Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kwamjibu wa shutuma za Mohamed Said na wamuungao mkono, ni DHULUMA ya waslamu na uislamu Tanzania,

Wanadai Mzee Nyerere ndie aliwatendea, lakini hapohapo ukiwasikiliza kwa umakini huku ukiwadadisi wanasema leo serikali inawadhulumu, chakushangaza zaidi nikuwa hapa hawamtaji Kikwete kama yeye!
 

Itafurahisha na kusaidia mjadala huu ikiwa ataleta hapa tujue mbinu wazifanyazo NECTA kuwadhulumu waislamu.
 
Ni kama inatumika nguvu kubwa kupingana na MS. Ye katukumbusha tu baadhi ya wapigania uhuru walosahaulika, Hilo ni jema, jema sana.
 
mpaka sasa mjadala huu,wanaompinga Mohamed Said wameshindwa kuleta ushahidi wa wanachotetea.Kilichobaki wanajifunza toka kwake kwa kuuliza maswali kadha wa kadha.Ni vizuri mumtafute mkasome zaidi hapa mnakosa mengi toka kwake.Yeye ni bahari ya historia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umenikumbushia mbali sana. Iraq information minister Muhammad Saeed al-Sahhaf na meneno yake yalitufurahisha sana wakati ule wa vita vya Iraq. '...the Americans were committing suicide by the hundreds at the city's gates..' huku picha nyuma yake zikionyesha hali tofauti kabisa ya kivita. Hata hapa mwenye akili timamu anajua nini kinachoendelea.


[h=1][/h]
 

Umenikumbusha mbali sana mkuu, heheee!

Kiongozi wao Shehe Mohamed Said kawatelekeza hawa vijana hapa jamvini, hawawezi hata kujenga hoja ama kujibu hoja
 
Kipi kinachokufanya uone nimewatelekeza?

Kuhusu Sheikh Issa Amir.
Nimepita kwa wengi.

Jina hili hawajapatapo kulisikia hata kwa masheikh
wa pembezoni.

Wengi wanadhani pana makosa kwa yule alopokea jina
kwa mara ya kwanza.

Wanadhani huyo atakuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir.
Lakini Sheikh Hassan alihamia Tanganyika mwaka 1940.

Alikuwa na umri wa miaka 60.

Hebu pitia upya kumbukumbu zako.
 
Haitawezekana kwa sasa.

Katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam cha wadau wa
elimu Waislam hawakuruhusiwa hata na karatasi moja kutokanayo
nje ya ukumbi.
 
1. Mzee Said unafikiri rais Kikwete na Dr Bilal wamechukua hatua za msingi kuondoa dhulma dhidi ya Waislamu?

2. Utawala wa CCM chini ya Kikwete unaweza kusema ni rafiki mzuri kwa Waislamu kuliiko utawala wa CCM chini ya Nyerere?

3. Je serikali ya Kikwete kuendelea kufanya kazi na BAKWATA (iliyoanzishwa na Nyerere) hakuendelezi dhulma ile ile dhidi ya Uislamu na uongozi wake?
 
Waislam duniani kote hata kwenye nchi zinazoongozwa kiislam wanalalamika wanaonewa..vitendo vya kujitoa mhanga ni dalili tosha ya kukata tamaa na kuona hamna njia zaidi.

Mtamaliza mda wenu mwingi kujenga hoja ila nawahakikishia hili ni swala la kiroho( spiritual) . Waislam walio salama na wanaoishi kwa amani ni wale waliopo kwenye nchi zenye wakristu wengi.

The same to palestina and israel. It will be like that till the end. Mpaka leo waislam hawajajua chanzo cha matatizo yao na solution ni nini.

Swali rahisi kwa waislam: Ni nani msemaji wa waislam duniani, ni nani msemaji wa waislam TANZANIA?
 
Ninashangaa Mohamed kashikia bango baadhi ya watu walioachwa ama kusahaulika kwenye historia ya uhuru!

Sasa nikukumbushe tu kuwa yapo mambo MUHIMU na ya maana sana ambayo hayatajwi wala kusemwa kwenye historia ya nchi hii:

Mfano: Maasi ya 1964,

Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.

Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say za akina Mohamed Said

Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi, Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo, hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.

Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia. Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona.

Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha Kigamboni. Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.

Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu.

Askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwanyakati tofauti kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.

Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari (makomandoo) wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta. Upinzani mkali waliupata kutoka kambi za jeshi kule Tabora ambapo mapigano ya yalichua karibu siku mbili kabla ya majeshi ya waasi Tanganyika kusalimu amri.

Walifanikiwa kutuliza maasi yale, na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi, ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wanamheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.

Kisha ukaja uasi wa mwaka 1982

lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Haya Mohamed kwanini haya hayatajwi kwenye historia ya nchi yetu?

Mwalimu angekuwa mpenda sifa na mchoyo wakutaka kila kitu kiwe yeye unadhani haya ambayo mimi nayaona ni muhimu kuliko madai yako angeyaacha yapite tu bila kutafutia umaarufu zaidi?
 
Maswali hayo kwa kweli si yangu kuulizwa.

Mimi naomba mniulize yaliyotokea wakati wa kupigania uhuru wa
Tanganyika.

Sababu yake ni kuwa ukumbi utapata ile historia ambayo si wengi wakiijua.

Hayo mengine ya Kikwete kwa kweli sina ujuzinayo.
 
Bahati mbaya hujaniskia nikizungumza kwengine inapofika wakati wa maswali
na majibu.

Mimi husema kuwa nastaajabishwa na Nyerere kuwa hili la yeye kuhusishwa na
kuasisi TANU kama ni yeye peke yake lilimkaa sana kiasi kwamba hakutaka hata
Abdu Sykes atajwe pamoja na yeye katika historia ya TANU.

Nyerere ana sifa nyingi sana kama ulivyoonyesha hapo lakini hizo zote inaelekea
hakuzipenda sana kama kuambiwa yeye ndiye aliyeasisi TANU.

Huu ndiyo muhali maana TANU chanzo chake ni AA na waasisi wake wanajulikana.
Nyerere kaja Dar es Salaam 1952 kamkuta Abdu Sykes na wenzake wako katika
mchakato wa kuunda TANU.

Iweje haya yote yageuke yawe yake?
Hili ndilo tatizo likapelekea kuandikwa historia ya TANU na Chuo Cha Kivukoni.

Matokeo ya kitabu kile sote tunayajua.
Hakikuwa kitabu cha historia ya TANU.
 
Maswali hayo kwa kweli si yangu kuulizwa.
Mimi naomba mniulize yaliyotokea wakati wa kupigania uhuru wa
Tanganyika.Sababu yake ni kuwa ukumbi utapata ile historia ambayo si wengi wakiijua.
Hayo mengine ya Kikwete kwa kweli sina ujuzinayo.
Mohamed, kwani EAMWS iliuawa wakati wa kupigania uhuru! mbona unaiongelea.

Hivi tatizo la namba za mitihani lilianza wakati wa kupigania uhuru, si wewe Mohamed uliyelileta kwa kusema lilikuwa halijulikani(ingawa umekiri ulikuwa uzushi)
NECTA haikuwepo wakati wa uhuru, si wewe unayepiga zumari kuhusu madhaila yake kila uchao.

Lingekuwa la Nyerere tungejibiwa hadi maongezi ya Malima na Nyerere ambayo yaliisha tu baada ya Mwalimu kutoa picha za waislam!

Hapa ndipo tunasema historia haiandikwi kwa kuchagua washiriki, nyakati na matukio.
Dhulma ya mwaka 1968 Mohamed anaijua kuliko yale ya Kikwete na Bilal.

MM amekimbia kwasababu maswali yanahusu wazee wake, tatizo la ngano ikikumbana na ukweli shida tupu.
 
Wana Jamvi, mimi mtanisamehe kwa sababu kubwa moja...napenda ukweli na sina uvumilivu na mtu ambaye kwa hali yoyote ile sina jina linalomfaa zaidi ya mchochezi kama alivyo Mohamed Said. Kwa kuendelea kujadiliana naye bila kutambua tunajadiliana na mtu hatari ambaye lengo lake hasa ni kuleta uchochezi kwa kupanda chuki baina ya Watanzania wenye imani tofauti na hivyo kuhatarisha usalama nchini tutakuwa hatulitendei haki taifa letu. Ni kweli kama anavyodai Mohamed Said, hii sumu ameweza kuieneza kwa kipindi kirefu bila upinzani na hivyo uwongo wake umeweza kuaminiwa kuwa ni kweli na Watanzania wachache wenye uelewa mdogo kama tunavyoshuhudia kwa mashabiki wake humu ndani.

