Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Remote, hawana tofauti hao, lao moja, na kila siku wapo sebuleni kupanga hila na uovu dhidi ya watanzania wenzao kwa kisingizio cha kumuenzi allah!

labda tuseme tofauti yake na Ilunga ni kwamba Ilunga yupo straight katika madhumuni yake na MS moyoni pia anaghiliba na madhumuni kama ya Ilunga ila anatumia njia ya kuzunguka.
 
Son of Alaska,

Naye alituambia kuwa ndani ya masaa 24 ataiweka hiyo hotuba leo unakwenda mwezi wa nne hakuna hotuba wala asemi chochote tena.

Ameona ni afadhali amgeukie Sheik Kassim bin Jumaa na kumpakazia! hawa ndio wale wanaowavua wenzao utanzania pindi wapatapo kibano!
 

Nani kakuambia Morogoro University ni ya Bakwata? ulifanya utafiti lini na kugundua Waislamu wa Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba na Iringa hawanunguniki? Kilimanjaro kuna Shule 2 za Waislamu zisizo za Bakwata Kirinjiko na Mudio zinazojitahidi kuinua vipaji na elimu ya Wanafunzi! kuna Shule nyingi za Bakwata ambazo kwa kweli haziridhishi! sasa wewe unazungumzia Shule au Waislamu kwa ujumla wao? Waislamu wa maeneo haya wanaathirika sana kimfumo kama wenzao wa maeneo mengine! malalamiko yako na kero zote za Waislamu wa nchi hii hazina mipaka! mfumo kristo unatandika kila mahali bila kujali huyu ni Kilimanjaro au Mwanza!
 
Ahahahah..Nguruvi3 wewe wazee wako ni wa mkoa gani?
Mbona swali gumu hili! najaribu nikishindwa nitakupa Jibu jepesi.

Wazee wangu ni wale wa Nyakatende hadi Mugango.Shirati hadi Kinesi. Kuanzia Lizabon hadi Peramiho. Wapo pia Isevya, Magila, Pongwe, Mjasani, Amani.Ninao kule Nanjoka, Mchukwi na Ikwiriri. Kuna wengine Bigwa Mwarusembe hadi Nyamato. Nyangao na Itigi. Kote Haidom hadi Longido na Maneromango. Malinyi Mtimbira hadi Mlimba na Mikindani. Kidogo basi mpaka viwanja sitini kupitia kidodi na Zignali, kwamtipura, kiembe samaki, bububu hadi mifenesini Mtaa wa Matombo, Ilala boma, Mkunguni nyumba ya nne kabla ya msikiti wa Manyema.
Orodha ni ndefu. Simply wazee wangu ni Watanzania wote walionitangulia ''waswahili au wakuja''
 
Ahahahhahah..Ubarikiwe sana mkuu.
 
Je, yule anayepanga kupeleka wanafunzi kuandamana kesi ya Ponda ana muda wa kujali ubora wa elimu?

Na wale wanaopanga kupeleka vijana mahakamani kesi ya Lwakatware na kupanga kuandamana kila mara nao wana muda wa kujali elimu?
 
Ngano hii si fundisho la historia ya uhuru wetu, bali masimulizi ya mzee wako Salum Abdala.

Haijabeba historia ya uhuru wa Tanganyika na Julius Nyerere, bali imebebwa na historia ya Tanganyika na Julius Nyerere.
 
Mohamed Said,

..Thank u.

..ndiyo maana wengine tunaendelea kusisitiza kwamba matatizo ya Nyerere na wazee wako yalikuwa ni SIASA, na siyo dini.

..katika bandiko lako umesahau kumtaja Balozi Christopher Kassanga Tumbo kwamba aliwekwa kizuizini muda wote wa utawala wa Mwalimu Nyerere na alikuja kutolewa wakati Mzee Mwinyi anakaribia kuondoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Mh JokaKuu akimtia Balozi Christopher Kassanga Tumbo unadhani jukwaa aliloamua kulisimamia litamtosha.


 
Last edited by a moderator:

Joka Kuu,

Katika uandishi huwezi kuwalazimishe wasomaji wafikiri utakavyo.

Katika ugomvi wa babu yangu na Nyerere ambao ulianza 1962 kisa
kilikuwa siasa hapakuwa na suala la dini baina yao.

Ingawa baada ya hapo mengi yakaingia katika siasa za wakati ule na
dini ikawa moja ya sababu za farka.

Lakini Joka umemuona babu yangu?

Basi wakati ule wa mgomo miezi mitatu kavaa jampa suti ya khaki na hat
yuko vitani.

Halafu huwezi kusimamanae uso kwa uso dakika mbili utakuwa flat.

Siku alipojipeleka mwenyewe polisi aligoma kuingia selo na mkuu wa kituo
alikuwa kalasinga wanafahamiana vyema.

Hakuna askari aliyethubutu kumsogelea na yule Mkuu wa Kituo alijua hapa
inaweza ikaja hatari maana itabidi aonyeshwe silaha.

Ilibidi amrai sana na baba yangu mdogo alikuwapo pale na yeye alisaidia sana
hadi akaingia katika selo bila ya mtu kumgusa.

