Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mzee Mohamed na wanafunzi wako.

Naombeni mnitajie mabaya na mazuri ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi na mh.Jakaya Kikwete....mabaya yao na mazuri yao.

BD,

Mimi nakuomba ufungue uzi mpya kwa hayo.
Hapa tubakie na ''Uchochezi wa Mohamed Said.''
 
Hapana Mzee Saidi sijauliza kwa kupima uwezo wako bali ni kwa nia nzuri tu ya kutaka kuweka mambo sawa. Na ni muhimu vijana wetu wafahamu historia nzima mpaka uhuru wenyewe ulipopatikana.

Nyambala,
Siwezi kusema sana.

Lakini ungelitanguliza heshima na ustaarabu ukaja na picha
tuko kwenye barza tunazungumza ungekuja na lugha nzuri.

Huwa nasisitiza kuwa haya ni majadiliano hapana uhasama.
Najua kwenu nyie hakika maneno ninayoandika yanataabisha.

Hampendi kusikia kuwa kulikuwa na watu walifanya makubwa
na wala Nyerere walikuwa hawajasikia jina lake.

Lakini huu ndiyo ukweli.
 
BD,

Mimi nakuomba ufungue uzi mpya kwa hayo.
Hapa tubakie na ''Uchochezi wa Mohamed Said.''
Anhaa...kwahiyo kuorodhesha mabaya ya Nyerere na Mkapa ni sawa' ila kuorodhesha mabaya ya Mwinyi na Kikwete tufungue nyuzi mpya. Ama kweli nimeamini wafia dini wa gerezani kila kitu mnaangalia kwa jicho la dini kwanza.
 
Anhaa...kwahiyo kuorodhesha mabaya ya Nyerere na Mkapa ni sawa' ila kuorodhesha mabaya ya Mwinyi na Kikwete tufungue nyuzi mpya. Ama kweli nimeamini wafia dini wa gerezani kila kitu mnaangalia kwa jicho la dini kwanza.

BD,

Wapi yameorodheshwa mabaya hayo?
Unaweza kutuonyesha?
 
Hapana Mzee Saidi sijauliza kwa kupima uwezo wako bali ni kwa nia nzuri tu ya kutaka kuweka mambo sawa. Na ni muhimu vijana wetu wafahamu historia nzima mpaka uhuru wenyewe ulipopatikana.
Historia nzima iandikwe mara ngapi?.Iliyoandikwa tumesoma na wengi tumeelewa.Sehemu iliyobki malizia wewe.
 
Mzee Mohamed na wanafunzi wako.

Naombeni mnitajie mabaya na mazuri ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi na mh.Jakaya Kikwete....mabaya yao na mazuri yao.
Siyo kazi ya uzi huu.Hapa ni vioja vya Nyerere na wapigania uhuru wenzake hasa waislamu.
Habari za Kikwete na Mwinyi tutasoma kwengine.
 
Anataka nami niandike kitabu jambo ambalo sio la lalazima katika kupinga upotoshaji wa kizandiki kama aliofanya Mohamed Said
Kuandika kitabu kutaka kutetea jambo ni lazima.Kama huwezi sema na tujue huna hoja.
Unadhani maandiko yako hapa yatakuwa utetezi kweli!.
Tunataka hard copy ili iwe rahisi kufanya marejeo.
Hapa utawezaje kujua lipi lipo wapi hata ukitumia google utapotea.Majibu yametolewa zamani lakini bado anatokea mtu anauliza tena suali lenye jibu hilo hilo.
 
Mohamed Said, katika maandishi yangu kwenye uzi huu nimeeleza wazi usharika wa Shehe Issa Bin Amir sambamba na Padre Arestide, wakizileta pamoja fikra zao mpaka walipomuona mwana mtenzi shujaa wa nera Julius Burito Kambarage Nyerere akihudumu katika himaya ya mzungu pale Pugu,

Hili umekiri wazi hapo awali kuwa hukuwahi kupata habari hizi, hakika hii imekuwa habari mpya kwako,

Ninachoshukuru hujakanusha bali kuunga mkono kwa namna yake, lakini bado wazisimamia ngano tena kwa bidii,

Hebu tumueleze huyu mwanamfalme wa Tanganyika...

Lakini mtu huyu alikuwa tayari anadhamira ya kuikomboa afrika, kwani machipuzi ya siasa zake yaling'ara angali kinda ndani ya viunga vya Makerere nchi Uganda, akiunda na kuhudumu katika Chama chake cha siasa alichokiita TAWA, hiki ndicho chama kilichokuwa na filosofia ya ukombozi miongoni mwa vyama vyote vilivyoundwa Tanganyika, na kuonyesha uhalisia, filosofia/ideology yake ndio iliyounda TANU na kuisimama mpaka mwaka 1977.

Leo Mohamed unaingia kwenye lile kundi la akina Shehe Takadir walioonyesha chuki za wazi dhidi ya Mwalim alipokuwa anagombea urais wa TAA mwaka 1953 pale Anartouglo/mnazimmoja? Vivyo hivyo unaturudisha kwenye mpasuko wa TAA wa 1948 pale Tabora na kuundwa kwa chama cha kisiasa cha kiislamu cha AMNUT?

