zake ntajuaje kama hizi ni za ukweli au za uongo.. Sina utalaamu.

Vivyo hivyo Mzee MM, nguruvi3 na mg3 bila ya kumsahau Jasusi wakitoa nondo zao mimi ntajuaje kama hizi ni za ukweli au za uongo.

Ila mimi na tatizo na ukweli wa swala linalo itwa "dhulma" kwa waislamu.

Ingawa si mtaalaamu na sijabobea katika historia, lakini najua kutambua kama sehemu ina makosa. Hasa linapokuwa linahusu vitu vinavyoweza kuwa prove bila ya kutumia historia.

Huu mnakasha ni mrefu sana, vivyo nina uhakika ni watu wachache sana ambao wameufutalia neno kwa neno kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Ila katika fuatilia yangu mimi, mwanzoni Mzee Said, alionekana kuwakimbiza sana wanao mpinga, na hasa walionekana wanampinga tu kutokana na hisia zao binafsi na walikuwa hawana facts na hawaijui historia vizuri.

Kama umefuatilia vizuri hata wale Pro Mzee Said arguments,(zomba,Ritz, etc) walikuwa wapo kasi sana mwanzoni lakini sasa hivi wamepunguza spidi hata wao wenywe wamepungua (inawezekana pia majuku yamewashika)..

Vivyo hivyo kwa Anti-mzee Said au Pro -Yericko arguments, walikuwa hawana nguvu kabisa mwanzoni lakini sasa naona wameshika kwenye makali, na wako full force.

Kwanini

Na kuna sehemu moja ambayo pamekuwa moto ambapo Anti-Mzee Said, wamepashikilia.

WARSHA's Research

Hizi data zilitumiwa sana humu kwenye mnakasha, na hata kwenye mijadala mengine humu JF na kwenye mitandao mengine, data zilitumiwa kama scientific proof au Tangible truth dhidi ya "dhulma" kwa waislamu. Hizi data zilishika makali na zikakata kata.

Wakaja watu humu Anti-Mzee Said argument wakaleta na wao tangible proof kuonesha highly inaccuracy ya ile Research, the whole methodology wameonesha ina uwalakin, wameelezea kwa kirefu sihiitaji kuingia kiundani.

Hapo is where i come in. Mimi nikaja kumuuliza Mzee Said apinge na adispute (KITAALAMU) claims za kambi pinzani na kudhibitisha ile Research haiko inaccurate na haiwezi kutumiwa kama ushahidi wa kitaalamu wa dhulma dhidi ya waislamu.

Hakuna aliyekuja mpaka sasa hivi, sio Mzee Said wala Ritz, wala wewe Ami wala mtu yoyote.

Sasa wewe ukaja na kuanza kutoa sababu zakitoto kwnye maswala ya kitaalamu. Ukaanza kusema makosa ni ubinadamu, Mzee Said ni binadamu. Inawezekana this, inawezekana that.... Maelezo mengi ya kuexcuse kitu kilichofanyika hapa.

Watu wengi wakaja wakaeleza ni vipi tofauti ya makosa ya kiuandishi na factual errors. Na kwanini wanasema hii ni factual error na hivyo hii Research iko null and void, haiwezi kutumika tena kama kigezo na kielezo cha dhulma dhidi ya waislamu.

Nakama mtu anajua ukweli huu na bado anataka kuitumia Research hii kuaminisha watu wengi ambao anajua kabisa hawajui au hawezi kujua kama i
Zile data sio sawa huyo ni MCHOCHEZI period.

Na mimi naongeze kusema, Mzee Said, ni msomi tena msomi sana, wasifu wake wenyewe mmeuona hapa.

Yeye na watu waliofanya hii Research inaonekana ni watu waliokuwa wanajua kabisa kitu walichokuwa wanafanya. Inawezekana kweli wana VALID madai, au Madai Halal, lakini kutumia njia zisizo halal kudhibitisha madai yako si uungwana. Huku hakuna tofauti na uchakachuaji.

Ni sawa wakristu nao wachukue data za chuo Huko Zanzibar na kuzitumia kama kielezo cha kusema kuwa kweli waislamu hawadhulumiwi Tanzania.

Na hapo ndo lile swala la credibility nililolisema linapokuja...

Kama Research tu ina uwalakin? Kitu ambacho can be proven wrong... Vipi kuhusu reference nyingine ambazo haziwezi kudhibitishwa????

So nadhani hapo mimi ndo naposimamia. Sitaki kusema tuache kuzungumzuia Dai kuu, ila lipo na tunataka kulidhibitisha tulete ushahidi wa kihalali ma hata vijana wadogo wakislamu wajiridhishe kweli tunaonewa na kudhulumiwa au kuna tatizo somewhere...
 
Back
Top Bottom