Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Usipotoshe ndugu, alichofanya Mohamed ni kuwatenga zaidi, sio kuhuisha historia!

Unadhani waliosahauliwa katika historia ni wazee wakiislamu tu kama alivyofanya?[/QUOTE]
NDUGU YERICKO NYERERE THANKS KWA KUNIONA NA MIMI NA KUNIJIBU HOJA YANGU,NAKUSHUKURU KWA MOYO WAKO HUO,SASA NAOMBA NAMI NIKUONE NA NIKUJIBU BILA KUTARA DADI NJE YA MAUDHUI YAKO,

1.ALICHOKIFANYA NDUGU MOH' SAID SI KUWATENGA,LA HASHA NI KUIHUISHA ILE HISTORIA ILIYOFISHWA KWA MAKUSUDI.

2.WALIOKASAHAULIKA KATIKA HISTORIA ILE SI WAISLAM TUH,SWALI HILO LABDA NIKUULIZE WEWE,JE HAWA WAISLAM AMBAO WALIFUTWA KWA MAKUSUDI KWENYE HISTORIA YA UHURU WA NCHI HII,WANGEANDIKWA KAMA WALIVOANDIKWA HAO WAKRISTO,JE TUNGEKUWA KATIKA MJADALA HUU TULIONAO SASA??BILA SHAKA JIBU NI HAPANA,KUSAHAULIKA KWA WALE NDIKO KULIKO TULETA PAMOJA HAPA MIMI NA WEWE KATIKA MEZA YA MAJADILIANO,

YEYE ANA HAJA GANI YA KUANDIKA HISTORIA YA WATU ASIO WAFAHAM KWA UNDANI?UKITAKA APOTOSHE ILI TUH KUWAFURAHISHA?KAMA WEWE UNAZO HIZO HISTORIA,NANI KAKUZUIA KUANDIKA KITABU NA KUWEKA USHAHID KAMA ALIVOFANYA YEYE??MUNGU AKUBARIK SANA YERICKO.
 
Naona wewe haujamsoma Mzee wetu Mohamed hata kwa mabandiko yake humu.
 
hivi mzee mohamed anaposema waislam walitengwa na wakasahauliwa kwenye historia ya nchi hii anakuwa anamaanisha nini hasa! Hapa mzee wetu anapigania nini kama sio dini yake?

sasa naona unataka kumjaza yeye maneno yako wewe mdomoni mwake,,hii hoja nilishakujibu tayari..kwani wapi ameigusa dini ya uislam??ama kwa kuwa kawataja waislam??

Mfano,wewe ungekuwa ni mwandishi na unaandika sasa kuwaelezea wazee wa kikristo ambao wamesahaulika kwenye historia fulani,tuseme ya nchi hii,unataka sisi tukushutume wewe ya kwamba unapigana crusade war?tukuite wewe ni mdini??
Hebu twende sawa kidogo
 
 
naona wewe haujamsoma mzee wetu mohamed hata kwa mabandiko yake humu.

me namfuatilia vema sana huyu ndugu,tokea mwanzo wa page hadi sasa,hajaniacha hata nukta.


Don attack me,attack hoja zangu hapo juu.
 
Ingekuwa bora kabla ya kuandika ukafanya utafiti angalau kidogo.
Nani kakuambia kitabu cha historia cha Kivukoni haina mkono wa
Nyerere?

Kasome utangulizi wa kitabu.

Hilo lingine sina haja kulisemea.
Hilo lingine kama kawaida yako hauwezi kulisemea. Hilo linafanana na hili: Wazee wako hawa walipigania uhuru wa nchi hii kwa kutumwa na DINI yao? AA na baadae TAA zilianzia misikitini?
 
Muulize Mzee wetu Mohamed, waliosahaulika tena kwa makusudi kabisa, kwenye historia ya nchi hii ni watu wa DINI gani?
 

Nitajibu hilo moja tu la thesis na kwa professor nanaemjua mie.

Prof. Jonathon Glassman Northwestern University Chicago
anawaamuru wanafunzi wake wote wa Ph D kusoma kitabu
changu ikiwa somo ni Uislam Tanzania.

Halikadhalika James Brenan, James Brandon na wengine wengi.

Kitabu kimenipatia marafiki dunia nzima.

Wazungu hawapungui kwangu.

Kiasi watoto wa mtaani wakimuoma Mzungu anazubaa mtaani kwetu wanamuuliza.

"Are you looking for Mzee Mohamed?"
 
muulize mzee wetu mohamed, waliosahaulika tena kwa makusudi kabisa, kwenye historia ya nchi hii ni watu wa dini gani?
afanaleki..!

