Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Jasusi,
Ahsante sana ndugu yangu.

Damu nzito kuliko maji.
Umetaabika kuona nduguyo nasulubiwa.

Othman Chande sasa ni prof. wa kemia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Bubby yuko Dar anaendesha garage ya kaka yake Mushtak.

Wendo Mwapachu mjasiriamali alioa kwa kina Chagula.
Hatuchezi mbali na ni babu sasa.

Abdu Mtemvu yuko mjini Dar.

Mohamed Chande Jaji Mkuu kaoa kwa Mzee Maamry
Waarabu wenzao.

Umemsahau Yusuf Zialor marehemu.

Alitajirika sana akahamia London na mkewe Shufaa na watoto.
Wakiishi Surrey nyuma ya Wembley Stadium.

Nikiwatembelea sana miaka ya 1990s.

Ebby Sykes mimi na Ebby tumepishana siku moja kuzaliwa.

Kitanda alicholazwa mama yake Ebby Bi. Regina ndicho kalala
mama yangu siku ya pili nikazaliwa mimi.

Abraham ni babu sasa yuko Dar ana mtoto saizi ya mjukuu wake.
Hahahaha!

Ukija Dar utakuwa mgeni mambo na watu wamebadilika sana lakini
mapenzi ni makubwa sana tukikutana.

Shida ni kuwa mpaka afe mtu ndiyo tunakutana.
Hii hainifurahishi sana.

Jasusi,

Kuna jambo muhimu sana nilisahau kukueleza kuhusu ile Mercedes.
Gari ile alinunuliwa Aga Khan alipokuja Tanganyika 1956.

Ndiyo akitembelea na alipoondoka ikauzwa na ndipo ilipoangukia kwa
Abdu Sykes.
 
Mohamed Said,

Hujue watu hawapendi kuyasikia hayo.

Nashangaa humu jamvini watu hawajuhi Nyerere alimuelezeaje Abdulwahid katika hotuba yake ya kuaga.

Lakini ipo siku hiyo hotuba itapatikana na itasambaa kote watu waisikie.

Jiulize kwa nini hotuba za Nyerere wakati bado yupo madarakani wanazificha wanaonyesha zile ambazo kaishaondoka madarakani.

Ritz,
Ile hotuba ni "disaster" kubwa sana.

Unajua sisi tunaheshimu sana ihsani.
Kiasi Allah kaitaja katika Surat Rahman.

Kasema "jazau ihsan ila ihsan."
Ihsan hulipwa na ihsan.

Wafasiri wa Qur'an wakenda mbali zaidi katika
kusherehesha...

Wakasema huwezi kuilipa ihsani ulofanyiwa hata
kama kwa ubinadamu utarejesha wema.

Kwa waliokuwa wanaoijua historia ya watu wale
yale maneno yaliwashtua.

Nyerere kasahau cheo cha Abdu katika TAA!
Waarabu wana msemo wanasema hivi:

"Ukiijua sababu ile ajabu huondoka."

Lakini hii ndiyo dunia.
Angalau leo wazee wetu wako ndani ya JF.

Hivyo hivyo wanakejeliwa lakini wanatajwa
na waliokuwa hawawajui sasa wamewajua.

Hili si dogo.
 
Umetaja Qur'an Surat Rahman kuna vitu maneno mazito sana ndugu yangu.

Allah anasema jua na mwezi huenda kwa hisabu, na mbingu ameziinua na ameweka mizani.

Anatuambia tuweke mizani kwa haki wala msipunje katika mizani,

Msidhulumu wala msikubali kudhulumiwa.
 
Ritz , sina haja ya kukuelezea maana ya "mswahili"kwani neno lenyewe linajieleza ila kwa ubishi wako wa siku nyingi ambao nimeusoma sana hapa JF , na ukweli wewe ndio ID ya uislamu wenye chuki hapa jamii forums sioni ajabu unavyoshabikia hoja mfu za huyo baba yako wa kifikra (mohamed) aliyechota pande kubwa la ufahamu wako, kuendelea kusapoti hizi fikra mnato ni mwendelezo wa yale unayooamini kuwa wewe ni ISLAMIST LEBEL.
 
Juha na starehe zake.
 
