Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Remote, hawana tofauti hao, lao moja, na kila siku wapo sebuleni kupanga hila na uovu dhidi ya watanzania wenzao kwa kisingizio cha kumuenzi allah!

labda tuseme tofauti yake na Ilunga ni kwamba Ilunga yupo straight katika madhumuni yake na MS moyoni pia anaghiliba na madhumuni kama ya Ilunga ila anatumia njia ya kuzunguka.
 
Son of Alaska,

Naye alituambia kuwa ndani ya masaa 24 ataiweka hiyo hotuba leo unakwenda mwezi wa nne hakuna hotuba wala asemi chochote tena.

Ameona ni afadhali amgeukie Sheik Kassim bin Jumaa na kumpakazia! hawa ndio wale wanaowavua wenzao utanzania pindi wapatapo kibano!
 
Huu mjadala ni mzuri sana. Ila kuna jambo ambalo kwa maoni yangu Ndugu yangu Mohammed Said analikosea au labda kwa bahati mbaya hajaliona. Ni kwamba ukichukua msimamo fulani katika mjadala, lazima uwape usawa unaowazungumza. Mzee Mohammed Said umeamua kuyatazama matukio yote ya kabla ya uhuru na baada yake kwa "lens" ya uislamu na waislamu. Sasa basi utaifa sio tija hapa. Hakuna Mwingereza hapa (kuna Mwanglikana) na hakuna Nyerere hapa wala Wajerumani (kuna Mkatoliki au Ukatoliki). Mtazamo wa mzee Mohammed Said lazima utampa jibu moja tu kwamba waislamu ndio waliopigania uhuru, ndio waliosimamia harakati zote n.k. Tatizo la "position" yako ni kuwa unapotaja dhulma za wakoloni sasa unatumia utaifa wao badala ya dini zao. Unapomtaja Mwl. Nyerere ajabu unatanguliza Ubara (U-musoma) wake kwanza (sio Ukatoliki)lakini unapotaja wazee wa TAA na TANU unatanguliza uislamu wao kwanza na sio kabila zao. Unapotaja askari waliopindua zanzibar unahamia KABILA lao kwanza, sio dini yao. HAPA HAPAKUBALIKI. Unatakiwa ulete Ushahidi Mzee Mohammed Said kwamba wazee wa TAA na TANU enzi hizo walijiunga pamoja kama WAISLAMU TUU NA SIO WAAFRIKA WA TANGANYIKA. Lete ushahidi. Pia, leta ushahidi kuwa wazee hao walimwalika asiyekuwa mwislamu kujiunga nao kinyume na katiba ya chama chao. Naomba ujibu, kuwa Umoja wa Mataifa ulikabidhi koloni la Tanganyika kwa Kanisa la Anglikana au kwa himaya ya Kiingereza? Binafsi napinga kabisa kuchangaya kuwaita baadhi ya watu ni wa Musoma au Wajerumani au Waingereza huku huku kundi moja umeamua kuliita ni la kiislamu. Lazima uchague kigezo kimoja na ukitumie hicho kwa mjadala wote. Kama unaangalia dini zao tuu, basi yabidi tutumie kigezo hicho kwa wote kuanzia wazee wa TANU hadi ma-settler. Nimeona muda mwingi sana Mzee wangu Mohammed Said umeutumia kumlaumu Mwl Nyerere. Mimi simtetei. Ila ni vizuri kukiri madhaifu yako kama unayo. Hivi ni kweli kwamba matajiri wa kiislamu waliosheheni nchi hii, ni mfumo kristo unawazuia kujenga hospitali na chuo kikuu? Mbona kila leo twawaona wakigharamia burudani za gharama mbaya? Lakini, kina Aga Khan ni dini gani? Mbona wao wana vyuo vikuu na mahospitali makubwa? Wamekwepaje hujuma za mfumo Kristo? Au hawa Answar Sunna na hela zao wanazoanzishia redio na TV nani kawazuia kuanzisha hospitali ya maana? Sote twaona bidii ni kushushua zaidi waislamu wenziwao. Bakwata wana Chuo Kikuu cha Waislamu pale Morogoro, sasa kosa liko wapi kama wakiandikiana MoU na Serikali kuhusu wahitimu wake kupata kazi pindi wakimaliza? Nimeona nakala ya MoU humu kwenye mjadala, WRONG. Nyie hamkutakiwa eti kuleta nakala ya Mou kati, ya Taasisi ya Kikristo na Serikali kuhusu Taasisi hiyo kupata faida TOKA serikalini, hapa mlitakiwa kuleta MoU au mawasiliano yoyote ya siri kati ya Makanisa (moja au yote)na Serikali kwamba ikitokea Waislamu wakajipanga na kuja na "a similar request" basi WASIPEWE au HAWATAPEWA. Hiyo ndio ilikuwa hoja. Ile MoU haina mahali inaahidi hujuma kwa waislamu. Sasa kilio cha kubeba documents za wenzio ni cha nini? Hapa paletwe ushahidi kuwa mwaka fulani serikali ilikataa kutiliana MoU na waislamu juu ya Taasisi fulani japo ilishawekeana MoU na wakiristo. Ni vizuri sana Ndugu yangu Mohammed Said akajua kuwa tatizo kubwa la Waislamu hapa nchini ni katika kujipanga. Wakiristo wapo-organized sana. Hii inawasaidia sana katika upangaji wa shughuli zao. Ndio maana japo kimadhehebu zipo tofauti hadi za sikukuu, huwasikii wakipandishiana ma-speaker na kukashifu viongozi wa kidini maredioni. Katika hali kama hiyo lazima yule ambaye ametulia lazima atasonga mbele. Lakini eti leo miaka 45 baadaye ukilalamika Waislamu haturuhusiwi kujipanga ila kupitia kibaraka Bakwata Wallah mimi sikuelewi. Hivi wanaoitukana Bakwata kupitia redio na TV zao ni dini gani? wao wanaruhusiwa na nani? Nyerere pia?. Nenda Mwanza, Iringa, Bukoba na Kilimanjaro utakuta Waislamu wasio na manunguniko yasiyoisha. Wao ni kujenga shule na kutafuta waalimu wazuri, shule zinafanya vizuri na hata wakiristo wanapeleka watoto huko. Mwisho ni kuwa haitatokea katika dunia hii eti historia ya mahali iandikwe kwa kuweka kwenye daftari kila jambo lililofanywa na kila aliyekuwapo. Sio Marekani, wala Afrika Kusini, wala Kenya wala Iraq. Ndio maana hata vitabu vya dini havihangaiki kutuandikia eti nani alimwazima mtume fulani farasi au punda wakati huo kwa ajili ya kwenda kuwalingania watu. Nyerere na wazee waliopita wamechuma waliyoyachuma. Waache wapumzike.

