Nguruvi3 na
Mzee Mwanakijiji.
Hata siku mmoja hatujawahi kuyasoma mabandiko yenu humu jamvini mkiwaelezea hata kwa chembe ya uzuri ambayo wameyafanywa na hawa wazee wa Dar es Salaam katika harakati za kupigania uhuru.
Mtu makini akiwasoma ataona hata nyie mpo upande wa wazee wa kikiristo ambao walipigania uhuru kwa maana hiyo wote mnaangukia kundi moja. Nyie mnatetea wazee wenu wa kikistu na Mohamed Said anatetea wazee wake wa kiislam.
Mzee Mwanakijiji,
Nguruvi3,
Yericko Nyerere,
Mag3, ni wakati wenu sasa kukaa chini na kuunganisha nguvu zenu kuandika kitabu ambacho kije kuboboa kabisa hizo "ngano" za Mohamed Said kama mnavyoziita.
Watanzania watajifunza mengi kupitia nyie.
Hilo ndilo swali la kujiuliza.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo hiyo nimeieleza humu.
Nyerere anatembea kwa miguu kafuatana na Abdu Sykes na Dossa.
Njiani salamu wanazopeana na wananchi ni "Uhuru."
Sheikh Hassan bin Amir anamuunga mkono Nyerere kwa dhati ya nafsi
yake.
Baraza la Wazee wa TANU wanaisimamia safari ya Nyerere UNO kwa mafanikio
makubwa sana.
Waislam wanaikataa AMNUT.
Uhuru unapatikana.
Ghafla Nyerere hataki kuwaona wazee wa Baraza la TANU pale New Street.
Ghafla TAA haina maana kwa kuwa hakikuwa chama cha siasa bali cha starehe.
Ghafla masheikh wanakamatwa usiku wa manane kama majambazi na kutupwa
kizuizini.
Ghafla EAMWS si jumuia halali Nyerere anaipiga marufuku.
Sheikh Hassan bin Amir anakamatwa na kurudishwa "kwao" Zanzibar.
Mfumokristo unachukua nafasi ya ukoloni.
Hali ya Waislam ndiyo hii ya kuwa raia daraja la tatu.
Hawana ruhusa hata kuhadithia historia ya mashujaa wao.
Hivi mlitegemea nini?
Mkuu Ritz, kwanza nimeweka post yako na Mohamed Said ili kutoa nafasi nzuri ya kujibu hoja zako. Kama wengi wanavyodhani, baadhi yetu hatupingi Historia kwasababu Historia ipo na wakati ukifika hujidhihiri.
Gari ya Nyerere aliyopewa na Dossa ipo, kuna nini cha kukataa hapo? Familia ya Sykes tokea wamehamia Tanganyika wapo na wanajulikana kwa harakati zao. Nini cha kukataa hapo!
Mshume Kiyate alikuwepo, Kyaruzi, Amir Kweyamba na wengine. Nyerere alizaliwa Butiama akahamia Dar es salaam nakuiukuta Dar ipo, nini cha kukataa? Kwa ufupi hakuna anayepinga historia kama ipo sahihi kwasababu yenyewe tu hujisahihi hata kama imepindwa ikapinduka.
Mohamed ameandika historia ya harakati za uhuru Tanganyika(kaandika hapo juu). Maana yake ni uhuru wa wananchi wa Tanganyika. Hakuna mahali Sykes au mwingine akiwemo Nyerere walipokaririwa wakisema wanapigania uhuru kwa ajili ya kuwakomboa Waislam au Wakristo. Hakuna na Mohamed anakubali hilo!
Tatizo linalojitokeza ni kuitumia Tanganyika kama sehemu fulani yenye watu fulani.
Kutumia mwamvuli wa dini katika kujenga hoja hasa kwa nyakati za leo.
Kudharau mchango wa watu wengine wenye dini na wasio na dini katika kupigania uhuru wa nchi hii.
Kutafuta mtu mmoja na kumfanya kama ndiye tatizo la Waislam(siyo Tanganyika tena) ili kujenga uhalali hoja
Tatizo ni kutumia historia iliyo wazi kuficha mambo kwa kusingizia mtu au taasisi nyingine.
Ni kuaminisha umma kuwa wazee wa Ms hawakuwa na tatizo hadi pale Nyerere na kanisa walipoingia katika uhuru.
Tatizo ni kuficha majina yasiyompendeza mwandishi na kuficha maovu yatokanayo na majina anayoyapenda ili kujenga chuki katika misingi ya upotoshaji, ubazazi na uzushi.
