Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hayo mambo ya maana sina ugomvi nayo unaweza kuyaweka
hapa jamvini tutayazungumza.

Kwangu mimi jambo kubwa lilikuwa kuandika historia ya TANU.
Nashukuru nimeiandika na leo hii tunaizungumza humu ukumbini.

Nashukuru pia kitabu kinasomeshwa vyuo vikuu Marekani na Ulaya.
Nashukuru kuwa maktaba kubwa za dunia kwenye katalogi ya Africa,
Islam, Politics kitabu changu utakikuta na jina la Mohamed Said utaliona.

Kwangu mimi hili ndilo jambo kubwa na la maana.

Kusema kweli kuwa hili ni jambo kubwa nadhani haiingii kichwani vizuri. Jambo kubwa ni kueleza ukweli. Huwezi kupima mafanikio ya kazi zako kwa kuanglaia wapi zinasomwa kwa sababu kusomwa peke yake au kukubaliwa maandishi yako siyo kipimo cha ukweli wa maandishi hayo. Kwenye library kuna vitabu vya kila namna na hilo peke yake si kipimo cha ukweli wa maandishi ya vitabu hivyo. Wanatarajia wasomaji wataweza kuvipima wao wenyewe na maandishi mengine.

Itakuwa ni ukosefu wa hekima kama mtu anachukua kitabu chake na kukisoma kama kitabu pekee kinachoeleza ukweli wote. Hakiwezi kuwa hivyo na kwa kweli wewe mwenyewe umesema siyo cha kuandika ukweli wote; ni ukweli kutokana na simulizi la wazee wako. Na kwa mtu msomi au aliyejua kidogo kusoma vitabu vya kihistoria kitabu chako kwa kweli siyo cha kihistoria kwani hakijafuata kanuni za uandishi wa sayansi ya historia.

Sidhani hata kama wewe mwenyewe ndugu yangu unajitambulisha kama mwanahistoria.
 
Mathalani AA ilianzishwa na wafanya kazi wa serikali, lakini hadi wakati huo kulikuwa tayari na vyama vya wakulima ambavyo kwa hasa ndivyo vilikuwa chimbuko la vugu vugu la mwamko dhidi ya utawala wa kikoloni. Kwa mifano miwili tu; katika jimbo la Ziwa BU (Buhaya Union) ilianzishwa mwaka 1924 ikiongzwa na Klemens Kiiza , katika jimbo la Kaskazini KNPA (Kilimanjaro Native Planters Union) ilianzishwa mwaka 1925 ikiongozwa na Joseph Melingo na kila sehemu ya nchi ni vyama vingi tu vilianzishwa kabla AA ya Dar es Salaam. Kwa wafanya kazi wa serikali huko Tanga TTACSA (Tanganyika Territory African Civil Service Association) ilianzishwa mwaka 1922 ikiongozwa na Martin Kayamba. Hii ni mifano michache tu.

Baadaye sana AA ya Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 1929 ikiongozwa na Cecil Matola.

Mzee mwenzangu; usidhani tunaandika haya ili kumjibu Mohammed Said; tayari kwa kiasi kikubwa mionngoni mwa wasomi wa Tanzania na vijana wetu hoja zake zimeshaonekana hazina ukweli wa historia na zimeoneshwa hazina credibility. Tumeweza kuwaonesha vijana wetu wa Kitanzania makosa ya hoja za Bw. Said na kwanini baada ya kuachwa kwa muda mrefu zimevutia watu wasiopenda kutafuta ukweli. Hivyo, tunavyoandika si kwa ajili ya kumshawishi Bw. Said abadili msimao wake la hasha; bali kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu na watu wengine kuuliza maswali ya msingi kila wanapomsikia anazungumza; tunawafundisha jinsi ya kuhoji hoja na kupima ukweli wa hoja kwa kutumia mantiki.

Mfano wa wazee uliotoa hapo waliojifunza historia ya Tanganyika kabla ya uhuru watakutana na majina hayo yote - pamoja na ya wazee wa Dar. Watu waliosoma watakutana na migomo ya Pare, mambo ya ardhi ya Mwanza, n.k Watajifunza kuwa harakati za uhuru hazikuanzia Dar wala hazikufanywa na wazee wa Dar peke yao na wala wazee wa Dar hawakuwa na ile nafasi ya kipekee ambayo Bw. Said amewaaminisha watu wa Dar waamini wazee wao walikuwa nayo.