Nani kakuambia Morogoro University ni ya Bakwata? ulifanya utafiti lini na kugundua Waislamu wa Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba na Iringa hawanunguniki? Kilimanjaro kuna Shule 2 za Waislamu zisizo za Bakwata Kirinjiko na Mudio zinazojitahidi kuinua vipaji na elimu ya Wanafunzi! kuna Shule nyingi za Bakwata ambazo kwa kweli haziridhishi! sasa wewe unazungumzia Shule au Waislamu kwa ujumla wao? Waislamu wa maeneo haya wanaathirika sana kimfumo kama wenzao wa maeneo mengine! malalamiko yako na kero zote za Waislamu wa nchi hii hazina mipaka! mfumo kristo unatandika kila mahali bila kujali huyu ni Kilimanjaro au Mwanza!
 
Ahahahah..Nguruvi3 wewe wazee wako ni wa mkoa gani?
Mbona swali gumu hili! najaribu nikishindwa nitakupa Jibu jepesi.

Wazee wangu ni wale wa Nyakatende hadi Mugango.Shirati hadi Kinesi. Kuanzia Lizabon hadi Peramiho. Wapo pia Isevya, Magila, Pongwe, Mjasani, Amani.Ninao kule Nanjoka, Mchukwi na Ikwiriri. Kuna wengine Bigwa Mwarusembe hadi Nyamato. Nyangao na Itigi. Kote Haidom hadi Longido na Maneromango. Malinyi Mtimbira hadi Mlimba na Mikindani. Kidogo basi mpaka viwanja sitini kupitia kidodi na Zignali, kwamtipura, kiembe samaki, bububu hadi mifenesini Mtaa wa Matombo, Ilala boma, Mkunguni nyumba ya nne kabla ya msikiti wa Manyema.
Orodha ni ndefu. Simply wazee wangu ni Watanzania wote walionitangulia ''waswahili au wakuja''
 
Ahahahhahah..Ubarikiwe sana mkuu.
 
Je, yule anayepanga kupeleka wanafunzi kuandamana kesi ya Ponda ana muda wa kujali ubora wa elimu?

Na wale wanaopanga kupeleka vijana mahakamani kesi ya Lwakatware na kupanga kuandamana kila mara nao wana muda wa kujali elimu?
 
