Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


@Ami
Asante kwa kuniita mpuuzi wa mwisho. In other words umeniita mwerevu/muungwana wa kwanza.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema: Kuna ushawishi wa "Nguvu ya hoja" na ushawishi wa "Hoja ya Nguvu".

Jipime!


"Hoja za nguvu" ndio kama hizo zinazoambatana na matusi!


@Ami
Ni bahati mbaya tu kuwa kwa sababu ya kuheshimiana, hakuna mtu anayekuambia kuwa hoja zako ni za kitoto. In fact hoja zako huwa zipo dhaifu sana mpaka unadhalilisha hata upande huo unaoutetea.
Je unaweza ukatoa ushahidi wa wazi (Bila kutaja Moh Said, Sivalon, Njozi, Van Bergen) kuonesha dhulma ya wakristo dhidi ya waislam?. Zunguka mitaani, sokoni, makazini , mashuleni (bila kufikiria hivyo vitabu) halafu utuoneshe hiyo dhulma ya mkristo dhidi ya muislam iko wapi? Utaishia kuleta hisia tu!!
 
Mdondoaji
Katika maisha ya kawaida, hujaona marafiki wakiitana "kichaa wangu", "We mjinga" huku maneno hayo yakitumika affectionately?
Hujaona black americans wakiitana Niggers?
Mwalimu wangu sekondari, kila alipokuwa anasisitiza jambo alikuwa anatuita "Nyie waswahili, fanyeni hiki na hiki". Katika darasa la watu 30, kulikuwa na waislam wanne tu, na hakuna hata mara moja ambapo tulimwelewa mwalimu kuwa alimaanisha darasa zima ni waislam. Usijikie vibaya siku tukikutana nikakwambia, "vipi mswahili wangu" Wala haina maana ya kuwa nitakuwa nimekuita "muislam wangu".

Mkuu,kuhusu suala la ubaguzi, ni bahati mbaya tu hujui ninafanya kazi gani, wala hujui ndugu na marafiki zangu ni wa dini gani. Ungekuwa unajua, ndio ungeelewa nime-recruit vijana wangapi wa dini mbalimbali kwa merits zao hapa kazini kwangu. Ubaguzi wa aina yoyote ule ni mbaya, na haufai. Na lazima tukubali kuwa, hizi dini tumezikuta, tutaziacha, na wote inabidi tuishi pamoja ndani ya Taifa hili.
 
Last edited by a moderator:
Kutokuamini ni jambo jengine lakini hivyo vitu vipo na ushahidi umetolewa.
Ikiwa nyinyi hamuamini wengi wetu tayari sasa kazi yenu ni kutubadilisha tusiamini kama mtaweza.

Ndio maana tuko hapa kuwaonyesheni kuwa ushahidi wenu ni magumashi tu. Mohamed ameshindwa kunijibu swali la Nyerere kutaifisha shule za misheni ili waislamu wapate fursa ya kusoma. Yeye hilo kwake halizungumzii kabisa. Wala hazungumzii kuwa elimu yake ameipata St. Joseph, shule ya wakatoliki. Hayo kwake hayagusi. Ukimlaumu Nyerere basi angalau mpe sifa kuwa alijitahidi kutoa fursa sawa za masomo kwa waislamu. Lakini hilo katu hamtasema kwa sababu mkisema hivyo mnamwagia maji theory yenu ya Nyerere kuwa mbaguzi wa Waislamu.
 

Lakini pesa za umma hazitumiki kununulia watu chakula cha iddi au Nyama ya Udhiya
 
Mimi sijaja kudhibitisha kama Mzee Saidi ni mchochezi, ila nimekuja kuona ushahidi wa dhulma kwa Waislamu.

ambayo sijaona mpaka sasa..... ila bado nasubiria

Jee, umekisoma kichwa cha mada? Jee, umeuona huo "uchochezi" na "dhihaka" ulioandikwa hapo? inaonesha wewe uko katika basi la Mbagala na unaelekea Tegeta.
 
Bahati mbaya sana kuna ndugu yangu mmoja hapendi kuambiwa nenda kasome kitabu fulani, anataka aambiwe kilichoandikwa humo. Binafsi naona kusoma ni bora zaidi kuliko kusimuliwa kwani msimulizi anaweza kuongeza au kupunguza chumvi kujenga msimamo wake. Kuna kazi za kitafiti zimefanywa kuhusiana na jambo hili na chimbuko la tafiti hizo ni risala aliyosomewa Rais Mkapa katika sherehe za sikuu ya Idd kusheherekea kuisha kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan Jumanne tarehe 19, mwaka 1999. Angalau ukianzia pale na utapata picha ya nini kinachozungumziwa na kulalamikiwa. Kama BAKWATA ilifikia hatua ya kulalamika namna ile na hiyo BAKWATA ndio inayolalamikiwa na waislamu w nchi hii basi utajua ukubwa wa tatizo. Kitabu liichotolewa na REDET Justice Rights and worship Religious and Politics in Tanzania kinaweza kuwa ufunguo wa kufikia kwenye ukweli kwa kuamsha kiu ya kutafuta ukweli kama hatutaishia kupinga tu au kukubali kile tulichokisoma bila kwenda mbele zaid
 
Hata hii ya DPP kufunga dhamana ya Ponda ni hisia?.
Ile ya Mwanza wakristo kukaidi agizo la serikali halafu katika fujo zilizofuata wa kulaumiwa wakawa waislamu?.