Mbona hujiulize kuwa hivi ni Nyerere tu pekee yake ndie aliyeyashinda yote hayo au alisimama na waislsamu watakatifu na wapenda amani?

Inasikitisha sana kuona leo Mohamed Said anaudharirisha uislamu nchini, uislamu ule wa uliosimamiwa na kiongozi mwana falsa za kenda Shehe Issa Bin Amir chini ya viunga vya Mchikichini ya leo, yule aliyehudumu bila kujali dini wala rangi, yule aliyekunywa chai na padre wa kikatoliki huku wanajadili ukoloni wa mjerumanu kisha utawala wa muingereza,

Mohamed wewe waamini uislamu upi duniani?
 
Nyambala,
Siwezi kusema sana.

Lakini ungelitanguliza heshima na ustaarabu ukaja na picha
tuko kwenye barza tunazungumza ungekuja na lugha nzuri.

Huwa nasisitiza kuwa haya ni majadiliano hapana uhasama.
Najua kwenu nyie hakika maneno ninayoandika yanataabisha.

Hampendi kusikia kuwa kulikuwa na watu walifanya makubwa
na wala Nyerere walikuwa hawajasikia jina lake.

Lakini huu ndiyo ukweli.

Kama kawaida Mzee Saidi, swali bado limesimama lakini unakuja na hii habari ya "nyie", sisi na nani? Mimi niko mwenyewe lakini ghafla unanitengenezea ushirika!!!!!!!!! Kama jibu hakuna si isemwe basi?? Na kwa taarifa tu mimi sitaabishwi na maneno hata siku moja ila huwa naatabishwa pale tu "urongo" unapofinyangwa na kuitwa ukweli.
 
Wewe unaniita kijana nilikuletea cheti cha kuzaliwa?
Kukuita kijana sijakufunga umri, lakini kuthubutu kusema wewe ni mdogo wangu hilo ni hitimisho na ndio nikakuhoji uhalali wa wewe kuniita mimi ni mdogo wako,
 
Kama kawaida Mzee Saidi, swali bado limesimama lakini unakuja na hii habari ya "nyie", sisi na nani? Mimi niko mwenyewe lakini ghafla unanitengenezea ushirika!!!!!!!!! Kama jibu hakuna si isemwe basi?? Na kwa taarifa tu mimi sitaabishwi na maneno hata siku moja ila huwa naatabishwa pale tu "urongo" unapofinyangwa na kuitwa ukweli.

Nyambala,

Niwie radhi kwa kukujumuisha kwa neno nyie.

Ikiwa ushaitikadi pana uongo katika maelezo yangu hiyo ni sababu
tosha ya mtu yoyote kunipuuza kwa sababu muongo hana muamana.

Katika Uislam ikishathibiti kuwa mtu ni muongo huo ndiyo mwisho wake
neno lake haliaminiki tena.

Mimi ni Muislam na kwa kuwa umeniita muongo hapa ndiyo mwisho wetu.
 
Mzee Mohamed said ukuna mtu humu alizungumzia swala la Biafra katika kipindi niliamini Nyerere ni mdini ni hii issue,kwanza ni issue ya wa ibo ilikoanzia na walioanzisha wanajulikana kwa mshangao wa wengi mpaka leo kwanini wahusika hawakushtakiwa kwa mauaji ya kimbari kama ilivyofanyika Rwanda na kwa Bashir wa sudan!!inasemekana kanisa katoliki na wasomi wa ki ibo waliwatumia wa ibo ambao walikuwa hawana elimu kuwaunga mkono katika uasi ule.Hebu fikiria uasi wa mwaka 1964 Nyerere aliomba msaadakutoka Naigeria na baadae ni Nyerere huyo huyo miaka michache aliwaunga mkono waasi wa Naigeria hapa ndio nikapata picha ya kwamba huyu baba alikuwa mdini na haya yanaoendelea hapa nchini kwetu ni mazao yake,
 
Ritz,

Muwie radhi Yericko Nyerere.

Tumegonga watazamaji 100,000 and still counting...
Nipe jina la uwanja...

Ni Aztec Stadium vile au ni upi?

Mohamed Said,

Stadio Azteca Mexico City inameza watu 105,000.

Sasa hivi tunaelekea North Korea Rungrado Stadium inameza watu 150,000.

Tukitoka apa takuambia tunaelekea wapi.

Kumekucha.
 
Mundungus Fletcher,

Kuwa wazi tu upande unao mtu akikosoma tu anajua fikra zako hakuna ubaya wewe kuwa na upende ni haki yako unajitahidi kubalance maandiko yako lakini watu makini tumekosoma.

Umesema wewe siyo mtaalamu wa histori lakini hapo hapo unasema huoni dhulma wanaofanyiwa Waislam.

Hayo maneno yako tu wala hayaitaji elimu ya chuo kikuu kutambua wewe upo upande gani.