Yoso,

Hebu soma hii hapo chini huenda ukapata picha ya watu ninaowazungumza.
Huyu ni babu yangu Salum Abdallah aliyeishi kati ya mwisho 1890s hadi 1974:

Kleist Sykes na Salum Abdallah licha ya kuwa walikuwa majirani, walikuwa wakifanya kazi pamoja katika Tanganyika Railway na wake zao Bi Mluguru bint Mussa, mke wa Kleist, na Bi Zena bint Farijala mkewe Salum Abdallah walikuwa mashoga. Ushoga mkubwa kabisa wa kufuliana vidani vya dhahabu. Mabibi hawa bila ya kujua athari za ushoga wao wamekujakuwa hazina kubwa sana kuhusu maisha ya waume zao na katika kueleza maisha hayo leo tumekuja kufahamu mengi kuhusu maisha ya watu wa Dar es Salaam na nyakati zao. Bi Zena juu ya kuwa alikuwa mama wa nyumbani alikuwa mpenzi wa Harry Belafonte na kila alipopata nafasi alipenda kuieleza senema “Island in the Sun” kwa wajuu zake (mmoja wapo akiwa mwandishi) alocheza Belafonte. Senema hii ilikuja Tanganyika katika miaka ya mwisho ya 1950 na ilisisimua wengi kwanza kwa haiba ya Belafonte mwenyewe na nyimbo alizoimba katika senema ile. Lakini kubwa zaidi ambalo nahisi Waafrika wengi walotazama senema ile lililowaathiri ni ile hadith yenyewe, maana ilikuwa inahusu mapambano kati aya Waafrika na ukoloni wa Muingereza.

Vilevile kulikuwa na kisa cha mapenzi kati ya Harry Belafonte aliyekuwa nyota wa mchezo na msichana wa Kizungu. Kilichomfurahisha sana Bi Zena ni kule yule msichana wa Kizungu kukataliwa na mtu mweusi, Belafonte. Wakati ule Belafonte ndiyo alikuwa anainukia na nyimbo zake kama “Round the Bay of Mexico,” “Banana Boat,” “Jamaica Farewell” na nyimbo nyingine zilikuwa zikisikika katia radio kila siku. Biti Farijala kama alivyokuwa Biti Mluguru, waume zao ndani ya nafsi zao walichukia kutawaliwa na huenda katika mazungumzo yao ya faragha hili lilijitokeza mara kwa mara. Hali ya wakati ule haikuruhusu Waafrika kudai waziwazi haki yao ya kujitawala lakini mambo yalipowiva wazalendo wa Tanganyika hawakusita kumuomba Muingereza kufunga virago na kurejea kwao.

Salum Abdallah alihamia Tabora mwaka wa 1947 baada ya “locoshed” kama karakana ya treni ilivyokuwa ikijulikana, ilipohamishiwa Tabora na mwaka huo huo Salum Abdallah aliongoza mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa relwe. Mwaka wa 1947 African Association Tabora ilikuwa imejiimarisha vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kushiriki katika mgomo ambao ulianza katika bandari ya Dar es Salaam uliokuwa ukiongozwa na Dockworkers Union chini ya uongoziwa Abdulwahid Sykes. Mgomo ulitambaa hadi kufika Tabora na kuungwa mkono na wafanyakazi wa relwe. Siku ya mgomo wafanyakazi wengi wao kutoka karakana ya magari moshi ya wakiongozwa na Salum Abdallah, walikusanyika katika viwanja vya Tabora Town School chini ya miembe. Kuanzia siku hiyo viwanja hivyo vikawa ndiyo mahali pa mikutano yote ya African Association.

Salum Abdallah aliishi Tabora hadi Mungu alipomuhitimisha mwaka 1974 na katika umri wake alifanya mengi katika siasa. Akiwa mwanachama wa African Association kutoka Dar es Salaam aliendeleza harakati pale Tabora na mwezi June 1954 yeye alikuwa mmojawapo wa wanachama wa TAA waliokutana kwa siri Town School kufanya mipango ya kumleta katibu wa TAA Tabora Germano Pacha kuja Dar es Salaam kuasisi TANU tarehe 7 Julai 1954. Sheikh Abubakar Mwilima aliyekuwa mmoja wa walimu wa Town School alikuwa akiwakaribisha wanaharakati wa TAA kufanya mikutano yao pale shule katika moja ya madarasa. Salum Abdallah alikuwa mtu wa ari na akijiweza sana. Nyumba yake pale Isevya, Kanoni Street alipokuwa akiishi inasemakana ndiyo ilikuwa moja ya nyumba za mwanzo kupata maji ya bomba na umeme na kuwa na simu.

