Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Na hakuna mahali ambapo Mohamed amesema kuwa alipokuwa st Joseph mfumokristo school aliwahi kubaguliwa.

Sasa hivi yupo mstari wa mbele kuelezea mfumokristo ambao yeye mwenyewe kwa experience yake st Joseph hajathubutu kuandika hata nusu mstari wa ubaguzi aliouona.

Hataki kuongelea st Joseph maana vijana watamuuliza kwanini mtoto wa ''wazee wa Dar es Salaam'' alikwenda kusoma katika shule ya ''makafir''

Yeye yupo bize kuwakataza wenzake wasipeleke watoto kutafuta elimu inapopatikana.
 
Mkuu Ritz hapo umeteleza kidogo.Padre ni kiongozi wa kiroho wa kanisa Katoliki.Mpake ufikie daraja la upadre kuna ngazi mbali mbali za kiimani utatakiwa kuzipitia.Mchungaji au wachungaji (wingi) ni viongozi wa makanisa (Protestant) Lutheran,Anglican,AIC na nk.Kufikia daraja la uchungaji kuna taratbu za mafunzo ya kiroho.Makanisa kama pentecoste/Assembly na mengine ya kiroho mchungaji si lazima usomee unaweza kukuta mtu ni mhandisi akaanzisha kanisa lake akajiita mchungaji au Askofu au Nabii/Mtume.Hizi title huwezi kuzikuta Lutheran,Catholic au Anglican.Nadhani umenielewa turejee kwenye mada.


Padre na Mchungaji ni sawa sawa jiwe na stone.
 
Nani ana wajibu wa kushughulikia tatizo la ukosefu wa mwamko wa elimu miongoni mwa Waislamu? Ni wote. Wazazi, viongozi wa dini na viongozi wa jamii za Kiislamu. Mohamed angekuwa anapita mitaani anahubiri umuhimu wa watoto wa waislamu kujiunga mashuleni ningefuatana naye. Mbona wachaga hawahitaji uamsho huo? Hii ya EAMWS ni kisingizio tu. Kulikuwepo mfarakano wa ndani ya kundi hilo. Mbona hatujaona wakifanya maajabu Kenya ambako pia walikuwepo?
 

kumbe mo said alisoma misheni...hapa Dodoma hiki ni kipindi cha shule lakini madrasa za bweni zimejaza watoto wa umri wa kwenda shule na zipo kila kona, sijui wahusika hili wanalitazamaje, kesho hawa watoto watakuwa nani kwa elimu ya dini peke yake.
 

Mkuu Ngongo,

Nashukuru kwa kunipa darsa nimekuelewa takuwa mchoyo wa Fadhwila kutokushukuru.
 
Last edited by a moderator:
Usipindishe jawabu!.
Unatumia kanuni ya mtafiti gani anayekubaliana na hoja yako?.
Nakuuliza tena ikiwa ni kupanda au kushuka kwa population jee inakubalika kushuka kwa kiasi hicho bila kuwepo sababu maalum?,
Bila sababu maalum kuwepo.Kushuka au kupanda huoni kwamba hiyo ni mbinu ya kimfumo ili kuleta manufaa fulani?.
Kwanini serikali ikatae kata kata kuingiza kipengele cha dini ili kujua idadi halisi ya watanzania na dini zao?.Huoni kuwa huo ni ushahidi wa kuficha ukweli wa hizo takwimu za 83/17 ?.
 

umeshindwa kutoa darasa nilidhani tungeweza kujadiliana na badala yake unanirudisha nyuma tena..
 

Sijui ni kwa kiasi gani unaamini kauli hiyo; ndani ya hiyo sentensi sijui hata kama umeona contradictions. Unasema Nyerere hatoenda kinyume na Kanisa lake halafu anasema awaambie maaskofu kuwa amemuweka Mlutheri kwa sababu ya imani yake? Walutheri na Wakatoliki? kwa kumuweka Mlutheri anaendeleza vipi Kanisa Katoliki? It just doesn't make any sense..
 
Katika vyote hapo juu kwanini waathirika wakubwa wawe ni waislamu tu.Huoni kuwa huo ni ushahidi wa makusudi.computer gani yenye chuki na waislamu tu?.Mwenye chuki atakuwa ni mtu wa kimfumo aliyeiongoza hiyo comyuter.
Vipi ukilinganisha na mauaji ya mwandishi Mwangosi? Ni ukristo huo?Siogopi kutajwa kwa hao waandishi.
Mwangosi pamoja na kuwa hawakilishi malalamiko ya kundi maalum lakini tume si iliundwa?.Kwanini masuala yote yanayowahusu waislamu hakuna haja ya kuundiwa tume?.
Ikiwa hutaki kuamini vitu vilivyoandikwa baada ya utafiti basi hakuna sababu ya kuamini mambo ya mitaani.Nakuonya usiendelee na utovu wa nidhamu kama huu.
Wewe vipi?.Unakimbilia ushahidi wa mitaani wakati watafiti waislamu kwa wakristo wamethibitisha kuwepo dhulma.
 