Mr. Nguruvi, mchango wako ni mzuri sana. Ila utaona kuwa hoja yangu haijapata majibu stahiki. Na sidhani kama yatapatikana. Upo ushahidi lukuki kuwa wazee wetu wa TAA na TANU walikuwa Watanganyika kwanza, na waislamu kibinafsi. Afro shiraz walipomwangusha Sultan walikuwa Waafrika kwanza na Waislamu kibinafsi. Hao askari waliotumika zanzibar ("jeshi la wamakonde") walikuwa askari kwanza dini binafsi. Kwanza, dini zao hazina msaada. Haitawezekana kuiandika historia kinyume na hivi. Katika historia Mr. Nguruvi huandiki kila kitu (kwa mfano dereva wa mashua iliyomleta Karume Dar siku husika n.k). Tatizo la mtazamo wa Mzee Said ni kuwa ukishafungulia mlango wa kudhania eti kila mtu na taasisi nchi yote hii lengo lake ni kukuhujumu wewe kwa sababu unaabudu vipi na kibla chako ni kipi, unakosea na unapoteza muda ambao ungeutumia kujiendeleza. Maelezo yako ya mashule kama Kibohehe, vyama kama AMNUT yananiunga sana mkono kwenye hoja yangu ya awali. Kwamba, waislamu adui nambari moja kwao ni "dis-organization". Sio Wakristo. Nisikilize vyema hapa. Marekani (wakiristo hao) walipomuua Osama bin Laden walihakikisha ndani ya kipindi husika wanamzika tena kwa taratibu za kiislamu (yaani walijiandaa!!!!). Libya (waislamu hao), walipomuua Muamar Gaddafi walianika maiti yake siku kadhaa hadi ikaanza kuoza huku ikiwa nusu uchi (dis-organised!!!!!). Utaulaumu mfumo Kristo Libya kwa kutomzika Gaddafi kiislamu pia? Hapana. Hayo angefanya Mtawala mkiristo ungesikia maandamano hadi Kariakoo. Syria, Marekani kachoka kupelekea silaha, kisa? jamaa hawako-organised!!!! Hapa ni kukosekana nidhamu. Njoo Bongo. Nusu ya nishati ya Waislamu inapotea ktk jinsi ya kuiua Bakwata. Sio jinsi ya kuiboresha. KUIUA. Kisa, Nyerere aliua EAMWS na Bakwata ni kibaraka wa Serikali. Come on Grow up!!!!, Hata muiue Bakwata bado mtaunda Taasisi nyingine. Watu kama Mzee wetu Mohammed Said wanafanikiwa zaidi kuwajaza waislamu "uislamu lawama" kwamba waislamu wapo nyuma kimaendeleo kwa sababu ya hujuma ya wakiristo. SIO KWELI. Tembelea Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Kagera, Songea, Singida, Dodoma na Mbeya kisha sema umeona nini. Chukua note book yako hapo mtaa wa Kongo hesabu dalala ngapi wamiliki wake wana majina ya kiislamu. Achilia mbali Ubungo bus terminal na Petrol stations ndio usiseme. Fuata Nyere road (Pugu Road) viwanda na majengo. Kosa lipo kwenye dis-organization. Huo ndio ukweli japo unauma. Kama serikali iliiunda Bakwata inabidi ipewe shukrani kwa vile kwa hii "dis-organization" tunayoiona sasa ya watu kugombea mwezi wa kufungulia na sio wa kufungia ndio kabisaaaa ingebakia matusi kuitana "makafiri" hao wanakula siku ya ramadhani huku shule hazijengwi. Mr. Nguruvi okay, mfumo Kristo haufai, sasa, kwanini Sultani wa Zanzibar alipopinduliwa asiende kuishi nchi za Kiislamu? Mbona ni Uingereza kwenye mfumo Kristo? Mbona waislamu wa kwanza kukimbia madhila kwa ajili ya dini yao walikwenda Abysinnia (afrika) kwa mtawala Mkiristo!!! Nachosema hapa hapa ni kuwa ni " absolutely WRONG ku-stereo type" watu au kuwaangalia kwa lens moja tuu kisha ukafikia maamuzi yako kwa kigezo hicho pekee. Na ndicho anachofanya Mzee Said. Ndio maana inashindikana kusema Jee, wazee wa TAA na TANU walivunja katiba za vyama vyao kukaribisha wasio waislamu miongoni mwa vyama hivyo? Hata mtu afanye lipi jibu ni kuwa hawa walikuwa Watanganyika. Full stop. Zingatia kwamba viongozi ni watu pia. Haiwezekani kuwa wazee wa TAA na TANU waliishi bila vikombe kugongana kabatini. Lakini sisi kama tuliorithi nchi toka kwao haitusaidii kujua siku wanakunywa chai nani alinunua sukari. Nimeona mahali juu ya Uislamu kuthamini ihsan (imetolewa aya). Ni kweli, ni kweli pia uislamu unakemea kuwa mlalamikaji wa kupindukia au kuwaongea watu katika namna isiyokuwa stahiki; Nayosema yasome kwenye link hii; utayakuta pia kwenye Quran (104:1; 68:11; 49:11)pia kuna maelezo mazuri kwenye hii link: [URL="http://http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833"]http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833
juu ya kujihadhari na masuala yanayogusa aibu na madhaifu ya watu wengine hadharani na sababu zake ziko wazi.
 
hana jibu atakuzungusha tu bila kupata kitu cha maana kutoka kwake..mimi nimesoma vitabu vyake na nimefuatilia mada zake hapa JF na nachukulia vitabu vyake kama riwaya za alfu lela ulela

Saint Ivuga,
Hakika hiyo ni haki yako nani atakulazimisha
kufikiri vinginevyo.

Mola kaumba kila mtu na uwezo wake wa akili.

Ikiwa hapo ndipo akili yako ilipokufikisha sawa
wala hapana haja ya ugomvi.

Lakini kuna watu walipokisoma kitabu changu waliathirika
pakubwa.

Vyuo vikanialika ili wanione na kunisikia.
Kwa ajili hii nimehadhiri kwingi Afrika, Ulaya na Marekani.

Kisa...