Salum Abdallah katika mkutano ule wa siri kuzungumzia kuunda TANU alitoa mchango wa shilingi ishirini kumsafirisha Pacha kuja Dar es Salaam. Wakati ule hizo zilikuwa fedha nyingi. Mwaka 1955 muda mfupi baada ya kuundwa TANU, Salum Abdallah alichaguliwa kama mwenyekiti muasisi wa Tanganyika RailwayAfrican Union (TRAU) chama cha wafanyakazi wa Reli kilichokuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru na kikitoa mchango mkubwa kwa TANU. Katibu wa TRAU alikuwa Chistopher Kassanga Tumbo. Mwaka 1960 TRAU chini ya uongozi huu iliiitsha mgomo uliodumu siku 82. Kwa takriban miezi mitatu si treni, meli na mabasi ya relwe yalitembea. Inasemekana hapajatokea mgomo ambao ulitayarishwa kwa ufundi na ustadi kama mgomo wa relwe wa mwaka 1960. Mgomo kama huu kamwe hautatokea tena.

TRAU ilipata fedha kutoka kwa rafiki zao Ujerumani ya Mashariki na wafanyakazi wa reli Uingereza. Msaada huu ndiyo uliowezesha TRAU kuhimili mgomo kwa miezi mitatu. Mwishowe serikali ya kikoloni ilisalimu amri na wafanyakazi wa relwe wakasitisha mgomo na kurudi kazini madai yao yote yakiwa yamekubaliwa. Mgomo huu miezi michache kabla ya Tanganyika kuwa huru ulimtisha sana Nyerere kwani alitambua kuwa kulikuwa na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliokuwa na nguvu sana na aliogopa baada Tanganyika kuwa huru vyama hivi chini ya viongozi kama hawa vitampa shida katika utawala wake. Katika mambo kama haya kunakuwa na mikasa mingi.

Salum Abdallah alikuwa na binti yake ambae kijana mmoja katika relwe alimpenda na akapeleka possa kwake kwa nia ya kutaka kufunga ndoa. Bahati mbaya kabla Salum Abdallah hajajibu posa ile mgomo ukawa umetokea. Sasa Yule kijana kwa bahati mbaya hakugoma kwa hiyo akawa katika kundi lililojulikana kama vibaraka. Salum Abdallah alihamaki sana kuwa yule kijana ambae alitegemea atajakuwa mkwe wake kaisaliti TRAU. Salum Abdallah akamwagiza mshenga wa yule kijana aje achuke majibu ya posa yake. Mshenga hakujua nini kinamsubiri. Siku ya siku ilipofika akajikusanya yeye na wenzake kwenda kupokea jibu la posa yao wakiwa na uhakika kuwa jibu litakuwa zuri na kitakachobaki ni kupanga siku ya harusi. Salum Abdallah alitoa kiti chake cha uvivu akakiweka sawasawa na mlango mkubwa wa nyumba yake anasubiri ujumbe ufike. Toka mbali Salum Abdallah anamuona mshenga na wapambe wake wale wanakuja na kanzu zao na kashda na ndani ya ujumbe kuna masheikh wawili watatu wa kuheshimika. Walitegemea chai nzito kwani Salum Abdallah hakuwa mtu mdogo katika jamii. Naam, hapakuwa chai wala salaam kama ilivyo kawaida wala Salum Abdallah hakumpa nafasi mchenga kusema chochote. Alinyanyuka na posa ya yule kijana akawatupia miguuni waiokote. Akawaambia, “Katafuteni mke kwa vibaraka wenzenu, nyumba yangu haingii kibaraka.”

Huyo ndiye Salum Abdallah Muyiki Samitungo Mwekapopo. Mungu alimjalia tambo kasimama kama futi sita hivi. Akikuangalia tu unaondoka hata kabla hajakugusa. Mwezi wa Ramadhani wapiga ngoma ya daku watazunguka kote kisha watafika nyumbani kwake. Mwenyewe anakuwa kaka barazani anawasubiri. Wakishafika pale wanazima ngoma kama kuashiria kuwa sasa wanaingia katika “track” nyingie na hapo lile goma kubwa sondo litaanza kurindima kumwimbia nyimbo yake ya kumsifia ikiitwa “Ndege Mwema.” Salum Abdallah atasikiza kisha atanyanyuka pale alipokaa atawaendea na kuwatunza fedha za kutosha hasa. Hapo watageuka na kuondoka huku “Ndege Mwema” ikirindima lakini kwa mpigo mwingine. Waswahili wana msemo, “Chini kunakwenda watu.”

