Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwa hiyo unakubali kuwa enzi za ukoloni na kabla yake hakukuwepo shule za waislamu. Unakubali kuwa wamisheni ndio walioshughulika kujenga shule. Sasa iweje leo uelekeze lawama zako kwa serikali ya Nyerere ambayo ilichukua jitihada kutoa nafasi ya elimu kwa Waislamu baada ya uhuru kwa kutaifisha shule za misheni? Mbona suala hili linakupa kigugumizi?
 
Mzee wetu anajichanganya tu hapa, hajui asimamie wapi.
 

Ushahidi huu ni mfano wa Baba anakula wali na mchuzi wa nyama pamoja na watoto wake huku nyama zote anakula mwenyewe na wanawe wali na mchuzi mtupu! Baba akiulizwa watoto nao wamekula wali na nyama? jibu ni ndio! watoto wakiulizwa mmekula? jibu ni ndio lakini bila nyama!

Mwanakijiji,
unadai vigogo hao hapo juu ni Waislamu! mbona ukipewa uwiano wa mgao wa madaraka ulivyo na ubaguzi TZ huwa unasema utajuaje kama Ali ni Mkristo au John ni Muislamu? sasa wewe umejuaje kama Ramadhani Dau au Nahodha na wengine ni Waislamu?
 
Reactions: Ami
 

Jasusi,
Tutazungushana hadi asubuhi.

Historia ya Nyerere na Waislam leo ni mashuhuri.
Hakuna asiyeijua.
 
Gwalihenzi, nionyeshe mahali mzee MS amesema yeye ndiye mwenye"historical knowledge"peke yake ya AA na TANU baba ficha upumbavu wako onyesha busara zako angekuwa na majivuno asinge jadiliana na vilaza kama wewe huku jf
Wewe mtoto, nilishakuambia kwamba hutumii akili yako na ndio maana unatukana hovyo humu jamvini. Hivi ni nani anayeonesha upumbavu? ni mimi au huyo mzee wako Mohamedi Said ambaye kwako wewe unamuona kama vile mtume! haya soma huu upumbavu wake hapa chini na kisha utoe hukumu sahihi juu yake;
WC,

Unataka tubishane kwa kitu ambacho waliasisi wazee wangu
na mie kuijua historia yake?

Hivi wewe utaijua AA kuliko mimi mjukuu wa waasisi hawa?
Hivi wewe utaujua undani wa TANU kunishinda?


Huo ni muhali.
Sasa umeuona upumbavu wa mzee wako? Ati kwakuwa AA na TANU waliasisi wazee wake, basi ni yeye tu (Mohamed Said) anayeujua undani wake! wengine hawawezi kujua! Kwani kuasisi chama ilikuwa ni miliki ya wazee wake tu? akina Cecil Matola hawakuwepo na hawakujua AA, Nyerere ambaye alikikuwa raisi wa kwanza wa TANU hakuijua TANU? Vipi taarifa za vyama hivyo igeuke kuwa miliki ya mzandiki Mohamedi Saidi?
 

Mkubwa nimekwambia nionyeshe mahali amesema niyeye tu anajua hitoria ya AA na TANU hujanioyesha humuelewi mzee au ni kiburi chako, huyu mzee humuwezi mfano wako na mzee MS ni sawa na mtu kupiga kichwa ukuta halafu unasikitikia ukuta badala ya kusikitikia kichwa chako upo hapo Dingi.
 
Hayo ndio matatizo ya ushabiki wa kijinga, huoni wala husikii chochote dhidi ya Mohamedi! basi baki na ututusa wako mjinga wewe.
 

Boko Haram,
Hakuna kitu kisichokuwa na mmiliki wake.

Ushahidi wa kuwa mimi najua kushida yoyote humu kuhusu TANU uko mwingi.

Nimeweka humu mambo mengi kuanzia nyaraka hadi picha nilizopewa na wazee
wangu kuhusu chama cha TANU.

Katika nyaraka hizo zimo hadi nyaraka za Nyerere mwenyewe.

Katika hali kama hii nani atasimama na mimi tushindane kuhusu kuijua historia ya
uhuru?

Hilo achilia mbali.
Nani hapa jamvini aelezaye historia ya TANU?

Nimeeleza kuwa baba yangu alikuwapo wakati wa harakati na kaona kila kitu kwa
jicho lake anakumbuka hadi siku alipomuona Nyerere kwa mara ya kwanza nyumbani
kwa Abdu Sykes Stanley Street mwaka 1952.

Hivi ni vitu vya kawaida ni historia ya watu ambayo haina sababu hata kidogo ya hata
kwa mbali kumghadhibiosha mtu na kuanza kutoa lugha zisizopendeza za ''uzandiki'' nk.

Ni mimi peke yangu kiasi nimevutia watazamaji 100,000 historia katika JF.
Wenyeji wananambia hii haijapata kutokea.
 


THERE IS NO HONOURABLE WAY OF DENYING THE TRUTH..
THERE IS NO GENTLE WAY OF DESTROYING IT,
THERE IS NOTHING GOOD IN OPPOSING IT EXCEPT ITS REALIZATION..
upokee tuh huo ukweli hata kama ni mchungu ndugu yangu..
 
