Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hayo mambo ya maana sina ugomvi nayo unaweza kuyaweka
hapa jamvini tutayazungumza.
Kwangu mimi jambo kubwa lilikuwa kuandika historia ya TANU.
Nashukuru nimeiandika na leo hii tunaizungumza humu ukumbini.
Nashukuru pia kitabu kinasomeshwa vyuo vikuu Marekani na Ulaya.
Nashukuru kuwa maktaba kubwa za dunia kwenye katalogi ya Africa,
Islam, Politics kitabu changu utakikuta na jina la Mohamed Said utaliona.
Kwangu mimi hili ndilo jambo kubwa na la maana.
Kusema kweli kuwa hili ni jambo kubwa nadhani haiingii kichwani vizuri. Jambo kubwa ni kueleza ukweli. Huwezi kupima mafanikio ya kazi zako kwa kuanglaia wapi zinasomwa kwa sababu kusomwa peke yake au kukubaliwa maandishi yako siyo kipimo cha ukweli wa maandishi hayo. Kwenye library kuna vitabu vya kila namna na hilo peke yake si kipimo cha ukweli wa maandishi ya vitabu hivyo. Wanatarajia wasomaji wataweza kuvipima wao wenyewe na maandishi mengine.
Itakuwa ni ukosefu wa hekima kama mtu anachukua kitabu chake na kukisoma kama kitabu pekee kinachoeleza ukweli wote. Hakiwezi kuwa hivyo na kwa kweli wewe mwenyewe umesema siyo cha kuandika ukweli wote; ni ukweli kutokana na simulizi la wazee wako. Na kwa mtu msomi au aliyejua kidogo kusoma vitabu vya kihistoria kitabu chako kwa kweli siyo cha kihistoria kwani hakijafuata kanuni za uandishi wa sayansi ya historia.
Sidhani hata kama wewe mwenyewe ndugu yangu unajitambulisha kama mwanahistoria.