Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wakati mwingine mi nadhani tuyatazame haya mambo kwa upande wa pili.
'
Hapa kuna watu wanaongozwa na imani zao kuamua mambo.
'
Na hata historia wanayotoa imeegemea kwenye mtazamo huo.
'
Hatuwezi kufika.
'
Itikadi,mtazamo na maamuzi yanapokuwa ya kidini huzua sintofahamu ya ajabu sana.
'
Ni kitu gani kinachofanya mtu aamini watu fulani walifanyiwa mambo fulani(kama ni kweli) kwa kuwa ni waumini wa dini fulani na sioambo mengine?
 
Sio IMANI tu. Na chuki kali za wazi kabisa kwa Mwalimu ambaye wala hakutuibia kabisa au kutubagua kama wanavyodai. Mwalimu ameng'atuka madarakani akamwachia ALI HASSAN MWINYI Muislam safi kabisa. Mzee Mohamed aende hapa jirani Kenya aone mfumokristo unavyofanyakazi. Hakuna Muislam atakuwa Rais wa Kenya kwa miaka 100 ijayo hata awe Mkikuyu, Mkamba, Mjaluo, Mluhya, Mnandi,!
 
Kinachonifurahisha katika historia yoyote ile duniani ni kuwa huwa inajiandika yenyewe! Ukiilazimisha kupotosha, itakurudisha kwenye ukweli tu.

Mohamed Said, historia ya kweli inakulazimisha urudi kundini hata kwa madhila uyapatayo.
 

Daaaah umetoa mfano hai sana ndugu yangu, hilo Mohamed Said kalimezea tu huku akihubiri maovu Tanzania
 
Enyi watu maskini wafikira, uduni wa hekima, mbumbumbu wa busara na wenye mitindio ya ustaarabu katika jamii inayojenga umoja, mshikamano na undugu tunawaomba sana muache na kutuondolea upumblaana hii mnayotuletea katika taifa letu la Tanzania. Pia ninaomba mamlaka za kiserikali kuwatafuta watu hawa wanaopandikiza chuki za kidini katika taifa letu na kuwaadhibu.

Nani asiyefahamu kuwa mitihani yote katika nchi hii inafanyika kwa kutumia namba ya mtahiniwa? Sasa leo tunaanza kuelezwa habari ya watoto fulani hawafaulu kwa sababu ya dini zao kwani inasahihishwa jina na dini ya mtu au mtihani?

Mwl Nyerere amefanya kwa uwezo wake na ameondoka akituacha kama taifa moja la watu wamoja tunaoishi na kuoana kama watu wamoja bila kujali dini ya mtu. Sasa ni jukumu letu tuliobaki kuendeleza alipotuacha bila ya kuangalia dini ya mtu.

Nasema tena acheni upuuzi huu la sivyo laana inawaandama si kwenu tu hata kwa vizazi vyenu.
 

Muislam daraja la tatu anakuwa tajiri
Muislam daraja la tatu anakuwa msomi
Muislam daraja la tatu anaishi popote Tanzania, Moshi kule ndani kwenye Wakristo chungu nzima
Muislam daraja la tatu tunashereheka naye Christmas, Idd, Maulid, Pasaka tukiwa wadogo.
Muislam daraja la tatu anakopa benki

Muislam daraja la tatu anaweza kuwa vyovyote anavyotaka kuhubiri chuki, kuchoma kanisa, kukashifu imani nyingine,
kuandika maandishi ya kuchochea chuki na akaishi kwenye nyumba kwa amani kabisa.

Nakumbuka nikiwa mdogo rafiki yangu wakati amemaliza mafunzo ya ubatizo alikuja kiwanjani akatuambia anataka kuchagua jina la Bakari na sisi tukamuunga mkono (wakati huo ilikuwa mwanzoni 90's). Masikini nchi hii hata kuhisi tu jina linatumika na watu wa Imani nyingine wala hatukufikiria................Nani anawaza ubaguzi?

Tunacheza viwanja vya Kanisa na Msikiti tena wakati mwingine mnasubiriana mmoja wenu atoke kwenye ibada (kama si kuingia ndani!) ili mkapige chandimu!!

Najiuliza kwa hizi "spinning" za MS baada ya miaka 30 tutaishi pamoja kama dalili zenyewe tumeshaziona?
 
ni kweli hata mimi ningependa kulijua hilo
 
?..........Nakumbuka nikiwa mdogo rafiki yangu wakati amemaliza mafunzo ya ubatizo alikuja kiwanjani akatuambia anataka kuchagua jina la Bakari na sisi tukamuunga mkono (wakati huo ilikuwa mwanzoni 90's). Masikini nchi hii hata kuhisi tu jina linatumika na watu wa Imani nyingine wala hatukufikiria................Nani anawaza ubaguzi?

Tunacheza viwanja vya Kanisa na Msikiti tena wakati mwingine mnasubiriana mmoja wenu atoke kwenye ibada (kama si kuingia ndani!) ili mkapige chandimu!!

Najiuliza kwa hizi "spinning" za MS baada ya miaka 30 tutaishi pamoja kama dalili zenyewe tumeshaziona?[/QUOTE]

Nimeipenda hii
 

Nimeipenda hii, tutazame nini kifanyike.
 