Leo hii histohisia ya Bw. Said imeanza kujibiwa vizuri, kusahihishwa na tumeweza kuonesha pasi ya shaka kuwa hawezi kujibu maswali ya msingi sana katika historia. Tumeweza kuwaonesdha watu kuwa wanachosoma katika maandishi ya Bw. Said siyo historia hata kidogo ni hisia zake kutokana na msimamo wake wa kidini. Kwamba, anaanglaia historia ya nchi yetu kwa mwanga wa "sisi dhidi ya wao" - sisi akimaanisha "Waislamu" na wao akimaanisha "Wakristu".

Ni jukumu letu kuwasaidia vijana wetu kuchambua ukweli kidogo uliofichika katika maandishi ya Bw. Said na hisia nyingi (zisizoweza kuthibitishwa na ukweli) ambazo zimejazana katika kurasa mbalimbali. Kwa mfano, mwandishi anaponukuu maandishi yake yeye mwenyewe kuthibitisha madai yake na kufanya watu waamini ni kweli basi ni tatizo. Kwa mfano, kila ukimuuliza maswali ananukuu kutoka maandishi yake kama ushahidi wa madai yake hili haliwezi kuwa jambo zuri.
 
acha kulazimisha ajibu unavyotaka wewe.Nimeona post zako juu ya Mohamed Said unamshutumu sana kuhusu udini.Jitulize angalia nawe unachotetea na unaowatetea hakina udini.mmeshindwa kupinga anachosma kuhusu historia ya uhuru mnaanza habari za kikwete
Huna ujui nayo au hutaki kuonekena unamshambulia Muislamu mwenzako? Hivi siyo serikali ya Shein na Kikwete (wote Waislamu) waliowafunga mashehe wa Kiislamu? Leo hii rafiki yako wa karibu Shehe Ponda Issa Ponda siyo yuko jela kwa sababu ya amri za Kikwete, Mwema na Othman (wote Waislamu)?

Na umekuwa ukizungumzia dhulma dhidi ya Waislamu leo hii unataka kutuambia kuwa Dhulma hiyo haipo? Maana kama haipo na Waislamu leo wanaishi wakifurahia matunda ya uhuru kama Wakristu?

Wengine tumeweza kuwaandika hawa kina Sykes na kuwataja kwa majina - kutokana na mazungumzo yetu na wewe - lakini hatukuishia kwao tu tukakumbusia wazee wetu wote (bila kujali dini zao). Leo Ikulu imewapa nishanibaadhi yao na marehemu Regia Mtema akaingiza majina yao kwenye hotuba yake kuhusu masuala ya kazi - kuna hata aliyemshukuru Binti yule kutaja majina ya wazee hawa Bungeni?

Leo wengine tumetoa pendekezo la kuundwa kwa Tume ya Historia na Ukweli ili taarifa za wazee wetu wote wa kila kona ya nchi na wale wote walioshiriki katika kupigania uhuru itengenezwe rasmi na waheshimiwe wote nani katuunga mkono? Badala ya kujaribu kuangalia historia kwa mwanga wa dini sisi wengine tunataka kuangalia historia yetu kwa maana ya ujumla wake wote maana ukisema hivyo unaweza kufikiria watu pekee walioshiriki harakati za Uhuru walikuwa ni Waislamu.

Kuna Wahindi ambao watu hata majina yao hawayajui kabisa na walitoa mchango mkubwa sana kwa TANU lakini sidhani kama utasikia Wahindi wanasema wanadhulumiwa au wazee 'wao' wamesahauliwa.

Swali langu hili naweza kusema linasimama: Je, Dhulma dhidi ya Uislamu na Waislamu leo hii zimekoma Tanzania? Nakuuliza hili kwa sababu umekuwa ukijipambanua kama unapigania haki za Waislamu; utanishangaza ukisema kuwa hiili huna ujuzi nalo.
 
Last edited by a moderator:
mzee mwenzangu; usidhani tunaandika haya ili kumjibu mohammed said; tayari kwa kiasi kikubwa mionngoni mwa wasomi wa tanzania na vijana wetu hoja zake zimeshaonekana hazina ukweli wa historia na zimeoneshwa hazina credibility. Tumeweza kuwaonesha vijana wetu wa kitanzania makosa ya hoja za bw. Said na kwanini baada ya kuachwa kwa muda mrefu zimevutia watu wasiopenda kutafuta ukweli. Hivyo, tunavyoandika si kwa ajili ya kumshawishi bw. Said abadili msimao wake la hasha; bali kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu na watu wengine kuuliza maswali ya msingi kila wanapomsikia anazungumza; tunawafundisha jinsi ya kuhoji hoja na kupima ukweli wa hoja kwa kutumia mantiki.