Kitabu changu kimekuja na mambo mapya waliokuwa hawajayasikia
kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
 
Mr. Nguruvi, mchango wako ni mzuri sana. Ila utaona kuwa hoja yangu haijapata majibu stahiki. Na sidhani kama yatapatikana. Upo ushahidi lukuki kuwa wazee wetu wa TAA na TANU walikuwa Watanganyika kwanza, na waislamu kibinafsi. Afro shiraz walipomwangusha Sultan walikuwa Waafrika kwanza na Waislamu kibinafsi. Hao askari waliotumika zanzibar ("jeshi la wamakonde") walikuwa askari kwanza dini binafsi. Kwanza, dini zao hazina msaada. Haitawezekana kuiandika historia kinyume na hivi. Katika historia Mr. Nguruvi huandiki kila kitu (kwa mfano dereva wa mashua iliyomleta Karume Dar siku husika n.k). Tatizo la mtazamo wa Mzee Said ni kuwa ukishafungulia mlango wa kudhania eti kila mtu na taasisi nchi yote hii lengo lake ni kukuhujumu wewe kwa sababu unaabudu vipi na kibla chako ni kipi, unakosea na unapoteza muda ambao ungeutumia kujiendeleza. Maelezo yako ya mashule kama Kibohehe, vyama kama AMNUT yananiunga sana mkono kwenye hoja yangu ya awali. Kwamba, waislamu adui nambari moja kwao ni "dis-organization". Sio Wakristo. Nisikilize vyema hapa. Marekani (wakiristo hao) walipomuua Osama bin Laden walihakikisha ndani ya kipindi husika wanamzika tena kwa taratibu za kiislamu (yaani walijiandaa!!!!). Libya (waislamu hao), walipomuua Muamar Gaddafi walianika maiti yake siku kadhaa hadi ikaanza kuoza huku ikiwa nusu uchi (dis-organised!!!!!). Utaulaumu mfumo Kristo Libya kwa kutomzika Gaddafi kiislamu pia? Hapana. Hayo angefanya Mtawala mkiristo ungesikia maandamano hadi Kariakoo. Syria, Marekani kachoka kupelekea silaha, kisa? jamaa hawako-organised!!!! Hapa ni kukosekana nidhamu. Njoo Bongo. Nusu ya nishati ya Waislamu inapotea ktk jinsi ya kuiua Bakwata. Sio jinsi ya kuiboresha. KUIUA. Kisa, Nyerere aliua EAMWS na Bakwata ni kibaraka wa Serikali. Come on Grow up!!!!, Hata muiue Bakwata bado mtaunda Taasisi nyingine. Watu kama Mzee wetu Mohammed Said wanafanikiwa zaidi kuwajaza waislamu "uislamu lawama" kwamba waislamu wapo nyuma kimaendeleo kwa sababu ya hujuma ya wakiristo. SIO KWELI. Tembelea Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Kagera, Songea, Singida, Dodoma na Mbeya kisha sema umeona nini. Chukua note book yako hapo mtaa wa Kongo hesabu dalala ngapi wamiliki wake wana majina ya kiislamu. Achilia mbali Ubungo bus terminal na Petrol stations ndio usiseme. Fuata Nyere road (Pugu Road) viwanda na majengo. Kosa lipo kwenye dis-organization. Huo ndio ukweli japo unauma. Kama serikali iliiunda Bakwata inabidi ipewe shukrani kwa vile kwa hii "dis-organization" tunayoiona sasa ya watu kugombea mwezi wa kufungulia na sio wa kufungia ndio kabisaaaa ingebakia matusi kuitana "makafiri" hao wanakula siku ya ramadhani huku shule hazijengwi. Mr. Nguruvi okay, mfumo Kristo haufai, sasa, kwanini Sultani wa Zanzibar alipopinduliwa asiende kuishi nchi za Kiislamu? Mbona ni Uingereza kwenye mfumo Kristo? Mbona waislamu wa kwanza kukimbia madhila kwa ajili ya dini yao walikwenda Abysinnia (afrika) kwa mtawala Mkiristo!!! Nachosema hapa hapa ni kuwa ni " absolutely WRONG ku-stereo type" watu au kuwaangalia kwa lens moja tuu kisha ukafikia maamuzi yako kwa kigezo hicho pekee. Na ndicho anachofanya Mzee Said. Ndio maana inashindikana kusema Jee, wazee wa TAA na TANU walivunja katiba za vyama vyao kukaribisha wasio waislamu miongoni mwa vyama hivyo? Hata mtu afanye lipi jibu ni kuwa hawa walikuwa Watanganyika. Full stop. Zingatia kwamba viongozi ni watu pia. Haiwezekani kuwa wazee wa TAA na TANU waliishi bila vikombe kugongana kabatini. Lakini sisi kama tuliorithi nchi toka kwao haitusaidii kujua siku wanakunywa chai nani alinunua sukari. Nimeona mahali juu ya Uislamu kuthamini ihsan (imetolewa aya). Ni kweli, ni kweli pia uislamu unakemea kuwa mlalamikaji wa kupindukia au kuwaongea watu katika namna isiyokuwa stahiki; Nayosema yasome kwenye link hii; utayakuta pia kwenye Quran (104:1; 68:11; 49:11)pia kuna maelezo mazuri kwenye hii link: [URL="http://http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833"]http://www.islamweb.net/emainpage/index.php?page=articles&id=170833
juu ya kujihadhari na masuala yanayogusa aibu na madhaifu ya watu wengine hadharani na sababu zake ziko wazi.

Wickama,
Nimekusoma.

Kwa ufupi tu ni kuwa huijui historia ya Waislam na ndiyo
umekuja na maneno ''disorganised'' nk.