Huu ndio uthibitisho wa kazi thabiti ya hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyoifanya baada tu yakupata uhuru!
 
"wasomi", mpaka leo, miaka 15 imepita tangu kitabu cha mzee wetu bwana Mohamed Said kitoke, hivi kinaenda tolea la tatu, hawajaja na kitabu mbadala ku-counter argue yale yooooote aliyoyazungumza

"wasomi" wanabaki kubwabwaja na kulalama.
 
Mkuu, Mohamed, naomba tena kukuuliza msimamo wako kuhusu masuala haya hapa chini, ambayo bila shaka yalikuwa ni kati ya misingi iliyokufanya uandike historia ya wazee wako waliosahaulika. Je bado unaamini kuwa haya mambo ni kweli?

Kwamba:

1. Vita ya maji maji ilikuwa ni baina ya Waislam na Wakristo.

2. Hapa nchini kuna waislam na wakristo tu, hamna wapagani.

3. Majina yanaashiria dini fulani, kwa mfano Ally Songea lazima alikuwa muislam, na John Smith lazima alikuwa mkristo.

4. Kwamba kwa ujumla, waislam Tanzania ni wengi kuliko wakristo, ila kwasabau ya kukandamizwa/uonevu kwa waislam, ndio maana waislam wanakuwa wachache katika elimu ya juu, makazini na serikalini

5. Kwamba kanisa katoliki (Tanzania) lilikuwa na bado lina uadui na uislam na lina mpango mkakati wa kudhoofisha uislam afrika mashariki.

6. Mkatoliki Nyerere alikuwa anatimiza maagizo ya kanisa kuutokomeza uislam na ndio maana hata wizara ya elimu iliwahi kuongozwa na padre, na kwamba hata kupendekezwa kwake na kanisa kwenye sainthood kunatokana na kazi aliyofanya ya kudhibiti uislam
 
Mkuu Ritz, kwanza nimeweka post yako na Mohamed Said ili kutoa nafasi nzuri ya kujibu hoja zako. Kama wengi wanavyodhani, baadhi yetu hatupingi Historia kwasababu Historia ipo na wakati ukifika hujidhihiri.

Gari ya Nyerere aliyopewa na Dossa ipo, kuna nini cha kukataa hapo? Familia ya Sykes tokea wamehamia Tanganyika wapo na wanajulikana kwa harakati zao. Nini cha kukataa hapo!

Mshume Kiyate alikuwepo, Kyaruzi, Amir Kweyamba na wengine. Nyerere alizaliwa Butiama akahamia Dar es salaam nakuiukuta Dar ipo, nini cha kukataa? Kwa ufupi hakuna anayepinga historia kama ipo sahihi kwasababu yenyewe tu hujisahihi hata kama imepindwa ikapinduka.

Mohamed ameandika historia ya harakati za uhuru Tanganyika(kaandika hapo juu). Maana yake ni uhuru wa wananchi wa Tanganyika. Hakuna mahali Sykes au mwingine akiwemo Nyerere walipokaririwa wakisema wanapigania uhuru kwa ajili ya kuwakomboa Waislam au Wakristo. Hakuna na Mohamed anakubali hilo!

Tatizo linalojitokeza ni kuitumia Tanganyika kama sehemu fulani yenye watu fulani.
Kutumia mwamvuli wa dini katika kujenga hoja hasa kwa nyakati za leo.
Kudharau mchango wa watu wengine wenye dini na wasio na dini katika kupigania uhuru wa nchi hii.
Kutafuta mtu mmoja na kumfanya kama ndiye tatizo la Waislam(siyo Tanganyika tena) ili kujenga uhalali hoja

Tatizo ni kutumia historia iliyo wazi kuficha mambo kwa kusingizia mtu au taasisi nyingine.
Ni kuaminisha umma kuwa wazee wa Ms hawakuwa na tatizo hadi pale Nyerere na kanisa walipoingia katika uhuru.

Tatizo ni kuficha majina yasiyompendeza mwandishi na kuficha maovu yatokanayo na majina anayoyapenda ili kujenga chuki katika misingi ya upotoshaji, ubazazi na uzushi.

Baadhi yetu tunasema aa! wait a minute hapa si kweli hapa ni kweli. Hatupo tayari kulishwa ngano na mashudu kwa kumeza tu. Hatupo hapa kusema hewala ili mradi kumpendeza mtu na wala hatupo hapa kupinga ukweli ulio wazi.

Ukiangalia nukuu ya MS hapo juu, kwa mara ya kwanza amekiri kuwa ''waislam waliikataa AMNUT'' ili kuunga mkono harakati za uhuru chini ya Nyerere. Hilo halipo katika kitabu chake na tunashukuru amejifunza kutoka kwetu.
Wangapi walijua AMNUT ilikataliwa na Waislam? MS hakuwahi kusema lakini sasa anakiri.