Mfano wa wazee uliotoa hapo waliojifunza historia ya tanganyika kabla ya uhuru watakutana na majina hayo yote - pamoja na ya wazee wa dar. Watu waliosoma watakutana na migomo ya pare, mambo ya ardhi ya mwanza, n.k watajifunza kuwa harakati za uhuru hazikuanzia dar wala hazikufanywa na wazee wa dar peke yao na wala wazee wa dar hawakuwa na ile nafasi ya kipekee ambayo bw. Said amewaaminisha watu wa dar waamini wazee wao walikuwa nayo.

Leo hii histohisia ya bw. Said imeanza kujibiwa vizuri, kusahihishwa na tumeweza kuonesha pasi ya shaka kuwa hawezi kujibu maswali ya msingi sana katika historia. Tumeweza kuwaonesdha watu kuwa wanachosoma katika maandishi ya bw. Said siyo historia hata kidogo ni hisia zake kutokana na msimamo wake wa kidini. Kwamba, anaanglaia historia ya nchi yetu kwa mwanga wa "sisi dhidi ya wao" - sisi akimaanisha "waislamu" na wao akimaanisha "wakristu".

Ni jukumu letu kuwasaidia vijana wetu kuchambua ukweli kidogo uliofichika katika maandishi ya bw. Said na hisia nyingi (zisizoweza kuthibitishwa na ukweli) ambazo zimejazana katika kurasa mbalimbali. Kwa mfano, mwandishi anaponukuu maandishi yake yeye mwenyewe kuthibitisha madai yake na kufanya watu waamini ni kweli basi ni tatizo. Kwa mfano, kila ukimuuliza maswali ananukuu kutoka maandishi yake kama ushahidi wa madai yake hili haliwezi kuwa jambo zuri.

mimi nilitaraji kuona yakipingwa yale yaliyoandikwa kwa ushahidi mbadala,kwa maana ya kwamba nilikuwa natarajia wenye hekima kama ninyi mje sasa mseme hapo moh' said ulichoandika sicho,na kinachopaswa kuandikwa ni hiki,lakin cha kushangaza ama kustaajabu sion kitu hicho,pia si haki kuzungumzia maono ya watu wengine kwa kuyafanyia conclusion,wapo ambao hamjayaamin pia tupo wengi ambao tumeyaamini pasi na ushawish wowote wa kiimani katika maandishi yale,bali kwa fact zilizomo.
 
acha kulazimisha ajibu unavyotaka wewe.nimeona post zako juu ya mohamed said unamshutumu sana kuhusu udini.jitulize angalia nawe unachotetea na unaowatetea hakina udini.mmeshindwa kupinga anachosma kuhusu historia ya uhuru mnaanza habari za kikwete

hata namimi namshangaa kwa kweli,na ukiona mtu kaacha kuzijibu hoja na kukimbilia kumwandama mtoa hoja basi ujue ni ishara tosha ya kuishiwa hoja za mtu husika
 
hili ndo tatizo lenu wagala,kuhamisha hoja,angalia maswali yako na mjadala ulioko ukumbini.Akili na fikra zako zemekaa kidini dini sana.Kila
1. Mzee Said unafikiri rais Kikwete na Dr Bilal wamechukua hatua za msingi kuondoa dhulma dhidi ya Waislamu?

2. Utawala wa CCM chini ya Kikwete unaweza kusema ni rafiki mzuri kwa Waislamu kuliiko utawala wa CCM chini ya Nyerere?

3. Je serikali ya Kikwete kuendelea kufanya kazi na BAKWATA (iliyoanzishwa na Nyerere) hakuendelezi dhulma ile ile dhidi ya Uislamu na uongozi wake?
 
mimi nilitaraji kuona yakipingwa yale yaliyoandikwa kwa ushahidi mbadala,kwa maana ya kwamba nilikuwa natarajia wenye hekima kama ninyi mje sasa mseme hapo moh' said ulichoandika sicho,na kinachopaswa kuandikwa ni hiki,lakin cha kushangaza ama kustaajabu sion kitu hicho,pia si haki kuzungumzia maono ya watu wengine kwa kuyafanyia conclusion,wapo ambao hamjayaamin pia tupo wengi ambao tumeyaamini pasi na ushawish wowote wa kiimani katika maandishi yale,bali kwa fact zilizomo.

