Embu tujadili hili: 83/17 ni nini? miye sijui...
Kuna kitu kimoja ambacho wanaolia "dhulma" wanadhani Watanzania hawakijui sana. Wakati wa Nyerere kama kuna kitu kilikuwa kinapigwa vita sana ni kile alichokiita "undugunization" yaani kwa neno la kimombo "nepotism". Tafsiri moja ya nepotism inasema ni "patronage bestowed or favoritism shown on the basis of family relationship, as in business and politics".
Sasa undugunization ulianza kwa kasi baada ya kuanza kuwa na kada ya watumishi wa umma wasomi ambao wameanza kushika nafasi. Kwa kiasi wale waliopata nafasi kidogo walianza kuwaingiza wana familia wao kwenye hizo ajira. Kama Baba alikuwa meneja wa Benki basi mtoto wake akigraduate naye anatafutiwa kazi benki; hii ilikuwa kweli kwenye polisi, na ilikuwa kweli kwenye ajira nyingi sana. Na kwa kadiri watu walivyozidi kupata nafasi za juu ndivyo nao walivyozidi kuwaingiza ndugu zao kwenye ajira na hawakufungwa na ofisi zao kwani waliweza kuwaunganisha na marafiki zao kwenye kada nyingine. Hivyo, mtu anaweza kuwa yuko Ikulu lakini mtoto au jamaa yake akaunganishwa kupata kazi Benki Kuu, au taasisi nyingine.
Lakini hili halikuishia tena kwenye undugu wa damu likawa limeingia hata kwenye undugu wa "kijiji kimoja"; ambapo hapa utakuta watu ambao wanatoka kijiji kimoja (hata kabila moja) wanadai undugu na kuombeana msaada. Hivyo, mtoto atatoka Tarime na kwenda kwa 'mjomba' Arusha ambaye ni afisa wa JWTZ ambaye atamtafuta kazi kujiunga na jeshi. Matokeo yake utakuta watu wa kabila moja nao wakiwa wamejazana sehemu fulani.
Huu undugunization ndio kwa kiasi kikubwa sana umekithiri na sijui kama kuna Mtanzania ambaye hana ndugu au jamaa aliyenufaika na kumfahamu mtu fulani. Lakini katika maana yake pana zaidi huu 'undugunization' ulifika hadi kwa marafiki. Watu waliosoma pamoja wanasaidiana na marafiki wanapeana nafasi na hata kwa watoto wao. Kwa mfano, mtu ambaye ni Mkristu mwenye tafiki Muislamu anaweza kuombwa na rafiki yake kumtafutia "binti" yake ajira na akafanya hivyo. Yule binti ataingia kwenye ajira na hakuna mtu ataweza kuona upendeleo kwa sababu aliyeingia ni Muislamu na kaingizwa na Mkristu (au kinyume chake).
Hili unaliona hata kwenye teuzi mbalimbali. Mtu Muislamu anaweza akamteua mtu Mkristu ambaye anaweza asiwe na uwezo sana lakini watu wasione "upendeleo" kwa sababu wamefungwa na kuangalia dini tu. Ukiniuliza mimi kitu kinachowanyima watu nafasi kuendelea katika ajira siyo "dini" hasa bali 'undugu" ambapo pamoja na nepotism sasa kuna 'cronyism' yaani 'thepracticeoffavoringone'sclosefriends,especiallyinpoliticalappointments.'
Mfano mzuri sana wa haya mawili ni nafasi za ajira kule BoT ambao tuliona majina ya watoto wa vigogo yakijazana na kupeana nafasi mbalimbali. Sidhani kama kuna mtu anaweza akasema wale walipewa upendeleo kwa sababu ya dini zao. Na hivi karibuni tumeona pia kwenye viwanja vilivyouzwa kule Kigamboni ambapo wanasiasa na watumishi wakubwa serikalini wamepewa viwanja hivyo kwa kufahamiana na wahusika.
Una uhakika huijui? au umesahau mjadala wa nyuzi za Mohamed Said zilizopita?
Sijui, nifahamishe.
