Wickama, naomba nichangie hoja zako kidogo. Zimenigusa na afadhali mwingine aseme maana sisi tushapewa kila tusi na kila jina
Wickama;5994279]Huu mjadala ni mzuri sana. Ila kuna jambo ambalo kwa maoni yangu Ndugu yangu Mohammed Said analikosea au labda kwa bahati mbaya hajaliona. Ni kwamba ukichukua msimamo fulani katika mjadala, lazima uwape usawa unaowazungumza. Mzee Mohammed Said umeamua kuyatazama matukio yote ya kabla ya uhuru na baada yake kwa "lens" ya uislamu na waislamu
Na katika kuhakikisha kuwa ''lens'' inalenga alipotarajia ametumia utafiti kwa kuondoa baadhi ya viungo muhimu vya historia au kulazimisha baadhi ya mambo.Mfano, katika kuondoa mambo ameweza kumuondoa mwanzilishi wa AA kwa vile yeye si mlengwa wa lens, amemuondoa rais wa TAA kwa nyakati fulani kwasababu si mlengwa.
Amefunika majina na matukio kwasababu hayakulengwa. Na katika kulazimisha mambo amefikia mahali pa kulazimisha kuwa AA ilkuwa chama cha familia na kwamba TANU haikundwa mwaka 1954 na wala Nyerere hakuwa rais wake wa kwanza bali alikabidhiwa chama kutoka kwa wazee wake.
Laiti angefanya utafiti wa kweli na unaokubalika kitafiti hakuna shaka kuwa wasomaji wangeweza kufikia conclusion pengine inayokubaliana na masuala yake bila kutia chumvi, kumwagia maji, kumdhalilisha mtu au kumkweza
Hakuna Mwingereza hapa (kuna Mwanglikana) na hakuna Nyerere hapa wala Wajerumani (kuna Mkatoliki au Ukatoliki). Mtazamo wa mzee Mohammed Said lazima utampa jibu moja tu kwamba waislamu ndio waliopigania uhuru, ndio waliosimamia harakati zote n.k. Tatizo la "position" yako ni kuwa unapotaja dhulma za wakoloni sasa unatumia utaifa wao badala ya dini zao. Unapomtaja Mwl. Nyerere ajabu unatanguliza Ubara (U-musoma) wake kwanza (sio Ukatoliki)lakini unapotaja wazee wa TAA na TANU unatanguliza uislamu wao kwanza na sio kabila zao.
Na hata kwenda mbali na kuwagawa wazee wa AA na TAA kwa kutumia Uzulu na Umanyema.
Kila aliyefanya jambo jema basi kiunganisho cha Uzulu au umanyema kinatangulia.
Mohamed anatumia majina ya wakoloni kwasababu wanajulikana dini yao, kwa Nyerere ni ngumu kama hakuna kiunganisho baina yake na wakoloni ambacho ni dini yake.
Unapotaja askari waliopindua zanzibar unahamia KABILA lao kwanza, sio dini yao. HAPA HAPAKUBALIKI. Unatakiwa ulete Ushahidi Mzee Mohammed Said kwamba wazee wa TAA na TANU enzi hizo walijiunga pamoja kama WAISLAMU TUU NA SIO WAAFRIKA WA TANGANYIKA.
Kuna ushihidi wa maelezo ya wazee hao kutoka kwa Mohamed yakionyesha kuwa, wazee walipigana na ukoloni ili kumkomboa Mwafrika na hakuna ushahidi wa kitafiti unaonyesha kuwa walijiunga kwa ajili ya kupigania Uislam tu.
Hata pale walipojiunga kama AMNUT jitihada zao zilipingana na walio wengi na kujikuta wakiwa hawana mahali pa kusimamia.
Hicho ndicho kiliua AMNUT.
Leta ushahidi kuwa wazee hao walimwalika asiyekuwa mwislamu kujiunga nao kinyume na katiba ya chama chao. Naomba ujibu, kuwa Umoja wa Mataifa ulikabidhi koloni la Tanganyika kwa Kanisa la Anglikana au kwa himaya ya Kiingereza? Binafsi napinga kabisa kuchangaya kuwaita baadhi ya watu ni wa Musoma au Wajerumani au Waingereza huku huku kundi moja umeamua kuliita ni la kiislamu. Lazima uchague kigezo kimoja na ukitumie hicho kwa mjadala wote.