HIvi unatusoma kweli? Mbona tumeweka ushahidi mzito tu?

  • Mohammed Said anasema Nyerere alianza siasa mwaka 1953 tumemuonesha si KWELI alianza siasa tangu 1947
  • Mohammed Said anasema Nyerere aliamua kuingia siasa baada ya kushauriwa na kina Dossa; tumeonesha si kweli Nyerere aliamua kuingia full time politics akiwa Uingereza (kwa maneno yake Nyerere mwenyewe)
  • Mohammed Said amesema kuwa waliosahauliwa ni wazee wa Kiislamu kwa sababu ya Uislamu wao; tumeonesha kuwa waliosahauliwa katika historia ni pamoja Wakristu wengi tu - hatukusema kwa sababu ya Ukristu wao!
  • Mohammed Said amedai kuwa Nyerere aliwadhulumu Waislamu; tumeonesha kuwa hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wa kkuonesha ilo ila upo ushahidi wa kutosha kuwa Nyerere alikuwa ni rafiki mzuri wa Waislamu na Uislamu Tanzania
  • Mohammed Said amejaribu kkuonesha kuwa maamuzi mbalimbali ya utawala yaliyogusa maslahi ya Waislamu wakati wa Nyerere yalisababishwa na udini wa Nyerere lakini tumeonesha kuwa maamuzi kama hayo yamechukuliwa na viongozi wa Waislamu kama Mwinyi na Kikwete lakini haamini ni kwa sababu wanataka kudhulumu Uislamu (double standard)

Unataka tupinge vipi? Tumempinga kwa facts, tumempinga kwa mantiki, na tumempinga kwa ushahidi na hajawahi kukanusha kusema tumesema uongo. Amekubali na kuheshimu mawazo yetu - yaani ameshindwa kuyapinga.
 
Mzee mwenzangu; usidhani tunaandika haya ili kumjibu Mohammed Said; tayari kwa kiasi kikubwa mionngoni mwa wasomi wa Tanzania na vijana wetu hoja zake zimeshaonekana hazina ukweli wa historia na zimeoneshwa hazina credibility. Tumeweza kuwaonesha vijana wetu wa Kitanzania makosa ya hoja za Bw. Said na kwanini baada ya kuachwa kwa muda mrefu zimevutia watu wasiopenda kutafuta ukweli. Hivyo, tunavyoandika si kwa ajili ya kumshawishi Bw. Said abadili msimao wake la hasha; bali kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu na watu wengine kuuliza maswali ya msingi kila wanapomsikia anazungumza; tunawafundisha jinsi ya kuhoji hoja na kupima ukweli wa hoja kwa kutumia mantiki.

Mfano wa wazee uliotoa hapo waliojifunza historia ya Tanganyika kabla ya uhuru watakutana na majina hayo yote - pamoja na ya wazee wa Dar. Watu waliosoma watakutana na migomo ya Pare, mambo ya ardhi ya Mwanza, n.k Watajifunza kuwa harakati za uhuru hazikuanzia Dar wala hazikufanywa na wazee wa Dar peke yao na wala wazee wa Dar hawakuwa na ile nafasi ya kipekee ambayo Bw. Said amewaaminisha watu wa Dar waamini wazee wao walikuwa nayo.

Leo hii histohisia ya Bw. Said imeanza kujibiwa vizuri, kusahihishwa na tumeweza kuonesha pasi ya shaka kuwa hawezi kujibu maswali ya msingi sana katika historia. Tumeweza kuwaonesdha watu kuwa wanachosoma katika maandishi ya Bw. Said siyo historia hata kidogo ni hisia zake kutokana na msimamo wake wa kidini. Kwamba, anaanglaia historia ya nchi yetu kwa mwanga wa "sisi dhidi ya wao" - sisi akimaanisha "Waislamu" na wao akimaanisha "Wakristu".

Ni jukumu letu kuwasaidia vijana wetu kuchambua ukweli kidogo uliofichika katika maandishi ya Bw. Said na hisia nyingi (zisizoweza kuthibitishwa na ukweli) ambazo zimejazana katika kurasa mbalimbali. Kwa mfano, mwandishi anaponukuu maandishi yake yeye mwenyewe kuthibitisha madai yake na kufanya watu waamini ni kweli basi ni tatizo. Kwa mfano, kila ukimuuliza maswali ananukuu kutoka maandishi yake kama ushahidi wa madai yake hili haliwezi kuwa jambo zuri.

hakika mie ni mmojawapo niliyehadaika na "histohisia" yake;

hakika mnakasha huu umeniemilisha mengi kijana mie wa 90's mungu awabariki
 
Mie sikuja humu kupingana.
Nimeingia humu kueleza habari za wazee wangu.