Yalipotokea maasi ya Tanganyika Rifles (TR) tarehe 20 Januari 1964, Salum Abdallah alikamatwa na kutupwa kuzuizini pamoja na viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na masheikh. Sababu zilizotolewa ni kuwa kulikuwa na njama za kupindua serikali ya Nyerere na viongozi hao pamoja na masheikh walihusika katika njama hizo. Shutuma nyingine hasa kwa masheikh ilikuwa masheikh walikuwa “wanachanganya dini na siasa.” Mwaka wa 1963 Baraza la Wazee wa TANU lilivunjwa rasmi na sababu alizotoa Nyerere ni kuwa wazee waliokuwa katioka baraza hilo ambao wote walikuwa Waislam walikuwa “wanachanganya dini na siasa.” Sintofamu kubwa kati ya Waislam na serikali ya Nyerere ilifuatia. Katika waazuoni maarufu waliokubwa na hali hii alikuwa Shariff Hussein Badawy na mdogo wake Mwinyibaba. Hawa walikuwa walimu katika Masjid Badawy Kisutu karibu na Soko Mjinga. Msikiti huu sasa unaitwa Rawdha. Hawa walifukuzwa nchini na kurejeshwa kwao Mombasa. Ilikuwa katika utawala wa Ali Hassan Mwinyi ndipo waliporuhusiwa kurudi tena Tanzania. Shariff Hussein wakati ule miaka 1960 alikuwa kijana na akicheza mpira club ya Cosmopolitan. Matatizo haya yakaendelea hadi kufika mwaka 1968 Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika na Zanzibar nae akakamatwa na kurejeshwa Zanzibar na akapigwa marufuku asifike Tanzania Bara kama alivyofanyiwa Shariff Hussein Badawy na mdogo wake Mwinyibaba.

Salum Abdallah alipotoka kizuzini jela ya Uyui, si tu aliichukia TANU chama alichokipenda bali alimchukia hata Nyerere mwenyewe na hakujihushisha tena na siasa na alitumia muda wake mwingi katika ukulima wa tumbuku Urambo na alifanikiwa sana. Jina la Nyerere lilikuwa halitajwi katika nyumba yake. Katika mazishi yake TANU ilikuja na ilisoma taazia iliyomsifu sana Salum Abdallah kuwa alikuwa mzalendo wa kweli na aliupigania uhuru wa Tanganyika kwa dhati. Haya ndiyo katika maajabu wa siasa. Kabla hajafa Salum Abdallah akitembea na shutuma kuwa yeye na wenzake walipanga njama za kupindua serikali ingawa kesi ile ya maasi ya jeshi ilipokwenda mahakamani Salum Abdallah na viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi na msheikh hawakuunganishwa katika mashtaka ya uhaini.
Ngano hii si fundisho la historia ya uhuru wetu, bali masimulizi ya mzee wako Salum Abdala.

Haijabeba historia ya uhuru wa Tanganyika na Julius Nyerere, bali imebebwa na historia ya Tanganyika na Julius Nyerere.
 
Mohamed Said,

..Thank u.

..ndiyo maana wengine tunaendelea kusisitiza kwamba matatizo ya Nyerere na wazee wako yalikuwa ni SIASA, na siyo dini.

..katika bandiko lako umesahau kumtaja Balozi Christopher Kassanga Tumbo kwamba aliwekwa kizuizini muda wote wa utawala wa Mwalimu Nyerere na alikuja kutolewa wakati Mzee Mwinyi anakaribia kuondoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Mh JokaKuu akimtia Balozi Christopher Kassanga Tumbo unadhani jukwaa aliloamua kulisimamia litamtosha.

Mohamed Said,

..Thank u.

..ndiyo maana wengine tunaendelea kusisitiza kwamba matatizo ya Nyerere na wazee wako yalikuwa ni SIASA, na siyo dini.

..katika bandiko lako umesahau kumtaja Balozi Christopher Kassanga Tumbo kwamba aliwekwa kizuizini muda wote wa utawala wa Mwalimu Nyerere na alikuja kutolewa wakati Mzee Mwinyi anakaribia kuondoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said,

..Thank u.

..ndiyo maana wengine tunaendelea kusisitiza kwamba matatizo ya Nyerere na wazee wako yalikuwa ni SIASA, na siyo dini.