Baadhi yetu tunasema aa! wait a minute hapa si kweli hapa ni kweli. Hatupo tayari kulishwa ngano na mashudu kwa kumeza tu. Hatupo hapa kusema hewala ili mradi kumpendeza mtu na wala hatupo hapa kupinga ukweli ulio wazi.
Ukiangalia nukuu ya MS hapo juu, kwa mara ya kwanza amekiri kuwa ''waislam waliikataa AMNUT'' ili kuunga mkono harakati za uhuru chini ya Nyerere. Hilo halipo katika kitabu chake na tunashukuru amejifunza kutoka kwetu.
Wangapi walijua AMNUT ilikataliwa na Waislam? MS hakuwahi kusema lakini sasa anakiri.
Tunamuonyesha uandishi wake ulipovuka mipaka kwa ushabiki na unazi. Mfano, hapo juu anasema Nyerere alipiga marufuku EAMWS. Ukisoma maandiko ya MS hakuna mahali ameandika Mwinyi aliwafunga waislam waliovunja mabucha ya Nguruwe. Atatumia neno serikali. Panapomhusu Mwinyi na Kikwete ni serikali, panapomhusu Nyerere na Mkapa ni Wakatoliki, hii haipo katika uandishi. Huu ni unazi unao adulterate hata zile chenga chache za ngano.
Gunia la la mahindi likiwa na pumba nyingi kuliko mahindi haliitwi gunia la mahindi linaitwa gunia la pumba.
Tunachofanya hapa wengine ni kumuambia MS kuwa lazima aingalie nchi na dunia kwa umbali mkubwa.
Jitihada za kuchochea chuki na vurugu hazitatoa suluhu ya tatizo.
Somalia wamejaribu a hapo ndipo walipo kama wanavyofanya Nigeria n.k.
Tunamwambia MS awe mkweli kwa jamii inayomhusu kwavile kila mmoja ana responsibility katika jamii yake.
Kuwaaminisha watu habari za kutunga ili kujenga chuki ni kupumbaza jamii hiyo.
Badala ya kumlaumu Nyerere kwa kuua EAMS alitakiwa akemee BAKWATA na Ponda kwa ujinga unaoendelea Chang'ombe.
Badala ya kulaani mfumokristo anatakiwa aende Kilwa awaambie wasifunge shule, aende Mtambani amwambie ustadhi watoto wasiende kusikiliza kesi za wajinga kiustu.
MS anatakiwa aelimishwe kuwa profesa Safari hakuteuliwa kuwa profesa, Twaha Taslim hakupigiwa kura kuwa lawyer, mchumi nguli duniani profesa Lipumba hakupewa kwa nafasi za upendeleo kutoka Afrika au Tabora.
Wamefuzu kwa merits na ni matunda ya jitihada zao na wazazi wao.
MS aulizwe, hivi tofauti ya wanafunzi wa shule ya FEZA na Kinondoni ni ipi? kwanini mfumokristo uchague mahali pa kupiga? Kwanini Mariam Hussein bin Thuain akiwa Masjid Quba afeli na Mariam Hasssan Aqureish mwingine akiwa Marian sec bagamoyo aongoze tena ndani ya mfumokristo.
Ni kupitia majadiliano haya MS amekubali kuwa namba za mitihani hazikuletwa na Malima.
Amekiri kuwa ni ngumu kufaham kwanini mtaa wa mshume kiyate hakuwekwa na wala si Nyerere.
Amekiri kuwa kitabu cha Bergen hakijapigwa marufuku kama alivyosema na amekiri kuwa hujuma za kitabu chake UDSM ni za kuambiwa. Ritz, hivi huoni hapo tunaisadia jamii na MS mwenyewe!
Mwisho, umesema hatujaandika neno zuri kuhusu wazee wa MS. Ukirudi nyuzi moja nyuma nimeandika hivi. '' kwanini MS asifikirie kadhia inayowakuta wazawa wa
kariakoo-mzizima (katika mnakasha huu mimi ndiye peke yangu nimewaita mzizima kwa heshima kubwa), nikasema wasiuze rasilimali zilizopiganiwa na akina Sykes na Mshume kwa sh milion 15 ikiwa thamani yake ni milion 400''. Je, hapo si neno zuri kwa wazee wake MS.
Nimesema kwanini MS na wenzake wasiangalie namna ya kutumia kiwanja cha Chang'ombe kuboresha maisha ya wenyeji wetu wa Dar a.k.a wazee wa mzee. Je, hilo si neno zuri.
Je, ni wapi ambapo nimeandika neno baya kuhusu wazee wake katika mnakasha huu! just one word!
Tofauti baina yetu ipo moja, mimi nitasema hata kile mtu asichotaka kusikia, mzee atajaribu kumwagia kilo za sukari ili shubiri iwe tamu.