Habari ambazo nyie hata siku moja hamkupata
kuzisoma popote.

Nani kati yenu alipata kusoma historia ya Sheikh
Hassan bin Amir popote pale?

Si mliona mshtuko mliopata nilipokuambieni TANU
imeasisiwa na Abdulwahid Sykes?

Nani kati yenu alijua mkono wa Nyerere na Kanisa
Katoliki katika kuivunja EAMWS?

Si mnaona hadi sasa hamuamini histori hii?

Lengo la kitabu changu limetimia miaka 15 ilopita.

Siko humu kuchagiza mniamini.
Niko humu kueleza historia ya wazee wangu.

Hilo tu basi.
 
HIvi unatusoma kweli? Mbona tumeweka ushahidi mzito tu?

  • Mohammed Said anasema Nyerere alianza siasa mwaka 1953 tumemuonesha si KWELI alianza siasa tangu 1947
  • Mohammed Said anasema Nyerere aliamua kuingia siasa baada ya kushauriwa na kina Dossa; tumeonesha si kweli Nyerere aliamua kuingia full time politics akiwa Uingereza (kwa maneno yake Nyerere mwenyewe)
  • Mohammed Said amesema kuwa waliosahauliwa ni wazee wa Kiislamu kwa sababu ya Uislamu wao; tumeonesha kuwa waliosahauliwa katika historia ni pamoja Wakristu wengi tu - hatukusema kwa sababu ya Ukristu wao!
  • Mohammed Said amedai kuwa Nyerere aliwadhulumu Waislamu; tumeonesha kuwa hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wa kkuonesha ilo ila upo ushahidi wa kutosha kuwa Nyerere alikuwa ni rafiki mzuri wa Waislamu na Uislamu Tanzania
  • Mohammed Said amejaribu kkuonesha kuwa maamuzi mbalimbali ya utawala yaliyogusa maslahi ya Waislamu wakati wa Nyerere yalisababishwa na udini wa Nyerere lakini tumeonesha kuwa maamuzi kama hayo yamechukuliwa na viongozi wa Waislamu kama Mwinyi na Kikwete lakini haamini ni kwa sababu wanataka kudhulumu Uislamu (double standard)

Unataka tupinge vipi? Tumempinga kwa facts, tumempinga kwa mantiki, na tumempinga kwa ushahidi na hajawahi kukanusha kusema tumesema uongo. Amekubali na kuheshimu mawazo yetu - yaani ameshindwa kuyapinga.

Tatizo ni kubwa kuliko nilivyofikiri.
Nafikiri nyie endeleeni kuandika, wanaotaka kusoma na kielewa watafanya hivyo. Wanaotaka kuangalia maandishi kama picha nao wafanye hivyo pia.
:thumbup:
 
Huko unakokwenda tutaogelea sana.
Hayo yanahitaji uzi maalum.

Hapa tujikite katika historia ya TANU?
Kama hakuna jipya...

Let us call it a day.

Mzee hapa hatusimami kwa TANU tu, tunaangaza historia ya uhuru na wapigania uhuru huo tukitalii kila pembe ya kona za uhuru huo
 
Nishakueleza mara nyingi.
Bila ya nyinyi kunijibu kwa kuandika kitabu...

Itakuwa shida tu.

Kitabu changu kinasomwa vyuo vikuu vyote
vinavyosomesha African history.

Hivi ninavyoandika kitabu kinakwenda toleo la tatu.
Wewe unazungumza kukipinga JF...

Kitabu kipo Oxford, Cambridge, Harvard, Northwestern,
University of Dar es Salaam...

Kweli wewe uko makini kukipinga kitabu changu?
 
Binafsi sioni mantiki ya kutoka mapovu kujadili udini humu. Huyu Mohamed Said namsikia tu akitetea imani yake na kuponda ukristo. Mtu kama huyu akishawekewa ukweli mchache tu na aachwe na ukweli huo. Akiendelea kubisha hata wewe unayebishana nae unaonekana kishoka wa hoja. Mwacheni
 
Yericko Nyerere,

Fanya marekebisho kwenye bandiko lako kuhusu ubalozi wa Marekani Kinondoni.