Bibi yangu alikuwa akiniombea dua akisema kwa utani, ''Mume wangu nakupenda
sana lakini naogopa huo wazimu wenu sasa sijui kama na wewe umerithi mie
wanangu Allah kawanusuru, nawe Allah akunusuru.''
 
Ngano hii si fundisho la historia ya uhuru wetu, bali masimulizi ya mzee wako Salum Abdala.

Haijabeba historia ya uhuru wa Tanganyika na Julius Nyerere, bali imebebwa na historia ya Tanganyika na Julius Nyerere.

Bwana Nyerere,
Hakika ni simulizi za babu yangu.

Ukipenda unaweza ukaitenganisha historia ya wafanyakazi
na historia ya uhuru wa Tanganyika na ya Baba wa Taifa.

Elimu ni bahari.

Unaweza ukadanda na huo mwelekeo wako ukaandika kitu
kikapata reviews katika majarida makubwa ya historia duniani.
 
Ameona ni afadhali amgeukie Sheik Kassim bin Jumaa na kumpakazia! hawa ndio wale wanaowavua wenzao utanzania pindi wapatapo kibano!

Kadogoo,

Soma hii excerpt kutoka pp niliyotoa Chuo Kikuu Cha Kenyatta, Nairobi mwaka 2007 kuhusu Sheikh Kassim itakupa mwanga
wa mtu huyu na siasa alizokuwa akizicheza ambao mwishowe zilimwangamiza lakini kwa upande mmoja alipata alichokuwa akikitafuta:

''...Sheikh Kassim convinced that President Mwinyi as well as Prof. Malima were targets for attack because of their faith and nothing else, stood up to defend Mwinyi's rule.

Not having the instrument of power under his full control as the bureaucracy had their allegiance elsewhere, President Mwinyi could not influence public opinion nor could he control the state administrative machinery.

For the first time Sheikh Kassim's oratory skills, were put to defend not only President Mwinyi but Islam as well.

Sheikh Kassim began to mobilise Muslims to stand up against an unjust Christian dominated government.

Sheikh Kassim's Friday khutba changed assuming militant posture full of political rhetoric attacking the press and Christians whom he accused of undermining Mwinyi's rule simply because the Church could not stand a Muslim head of state.

Sheikh bin Kassim Juma in broad day light and with loud speakers blaring full blast at his Mtoro Mosque more than once mentioned Julius Nyerere, the former president, by name as an enemy of Islam.


Muslims were thrilled by Sheikh Kassim's khutbas and his sudden change against the establishment and Nyerere, his mentor.

Muslims in thousands now thronged the Mtoro Mosque to come and listen to Sheikh Kassim's Friday khutbas.

Mtoro Mosque overnight became a centre of resistance against forces opposing Mwinyi's rule. Sheikh Kassim called upon Muslims to rise up and over-throw the Christian dominated government which had oppressed them since independence.

Sheikh Kassim's khutbas were recorded in cassettes and distributed by the Ansar Sunna movement throughout the country.

The press scandalised, ridiculed and poked fun at President Mwinyi with impunity, at times even questioning his appointments of Muslim functionaries.

The press also insinuated on the dropping from the cabinet of Kingunge Ngombale Mwiru, Getrude Mongela and Joseph Warioba as being influenced by religious sentiments.
[1]

Included in this war of words were selected Muslim Ministers.

It seemed Christians were irked that those powerful portfolios were in Muslims hands. The government and party owned media seemed to have lost allegiance to the government including loyalty to the president himself.

President Ali Hassan Mwinyi, Prof. Kighoma Malima, Fatma Said Ali, Hassan Diria then Minister of Foreign Affairs and International Co-operation and Mustapha Nyang'anyi became favourite targets of ridicule by the private tabloids.

Sheikh Kassim mobilised Muslims to stand firm behind President Mwinyi and all Muslims in his cabinet.

The Christian lobby was quietly waiting for the chance to get even with "Muslim fundamentalist" and teach them a lesson.

That chance came during Easter holidays in 1993 in the form of pork riots.
..


[1] See "Mwinyi's Dilemma," New Afrcan, June, 1989, Also Tanzania's Religious Politics," New African, November, 1989. Also see "Religious Controversy in Tanzania," Africa Events, November, 1989 and Warsha, ''Fitina inayotukabili Waislam 14 Julai, 1989, Dhul Haj,'' 1409 H.
 
labda tuseme tofauti yake na Ilunga ni kwamba Ilunga yupo straight katika madhumuni yake na MS moyoni pia anaghiliba na madhumuni kama ya Ilunga ila anatumia njia ya kuzunguka.

Remote,

Mimi huwezi kunilinganisha na Sheikh Ilunga.
Ilunga ni alim.

Mimi napiga goti nasomeshwa na Sheikh Ilunga.

Mimi akiwapo siwezi hata kunyanyua sauti yangu
kunong'ona achilia mbali kusema.

Heshima ya Sheikh Ilunga iko juu sana kwa Waislam.

Ndiyo maana umeona yeye ndiye aliyeaminiwa kutembea
nchi nzima kuwazindua Waislam kuhusu mfumokristo.