Tunamuonyesha uandishi wake ulipovuka mipaka kwa ushabiki na unazi. Mfano, hapo juu anasema Nyerere alipiga marufuku EAMWS. Ukisoma maandiko ya MS hakuna mahali ameandika Mwinyi aliwafunga waislam waliovunja mabucha ya Nguruwe. Atatumia neno serikali. Panapomhusu Mwinyi na Kikwete ni serikali, panapomhusu Nyerere na Mkapa ni Wakatoliki, hii haipo katika uandishi. Huu ni unazi unao adulterate hata zile chenga chache za ngano.
Gunia la la mahindi likiwa na pumba nyingi kuliko mahindi haliitwi gunia la mahindi linaitwa gunia la pumba.

Tunachofanya hapa wengine ni kumuambia MS kuwa lazima aingalie nchi na dunia kwa umbali mkubwa.
Jitihada za kuchochea chuki na vurugu hazitatoa suluhu ya tatizo.
Somalia wamejaribu a hapo ndipo walipo kama wanavyofanya Nigeria n.k.

Tunamwambia MS awe mkweli kwa jamii inayomhusu kwavile kila mmoja ana responsibility katika jamii yake.
Kuwaaminisha watu habari za kutunga ili kujenga chuki ni kupumbaza jamii hiyo.

Badala ya kumlaumu Nyerere kwa kuua EAMS alitakiwa akemee BAKWATA na Ponda kwa ujinga unaoendelea Chang'ombe.
Badala ya kulaani mfumokristo anatakiwa aende Kilwa awaambie wasifunge shule, aende Mtambani amwambie ustadhi watoto wasiende kusikiliza kesi za wajinga kiustu.

MS anatakiwa aelimishwe kuwa profesa Safari hakuteuliwa kuwa profesa, Twaha Taslim hakupigiwa kura kuwa lawyer, mchumi nguli duniani profesa Lipumba hakupewa kwa nafasi za upendeleo kutoka Afrika au Tabora.
Wamefuzu kwa merits na ni matunda ya jitihada zao na wazazi wao.

MS aulizwe, hivi tofauti ya wanafunzi wa shule ya FEZA na Kinondoni ni ipi? kwanini mfumokristo uchague mahali pa kupiga? Kwanini Mariam Hussein bin Thuain akiwa Masjid Quba afeli na Mariam Hasssan Aqureish mwingine akiwa Marian sec bagamoyo aongoze tena ndani ya mfumokristo.

Ni kupitia majadiliano haya MS amekubali kuwa namba za mitihani hazikuletwa na Malima.
Amekiri kuwa ni ngumu kufaham kwanini mtaa wa mshume kiyate hakuwekwa na wala si Nyerere.
Amekiri kuwa kitabu cha Bergen hakijapigwa marufuku kama alivyosema na amekiri kuwa hujuma za kitabu chake UDSM ni za kuambiwa. Ritz, hivi huoni hapo tunaisadia jamii na MS mwenyewe!

Mwisho, umesema hatujaandika neno zuri kuhusu wazee wa MS. Ukirudi nyuzi moja nyuma nimeandika hivi. '' kwanini MS asifikirie kadhia inayowakuta wazawa wa kariakoo-mzizima (katika mnakasha huu mimi ndiye peke yangu nimewaita mzizima kwa heshima kubwa), nikasema wasiuze rasilimali zilizopiganiwa na akina Sykes na Mshume kwa sh milion 15 ikiwa thamani yake ni milion 400''. Je, hapo si neno zuri kwa wazee wake MS.

Nimesema kwanini MS na wenzake wasiangalie namna ya kutumia kiwanja cha Chang'ombe kuboresha maisha ya wenyeji wetu wa Dar a.k.a wazee wa mzee. Je, hilo si neno zuri.
Je, ni wapi ambapo nimeandika neno baya kuhusu wazee wake katika mnakasha huu! just one word!

Tofauti baina yetu ipo moja, mimi nitasema hata kile mtu asichotaka kusikia, mzee atajaribu kumwagia kilo za sukari ili shubiri iwe tamu.
 
Mzee Mohamed Said, naomba nikuulize swali moja tu,

Katika maisha yako ulishawahi kufanya utafiti kujua upataji wa elimu na ubora wake kwa mtoto wa kiislama ndani ya skuli za kiislamu?

Nini ulikiona?
 
Mzee Mohamed Said, naomba nikuulize swali moja tu,

Katika maisha yako ulishawahi kufanya utafiti kujua upataji wa elimu na ubora wake kwa mtoto wa kiislama ndani ya skuli za kiislamu?

Nini ulikiona?
Hata kwa bunduki huwezi kumuambia Mohamed Said na wafuasi wake waangalie ubora elimu inayotolewa kwenye shule za kiislam. Tumejaribu sana huko nyuma. Wenyewe tatizo lao lipo NECTA.
Na hapa kwenye paper yake
Shule zinazojaa waislam lazima zifanyiwe mchezo mchafu na NECTA. Kama alivyouliza Nguruvi3, inakuwaje FEZA BOYS/GIRLS zinafanya vizuri lakini ni shule zinazoendeshwa na waislam?
 

Kuwa na subra basi swali kaulizwa Mohamed Said. Au tayari umeishamjibia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…