Historia ya uasi wa mwaka 1982 mbona ipo na inafahamika umesema Mwalimu Nyerere aliwasamehe waliotaka kumpindua. Mie nakumbuka mwaka 1985 Eugene Maganga na wenzake saba Suleiman Kamando, Zakaria Hans Pope, Vitalis Mapunda, Mbogolo, Kajaji Badru, Hatibu Gandhi (Hatty MacGhee) na Christopher Kadego, walihukumiwa kifungo cha maisha jela. Pius Lugangila alitoroka.

Mohamed Tamimu aliuawa hatua za hawali za maandalizi ya mapinduzi.

Mkuu tufahamishe waliopewa msamaha.
 
Last edited by a moderator:
ni kweli usemayo mzee wangu Mohamed Said,yaonekana imewauma sana ukweli kuwa wazi,kila kitu kukifanya ni cha nyerere.Sasa tumejua nyerere alikuwa 'mshamba' mbele ya wazee wetu na ndio waliomkaribisha mjini na kumfundisha kuvaa suruali.Pia tumejua hakuanzisha TANU.Waangalie wote wanaomtetea nyerere,angalia kwa nini kanisa linafanya kampeni awe mtakatifu,mchakato unaendelea na huchukua muda mrefu.Cheo hiki hupewa watu waliolifanyia jambo kubwa sana kanisa.Jiulize muda mrefu nyerere alikuwa madarakani,ni jambo gani kubwa amelifanyia kanisa mpaka litake awe mtakatifu? Kwanini ukitaja udhaifu wa nyerere au mabaya yake wakristo huja juu?Fatilia vizuri huu mjadala utaona hata hapa haya ninayosema
Mie sikuja humu kupingana.
Nimeingia humu kueleza habari za wazee wangu.

Habari ambazo nyie hata siku moja hamkupata
kuzisoma popote.

Nani kati yenu alipata kusoma historia ya Sheikh
Hassan bin Amir popote pale?

Si mliona mshtuko mliopata nilipokuambieni TANU
imeasisiwa na Abdulwahid Sykes?

Nani kati yenu alijua mkono wa Nyerere na Kanisa
Katoliki katika kuivunja EAMWS?

Si mnaona hadi sasa hamuamini histori hii?

Lengo la kitabu changu limetimia miaka 15 ilopita.

Siko humu kuchagiza mniamini.
Niko humu kueleza historia ya wazee wangu.

Hilo tu basi.
 
Last edited by a moderator:
Nishakueleza mara nyingi.
Bila ya nyinyi kunijibu kwa kuandika kitabu...

Itakuwa shida tu.

Kitabu changu kinasomwa vyuo vikuu vyote
vinavyosomesha African history.

Hivi ninavyoandika kitabu kinakwenda toleo la tatu.
Wewe unazungumza kukipinga JF...

Kitabu kipo Oxford, Cambridge, Harvard, Northwestern,
University of Dar es Salaam...

Kweli wewe uko makini kukipinga kitabu changu?

Kusomeshwa kwa kitabu chako huko ughaibuni kwa wasiojua ukweli, sio turufu yako kwetu katika mnakasha huu mzee wangu
 
tulizana kijana,'mume' wamemtaka wenyewe mpaka waseme huyu mume ni mkubwa ndo wataachiwa
Binafsi sioni mantiki ya kutoka mapovu kujadili udini humu. Huyu Mohamed Said namsikia tu akitetea imani yake na kuponda ukristo. Mtu kama huyu akishawekewa ukweli mchache tu na aachwe na ukweli huo. Akiendelea kubisha hata wewe unayebishana nae unaonekana kishoka wa hoja. Mwacheni
 
Binafsi sioni mantiki ya kutoka mapovu kujadili udini humu. Huyu Mohamed Said namsikia tu akitetea imani yake na kuponda ukristo. Mtu kama huyu akishawekewa ukweli mchache tu na aachwe na ukweli huo. Akiendelea kubisha hata wewe unayebishana nae unaonekana kishoka wa hoja. Mwacheni

Hapana mkuu, hapo unatuvunjia heshima sisi tunaosonga na mnakasha huu, kumbuka hapa hanufaiki Mohamed Said au mimi tu, bali mamia ya wanaofuatilia mnakasha huu.
 
Back
Top Bottom