Historia ya Waislam Tanganyika ni nzuri sana na ndiyo maana
hakuna anaetaka kuitafiti na kuiandika.

Mimi ndiyo mwandishi wa kwanza kuiandika.
Wazee wetu walikuwa mabingwa wa mipango.

Naishia hapa sioni sababu ya kujirudia.
Nipo hapa JF sasa mwezi wa tatu.

Pitia post zangu za nyuma ikiwa umeingia
hivi karibuni.

Mna mengi ya kujifunza.
 
Mwenye kutokuelewa ni wewe. Malkia ni Mkuu wa Uingereza. The post is ceremonial. Malkia ni Mkuu wa Kanisa la Uingereza. The post is ceremonial. The difference is the same. Sihitaji maneno marefu kama wewe kusisitizia point kuwa Malkini ndiye mkuu wa Kanisa la Uingereza.

She is Supreme Governor of the Church of England and, in some of her realms, carries the title of Defender of the Faith as part of her full title.
Sasa misumari iko wapi ndugu yangu?

Hivi maana ya kuwa na post ya Ceremonial. Labda nikudondolee ni post ambayo haiathiri kitu chochote katika maamuzi au ni kusema haina meno. Tofauti na Papa ambapo document ya Vatican haitoki bila ya kuwa na muhuri wa pete yake pale kidoleni. Fahamtu!!!!!
 
Mkuu Jasusi
Kwenye suala la Vatican, ni vigumu sana kuwashawishi watu ambao dai lao la TZ kujiunga na OIC limejengwa tu kwenye msingi kuwa OIC ni Taasisi kama ilivyo Vatican. Kukubali kuwa Vatican ni Nchi, maana yake misingi ya dai lao inabomoka. Ndio maana wanahangaika kutafuta references za ajabu ajabu ili tu kuthibitisha kuwa Vatican sio nchi. Na ndio maana kwenye arguements zao wanasema " tujiunge na OIC au la ubalozi wa Vatican ufungwe"

Perhaps nikuulize wewe unayeweza kutuambia Vatican nchi:-

a. Nani alizaliwa Vatican, amekulia vatican na akafia Vatican? Kuna familia gani zimeanzia vatican na kuishi hapo? Watu 300 wanaoishi Vatican wote ni wahamiaji au kwa jina jengine migrants sasa tujibu wewe wazawa wa Vatican wako wapi?

b. Serikali ya Vatican ipi? Holy See au Vatican? Tunaona kuwa mahusiano ya Vatican yanatokana na mahusiano ya kiroho yaliyopo Holy See na waumini wake duniani. Sasa tuambie Vatican ni mdudu gani?

c. Kwenye International Law a state in vipengele hivi soma hapa:-

According to the Montevideo Convention on the Rights and Duties of States: “The state as a person of international law should possess the following qualifications: a) a permanent population; b) a defined territory; c) government; and d) capacity to enter into relations with the other states.

Sasa naomba majibu yafuatayao?

a. What is a permanent population of Vatican?
b. Where is the territory of the Vatican ?
c. What is Government of the Vatican?
d. Under what capacity has the Vatican City enter into a relationship with other countries.

Holy See is the supreme organ of the government for all Catholics World Wide.It does not have the capacity to say it represent a particular area or population.

Naomba majibu please.
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Kwa kuongezea nilikuwa nimesahau nanukuu kutoka kwenye kitabu:

According to the Montevideo Convention on the Rights and Duties of States: "The state as a person of international law should possess the following qualifications: a) a permanent population; b) a defined territory; c) government; and d) capacity to enter into relations with the other states."34 These four factual criteria for determining statehood are founded upon principles that have been accepted by a host of international law scholars and are consistent with the foreign laws of some nations.35 The Holy See does not satisfy this definition. Almost by definition, it does not possess a defined territory Because the Holy See is the supreme organ of government for Catholics worldwide, it cannot be said to have a "permanent population." Finally, the Holy See is itself the government of both the Roman Catholic Church and the Vatican City It cannot therefore be regarded as an entity that possesses a government.

Haya naomba majibu......
 
Aaaah Nguruvi siishiwi furaha ninaposoma comment zako, ukweli unagonga mle mle.

Yoso,

Hebu soma hii hapo chini huenda ukapata picha ya watu ninaowazungumza.
Huyu ni babu yangu Salum Abdallah aliyeishi kati ya mwisho 1890s hadi 1974:

Kleist Sykes na Salum Abdallah licha ya kuwa walikuwa majirani, walikuwa wakifanya kazi pamoja katika Tanganyika Railway na wake zao Bi Mluguru bint Mussa, mke wa Kleist, na Bi Zena bint Farijala mkewe Salum Abdallah walikuwa mashoga. Ushoga mkubwa kabisa wa kufuliana vidani vya dhahabu. Mabibi hawa bila ya kujua athari za ushoga wao wamekujakuwa hazina kubwa sana kuhusu maisha ya waume zao na katika kueleza maisha hayo leo tumekuja kufahamu mengi kuhusu maisha ya watu wa Dar es Salaam na nyakati zao. Bi Zena juu ya kuwa alikuwa mama wa nyumbani alikuwa mpenzi wa Harry Belafonte na kila alipopata nafasi alipenda kuieleza senema "Island in the Sun" kwa wajuu zake (mmoja wapo akiwa mwandishi) alocheza Belafonte. Senema hii ilikuja Tanganyika katika miaka ya mwisho ya 1950 na ilisisimua wengi kwanza kwa haiba ya Belafonte mwenyewe na nyimbo alizoimba katika senema ile. Lakini kubwa zaidi ambalo nahisi Waafrika wengi walotazama senema ile lililowaathiri ni ile hadith yenyewe, maana ilikuwa inahusu mapambano kati aya Waafrika na ukoloni wa Muingereza.