Na ile ya NECTA waislamu kupasi somo la uislamu kwenye shule zenu lakini wakafeli kwenye shule za kiislamu.
Na redio Imani kufungiwa kwa kosa la sensa.
Na serikali kukosa pesa za kuchunguza Mwembechai lakini ikawa na pesa za kuchunguza mbwa?.
Zote hizo ni hisia?.Hayo mengine yapo mitaani na ni mapya kuongezea na yale yaliyotajwa na akina Mohammed Said.
Na kwanini unaogopa kutajwa Mohammed,Sivalon na Njozi?.Kwanza si ulete ushahidi wa kukanusha hayo waliyotaja wao kama ushahidi wetu halafu ndio utake mapya ya mitaani.
Kama wewe ni hodari wa kujibu hoja basi wasaidie Mwanakijiji na Nguruvi KUJIBU HII


 
Inahuzunisha kuona kuwa mtu anaemwamini na kuamini kuwa ana kichwa kizuri akatokea akafanya mambo bila tafakuri kwa vile tu amebebwa na mhemuko au amekuwa 'fanatic'. Katika hotuba yake ya kwanza kabisa kama rais wa nchi akihutubia bunge Nyerere alikiri kuwepo tatizo. Nyerere alipojiunga TAA na badae TANU akakuta kuwa lengo kuu la vyama hivyo ni kuondoa tatizo la kubaguliwa kielimu na kutokuwa na taasisi imara za kiisalmu kwa kuwa mfumo wa kikoloni ulikuwa wa kikristo, wale wazee lengo alo lilikuwa ni kubadili hali ile. Wale wazee ambao walikuwa viongozi wa EAMWS ndio hao hao walikuwa viongozi wa TANU kupitia kamati ya wazee wa TANU. Walisimama kidete kuhakikisha Chuo Kikuu kinajengwa. Harakati zilipofikia hatua ya kuingia mkataba, kamati ile ikavunjwa na wazee wote wakaondolewa katika TANU na kundi kubwa la waislamu imara walioshirikiana na Nyerere katika kufikia hapo wakawekwa kizuizini na kukafuatiwa kuvunjwa kwa EAMWS.Kutaifisha shule hakukuendana na progamu yeyote ya kuwasaidi wale walioachwa nyuma kielimu, ilikuwa hatua ya kisiasa tu kama vile ujenzi wa sasa wa shule za kata. Mohamed Said kusoma St. Joseph hakuondoi ukweli wa mambo yaliyofanyika kuwadhulumu waislamu. Mohamed Said kusoma St Joseph kunaonesha jinsi gani wazee wake walivyothamini elimu na inadhihirisha nafasi waliyokuwa nayo katika nchi hii lakini kwa uungwana wao wakaona kupata elimu kwa mtoto wao tu hakutoshi bali kundi kubwa la waislamu waliokosa mtetezi nao wapate fursa ya elimu. Si zama zile tu hata sasa, sehemu ambazo wanaishi waislamu wengi muamko wa elimu ni mdogo kama ilvyo kwa wafugaji. Serikali yetu leo ipo tayari kuwahamasisha wafugaji kwa mabilioni ya pesa waende shule lakini hawafanyi hivyo katika jamii za kiislamu ingawa wote ni raia wa nchi hii na wana haki sawa kuhudumiwa na kushughulikiwa na serikali yao. Kam kukosa muamko wa elimu kwa waislamu ni tatizo, mbona tatizo hili halishughulikiwi basi
 
Jee, umekisoma kichwa cha mada? Jee, umeuona huo "uchochezi" na "dhihaka" ulioandikwa hapo? inaonesha wewe uko katika basi la Mbagala na unaelekea Tegeta.

Kichwa cha habari

"Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar."

Ila kama ungekuwa umenisoma tangu mwanzo ungenielewa.

Ngoja nijaribu

Katika huu uzi, mengi yameongelewa, na mimi katika kuufuatilia nikakuta kitu kilicho ni intrigue.

Madai ya dhulma kwa waislamu.

Ndo hilo lililo nileta hapa.kuja kuuona huo ushaidi wa dhulma kutoka kwa wale wanao dai upo. Mi nimesema sijaona bado hiyo dhulma lakini inawezekana ipo, ila mpka ushahidi usiopingika.

Sasa kama basi la mbagala nililodandia litageuza na kwenda Tegeta basi ntageza nalo. Si ili mradi kufika.
 