Katika kujenga hoja kigezo kimoja kinaweza kuvunja nguvu ya hoja na mantiki ya lens.
Kwahiyo utafiti ulikuwa na variable values kulingana na wakati gani mtafiti alitaka jambo liwe.
Hakuna ushahidi wa kuwa na katiba iliyotoa fursa kwa wazee kutoa offer kwa ''wakuja'' kinyume chake wazee hao waliungana na Mwalim hata katika mambo waliyokuwa tofauti kama imani za dini wakiwa na lengo moja kutuweka huru
Kama unaangalia dini zao tuu, basi yabidi tutumie kigezo hicho kwa wote kuanzia wazee wa TANU hadi ma-settler. Nimeona muda mwingi sana Mzee wangu Mohammed Said umeutumia kumlaumu Mwl Nyerere.
Bila kumlaumu Nyerere dhana nzima itakuwa haina mashiko.
Ni lazima kiwepo chanzo cha matatizo na hapa chanzo ni Nyerere.
Lakini pia Nyerere ni ''conduit'' the final destination ni kwa wakristo ili baadaye ijengwe hoja kama ya mfumo kristo ambao hauna maelezo yanayojisimamia isipokuwa kwa kuunga unga na kiunganisho kizuri kati ya kanisa na waislam, waislam na wakoloni ni Nyerere. Ukimuondoa Nyerere ingawa historia hairuhusu kimantiki basi unavunja link iliyotarajiwa.Kwa maneno mengine Nyerere ni victim of circumstance
Hivi ni kweli kwamba matajiri wa kiislamu waliosheheni nchi hii, ni mfumo kristo unawazuia kujenga hospitali na chuo kikuu? Mbona kila leo twawaona wakigharamia burudani za gharama mbaya? Lakini, kina Aga Khan ni dini gani? Mbona wao wana vyuo vikuu na mahospitali makubwa? Wamekwepaje hujuma za mfumo Kristo? Au hawa Answar Sunna na hela zao wanazoanzishia redio na TV nani kawazuia kuanzisha hospitali ya maana?
Agakhan ndiye alikuwa mlezi wa EAMWS na tangu imevunjwa amebaki katika shirika lake na Tanzania akifanya yale aliyotarajia.
Ndivyo wafanyavyo Mabohora na Mashia ambao wana shule na Hospitali zao wenyewe kwa mipango yao.
Ukiangalia hayo kwa jicho hilo utakuwa umekwenda kupata jawabu lisiloshabihiana na lens ya utafiti.
Njia rahisi na ya mkato ni kutumia Nyerere kuua EAMWS kwa mfumokristo ambao umeshika sehemu zote na hivyo kuzuia ujenzi wa chuo cha ufundi Kibaha hadi kikahamishiwa Mbale Uganda!!
Jitihada za matajiri unaosema kujenga huduma za jamii zinakwazwa na mfumo alioasisi Nyerere na alioupokea kutoka kwa mkoloni. Ndiyo maana nilisema ukimuondoa Nyerere kutoka katika hadithi hii basi utakuwa umekosa link muhimu na link hiyo ndiyo inayowasamehe matajiri kutoa huduma za jamii zaidi ya zile za burudani.
Ni makosa hayo ndiyo yanapelekea kuanzishwa kwa TV na Redio ambazo badala ya kuiangalia jamii na matatizo yake kwa ujumla zimekuwa mstari wa mbele kufanya elimu inayopingana na dhana nzima ya habari.
Badala ya kujadili kwanini kunatatizo katika huduma za jamii kwa jamii husika, vyombo hivyo vimekuwa vinajadili kwanini fulani anafanikiwa kwa njia zisizotoa elimu. Wivu wa maendeleo ni tofauti na wivu wa chuki
Sote twaona bidii ni kushushua zaidi waislamu wenziwao. Bakwata wana Chuo Kikuu cha Waislamu pale Morogoro, sasa kosa liko wapi kama wakiandikiana MoU na Serikali kuhusu wahitimu wake kupata kazi pindi wakimaliza?
Na wala tatizo si kuandika MoU na serikali, dunia sasa hivi inahitaji wasomi hivyo basi ni muhimu chuo hicho kikawa na elimu bora watu wataajiriwa kabla hawajamaliza.
Moja ya sifa ya UDSM ni kutoa wanasheria nguli ukanda huu wa Afrika Mashariki. Ni heshima hiyo ndiyo inapelekea wahitimu wake kuhitajiwa katika soko na wala si upendeleo.