Mimi kutokuonekana humu jamvini kwanza nilipewa ban na nikawa nimebanwa na kazi pia.

Ritz
Mimi naamini sina upande. Inawezekana ninao lakini sijajua bado.

Nikweli nimesema sioni dhulma, lakini haimanishi siamini kuwa kunauwezekanao ipo ila mimi sijaiona bado, ndo mana mnakasha huu nimeupenda na nimeamua kuwa neautral ili nijaribu kuangalia kwa jicho la pili ushahidi yakinifu wa madai haya.

Mimi nipo hapa natafuta kwelj na ushahidi wa madai haya ya muda mrefu. Ndo mana nimepinga ushahidi wa Research ya Warsha kwasababu makosa yake yameokena na nikasema si vyema kutumia takwimu zile kama kielezo cha dhulma dhidi ya waislamu kwasababu haikuchukuliwa kitaalamu.

As so for historia, kama Mzee Said alivyoiandika, nivigumu kwangu kujua ukweli kwasababu

Kwanza ni Historia na mimi sina utaalamu

Pili any events za historia lazima zisapotiwe na wana historia wengine kuipa uhalali wake. Lasivyo mtu yoyote anaweza akaweka event yake kwenye historia hata kama haikuwepo na kung'ang'ania ni kweli.

Lakini ushahidi huu wa hisrtoria nikasema nimeanza kuwa na wasiwasi nao kwasababu Mzee Saidi ameshaanza kuonesha makosa madogo madogo lakini yenye uzito mkubwa kwenye kitabu chake (na mwenyewe amekiri kama ni makosa ya kibinadamu) kiasi mtu unajiuliza how can believe the rest of the story....????

So mimi bado naheshimu madai ya watu wanaosema waislamu wanadhulumiwa na mfumo kristo, lakini bado natafuta ushahidi nijiridhishe.

Ila pia kuna kitu nimeona labda ningepata ufafanuzi,

Kipindi cha uhuru mnasema Kanisa na Nyerere walikandamiza waislamu,

Wakati Yule sheikh msouth africa alivyorudishwa mkasema kanisa lika mshinikiza Mwinyi kumfukuza (manake mmemtoa Mwinyi kwenye makosa, kwamba kosa sio lake bali alishinikizwa)

Kipindi hiko hiko mnamlaumu waziri wa mambo ya ndani Mrema aliwakandamiza na kuwauwa Waislamu lakini Raisi Mwinyi hausishwi.

Kipindi cha Mwembe chai wakati wa Mkapa mkasema laana ya damu ya waislamu ipo mikononi mwake,

Kipindi hiki cha kikwete ambapo kuna viongozi waandamizi wengi sana waislamu, kuanzia Raisi, makamo wa Raisi, mkuu wa Polisi na kamanda Kova nae, mnasema kanisa ndo linashinikiza na kupiga vita, wamekamatwa wakina Ponda lawama hazijaenda kwa Kwikwete wala IGP wala kova bali kanisa.

Sasa je hamuoni mko selective jinsi mnavyo laumu?

Mnachagua nani wakumlaumu na wakumluka?

Lasivyo basi tuite dhulma zidi ya waislamu kutoka mfumo kristo, kanisa na waislamu wenyewe...

Ambapo tutarudi kwenye swali la msingi, Je hao waislamu wanaodhulumiwa mpaka na waislamu wenzao ni waislamu gani???
 
kutoa fikra zinazohusiana na historia halafu kwa makusudi ukapindisha historia hiyo, si ndo uongo mwenyewe?
Na zaidi ya hapo, kuandika maandishi ikiwa ni pamoja na takwimu ambazo leo tunajua hazina ukweli huku ukiwaaminisha watu kwa miaka 15 si bahati mbaya ni makusudi.

Siamini katika vyuo ulivyotoa mihadhara na wasomi uliokutana nao hakuna hata mmoja aliyewahi kukueleza kuhusu mapungufu ya takwimu za utafiti wako. Bahati mbaya inaweza kuwa miezi au mwaka siyo miaka 15.

Lakini pia Mohamed anasababu! mathalan kumsema Kawawa kama makamu wa kwanza wa rais ilikuwa kutia uzito wa hoja zake. Pengine angekuwa hakukusdia angelieweza kurudi maktaba na kujiridhirisha kuwa hicho alichokiandika au kusudia kukisema kina ukweli.

Kuwaambia watu kwa miaka 15 kwamba Nyerere alifundishwa siasa na Sykes huku ukijua kuwa alikuwa msomi na alianza harakati hizo siku nyingi si bahati mbaya ni makusudi ili kufikia lengo.

orodha ni ndefu but the bottom line is, Mohamed anachokifanya ni makusudi wala si mapungufu.
Huwezi kuniambia amejua leo kuwa Maryknoll walitoa ticket au Nyerere alikuwa katibu wa AA Tabora kabla ya kukutana na Sykes! no! ni makusudi ambayo leo anakiri ni mapungufu ya kibinadamu. No thank you Sir!
 
Back
Top Bottom