Vilevile kulikuwa na kisa cha mapenzi kati ya Harry Belafonte aliyekuwa nyota wa mchezo na msichana wa Kizungu. Kilichomfurahisha sana Bi Zena ni kule yule msichana wa Kizungu kukataliwa na mtu mweusi, Belafonte. Wakati ule Belafonte ndiyo alikuwa anainukia na nyimbo zake kama "Round the Bay of Mexico," "Banana Boat," "Jamaica Farewell" na nyimbo nyingine zilikuwa zikisikika katia radio kila siku. Biti Farijala kama alivyokuwa Biti Mluguru, waume zao ndani ya nafsi zao walichukia kutawaliwa na huenda katika mazungumzo yao ya faragha hili lilijitokeza mara kwa mara. Hali ya wakati ule haikuruhusu Waafrika kudai waziwazi haki yao ya kujitawala lakini mambo yalipowiva wazalendo wa Tanganyika hawakusita kumuomba Muingereza kufunga virago na kurejea kwao.

Salum Abdallah alihamia Tabora mwaka wa 1947 baada ya "locoshed" kama karakana ya treni ilivyokuwa ikijulikana, ilipohamishiwa Tabora na mwaka huo huo Salum Abdallah aliongoza mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa relwe. Mwaka wa 1947 African Association Tabora ilikuwa imejiimarisha vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kushiriki katika mgomo ambao ulianza katika bandari ya Dar es Salaam uliokuwa ukiongozwa na Dockworkers Union chini ya uongoziwa Abdulwahid Sykes. Mgomo ulitambaa hadi kufika Tabora na kuungwa mkono na wafanyakazi wa relwe. Siku ya mgomo wafanyakazi wengi wao kutoka karakana ya magari moshi ya wakiongozwa na Salum Abdallah, walikusanyika katika viwanja vya Tabora Town School chini ya miembe. Kuanzia siku hiyo viwanja hivyo vikawa ndiyo mahali pa mikutano yote ya African Association.

Salum Abdallah aliishi Tabora hadi Mungu alipomuhitimisha mwaka 1974 na katika umri wake alifanya mengi katika siasa. Akiwa mwanachama wa African Association kutoka Dar es Salaam aliendeleza harakati pale Tabora na mwezi June 1954 yeye alikuwa mmojawapo wa wanachama wa TAA waliokutana kwa siri Town School kufanya mipango ya kumleta katibu wa TAA Tabora Germano Pacha kuja Dar es Salaam kuasisi TANU tarehe 7 Julai 1954. Sheikh Abubakar Mwilima aliyekuwa mmoja wa walimu wa Town School alikuwa akiwakaribisha wanaharakati wa TAA kufanya mikutano yao pale shule katika moja ya madarasa. Salum Abdallah alikuwa mtu wa ari na akijiweza sana. Nyumba yake pale Isevya, Kanoni Street alipokuwa akiishi inasemakana ndiyo ilikuwa moja ya nyumba za mwanzo kupata maji ya bomba na umeme na kuwa na simu.

Salum Abdallah katika mkutano ule wa siri kuzungumzia kuunda TANU alitoa mchango wa shilingi ishirini kumsafirisha Pacha kuja Dar es Salaam. Wakati ule hizo zilikuwa fedha nyingi. Mwaka 1955 muda mfupi baada ya kuundwa TANU, Salum Abdallah alichaguliwa kama mwenyekiti muasisi wa Tanganyika RailwayAfrican Union (TRAU) chama cha wafanyakazi wa Reli kilichokuwa na nguvu sana wakati wa kupigania uhuru na kikitoa mchango mkubwa kwa TANU. Katibu wa TRAU alikuwa Chistopher Kassanga Tumbo. Mwaka 1960 TRAU chini ya uongozi huu iliiitsha mgomo uliodumu siku 82. Kwa takriban miezi mitatu si treni, meli na mabasi ya relwe yalitembea. Inasemekana hapajatokea mgomo ambao ulitayarishwa kwa ufundi na ustadi kama mgomo wa relwe wa mwaka 1960. Mgomo kama huu kamwe hautatokea tena.

TRAU ilipata fedha kutoka kwa rafiki zao Ujerumani ya Mashariki na wafanyakazi wa reli Uingereza. Msaada huu ndiyo uliowezesha TRAU kuhimili mgomo kwa miezi mitatu. Mwishowe serikali ya kikoloni ilisalimu amri na wafanyakazi wa relwe wakasitisha mgomo na kurudi kazini madai yao yote yakiwa yamekubaliwa. Mgomo huu miezi michache kabla ya Tanganyika kuwa huru ulimtisha sana Nyerere kwani alitambua kuwa kulikuwa na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliokuwa na nguvu sana na aliogopa baada Tanganyika kuwa huru vyama hivi chini ya viongozi kama hawa vitampa shida katika utawala wake. Katika mambo kama haya kunakuwa na mikasa mingi.