Bado najiuliza Huyu Mwl Nyerere mwenye 'chuki' na Wazee wa Mohamed kwanini hakuwachukulia hatua hao wazee kwa UFISADI wa hiyo nyumba ya new street?
 
ami
Nitakujibu maswali yako kwa maswali:
Hata hii ya DPP kufunga dhamana ya Ponda ni hisia?.
Je huo ni ushahidi wa dhulma ya ukristo dhidi ya uislam? DPP sio ukristo. Na je ni Ponda peke yake ambaye amewahi kukataliwa dhamana na DPP?
Ile ya Mwanza wakristo kukaidi agizo la serikali halafu katika fujo zilizofuata wa kulaumiwa wakawa waislamu?.
Je huo ni ushahidi wa dhulma ya ukristo dhidi ya uislam? Kama serikali ndiyo imewalaumu, je maana yake muislam kalaumiwa na mkristo? Na je kuhusiana na hizo vurugu, hakukuwa na lawama zilizopelekwa kwa wakristo?
Na ile ya NECTA waislamu kupasi somo la uislamu kwenye shule zenu lakini wakafeli kwenye shule za kiislamu.
Je huo ni ushahidi wa dhulma ya ukristo dhidi ya uislam? Je NECTA ni synonymous na ukristo? Na una uhakika gani kuwa hamna wasio waislam ambao walikuwa affected na ile computer glitch?
Na redio Imani kufungiwa kwa kosa la sensa.
Je huo ni ushahidi wa dhulma ya ukristo dhidi ya uislam?, Radio ya kwa Neema, nayo imefungiwa, je ni dhulma ya ukristo dhidi ya uislam?
Na serikali kukosa pesa za kuchunguza Mwembechai lakini ikawa na pesa za kuchunguza mbwa?.
Je huo ni ushahidi wa dhulma ya ukristo dhidi ya uislam?, Vipi ukilinganisha na mauaji ya mwandishi Mwangosi? Ni ukristo huo?
Na kwanini unaogopa kutajwa Mohammed,Sivalon na Njozi?.Kwanza si ulete ushahidi wa kukanusha hayo waliyotaja wao kama ushahidi wetu halafu ndio utake mapya ya mitaani.Kama wewe ni hodari wa kujibu hoja basi wasaidie Mwanakijiji na Nguruvi KUJIBU HII.
Siogopi kutajwa kwa hao waandishi. Niliomba usirejee vitabu hivyo kwasababu, wote tumeishaviona. Wewe unakubaliana navyo, mimi sikubaliani navyo, hasa hasa zile hisia zilizopandikizwa kuwa kuna watu wa dini fulani ndio wanaonewa na wa dini nyingine. Lakini kikubwa ni kwamba, penye dhulma, mara nyingi huwa kuna ushahidi wa wazi, Ndio maana nikasema, hivi kwa mtu ambaye hajawa-influenced na hisia za kwenye hivyo vitabu, je anaweza akatoa ushahidi ulio wazi na usiopingika, kuonesha kuwa waislam wanadhulmiwa na wakristo? Au ushahidi ndio hayo maswali uliyoniuliza hapo juu???
 

Mzee wako anasema Cecil Matola hakuwa na umuhimu kama akina sykes
 
Umenena vyema, waislamu wangeendelea kulalamika hata kama hao uliowataja wangekuwa waislamu. Waislamu hawataki mtu apewe tu kwa vile yeye ni muislamu balai wanataka haki itendeke. Haki ndio neno kubwa kuliko yote
 
Mzee wako anasema Cecil Matola hakuwa na umuhimu kama akina sykes
Hakika, hakuwa, hata wewe wafahamu ndani ya hakuwa muhimu katika suala zima la vugvugu la uhuru na utambuzi wa kuwa mtanzania asiye chini ya Queen, inawezekana alikuwa na umuhimu katika nyanja nyingine
 

Eti ndo mwalimu wako anakufananisha na Nguruvi3!
My foot!

wewe ni bure kabisa
 
Last edited by a moderator:
Hakika, hakuwa, hata wewe wafahamu ndani ya hakuwa muhimu katika suala zima la vugvugu la uhuru na utambuzi wa kuwa mtanzania asiye chini ya Queen, inawezekana alikuwa na umuhimu katika nyanja nyingine

Uko serious kabisa?
Hautanii!!!?
 
Hebu rudi usome post yangu kwa umakini na ukiwa umetuliza akili tena sehemu uliyokazia kwa rangi ya zambarau

Nimesema hivi ''Mohamed anatakiwa afahamu kuwa population ni ''variable value'' kwamba si lazima asilimia 67 ya mwaka 1967 ibaki kama ilivyo.Kuna uwezekano iliongezeka na kufikia 80 au kupungua na kufikia 40 kwahiyo alitakiwa kwanza apate the most recent stats.
Kufanya extrapolation ya mwaka 1967 ni sawa na mtu kupanga mipango ya maendeleo ya nchi kwa kutumia stats za 1967. Huku ni kupotosha vijana kusikoweza kuvumilika hata kidogo. Wrong! Mohamed denounce this ASAP!''

Sikuwahi kusema kuwa population imepungua hadi 40%. Narudia tena population ni variable value. Kuna uwezekano kuwa wakati Mohamed anaandika kitabu population ua waislam ya mwaka 1967 iliongezeka na kufikia 80% au ilipungua na kufikia 40%.

Ukisoma maandishi usisome ukiwa na dhana tayari, hayo ndiyo matatizo yanayomkumba Mo. Naona karithisha vijana wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…