Ninashangaa Mohamed kashikia bango baadhi ya watu walioachwa ama kusahaulika kwenye historia ya uhuru!
Sasa nikukumbushe tu kuwa yapo mambo MUHIMU na ya maana sana ambayo hayatajwi wala kusemwa kwenye historia ya nchi hii:
Mfano: Maasi ya 1964,
Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.
Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say za akina Mohamed Said
Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi, Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo, hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.
Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia. Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona.
Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha Kigamboni. Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.
Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu.
Askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwanyakati tofauti kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.
Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari (makomandoo) wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta. Upinzani mkali waliupata kutoka kambi za jeshi kule Tabora ambapo mapigano ya yalichua karibu siku mbili kabla ya majeshi ya waasi Tanganyika kusalimu amri.
Walifanikiwa kutuliza maasi yale, na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi, ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wanamheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.
Kisha ukaja uasi wa mwaka 1982
lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,
Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!
Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,
Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,
Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!
Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,
akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa
"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"
jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema
"nimewasamehe wote"
na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!
Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!
Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.
Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!
Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,
Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa
Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!
Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!
Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!
Haya Mohamed kwanini haya hayatajwi kwenye historia ya nchi yetu?
Mwalimu angekuwa mpenda sifa na mchoyo wakutaka kila kitu kiwe yeye unadhani haya ambayo mimi nayaona ni muhimu kuliko madai yako angeyaacha yapite tu bila kutafutia umaarufu zaidi?