NYERERE, KARUME WATAJWA KESI YA WAFUASI WA PONDA

Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere
Shahidi wa utetezi na Mwanzilishi wa Baraza la Misikiti Tanganyika, Bilali Waikela (87), amedai mahakamani katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49, kwamba Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Shekhe Abeid Karume, walivunja Umoja wa Waislamu wa Af...rika Mashiriki.

Waikela alidai kuwa umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kuwatetea na kuwasaidia Waislamu na kwamba Tanzania ilipata kiwanja cha Chang’ombe Marcas kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Misri.

Waikela ambaye ni shahidi wa 48 wa upande wa utetezi katika kesi hiyo alidai kuwa, umoja huo ulifutwa baada ya Karume kudanganywa kuwa wana mpango wa kufanya mapinduzi na kuwarudisha Waarabu Zanzibar.

“Mwalimu Nyerere ndiye aliyemtuma Karume afanye hivyo na mwaka 1964 nilifungwa baada ya kukataa kupokea Shilingi 40,000 ili nikubali kuvunja umoja huo, na Kassim bin Juma, Adam Simba na Salehe Masasi waliotumiwa kuhamasisha watu kuvunja umoja huo,” alidai.

Alidai kuwa ofisi za umoja huo zilifungwa hadi mwaka 1968 lilipoundwa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na kukabidhiwa ofisi pamoja na mali zote kikiwamo kiwanja cha Chang’ombe markazi kilichokuwa kimejengwa shule ya Waislamu.

CHANZO: NIPASHE, 21st March 2013See More
 
Wewe ni mzee mpuuzi na muongo wa kutisha sana! hayo majivuno na majigambo yasiyo na maana wala ukweli wapelekee watu wako wa kwenye mihadhara yako ambao wanakuona kama mtume wao. TANU ilikuwa "mass party"ikiwahusisha watanganyika wengi sana ambao kwa kila siku waliongezeka idadi. Iweje wewe useme ni wewe pekee ndie unayejua historia ya uhuru.?
Mara ngapi humu jamvini umeoneshwa uongo na uzandiki wako, na wewe kwa aibu sana ukaishia kudai kuwa umeandika historia ya wazee wako na hivyo wengine waandike ya kwao? vipi sasa unakuja na majivuno ya kipumbavu ati wewe pekee ndie unayejua historia ya uhuru?
Unakuja na swali la kipumbavu ati "ninani hapa jamvini aelezae historia ya TANU?", Mohamed, mara hii umesahau kuwa ulidai kuwa uliandika historia ya wazee wako waliosahauliwa na sio historia ya TANU? umekosa mshipa wa aibu katika umri wako mkubwa? Mara ngapi umeoneshwa ushiriki wa watu wengine nje ya Gerezani na Tandamti katika harakati za TANU kupigania uhuru ukabaki ni vilio vya kipumbavu vya historia ya wazee wako?
Mohamed Said, nakwambia wazi kabisa kwamba wewe huna unalolijua kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyiaka zaidi ya uzandiki, uzushi, uongo, uchochezi, fitina, majungu na kuwakatisha tamaa vijana wa kiislam wa Tanganyika wasijiamini ili wewe uwatumie katika kujipatia umaarufu wakipumbavu ambao kwa umri wako mkubwa hautakuwa na manufaa yoyote zaidi ya kuchukiwa na wapenda amani wa nchi hii.
 

Dah sawa mkubwa sio makosa yako ni aliyekuleta mjini
 


Mwanzoni pale nilipata huzuni na kuhisi ya kwamba utatuacha na kuondoka zako,ila nimefarijika kwa uwepo wako hadi dakika hii,kwa kweli mengi nimenufaika kwa elimu yako,,

Nawaonea huruma hao aliowasema boko haramu wanaojaribu kupiga kichwa ukuta na kuishia kuusikitikia ukuta badala ya kusikitikia vichwa vyao..
Hawakuwezi na hawatakuweza..
 

inaonekana umeshindwa kuelewa point niliyokuwa najaribu kuionesha; Mwalimu wenu hapa wa mantiq amesema wanaokula matunda ya Uhuru ni "nyinyi peke yenu"; manake ni kuwa hakuna Muislamu anayefurahia matunda ya Uhuru isipokuwa Wakristu. Kwenye mantiq ukiweza kuonesha inconsistency kwenye moja basi hoja nzima inaanguka isipokuwa kama imekuwa qualified. MS hajui kuqualify sentensi ndio maana nimesema mahali huko nyuma huyo aliyemfundisha Mantiq angecharazwa viboko!

Lakini la pili ni kuwa utaona nimewataja wale tu ambao wamejitambulisha na kuonesha imani yao ni Waislamu; Dau, Kikwete na wengine sijawasingizia; wamejitambulisha hivyo hadharani na wengine tunafahamu historia yao katika harakati hizi za kupinga 'dhulma' huku wao wakila na kufurahia matunda ya uhuru! Lakini kama wanaokula matunda ya Uhuru ni Wakristu 'peke' yao basi hawa wengine wote ambao wanajitambulisha kuwa ni Waislamu na wanakula matunda ya Uhuru kwa hakika si Waislamu bali ni Wakristu waliojifisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…