AA anayodai ilianzishwa na Wazee wake mwaka 1929 haikuasisiwa kwa malengo ya kisiasa na wala kwa misingi ya dini. Baada ya vita vya pili mwaka 1918 na Wajerumani kushindwa, wazee wa Mohamed Said ambao hasa walikuwa walowezi walioletwa Tanganyika kwa lengo la kuwakandamiza wazawa waligundua mapema kuwa siku zao za kuneemeka kama manamba wa kijerumani zimefika mwisho. Kwao, ushindi wa Muingereza, ulikuwa pigo kubwa kwa maslahi yao na hawakuupa ushirikiano kama walivyoupa utawala wa mkoloni, Ujerumani. Lakini tofauti na wazawa hasa Watanganyika, ukoloni ulianza kupigwa vita siku nyingi tu uwe wa Mwingereza au Mjerumani.

Mathalani AA ilianzishwa na wafanya kazi wa serikali, lakini hadi wakati huo kulikuwa tayari na vyama vya wakulima ambavyo kwa hasa ndivyo vilikuwa chimbuko la vugu vugu la mwamko dhidi ya utawala wa kikoloni. Kwa mifano miwili tu; katika jimbo la Ziwa BU (Buhaya Union) ilianzishwa mwaka 1924 ikiongzwa na Klemens Kiiza , katika jimbo la Kaskazini KNPA (Kilimanjaro Native Planters Union) ilianzishwa mwaka 1925 ikiongozwa na Joseph Melingo na kila sehemu ya nchi ni vyama vingi tu vilianzishwa kabla AA ya Dar es Salaam. Kwa wafanya kazi wa serikali huko Tanga TTACSA (Tanganyika Territory African Civil Service Association) ilianzishwa mwaka 1922 ikiongozwa na Martin Kayamba. Hii ni mifano michache tu.

Baadaye sana AA ya Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 1929 ikiongozwa na Cecil Matola.

Lengo la hivi vyama vyote ilikuwa ni kuwaunganisha Watanganyika waafrika bila kujali dini zao...halafu miaka 60 baadaye anakuja kutokea mchochezi anahubiri chuki kwa lengo la kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini! Huyu mtu si wa kumchekea, ni adui wa Taifa kwa maana yake halisi na ni jukumu la kila Mtanzania mpenda amani kumkemea na kumpiga vita kwa nguvu zile zile wazee wetu walizitumia kumpinga mkoloni aliyetaka kutugawa kikabila lakini akashindwa. Mohamed Said amepata kilichoitwa "free ride" kwa kipindi kirefu kwa watu kukaa kimya lakini nawashukuru wazalendo wote ambao wameamua sasa kukomaa naye kwa uwongo na chuki anazozipandikiza kwa kivuli cha dini.

Tuendelee...
 
Hayo mambo ya maana sina ugomvi nayo unaweza kuyaweka
hapa jamvini tutayazungumza.

Kwangu mimi jambo kubwa lilikuwa kuandika historia ya TANU.
Nashukuru nimeiandika na leo hii tunaizungumza humu ukumbini.

Nashukuru pia kitabu kinasomeshwa vyuo vikuu Marekani na Ulaya.
Nashukuru kuwa maktaba kubwa za dunia kwenye katalogi ya Africa,
Islam, Politics kitabu changu utakikuta na jina la Mohamed Said utaliona.

Kwangu mimi hili ndilo jambo kubwa na la maana.
 

Maelezo yako yanaonyesha wazi kuwa unathubutu kutujuza kuwa Mwalimu Nyerere alikuja Dar 1952 ndipo akaifahamu, akaijua na akajiunga na TAA.

Maswali:

Kule Tabora Mwalimu Nyerere alikuwa Katibu wa chama gani kabla ya kuhamia misheni Pugu?

Kama ni TAA unatuambiaje Nyerere aliijulia TAA Dar? Na unatuthibitishiaje kuwa Abdu ndie aliyemkaribisha Dar na kumwingiza TAA rasmi?
 
Nikuambie kitu?

Umeandika vizuri lakini tatizo una ghadhabu na hilo
Limekufanya utumie lugha ya matusi.

Katika anga za kisomi hii inakuondolea kila kitu cha maana.
Mimi babu yangu kaingia Tanganyika na jeshi la Wajerumani
kama askari na alikuwa Shirati bomani.

Hakuwa manamba.
Hizi ndizo athari za ukoloni.

