Mr. Nguruvi, mchango wako ni mzuri sana. Ila utaona kuwa hoja yangu haijapata majibu stahiki. Na sidhani kama yatapatikana. Upo ushahidi lukuki kuwa wazee wetu wa TAA na TANU walikuwa Watanganyika kwanza, na waislamu kibinafsi. Afro shiraz walipomwangusha Sultan walikuwa Waafrika kwanza na Waislamu kibinafsi. Hao askari waliotumika zanzibar ("jeshi la wamakonde") walikuwa askari kwanza dini binafsi. Kwanza, dini zao hazina msaada. Haitawezekana kuiandika historia kinyume na hivi. Katika historia Mr. Nguruvi huandiki kila kitu (kwa mfano dereva wa mashua iliyomleta Karume Dar siku husika n.k). Tatizo la mtazamo wa Mzee Said ni kuwa ukishafungulia mlango wa kudhania eti kila mtu na taasisi nchi yote hii lengo lake ni kukuhujumu wewe kwa sababu unaabudu vipi na kibla chako ni kipi, unakosea na unapoteza muda ambao ungeutumia kujiendeleza. Maelezo yako ya mashule kama Kibohehe, vyama kama AMNUT yananiunga sana mkono kwenye hoja yangu ya awali. Kwamba, waislamu adui nambari moja kwao ni "dis-organization". Sio Wakristo. Nisikilize vyema hapa. Marekani (wakiristo hao) walipomuua Osama bin Laden walihakikisha ndani ya kipindi husika wanamzika tena kwa taratibu za kiislamu (yaani walijiandaa!!!!). Libya (waislamu hao), walipomuua Muamar Gaddafi walianika maiti yake siku kadhaa hadi ikaanza kuoza huku ikiwa nusu uchi (dis-organised!!!!!). Utaulaumu mfumo Kristo Libya kwa kutomzika Gaddafi kiislamu pia? Hapana. Hayo angefanya Mtawala mkiristo ungesikia maandamano hadi Kariakoo. Syria, Marekani kachoka kupelekea silaha, kisa? jamaa hawako-organised!!!! Hapa ni kukosekana nidhamu. Njoo Bongo. Nusu ya nishati ya Waislamu inapotea ktk jinsi ya kuiua Bakwata. Sio jinsi ya kuiboresha. KUIUA. Kisa, Nyerere aliua EAMWS na Bakwata ni kibaraka wa Serikali. Come on Grow up!!!!, Hata muiue Bakwata bado mtaunda Taasisi nyingine. Watu kama Mzee wetu Mohammed Said wanafanikiwa zaidi kuwajaza waislamu "uislamu lawama" kwamba waislamu wapo nyuma kimaendeleo kwa sababu ya hujuma ya wakiristo. SIO KWELI. Tembelea Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Kagera, Songea, Singida, Dodoma na Mbeya kisha sema umeona nini. Chukua note book yako hapo mtaa wa Kongo hesabu dalala ngapi wamiliki wake wana majina ya kiislamu. Achilia mbali Ubungo bus terminal na Petrol stations ndio usiseme. Fuata Nyere road (Pugu Road) viwanda na majengo. Kosa lipo kwenye dis-organization. Huo ndio ukweli japo unauma. Kama serikali iliiunda Bakwata inabidi ipewe shukrani kwa vile kwa hii "dis-organization" tunayoiona sasa ya watu kugombea mwezi wa kufungulia na sio wa kufungia ndio kabisaaaa ingebakia matusi kuitana "makafiri" hao wanakula siku ya ramadhani huku shule hazijengwi. Mr. Nguruvi okay, mfumo Kristo haufai, sasa, kwanini Sultani wa Zanzibar alipopinduliwa asiende kuishi nchi za Kiislamu? Mbona ni Uingereza kwenye mfumo Kristo? Mbona waislamu wa kwanza kukimbia madhila kwa ajili ya dini yao walikwenda Abysinnia (afrika) kwa mtawala Mkiristo!!! Nachosema hapa hapa ni kuwa ni " absolutely WRONG ku-stereo type" watu au kuwaangalia kwa lens moja tuu kisha ukafikia maamuzi yako kwa kigezo hicho pekee. Na ndicho anachofanya Mzee Said. Ndio maana inashindikana kusema Jee, wazee wa TAA na TANU walivunja katiba za vyama vyao kukaribisha wasio waislamu miongoni mwa vyama hivyo? Hata mtu afanye lipi jibu ni kuwa hawa walikuwa Watanganyika. Full stop. Zingatia kwamba viongozi ni watu pia. Haiwezekani kuwa wazee wa TAA na TANU waliishi bila vikombe kugongana kabatini. Lakini sisi kama tuliorithi nchi toka kwao haitusaidii kujua siku wanakunywa chai nani alinunua sukari. Nimeona mahali juu ya Uislamu kuthamini ihsan (imetolewa aya). Ni kweli, ni kweli pia uislamu unakemea kuwa mlalamikaji wa kupindukia au kuwaongea watu katika namna isiyokuwa stahiki; Nayosema yasome kwenye link hii;
utayakuta pia kwenye Quran (104:1; 68:11; 49:11)pia kuna maelezo mazuri kwenye hii link: [URL="http://http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833"]http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833
juu ya kujihadhari na masuala yanayogusa aibu na madhaifu ya watu wengine hadharani na sababu zake ziko wazi.