Mdondoaji, kwanza naomba nirejee hoja yako ya ''waswahili;;. Nadhani unakosea kama wengi wanavyokosea kwa kudhani kuwa neo waswahili ni waislam.Jasusi,
Huyo mtu wako alikuwa na vigezo stahiki? Alikuwa amepitia mchakato wa uchaguzi? Kama alionewa kwasababu ya dini yake then you have a point. Umetaka mfano wa mahali mie kuna kijana aliitwa usaili wa kazi wizara ya fedha ana honours degree lakini waliochaguliwa yeye hakuwamo . IFM kuna wakuu wa faculty wote wakristo, wakurugenzi wote wakristo , wasaidizi wake wakristo je hakuna waislamu wanaofaa kuongoza?? Twende PPF mazingira ni hayo pia je is this a coincidence?
Hilo ndilo tatizo kubwa mlilo nalo, hamjui halafu mnajifanya manjuwa. Kaa upwe darsa la historia ya wazee wake na Mohamed Said.
Na mimi nnakuahidi ntakupa hilo darsa ambalo umesema hulijui.
Si unanikumbuka? au umenisahau?
Umewahi kumsoma John C. Sivalon?
Mdondoaji, kwanza naomba nirejee hoja yako ya ''waswahili;;. Nadhani unakosea kama wengi wanavyokosea kwa kudhani kuwa neo waswahili ni waislam.
Coincidentally watu wanaoongea kiswahili na hakika waliokisambaza ni waswahili (Sahel) ambao wengi wao wametokea kuwa waislam. Ndio maana mswahili hakawii kumwiga afande rire rimekuja ri aresti na wengine nao kusema huyo ni mswahili.
Mimi katika nyuzi hii nimetumia neno ''wamatumbi'',sikumaaanisha wamatumbi bali sisi waafrika.
Mtu aweza sema mnyamwezi akimaanisha Mtanzania. Hiyo ni misemo tu kama tunavyosikia watu wakisema ''aah waswahili bwana, nimemwambia aje saa 3 anakuja saa 6'' hao wanaoongea hivyo wote si waislam.
Ni makosa hayo hayo waislam wanayafanya kwa kudhani kuwa kofia za baraghashia ni Uislam.
Hayo ni mavazi tu na hayana hati miliki wala si alama za dini kama baadhi ya watu waliokosa hoja wanavyodai.
Mama Theresa wa Culcata alikuwa navaa hijab, je alikuwa miwslam? Kuvaa vile alidhihaki uislam?
Haya ni matatizo ya ufahamu tu vinginevyo hilo siyo suala kabisa!
Nikirudi katika nukuu yako, hakika nawe umejikuta katika mtego wa Mohamed.
It's unfortunate Mdondoaji! kwasababu sikudhani unaweza kunasa katika mtego mbovu na dhaifu kama huo.
Sorry. I have to be honest with you
Nashangaa sana unajenga hoja kuwa kuna wakristo ni wengi IFM na PPF.
Vipi kwanini usiangalie kuwa Walimu wengi ni wapi, Mabwana shamba wengi ni wapi, madaktari na wauguzi wengi ni wapi, mavetenari wengi ni wapi n.k.Kwanini mnadhani nafasi ni benki kuu, NSSF, PPF na IFM ni muhimu zaidi ya sehemu nilizozitaja
Ukiangalia shule nyingi za sekondari achilia mbali za msingi za waislam, tatizo lililopo ni ukosefu wa walimu.
Shule ya Al Hassan Mwinyi mwaka 2010/2011 ilikuwa na wanafunzi 250 na walimu wawili.
Hili ndilo tatizo na wala si mkuu wa Faculty IFM. Utapataje mkuu wa faculty kama mtoto hakufaulu huko nyuma?
Mohamed amechota akili za watu kudhani kuwa ukiwa na wakurugenzi 50 katika uwiano wa 0.5 basi matatizo ya waislam yamekwisha. Anawaaminisha watu kuwa ukiwa na mawaziri 20 kati ya 40 basi inflation imeondoka kwa waislam.