Sykes Mbuwanie, Afande Plantan na wao waliingia Tanganyika
kutoka Mozambique na Wajerumani chini ya uongozi wa Hermann
von Wissman.

Hawa walikuwa Pangani na baada ya kushiriki katika vita vya Bushiri
Bin Salim wakaenda Kalenga kupambana na Mkwawa.

Unaweza kusema kuwa walikuja kukandamiza Waafrika kama jeshi
la mamluki.

Huo ni msimamo pia.
Mimi naheshimu fikra zako na nina majibu ya kukupa.

Juu ya hawa wazee wangu kuwa watoto wa ''wakandamizaji''chini ya
Wajerumani lakini watoto wao walikuja kufanya makubwa dhidi ya ukoloni.

Kleist ndiyo huyo kafanya makubwa sana kiasi huwezi kuandika historia ya
TANU bila ya kumtaja yeye na wanae.

Babu yangu Salum Abdallah yeye alikuwa katika kamati ya siri ya TAA Tabora
iliyokuwa ikiratibu harakati pale New Street na 1955 akawa rais muasisi wa
Tanganyika Railway African Union (TRAU).

TRAU ilipigana bega kwa bega na TANU dhidi ya ukoloni.

Jitulize andika kwa utulivu na kwa busara.
Huu si ugomvi ni mahali tunashindanisha hoja.

Hapana haja ya kutukana.

Tuendelee...
 
Hapana sikimbii maswali.
Huwa sijibu kila kitu.

Ikiwa kitu sijui nasema hili sina ujuzi nalo.
Ikiwa nje ya maudhui huwa sisemi kitu.

Kipi cha kufanya nitimue mbio ilhal haya
Ni mazungumzo tu?

Kutumia lugha ya ukumbini ndiyo maana
sitokwi na povu.

Situkani mtu.
 
Maswali hayo kwa kweli si yangu kuulizwa.

Mimi naomba mniulize yaliyotokea wakati wa kupigania uhuru wa
Tanganyika.

Sababu yake ni kuwa ukumbi utapata ile historia ambayo si wengi wakiijua.

Hayo mengine ya Kikwete kwa kweli sina ujuzinayo.

Huna ujui nayo au hutaki kuonekena unamshambulia Muislamu mwenzako? Hivi siyo serikali ya Shein na Kikwete (wote Waislamu) waliowafunga mashehe wa Kiislamu? Leo hii rafiki yako wa karibu Shehe Ponda Issa Ponda siyo yuko jela kwa sababu ya amri za Kikwete, Mwema na Othman (wote Waislamu)?

Na umekuwa ukizungumzia dhulma dhidi ya Waislamu leo hii unataka kutuambia kuwa Dhulma hiyo haipo? Maana kama haipo na Waislamu leo wanaishi wakifurahia matunda ya uhuru kama Wakristu?

Wengine tumeweza kuwaandika hawa kina Sykes na kuwataja kwa majina - kutokana na mazungumzo yetu na wewe - lakini hatukuishia kwao tu tukakumbusia wazee wetu wote (bila kujali dini zao). Leo Ikulu imewapa nishanibaadhi yao na marehemu Regia Mtema akaingiza majina yao kwenye hotuba yake kuhusu masuala ya kazi - kuna hata aliyemshukuru Binti yule kutaja majina ya wazee hawa Bungeni?

Leo wengine tumetoa pendekezo la kuundwa kwa Tume ya Historia na Ukweli ili taarifa za wazee wetu wote wa kila kona ya nchi na wale wote walioshiriki katika kupigania uhuru itengenezwe rasmi na waheshimiwe wote nani katuunga mkono? Badala ya kujaribu kuangalia historia kwa mwanga wa dini sisi wengine tunataka kuangalia historia yetu kwa maana ya ujumla wake wote maana ukisema hivyo unaweza kufikiria watu pekee walioshiriki harakati za Uhuru walikuwa ni Waislamu.

Kuna Wahindi ambao watu hata majina yao hawayajui kabisa na walitoa mchango mkubwa sana kwa TANU lakini sidhani kama utasikia Wahindi wanasema wanadhulumiwa au wazee 'wao' wamesahauliwa.

Swali langu hili naweza kusema linasimama: Je, Dhulma dhidi ya Uislamu na Waislamu leo hii zimekoma Tanzania? Nakuuliza hili kwa sababu umekuwa ukijipambanua kama unapigania haki za Waislamu; utanishangaza ukisema kuwa hiili huna ujuzi nalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…