..katika bandiko lako umesahau kumtaja Balozi Christopher Kassanga Tumbo kwamba aliwekwa kizuizini muda wote wa utawala wa Mwalimu Nyerere na alikuja kutolewa wakati Mzee Mwinyi anakaribia kuondoka madarakani.

Joka Kuu,

Katika uandishi huwezi kuwalazimishe wasomaji wafikiri utakavyo.

Katika ugomvi wa babu yangu na Nyerere ambao ulianza 1962 kisa
kilikuwa siasa hapakuwa na suala la dini baina yao.

Ingawa baada ya hapo mengi yakaingia katika siasa za wakati ule na
dini ikawa moja ya sababu za farka.

Lakini Joka umemuona babu yangu?

Basi wakati ule wa mgomo miezi mitatu kavaa jampa suti ya khaki na hat
yuko vitani.

Halafu huwezi kusimamanae uso kwa uso dakika mbili utakuwa flat.

Siku alipojipeleka mwenyewe polisi aligoma kuingia selo na mkuu wa kituo
alikuwa kalasinga wanafahamiana vyema.

Hakuna askari aliyethubutu kumsogelea na yule Mkuu wa Kituo alijua hapa
inaweza ikaja hatari maana itabidi aonyeshwe silaha.

Ilibidi amrai sana na baba yangu mdogo alikuwapo pale na yeye alisaidia sana
hadi akaingia katika selo bila ya mtu kumgusa.

Bibi yangu alikuwa akiniombea dua akisema kwa utani, ''Mume wangu nakupenda
sana lakini naogopa huo wazimu wenu sasa sijui kama na wewe umerithi mie
wanangu Allah kawanusuru, nawe Allah akunusuru.''
 
Ngano hii si fundisho la historia ya uhuru wetu, bali masimulizi ya mzee wako Salum Abdala.

Haijabeba historia ya uhuru wa Tanganyika na Julius Nyerere, bali imebebwa na historia ya Tanganyika na Julius Nyerere.

Bwana Nyerere,
Hakika ni simulizi za babu yangu.

Ukipenda unaweza ukaitenganisha historia ya wafanyakazi
na historia ya uhuru wa Tanganyika na ya Baba wa Taifa.

Elimu ni bahari.

Unaweza ukadanda na huo mwelekeo wako ukaandika kitu
kikapata reviews katika majarida makubwa ya historia duniani.
 
Ameona ni afadhali amgeukie Sheik Kassim bin Jumaa na kumpakazia! hawa ndio wale wanaowavua wenzao utanzania pindi wapatapo kibano!

Kadogoo,

Soma hii excerpt kutoka pp niliyotoa Chuo Kikuu Cha Kenyatta, Nairobi mwaka 2007 kuhusu Sheikh Kassim itakupa mwanga
wa mtu huyu na siasa alizokuwa akizicheza ambao mwishowe zilimwangamiza lakini kwa upande mmoja alipata alichokuwa akikitafuta:

''...Sheikh Kassim convinced that President Mwinyi as well as Prof. Malima were targets for attack because of their faith and nothing else, stood up to defend Mwinyi's rule.

Not having the instrument of power under his full control as the bureaucracy had their allegiance elsewhere, President Mwinyi could not influence public opinion nor could he control the state administrative machinery.

For the first time Sheikh Kassim's oratory skills, were put to defend not only President Mwinyi but Islam as well.

Sheikh Kassim began to mobilise Muslims to stand up against an unjust Christian dominated government.

Sheikh Kassim's Friday khutba changed assuming militant posture full of political rhetoric attacking the press and Christians whom he accused of undermining Mwinyi's rule simply because the Church could not stand a Muslim head of state.

Sheikh bin Kassim Juma in broad day light and with loud speakers blaring full blast at his Mtoro Mosque more than once mentioned Julius Nyerere, the former president, by name as an enemy of Islam.

Muslims were thrilled by Sheikh Kassim's khutbas and his sudden change against the establishment and Nyerere, his mentor.

Muslims in thousands now thronged the Mtoro Mosque to come and listen to Sheikh Kassim's Friday khutbas.

Mtoro Mosque overnight became a centre of resistance against forces opposing Mwinyi's rule. Sheikh Kassim called upon Muslims to rise up and over-throw the Christian dominated government which had oppressed them since independence.

Sheikh Kassim's khutbas were recorded in cassettes and distributed by the Ansar Sunna movement throughout the country.

The press scandalised, ridiculed and poked fun at President Mwinyi with impunity, at times even questioning his appointments of Muslim functionaries.

The press also insinuated on the dropping from the cabinet of Kingunge Ngombale Mwiru, Getrude Mongela and Joseph Warioba as being influenced by religious sentiments.
[1]

Included in this war of words were selected Muslim Ministers.