Sasa moto umepamba tunakutana na hoja za IFM na PPF
Watu wamefunga macho kabisa kutambua kuwa Kilwa Shule imefungwa kwa wanafunzi kukimbia, jicho lipo kwa Wakurugenzi watatu au wanne IFM.
Huu ni mwendelezo ule ule wa fikra za kuwa Mwanerongo ilikuwa na shule ya kiislam na sasa imerudi nyuma kwasababu EAMWS haikuruhusiwa kujenga chuo kikuu.
Watu wenye fikra hizi za ajabu hawajui kuwa kule kule Mwaneromango sasa hivi wakazi wanafukuzwa na ardhi inaporwa na wawekezaji. Hawana habari kabisa kwasababu jicho lao lipo katika kutafuta ubaya wa wakristo na wala si ubaya wa mfumo wa utawala au madhila wanayopata watu.
Hilo halishughulishi vichwa vyao wao wanashughulika kuandaa data za udanganyifu.
Mohamed daah! kaiharibu jamii ipasavyo. Ni kwa fikra zake kuna mtu hapo nyuma kasema NECTA ni kigango cha kanisa na imeshawahi kuongozwa na Padre. Nimamuuliza Padre aliyeongoza NECTA alikuwa nani na lini, masikini hana jibu.
Sababu kubwa ni kula ngano ya Mo kama ilivyo, haichukui nukta ukimpeleka kwenye kona hana hoja.
Watu wamemeza ngano na data mbichi sasa hivi wanazunguka wakiazima majenereta huko vijijini kuelezea ushahidi wasiojua kuwa wamelaghaiwa. Kasema Mohamed mwenyewe kuhusu majenereta.
Leo tunamuuliza vipi mwenzetu kuhusu utafiti kulikoni ! anasema ni makosa ya kibinadamu.
Bado watu hawajaona tu! Sad
Hakuna ushahidi wowote wa dhulma dhidi ya Waislamu Tanzania; zipo tuhuma zinazotolewa lakini hakuna mtu ambaye ameweza kuthibitisha uwepo wa dhulma. Watanzania wa dini zote wanapata matatizo yale yale kwenye ajira, elimu, maisha na waliofanikiwa nao wamefanikiwa katika dini zote.
Ritz, imesuniwa kuvaa kofia lakini si hati miliki kwamba hakuna mwingine anayeweza kuvaa kofia, hakuna.Nguruvi3,
Sijui kama unajua hijabu ni nini Mama Theresa alikuwa anavaa mtandio au ushungi tu lakini siyo hijabu.
Waislam hawafanyi makosa kunasibisha kofia na dini yao Muislam kuvaa kofia ni Sunna.
Halafu unatakiwa uelewe siyo kila kitu mtu akikisema basi kaambiwa na Mohamed Said vitu vingine vipo wazi kwa macho tu hivi kujua kuwa Wakiristo wamekamata ajira nyingi serikalini na kwenye mashirika ya umma mpaka uambiwe na Mohamed Said.
Kwa hiyo unataka kutuambia matatizo ya shule za Kilwa na Al Hassan Mwinyi ndiyo yamesababisha Wakirsto wawe wengi Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara zote.
Mashirika ya Umma yamejaa wafanyakazi Wakirsto achalia mbali Wakurugenzi.
Nenda TANAPA, BOT, TCRA, TBC, TBS, TANESCO, BIMA, ITCL, TCCL, na mengine haya yote kuwajaza Wakirsto unadhani limefanyika kwa bahati mbaya Mfumo Kirsto.
Uwa mnanifuarahisha sana mnataka tuwe tujadili matizo ya shule za Kilwa na Mtwara lakini hata siku moja amtaki kujadili kwa nini Wakirsto wameodhi ajira serikalini na kwenye mashirika ya umma.
Wanaofanyiwa dhulma ni Chadema.
Ritz, imesuniwa kuvaa kofia lakini si hati miliki kwamba hakuna mwingine anayeweza kuvaa kofia, hakuna.