Zama hizo ukiwa umetoka Arusha Tech, Tanga Tech School au Dar Tech wewe ni mwajiriwa tu.
Ubora kwanza, lakini je kuna watu wanaliona hilo endapo tayari wanafikra kuwa wao ni duni?
Je, yule anayepanga kupeleka wanafunzi kuandamana kesi ya Ponda ana muda wa kujali ubora wa elimu?
Je,mtu anayefikiri kuwa chuo kikuu kilikuwa kijengwe mwaka 1967 anawazo la kuboresha chuo hicho mwaka 2013?
Nimeona nakala ya MoU humu kwenye mjadala, WRONG. Nyie hamkutakiwa eti kuleta nakala ya Mou kati, ya Taasisi ya Kikristo na Serikali kuhusu Taasisi hiyo kupata faida TOKA serikalini, hapa mlitakiwa kuleta MoU au mawasiliano yoyote ya siri kati ya Makanisa (moja au yote)na Serikali kwamba ikitokea Waislamu wakajipanga na kuja na "a similar request" basi WASIPEWE au HAWATAPEWA. Hiyo ndio ilikuwa hoja. Ile MoU haina mahali inaahidi hujuma kwa waislamu. Sasa kilio cha kubeba documents za wenzio ni cha nini? Hapa paletwe ushahidi kuwa mwaka fulani serikali ilikataa kutiliana MoU na waislamu juu ya Taasisi fulani japo ilishawekeana MoU na wakiristo. Ni vizuri sana Ndugu yangu Mohammed Said akajua kuwa tatizo kubwa la Waislamu hapa nchini ni katika kujipanga.
Nadhani atakuwa na jibu na atatusaidia sana.Siyo kujipanga tu, tatizo zito zaidi ni kujitazama na kujitathmini.
Huwezi kutafuta maendeleo huku ukiidhulumu nafsi yako kuiambia ukweli. Chuo cha Ufundi kilichohamishiwa Mbale tatizo si kiwanja au kibali, tatizo ni pesa kutafunwa kabla ya mradi.Kama watu hawakubali ukweli huu ni upi wataukubali?
Kama watu wanatafuta visingizio kuficha ukweli huu, ukweli halisi utatoka kwa nani?
Na wala mtu asidhani huko makanisani ni salama, pesa na miradi inatafunwa sana.
Tofauti ni kuwa wao hawatafuti ''mbuzi wa kafara'' wanahangaika na tatizo lao wakijua limetoka kwao.
Kwanini basi Mohamed asijiulize kwenye shule ya watoto 250 na walimu 2 uwezekano wa kupata mwanafunzi wa kuingia chuo kikuu ni asilimia ngapi na ni nani wa kulaumiwa endapo shule hiyo inaongozwa na waislam wenyewe.
Kwanini watu wadhani NECTA ndio kikwazo, hivi huo ndio ukweli?
Lakini eti leo miaka 45 baadaye ukilalamika Waislamu haturuhusiwi kujipanga ila kupitia kibaraka Bakwata Wallah mimi sikuelewi. Hivi wanaoitukana Bakwata kupitia redio na TV zao ni dini gani? wao wanaruhusiwa na nani? Nyerere pia?
Ndiyo maana nasema kuna tatizo ni kujitathmini.
Leo kuna taasisi zaidi ya 10 Dar es Salaam. Kama haziwezi kuwa under one umbrella ili kuiondoa Bakwata automatically nani wa kulaumiwa?
Nenda Mwanza, Iringa, Bukoba na Kilimanjaro utakuta Waislamu wasio na manunguniko yasiyoisha. Wao ni kujenga shule na kutafuta waalimu wazuri, shule zinafanya vizuri na hata wakiristo wanapeleka watoto huko.
Katika miaka ya 70 na 80 shule kama Kibohehe ilikuwa hotcake. Guess what, mwalimu mkuu alikuwa anaitwa T.G Martin, walimu walipewa kazi kwa sifa na si majina.
Sasa hivi hilo linaonekana kama ni tatizo ni heri mwanafunzi wa form six kuliko mwenye shahada kwasababu tu anajina tofauti.
Kwa mtazamo huo hivi watu hawaoni tatizo kweli hadi watafute uzi wa kumuunganisha Nyerere na matatizo yaliyo usoni mwao.