It seemed Christians were irked that those powerful portfolios were in Muslims hands. The government and party owned media seemed to have lost allegiance to the government including loyalty to the president himself.

President Ali Hassan Mwinyi, Prof. Kighoma Malima, Fatma Said Ali, Hassan Diria then Minister of Foreign Affairs and International Co-operation and Mustapha Nyang'anyi became favourite targets of ridicule by the private tabloids.

Sheikh Kassim mobilised Muslims to stand firm behind President Mwinyi and all Muslims in his cabinet.

The Christian lobby was quietly waiting for the chance to get even with "Muslim fundamentalist" and teach them a lesson.

That chance came during Easter holidays in 1993 in the form of pork riots.
..

[1] See "Mwinyi's Dilemma," New Afrcan, June, 1989, Also Tanzania's Religious Politics," New African, November, 1989. Also see "Religious Controversy in Tanzania," Africa Events, November, 1989 and Warsha, ''Fitina inayotukabili Waislam 14 Julai, 1989, Dhul Haj,'' 1409 H.
 
labda tuseme tofauti yake na Ilunga ni kwamba Ilunga yupo straight katika madhumuni yake na MS moyoni pia anaghiliba na madhumuni kama ya Ilunga ila anatumia njia ya kuzunguka.

Remote,

Mimi huwezi kunilinganisha na Sheikh Ilunga.
Ilunga ni alim.

Mimi napiga goti nasomeshwa na Sheikh Ilunga.

Mimi akiwapo siwezi hata kunyanyua sauti yangu
kunong'ona achilia mbali kusema.

Heshima ya Sheikh Ilunga iko juu sana kwa Waislam.

Ndiyo maana umeona yeye ndiye aliyeaminiwa kutembea
nchi nzima kuwazindua Waislam kuhusu mfumokristo.

Mimi siwezi hata kumbebea viatu vyake.
 
Na wale wanaopanga kupeleka vijana mahakamani kesi ya Lwakatware na kupanga kuandamana kila mara nao wana muda wa kujali elimu?

Kadogoo,

Nilikuwa naangalia mashindano ya magari Formula 1 Malaysian Grand Prix huku nakunywa gahawa na kashata za Jidah nimesoma post yako nimecheka sana.
 
Remote,

Mimi huwezi kunilinganisha na Sheikh Ilunga.
Ilunga ni alim.Mimi napiga goti nasomeshwa na Sheikh Ilunga.Mimi akiwapo siwezi hata kunyanyua sauti yangu
kunong'ona achilia mbali kusema.Heshima ya Sheikh Ilunga iko juu sana kwa Waislam.

Ndiyo maana umeona yeye ndiye aliyeaminiwa kutembea
nchi nzima kuwazindua Waislam kuhusu mfumokristo.
Mimi siwezi hata kumbebea viatu vyake.
Kwahiyo kauli yake inayochochea mauaji ni kauli mbiu aliyopewa na waislam?
Nina uhakika Mohamed hutajibu swali hilo hapo juu. Utasubiri baada ya post kadha unirushie kombora la matusi.

Kwanza nikuulize, unaposema ameaniwa na waislam ni waislam wapi hao kwa kuzingatia kuwa wapo BAKWATA na makundi mengine kila moja likiwa na agenda yake?

Mohamed Ilm si vitabu, paper au machapisho tu. Ilm ni maarifa aliyo nayo mtu katika kukabiliana na mazingira yake kwa ujumla.
Kitu muhimu sana kwa mwenye Ilm ni mawasiliano.Endapo mtu hana mawasiliano basi hapo Ilm inakosa maana yake halisi.

Sijui Sheikh Ilunga ana Ilm ya kiwango gani katika hii iitwayo elimu dunia hadi kufikia mahali pa kupewa jukumu la kuueleza mfumo nchi nzima.Sijui kama anachokiongea anafahamu madhara na athari zake.

Nisichokubaliana nawe ni hoja ya kumpa wadhifa wa kuongea kwa niaba ya waislam.
Nina uhakika katika waislam wanaomsikiliza na kumfuatilia wapo mamilioni wasiokubaliana na hoja zake.
Hao nao umeamua kuwachanganya na wale wanaokubaliana naye katika chungu kimoja cha waislam ''wamemtuma''

Ukiangalia ile video ni ngumu sana kuamini kuwa bado unaweza kusimama na kusema ametumwa na waislam.
Hata wewe tumekuuliza unakubaliana na video ile? hakika hukujibu kwasababu unafahamu wazi kuwa kile si kitu sahihi kidini, kidunia na kijamii.