Mimi siwezi hata kumbebea viatu vyake.
 
Na wale wanaopanga kupeleka vijana mahakamani kesi ya Lwakatware na kupanga kuandamana kila mara nao wana muda wa kujali elimu?

Kadogoo,

Nilikuwa naangalia mashindano ya magari Formula 1 Malaysian Grand Prix huku nakunywa gahawa na kashata za Jidah nimesoma post yako nimecheka sana.
 
Nina uhakika Mohamed hutajibu swali hilo hapo juu. Utasubiri baada ya post kadha unirushie kombora la matusi.

Kwanza nikuulize, unaposema ameaniwa na waislam ni waislam wapi hao kwa kuzingatia kuwa wapo BAKWATA na makundi mengine kila moja likiwa na agenda yake?

Mohamed Ilm si vitabu, paper au machapisho tu. Ilm ni maarifa aliyo nayo mtu katika kukabiliana na mazingira yake kwa ujumla.
Kitu muhimu sana kwa mwenye Ilm ni mawasiliano.Endapo mtu hana mawasiliano basi hapo Ilm inakosa maana yake halisi.

Sijui Sheikh Ilunga ana Ilm ya kiwango gani katika hii iitwayo elimu dunia hadi kufikia mahali pa kupewa jukumu la kuueleza mfumo nchi nzima.Sijui kama anachokiongea anafahamu madhara na athari zake.

Nisichokubaliana nawe ni hoja ya kumpa wadhifa wa kuongea kwa niaba ya waislam.
Nina uhakika katika waislam wanaomsikiliza na kumfuatilia wapo mamilioni wasiokubaliana na hoja zake.
Hao nao umeamua kuwachanganya na wale wanaokubaliana naye katika chungu kimoja cha waislam ''wamemtuma''

Ukiangalia ile video ni ngumu sana kuamini kuwa bado unaweza kusimama na kusema ametumwa na waislam.
Hata wewe tumekuuliza unakubaliana na video ile? hakika hukujibu kwasababu unafahamu wazi kuwa kile si kitu sahihi kidini, kidunia na kijamii.

Wapo waislam si kuwa wameudhika bali kukirihika sana na maneno ya mentor wako.

Labda utupe Ilm sisi wengine kuhusu Uislam ya kuwa wapi imeelezwa kuwa dini ya uislam itaenezwa kwa chuki na farki?
Je, yale maneno (niwieni radhi kama nitakosea) yanayosema '' walinganieni wasio waislam kuingia katika dini kwa hoja'' yalilenga nini na kwa nani? Na je, ndio hoja za Ilunga azisemazo

Njaribu kufikiri hivi kama yupo aliyetamani kuwa mwislam halafu akaiona ile video, je huyo mtu atakuwa amelinganiwa kuingia katika dini kwa maneno yale? Je, pale kuna ilm ya aina yoyote kweli na kwa msingi huo ilim ya kueleza mfumokristo ipo kwa hoja mantiki na busara!

Mohamed, ifike mahali kila mtu atambue kuwa imani ni suala la mtu binafsi na si chama cha ushirika au cha kisiasa.
Ni makosa kuchukua maneno ya mtu mmoja na kuyafanya ya waislam mamilioni wa Tanzania.

Ningeshauri siku nyingine useme ''ndiyo maana Ilunga ameaminiwa na kundi lenu kueleza mfumokristo'' na wala si waislam.
Unless uniambie anaongea kwa niaba ya waislam gani kauli yangu inabaki kama ilivyo.
 
Mohamed Said,

..mimi kisa cha babu yako nimekipenda sana.

..una mambo mengi sana ya kuwaeleza wa-Tz, tatizo ni pale unapoelemewa na udini.

..tatizo lingine, ni kwamba umetugawa wa-Tz ktk makundi. mara nyingine ukitumia maneno "hawa" au "sisi."

..hata kama kuna conclusions fulani fulani ambazo unazo, nadhani ungetuachia wasomaji wako tutoe conclusions hizo.

..kuhusu Kassanga Tumbo, je una mpango wowote ule wa kuandika kuhusu maisha yake?? I think his story has to be told hata kama alikuwa na hatia na masuala aliyokuwa akituhumiwa nayo.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,unatisha kumkichwa kama ukoma! Kwakweli unajua kujenga hoja zilizosheheni nondo za nguvu.

Nakuhakikishia watanzania wote wanaofatilia mtanange huu wanakusoma wewe, Mwanakijiji,Mag3,Jasus na Yericko nyerere kwa hoja zenu mzuri na zenye kujenga na kuelimisha.

Pia wanamsoma Mohamed said,Ritz,Boko haramu,Ami,kadogoo,The Big Show na wafia dini wengine kwa hoja zao dhaifu zenye kuleta majibu mepesi kwenye maswali magumu...kwa hakika kundi hili lipo hapa jamvini kwa aibu ya kutokukubali kuwa wameshindwa na wanachokifanya sasa ni kujibu kwa mipasho ili mradi waonekane wapo na hawajashindwa.

Nguruvi3, endelea na usichoke....watanzania wanakusoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…