Pili, hijab ni vazi la kujisetiri. Ukiamua unaweza kuita mtandio n.k. Kwa maneno mengine pia hiyo haina maana afanyaye hivyo basi keshakuwa mwislam. Mwislam nimuumini wa dini ya kiislam ingawa si kila mwislam ni muumini, kila muumini ni mwaislam. Hivyo mtu atapimwa kwa matendo yake.
Pili, Mohamed amesema kuna waislam wanaopewa menial job ingawa wapo educated. Tume m-challenge atupe mtu mmoja tu mwenye Ph, Master au 1st degree aliyepewa kazi ya udereva au ufagizi. Haukuweza.
Kuhusu waislam kutokuwepo katika maeneo uliyoyataja, tofauti na wewe mimi naangalia mizizi wewe unaangalia matawi.
Kama shule imefungwa hakuna wanafunzi, 10 yrs down the road utapata nani wa kufanya kazi huko ulikotaja?
Lakini muhimu sana nikuulize hebu niunganishe na Zoologist wowote yule wa kiislam, kuna shirika lainatafuta sana mtu huyo Tanzania. Anatakiwa awe na PhD. Kama yupo na mfumo umemwacha nje tafadhali sana sana sana tuwasiliane haraka maana hiyo kazi ni ya dollar za maana.
Kama hutakuwa na yoyote, nitakuuliza yupi aliyenyimwa nafasi?
Jiulize kwanza do you have qualified people?
Huko ulikotaja ni sehemu ndogo, soko huria linaangalia qualifications (what you will bring on the table) siyo umri, dini au kabila. Kama hakuna maandalizi au ndiyo hayo ya kuangalia mambo kwa makengeza kesho watakuja Wakenya, waganda, Wazimbabwe sijui utasingizia nini.
Tazame mbali, siyo data za Mohamed ambazo hawezi kusimama na kuzitete yeye mwenyewe, anawatupia mkadhalilike nazo mbele ya umma. Please!
kwani Chadema na wenyewe wana inferiority complex?
Kamuulize Dr Slaa yeye si ndiyo alisema ataakikisha nchi hatawaliki tena.
sasa wewe unaleta madai, nakutwanga swali unakimbilia nikamuulize Dr Slaa... Pole sana ndugu yangu Ritz umekwisha athirika kisaikolojia kutokana na dhulma mnazofanyiwa, mdogo wako alifanyiwa dhulma mpaka akakimbilia Japan pole sana... Ila kuna siku ambayo haijulikani hizo dhulma zitaisha tu sio Tanzania tu bali ni dunia yote.
Hayo maswali ulionitwanga jibu lake si ndiyo hilo kaka nimekupa.
Halafu unatakiwa uelewe siyo kila kitu mtu akikisema basi kaambiwa na Mohamed Said vitu vingine vipo wazi kwa macho tu hivi kujua kuwa Wakiristo wamekamata ajira nyingi serikalini na kwenye mashirika ya umma mpaka uambiwe na Mohamed Said.
Kwa hiyo unataka kutuambia matatizo ya shule za Kilwa na Al Hassan Mwinyi ndiyo yamesababisha Wakirsto wawe wengi Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara zote.
Mashirika ya Umma yamejaa wafanyakazi Wakirsto achalia mbali Wakurugenzi.
Nenda TANAPA, BOT, TCRA, TBC, TBS, TANESCO, BIMA, ITCL, TCCL, na mengine haya yote kuwajaza Wakirsto unadhani limefanyika kwa bahati mbaya Mfumo Kirsto.
Wewe umemsoma? Au tu mnamtumia kama punching bag? Nimemuuliza Mohamed ni ukurasa gani au sura gani ameandika kuwa kanisa liliuona Uislamu kama adui hajajibu hadi leo.
NInashukuru kwa kujitolea kuwa Mwalimu. Sawa nipe darasa; hii namba 83/17 ni ya nini?
Hili swali lako la aina hii lisitupotezee muda tena.Umejibiwa mara 100 bado unauliza.Ritz, Waislamu wanafanyiwa dhulma gani? Na wanafanyiwa na nani?