Salum Abdallah alikuwa na binti yake ambae kijana mmoja katika relwe alimpenda na akapeleka possa kwake kwa nia ya kutaka kufunga ndoa. Bahati mbaya kabla Salum Abdallah hajajibu posa ile mgomo ukawa umetokea. Sasa Yule kijana kwa bahati mbaya hakugoma kwa hiyo akawa katika kundi lililojulikana kama vibaraka. Salum Abdallah alihamaki sana kuwa yule kijana ambae alitegemea atajakuwa mkwe wake kaisaliti TRAU. Salum Abdallah akamwagiza mshenga wa yule kijana aje achuke majibu ya posa yake. Mshenga hakujua nini kinamsubiri. Siku ya siku ilipofika akajikusanya yeye na wenzake kwenda kupokea jibu la posa yao wakiwa na uhakika kuwa jibu litakuwa zuri na kitakachobaki ni kupanga siku ya harusi. Salum Abdallah alitoa kiti chake cha uvivu akakiweka sawasawa na mlango mkubwa wa nyumba yake anasubiri ujumbe ufike. Toka mbali Salum Abdallah anamuona mshenga na wapambe wake wale wanakuja na kanzu zao na kashda na ndani ya ujumbe kuna masheikh wawili watatu wa kuheshimika. Walitegemea chai nzito kwani Salum Abdallah hakuwa mtu mdogo katika jamii. Naam, hapakuwa chai wala salaam kama ilivyo kawaida wala Salum Abdallah hakumpa nafasi mchenga kusema chochote. Alinyanyuka na posa ya yule kijana akawatupia miguuni waiokote. Akawaambia, "Katafuteni mke kwa vibaraka wenzenu, nyumba yangu haingii kibaraka."

Huyo ndiye Salum Abdallah Muyiki Samitungo Mwekapopo. Mungu alimjalia tambo kasimama kama futi sita hivi. Akikuangalia tu unaondoka hata kabla hajakugusa. Mwezi wa Ramadhani wapiga ngoma ya daku watazunguka kote kisha watafika nyumbani kwake. Mwenyewe anakuwa kaka barazani anawasubiri. Wakishafika pale wanazima ngoma kama kuashiria kuwa sasa wanaingia katika "track" nyingie na hapo lile goma kubwa sondo litaanza kurindima kumwimbia nyimbo yake ya kumsifia ikiitwa "Ndege Mwema." Salum Abdallah atasikiza kisha atanyanyuka pale alipokaa atawaendea na kuwatunza fedha za kutosha hasa. Hapo watageuka na kuondoka huku "Ndege Mwema" ikirindima lakini kwa mpigo mwingine. Waswahili wana msemo, "Chini kunakwenda watu."

Yalipotokea maasi ya Tanganyika Rifles (TR) tarehe 20 Januari 1964, Salum Abdallah alikamatwa na kutupwa kuzuizini pamoja na viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na masheikh. Sababu zilizotolewa ni kuwa kulikuwa na njama za kupindua serikali ya Nyerere na viongozi hao pamoja na masheikh walihusika katika njama hizo. Shutuma nyingine hasa kwa masheikh ilikuwa masheikh walikuwa "wanachanganya dini na siasa." Mwaka wa 1963 Baraza la Wazee wa TANU lilivunjwa rasmi na sababu alizotoa Nyerere ni kuwa wazee waliokuwa katioka baraza hilo ambao wote walikuwa Waislam walikuwa "wanachanganya dini na siasa." Sintofamu kubwa kati ya Waislam na serikali ya Nyerere ilifuatia. Katika waazuoni maarufu waliokubwa na hali hii alikuwa Shariff Hussein Badawy na mdogo wake Mwinyibaba. Hawa walikuwa walimu katika Masjid Badawy Kisutu karibu na Soko Mjinga. Msikiti huu sasa unaitwa Rawdha. Hawa walifukuzwa nchini na kurejeshwa kwao Mombasa. Ilikuwa katika utawala wa Ali Hassan Mwinyi ndipo waliporuhusiwa kurudi tena Tanzania. Shariff Hussein wakati ule miaka 1960 alikuwa kijana na akicheza mpira club ya Cosmopolitan. Matatizo haya yakaendelea hadi kufika mwaka 1968 Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika na Zanzibar nae akakamatwa na kurejeshwa Zanzibar na akapigwa marufuku asifike Tanzania Bara kama alivyofanyiwa Shariff Hussein Badawy na mdogo wake Mwinyibaba.

Salum Abdallah alipotoka kizuzini jela ya Uyui, si tu aliichukia TANU chama alichokipenda bali alimchukia hata Nyerere mwenyewe na hakujihushisha tena na siasa na alitumia muda wake mwingi katika ukulima wa tumbuku Urambo na alifanikiwa sana. Jina la Nyerere lilikuwa halitajwi katika nyumba yake. Katika mazishi yake TANU ilikuja na ilisoma taazia iliyomsifu sana Salum Abdallah kuwa alikuwa mzalendo wa kweli na aliupigania uhuru wa Tanganyika kwa dhati. Haya ndiyo katika maajabu wa siasa. Kabla hajafa Salum Abdallah akitembea na shutuma kuwa yeye na wenzake walipanga njama za kupindua serikali ingawa kesi ile ya maasi ya jeshi ilipokwenda mahakamani Salum Abdallah na viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi na msheikh hawakuunganishwa katika mashtaka ya uhaini.
 