Kabla kuja kwa walutheri na wakatoliki kwanza ulipaswa ujibu jee kwa Nyerere kusema amemuweka aliyemuweka kutokana na imani yake ni Udugunization au la.
Hii ndio tabia yako unapokosa jibu unauliza swali.
 
Kwa vijana wadogo ni vigumu sana kuelewa mambo yalivyokuwa huko nyuma na hivyo wanakuwa wepesi mno kumeza ngano wanazolishwa na Mohamed Said...kwa mfano, je wanajua, wakati wa mkoloni, ushindani uliokuwapo baina ya dhehebu mbali mbali za Kikristo na hasa Wakatoliki, Walutheri na Waprotestant ndio chachu iliyowezesha maendeleo makubwa kupatikana sehemu zote walizopiga kambi.

Kulikuwa na ushindani katika utoaji wa huduma za kiroho, hospitali na shule...hivyo mathalani kila moja wao alipofungua shule eneo fulani na mwenziwe alifanya hivyo hivyo kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi. Bahati mbaya kwenye mikoa ya mwambao yenye Waislaam wengi walipata upinzani mkali kupokewa kama inavyosimuliwa hapa na Mwandishi wa historia Philemon Andrew K Mushi katika kitabu chake History and Development of Education in Tanzania, nanukuu;
Mwandishi na mtafiti Philemon Andrew K Mushi, anaendelea;
Je, Mwalimu Nyerere alirithi nini mwaka 1961 tukipata uhuru, Mwandishi na mtafiti anaendelea kutoa darasa;
After independence the new government under its leader Mwalimu Nyerere was committed to educational policies and strategies aimed at addressing the observed inequalities in education provision. The first thing Mwalimu did was to address the issue by nationalizing all mission schools to give equal opportunity to all Tanganyikans/Tanzanians and this made it possible for people like Mohamed Said to see the inside of a classroom at St Josephs...sasa shuhudieni kejeli na dhihaka zake kwa Mwalimu, kweli shukhrani ya punda ni mateke.
 
Last edited by a moderator:


Sasa population inapungua vipi hadi kufikia 40% from 67%??

kilitokea nini??NUNGWI zilikua nyingi sana nin??

naona NGURUVI'S HISTOHISIA BADO ZINAENDELEA..

poleni sana..
 
Reactions: Ami
Kabla kuja kwa walutheri na wakatoliki kwanza ulipaswa ujibu jee kwa Nyerere kusema amemuweka aliyemuweka kutokana na imani yake ni Udugunization au la.
Hii ndio tabia yako unapokosa jibu unauliza swali.

Umejuaje kama Nyerere alisema hicho anachodaiwa kusema kwenye kitabu cha Bergen?
 
Umejuaje kama Nyerere alisema hicho anachodaiwa kusema kwenye kitabu cha Bergen?

Kwa kuwa yeye mwenyewe hakukanusha kilichoandikwa dhidi yake! wakati akiwa hai kitabu kinasomwa inakuwaje wewe unakanusha baada ya mhusika kufa? Nyerere akisingiziwa mara moja hukanusha ndio maana mwaka 1992 alikanusha madai ya Kambona kuwa anamiliki mali kibao na ameweka fedha nyingi ktk benki ya Uswissi yeye na Amir Jamal na Kawawa! madai haya ya Kambona alitoa wakati akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Jangwani!
 
Reactions: Ami
Ma3, I was there and as a Moslem I benefited from Nyerere's decision to nationalize mission schools.
 
Kwa namna huu mjadala unavyoendelea Mag3, Nguruvi, Mwanakijiji, Jasusi etc. mjiandae pale toleo la tano la kitabu cha Mzee Saidi litakapokuja na madai:


Hahahaha ahahahaha ahaha!!!!!!

Please haya ni maoni yangu and I responsibly own them.


Isn't this what we see on things we know, stuff that we saw, lived and experienced ndani ya simulizi za MS?
 
Kuna vitu vingi sana ambavyo Nyerere hakukanusha. Yaani mlitaka wakati wote kunapotokea kitabu Nyerere akanushe hadharani? Angefanya kazi yake saa ngapi? Unakumbuka alivyowajibu waandishi habari wa Kenya wakati mmoja kuhusu kuzaa na mama zao? Alitaka watumie akili zao. Nyerere hakujibu madai ya Kambona kuhusu kuwa na fedha katika benki ya Uswiss. Aliyejibu ni Amir Jamal katika interview niliyofanya naye wakati huo natumikia shirika moja la redio ya kimataifa.
 

Una uhakika alikanusha au unafikiria alikanusha; mtawapata hawa wadogo na watoto zetu na hii historia mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…