Wapo waislam si kuwa wameudhika bali kukirihika sana na maneno ya mentor wako.

Labda utupe Ilm sisi wengine kuhusu Uislam ya kuwa wapi imeelezwa kuwa dini ya uislam itaenezwa kwa chuki na farki?
Je, yale maneno (niwieni radhi kama nitakosea) yanayosema '' walinganieni wasio waislam kuingia katika dini kwa hoja'' yalilenga nini na kwa nani? Na je, ndio hoja za Ilunga azisemazo

Njaribu kufikiri hivi kama yupo aliyetamani kuwa mwislam halafu akaiona ile video, je huyo mtu atakuwa amelinganiwa kuingia katika dini kwa maneno yale? Je, pale kuna ilm ya aina yoyote kweli na kwa msingi huo ilim ya kueleza mfumokristo ipo kwa hoja mantiki na busara!

Mohamed, ifike mahali kila mtu atambue kuwa imani ni suala la mtu binafsi na si chama cha ushirika au cha kisiasa.
Ni makosa kuchukua maneno ya mtu mmoja na kuyafanya ya waislam mamilioni wa Tanzania.

Ningeshauri siku nyingine useme ''ndiyo maana Ilunga ameaminiwa na kundi lenu kueleza mfumokristo'' na wala si waislam.
Unless uniambie anaongea kwa niaba ya waislam gani kauli yangu inabaki kama ilivyo.
 
Joka Kuu,

Katika uandishi huwezi kuwalazimishe wasomaji wafikiri utakavyo.

Katika ugomvi wa babu yangu na Nyerere ambao ulianza 1962 kisa
kilikuwa siasa hapakuwa na suala la dini baina yao.

Ingawa baada ya hapo mengi yakaingia katika siasa za wakati ule na
dini ikawa moja ya sababu za farka.

Lakini Joka umemuona babu yangu?

Basi wakati ule wa mgomo miezi mitatu kavaa jampa suti ya khaki na hat
yuko vitani.

Halafu huwezi kusimamanae uso kwa uso dakika mbili utakuwa flat.

Siku alipojipeleka mwenyewe polisi aligoma kuingia selo na mkuu wa kituo
alikuwa kalasinga wanafahamiana vyema.

Hakuna askari aliyethubutu kumsogelea na yule Mkuu wa Kituo alijua hapa
inaweza ikaja hatari maana itabidi aonyeshwe silaha.

Ilibidi amrai sana na baba yangu mdogo alikuwapo pale na yeye alisaidia sana
hadi akaingia katika selo bila ya mtu kumgusa.

Bibi yangu alikuwa akiniombea dua akisema kwa utani, ''Mume wangu nakupenda
sana lakini naogopa huo wazimu wenu sasa sijui kama na wewe umerithi mie
wanangu Allah kawanusuru, nawe Allah akunusuru.''
Mohamed Said,

..mimi kisa cha babu yako nimekipenda sana.

..una mambo mengi sana ya kuwaeleza wa-Tz, tatizo ni pale unapoelemewa na udini.

..tatizo lingine, ni kwamba umetugawa wa-Tz ktk makundi. mara nyingine ukitumia maneno "hawa" au "sisi."

..hata kama kuna conclusions fulani fulani ambazo unazo, nadhani ungetuachia wasomaji wako tutoe conclusions hizo.

..kuhusu Kassanga Tumbo, je una mpango wowote ule wa kuandika kuhusu maisha yake?? I think his story has to be told hata kama alikuwa na hatia na masuala aliyokuwa akituhumiwa nayo.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,unatisha kumkichwa kama ukoma! Kwakweli unajua kujenga hoja zilizosheheni nondo za nguvu.

Nakuhakikishia watanzania wote wanaofatilia mtanange huu wanakusoma wewe, Mwanakijiji,Mag3,Jasus na Yericko nyerere kwa hoja zenu mzuri na zenye kujenga na kuelimisha.

Pia wanamsoma Mohamed said,Ritz,Boko haramu,Ami,kadogoo,The Big Show na wafia dini wengine kwa hoja zao dhaifu zenye kuleta majibu mepesi kwenye maswali magumu...kwa hakika kundi hili lipo hapa jamvini kwa aibu ya kutokukubali kuwa wameshindwa na wanachokifanya sasa ni kujibu kwa mipasho ili mradi waonekane wapo na hawajashindwa.

Nguruvi3, endelea na usichoke....watanzania wanakusoma.
 
Back
Top Bottom