Mbona sasa ndugu yangu nakuuliza hunijibu,,kisha unanishurutisha nimuulize mzee moh' said pasi nawewe kunijibu hoja zangu??please hebu kuwa muungwana na unijibu hizo hoja zangu tafadhali,hiyo ndio raha ya mnakasha
 
Kweli! Bila shaka Wazungu hawa ukristo wao sio kama ule wa Mwalimu! Nawaomba wakutembelee sana tu ili ukose muda wa kuktutengenezea "Al Qaeda" nyingine humu Tanzania.
 
Hili nalo neno.

Kweli! Bila shaka Wazungu hawa ukristo wao sio kama ule wa Mwalimu! Nawaomba wakutembelee sana tu ili ukose muda wa kuktutengenezea "Al Qaeda" nyingine humu Tanzania.
 
afanaleki..!

Mbona sasa ndugu yangu nakuuliza hunijibu,,kisha unanishurutisha nimuulize mzee moh' said pasi nawewe kunijibu hoja zangu??please hebu kuwa muungwana na unijibu hizo hoja zangu tafadhali,hiyo ndio raha ya mnakasha
Mh! Zimenishinda hoja zako.
 
Ndugu yangu tufanye mjadala wa busara.
Busara hii itumike pia tunapoandika, tunapohubiri kwenye nyumba za ibada na kwenye mihadhara mbalimbali. Sasa hivi Mwalimu ananuka misikitini. Jiulize mchango wako katika hili.
 
yericko nyerere hauko fair,wewe mara nyingi huwa unamshutumu mzee moh' said anachagua maswali ya kujibu wakati haiko hivo,wewe ndie unaechagua maswali ya kujibu,nakuuliza vitu vingi unakausha,mnakasha tutauendelezaje??kama hoja zangu ni za kijuha niambie tu ndugu,kuliko kukaa kimya,umeishiwa hoja??
Basi tumwache ndugu yetu aifanye kazi yake pasi na masemango,moh' said endelea kutupa darsa mkuu.
 
Busara hii itumike pia tunapoandika, tunapohubiri kwenye nyumba za ibada na kwenye mihadhara mbalimbali. Sasa hivi Mwalimu ananuka misikitini. Jiulize mchango wako katika hili.

Hilo ndilo swali la kujiuliza.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo hiyo nimeieleza humu.

Nyerere anatembea kwa miguu kafuatana na Abdu Sykes na Dossa.
Njiani salamu wanazopeana na wananchi ni "Uhuru."

Sheikh Hassan bin Amir anamuunga mkono Nyerere kwa dhati ya nafsi
yake.

Baraza la Wazee wa TANU wanaisimamia safari ya Nyerere UNO kwa mafanikio
makubwa sana.

Waislam wanaikataa AMNUT.

Uhuru unapatikana.

Ghafla Nyerere hataki kuwaona wazee wa Baraza la TANU pale New Street.
Ghafla TAA haina maana kwa kuwa hakikuwa chama cha siasa bali cha starehe.

Ghafla masheikh wanakamatwa usiku wa manane kama majambazi na kutupwa
kizuizini.

Ghafla EAMWS si jumuia halali Nyerere anaipiga marufuku.
Sheikh Hassan bin Amir anakamatwa na kurudishwa "kwao" Zanzibar.

Mfumokristo unachukua nafasi ya ukoloni.

Hali ya Waislam ndiyo hii ya kuwa raia daraja la tatu.
Hawana ruhusa hata kuhadithia historia ya mashujaa wao.

Hivi mlitegemea nini?
 
Kujenga NCHI moja isiyo na DINI wa UKABILA haikuwa kazi ya lelemama. Wapo ambao watakuwa walikwaruzwa katika kulifikia lengo hili na hasa kama walipingana waziwazi au kwa kificho na dhana hii. Katika hili, Mwalimu hakumbakiza yeyote hata kama angekuwa mtu wake wa karibu namna gani.

Kitabu chako kile na mahubiri yako ya sasa yanaturudisha huko taratibu lakini kwa uhakika. Mimi na wewe tumekua na kusoma kwa amani sana nchi hii. Sielewi tunakoelekea sasa na mahubiri haya na hisia hizi mpya kwa vijana wetu hawa ambao wamezaliwa miaka ya 80 kila kitu kimeanza kuvurugika.

Hivi kweli Muislam daraja la tatu anaweza kuwa RAIS wa nchi hii tena akawapanga kwenye UONGOZI nyeti wa taifa Waislam wenzake kadri anavyotaka?
 
Busara hii itumike pia tunapoandika, tunapohubiri kwenye nyumba za ibada na kwenye mihadhara mbalimbali. Sasa hivi Mwalimu ananuka misikitini. Jiulize mchango wako katika hili.

Hilo ndio linatufedhehesha watanzania kwakutohidhi hadhi za wanaukombozi wetu, wenzetu wanatugawa, wanaweka ubora wawo kwenye mambo ya wote!
 

Hii ni paper ya Mohamed Said ya mwaka 2011.
Angalia kwenye blue kwa walioikomboa Tanganyika kutoka ukoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…