Wickama, naomba nichangie hoja zako kidogo. Zimenigusa na afadhali mwingine aseme maana sisi tushapewa kila tusi na kila jinaNa katika kuhakikisha kuwa ''lens'' inalenga alipotarajia ametumia utafiti kwa kuondoa baadhi ya viungo muhimu vya historia au kulazimisha baadhi ya mambo.Mfano, katika kuondoa mambo ameweza kumuondoa mwanzilishi wa AA kwa vile yeye si mlengwa wa lens, amemuondoa rais wa TAA kwa nyakati fulani kwasababu si mlengwa.

Amefunika majina na matukio kwasababu hayakulengwa. Na katika kulazimisha mambo amefikia mahali pa kulazimisha kuwa AA ilkuwa chama cha familia na kwamba TANU haikundwa mwaka 1954 na wala Nyerere hakuwa rais wake wa kwanza bali alikabidhiwa chama kutoka kwa wazee wake.

Laiti angefanya utafiti wa kweli na unaokubalika kitafiti hakuna shaka kuwa wasomaji wangeweza kufikia conclusion pengine inayokubaliana na masuala yake bila kutia chumvi, kumwagia maji, kumdhalilisha mtu au kumkwezaNa hata kwenda mbali na kuwagawa wazee wa AA na TAA kwa kutumia Uzulu na Umanyema.
Kila aliyefanya jambo jema basi kiunganisho cha Uzulu au umanyema kinatangulia.
Mohamed anatumia majina ya wakoloni kwasababu wanajulikana dini yao, kwa Nyerere ni ngumu kama hakuna kiunganisho baina yake na wakoloni ambacho ni dini yake.Kuna ushihidi wa maelezo ya wazee hao kutoka kwa Mohamed yakionyesha kuwa, wazee walipigana na ukoloni ili kumkomboa Mwafrika na hakuna ushahidi wa kitafiti unaonyesha kuwa walijiunga kwa ajili ya kupigania Uislam tu.

Hata pale walipojiunga kama AMNUT jitihada zao zilipingana na walio wengi na kujikuta wakiwa hawana mahali pa kusimamia.
Hicho ndicho kiliua AMNUT.Katika kujenga hoja kigezo kimoja kinaweza kuvunja nguvu ya hoja na mantiki ya lens.
Kwahiyo utafiti ulikuwa na variable values kulingana na wakati gani mtafiti alitaka jambo liwe.

Hakuna ushahidi wa kuwa na katiba iliyotoa fursa kwa wazee kutoa offer kwa ''wakuja'' kinyume chake wazee hao waliungana na Mwalim hata katika mambo waliyokuwa tofauti kama imani za dini wakiwa na lengo moja kutuweka huruBila kumlaumu Nyerere dhana nzima itakuwa haina mashiko.
Ni lazima kiwepo chanzo cha matatizo na hapa chanzo ni Nyerere.

Lakini pia Nyerere ni ''conduit'' the final destination ni kwa wakristo ili baadaye ijengwe hoja kama ya mfumo kristo ambao hauna maelezo yanayojisimamia isipokuwa kwa kuunga unga na kiunganisho kizuri kati ya kanisa na waislam, waislam na wakoloni ni Nyerere. Ukimuondoa Nyerere ingawa historia hairuhusu kimantiki basi unavunja link iliyotarajiwa.Kwa maneno mengine Nyerere ni victim of circumstanceAgakhan ndiye alikuwa mlezi wa EAMWS na tangu imevunjwa amebaki katika shirika lake na Tanzania akifanya yale aliyotarajia.
Ndivyo wafanyavyo Mabohora na Mashia ambao wana shule na Hospitali zao wenyewe kwa mipango yao.

Ukiangalia hayo kwa jicho hilo utakuwa umekwenda kupata jawabu lisiloshabihiana na lens ya utafiti.
Njia rahisi na ya mkato ni kutumia Nyerere kuua EAMWS kwa mfumokristo ambao umeshika sehemu zote na hivyo kuzuia ujenzi wa chuo cha ufundi Kibaha hadi kikahamishiwa Mbale Uganda!!

Jitihada za matajiri unaosema kujenga huduma za jamii zinakwazwa na mfumo alioasisi Nyerere na alioupokea kutoka kwa mkoloni. Ndiyo maana nilisema ukimuondoa Nyerere kutoka katika hadithi hii basi utakuwa umekosa link muhimu na link hiyo ndiyo inayowasamehe matajiri kutoa huduma za jamii zaidi ya zile za burudani.

Ni makosa hayo ndiyo yanapelekea kuanzishwa kwa TV na Redio ambazo badala ya kuiangalia jamii na matatizo yake kwa ujumla zimekuwa mstari wa mbele kufanya elimu inayopingana na dhana nzima ya habari.

Badala ya kujadili kwanini kunatatizo katika huduma za jamii kwa jamii husika, vyombo hivyo vimekuwa vinajadili kwanini fulani anafanikiwa kwa njia zisizotoa elimu. Wivu wa maendeleo ni tofauti na wivu wa chukiNa wala tatizo si kuandika MoU na serikali, dunia sasa hivi inahitaji wasomi hivyo basi ni muhimu chuo hicho kikawa na elimu bora watu wataajiriwa kabla hawajamaliza.

Moja ya sifa ya UDSM ni kutoa wanasheria nguli ukanda huu wa Afrika Mashariki. Ni heshima hiyo ndiyo inapelekea wahitimu wake kuhitajiwa katika soko na wala si upendeleo.

Zama hizo ukiwa umetoka Arusha Tech, Tanga Tech School au Dar Tech wewe ni mwajiriwa tu.
Ubora kwanza, lakini je kuna watu wanaliona hilo endapo tayari wanafikra kuwa wao ni duni?

Je, yule anayepanga kupeleka wanafunzi kuandamana kesi ya Ponda ana muda wa kujali ubora wa elimu?
Je,mtu anayefikiri kuwa chuo kikuu kilikuwa kijengwe mwaka 1967 anawazo la kuboresha chuo hicho mwaka 2013?Nadhani atakuwa na jibu na atatusaidia sana.Siyo kujipanga tu, tatizo zito zaidi ni kujitazama na kujitathmini.

Huwezi kutafuta maendeleo huku ukiidhulumu nafsi yako kuiambia ukweli. Chuo cha Ufundi kilichohamishiwa Mbale tatizo si kiwanja au kibali, tatizo ni pesa kutafunwa kabla ya mradi.Kama watu hawakubali ukweli huu ni upi wataukubali?
Kama watu wanatafuta visingizio kuficha ukweli huu, ukweli halisi utatoka kwa nani?

Na wala mtu asidhani huko makanisani ni salama, pesa na miradi inatafunwa sana.
Tofauti ni kuwa wao hawatafuti ''mbuzi wa kafara'' wanahangaika na tatizo lao wakijua limetoka kwao.

Kwanini basi Mohamed asijiulize kwenye shule ya watoto 250 na walimu 2 uwezekano wa kupata mwanafunzi wa kuingia chuo kikuu ni asilimia ngapi na ni nani wa kulaumiwa endapo shule hiyo inaongozwa na waislam wenyewe.
Kwanini watu wadhani NECTA ndio kikwazo, hivi huo ndio ukweli? Ndiyo maana nasema kuna tatizo ni kujitathmini.
Leo kuna taasisi zaidi ya 10 Dar es Salaam. Kama haziwezi kuwa under one umbrella ili kuiondoa Bakwata automatically nani wa kulaumiwa?Katika miaka ya 70 na 80 shule kama Kibohehe ilikuwa hotcake. Guess what, mwalimu mkuu alikuwa anaitwa T.G Martin, walimu walipewa kazi kwa sifa na si majina.

Sasa hivi hilo linaonekana kama ni tatizo ni heri mwanafunzi wa form six kuliko mwenye shahada kwasababu tu anajina tofauti.
Kwa mtazamo huo hivi watu hawaoni tatizo kweli hadi watafute uzi wa kumuunganisha Nyerere na matatizo yaliyo usoni mwao.
Mohamed Said hawezi kuwa na majibu kwenye hizi hoja, atakchofanya ni kuwatuma watwana wake waje na majibu mepesi yaliyojaa kejeli na vijembe vya kitoto. Kwa mtu kama Ritz tofauti na wapiga kelele wengine ukweli huu anauona lakini anaogopa kumsaliti mzee wake Mohamedi.
 
Jasusi,
Ahsante sana ndugu yangu.

Damu nzito kuliko maji.
Umetaabika kuona nduguyo nasulubiwa.

Othman Chande sasa ni prof. wa kemia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Bubby yuko Dar anaendesha garage ya kaka yake Mushtak.

Wendo Mwapachu mjasiriamali alioa kwa kina Chagula.
Hatuchezi mbali na ni babu sasa.

Abdu Mtemvu yuko mjini Dar.

Mohamed Chande Jaji Mkuu kaoa kwa Mzee Maamry
Waarabu wenzao.

Umemsahau Yusuf Zialor marehemu.

Alitajirika sana akahamia London na mkewe Shufaa na watoto.
Wakiishi Surrey nyuma ya Wembley Stadium.

Nikiwatembelea sana miaka ya 1990s.

Ebby Sykes mimi na Ebby tumepishana siku moja kuzaliwa.

Kitanda alicholazwa mama yake Ebby Bi. Regina ndicho kalala
mama yangu siku ya pili nikazaliwa mimi.

Abraham ni babu sasa yuko Dar ana mtoto saizi ya mjukuu wake.
Hahahaha!

Ukija Dar utakuwa mgeni mambo na watu wamebadilika sana lakini
mapenzi ni makubwa sana tukikutana.

Shida ni kuwa mpaka afe mtu ndiyo tunakutana.
Hii hainifurahishi sana.
Bora umekiri wazi kwamba unasulubiwa na wanozijua hoja! chezea Nguruvi3 weye!
 
Nashindwa kumtofautisha mzee MS na SHEIKH ILUNGA.. Labda wanajamvi mnaweza nisaidia
 
Hongera MS kwa ku-reveal the truth, ni wenye fikra tegu na zilizotangulizwa na ghiriba ndio watakaokupinga, endelea kutujuza ndugu yetu
 
Nashindwa kumtofautisha mzee MS na SHEIKH ILUNGA.. Labda wanajamvi mnaweza nisaidia
Remote, hawana tofauti hao, lao moja, na kila siku wapo sebuleni kupanga hila na uovu dhidi ya watanzania wenzao kwa kisingizio cha kumuenzi allah!
 
Back
Top Bottom