Mkuu Ngongo mkuu sweke 34 sijamuona kitambo kidogo kwenye huu mnakashaMkuu Rapheri utakuwa hauwatendei haki Mohamed Said Ritz Ami Boko haram THE BIG SHOW Kadogoo hawa ndugu zangu michango yao si haba najua wameshindwa kujenga na kutetea hoja lakini kama wasingeshiki usingeona umahiri wa hali ya juu na uliotukuka wa Nguruvi3 Jasusi Mzee Mwanakijiji Mag3 Pasco Yericko Nyerere WildCard Mwita Maranya sweke 34 na Ngongo nisije nikajisahau ha ha ha ha.
Tujifunze kwa kukubali yale tuliokosea kuyarekebisha au hata kukiri tu kwamba wakati flani tulikosea. Tuweke DINI zetu kando.Ndugu yangu huu ni uwanja mpana wa fikra kila mwenye chochote kuhusu historia ya Tanganyika anakimwaga jamvini watu tunajifunza.
Kama na wewe una vitu vya historia ya Tanganyika ruksa utupe darsa hakuna mashindano humu watu tunajifunza.
Umemsahau na ndugu yetu zomba ingawa siku hizi anaonekana kwa nadra sana. Naamini mzee wetu Mohamed hawezi kuwa amebaki vile alivyokuwa mwaka 1998.
Historia ya TANU au NCHI yetu haiwezi kuandikwa na mtu mmoja kwa kutumia vikabrasha vya familia moja, akatangaza Mwalimu kuwasahau watu kwa DINI zao wakati Mwalimu hakuwahi kuandika historia ya nchi hii wala yake mwenyewe!
Mimi nakumbuka mara tatu. 1964, 1969(?) na 1982. Hakutaka kupinduliwa yeye, serikali yake ndio iliyotaka kupinduliwa. Tena waliotaka kuipindua serikali yake mara zote tatu wengi wao walikuwa WAKRISTO wenzake!WildCard,
Naomba unipe darsa kidogo sisi wengine tunajifunza kutoka kwenu.
Ni mara ngapi Nyerere alitaka kupinduliwa?
Mimi nakumbuka mara tatu. 1964, 1969(?) na 1982. Hakutaka kupinduliwa yeye, serikali yake ndio iliyotaka kupinduliwa. Tena waliotaka kuipindua serikali yake mara zote tatu wengi wao walikuwa WAKRISTO wenzake!
Mimi nakumbuka mara tatu. 1964, 1969(?) na 1982. Hakutaka kupinduliwa yeye, serikali yake ndio iliyotaka kupinduliwa. Tena waliotaka kuipindua serikali yake mara zote tatu wengi wao walikuwa WAKRISTO wenzake!
Majina yote siwezi kuyakumbuka. Mwaka 1964 yalikuwa ni maasi ya kikosi kizima pale Colito, sasa Lugalo. Kiongozi wa maasi yale hakupata kujitokeza wazi. Jaribio lile likazimwa.Naomba unitajie majina ya hao watu waliotaka kumpindua Nyerere kwenye ivyo vipindi vitatu. Ni kweli mahakama ziliwakuta na hatia.
Mohamed Said,Pasco,
Sina sababu ya kusema uongo.
Kama ni sifa na ushujaa hiyo ndiyo historia ya wazee wangu
ipo hapo siku zote sihitaji mimi kuzua mambo ili kuwakweza.
Nani anaeweza kuukataa mchango wa Abdu Sykes katika TANU?
Nani aneweza kufuta mchango wa Sheikh Hassan bin Amir katika
TAA Political Subcommittee na katika TANU?
Nani aneweza kuubadili mchango wa Idd Faiz Mafongo katika safari
ya Nyerere UNO 1955?
Nani aneweza kufuta historia ya Bi Titi Mohamed, Tatu bint Mzee,
Bi Shariffa bint Mzee, Bi Halima Selengia, Mama bint Maalim katika akina
mama walioinyanyua TANU?
Historia hii haihitaji mtu kuongopa.
Kuandika yalofanywa na mashujaa hawa ndiyo ''ill motives?''
Umemsahau na ndugu yetu zomba ingawa siku hizi anaonekana kwa nadra sana. Naamini mzee wetu Mohamed hawezi kuwa amebaki vile alivyokuwa mwaka 1998.
Historia ya TANU au NCHI yetu haiwezi kuandikwa na mtu mmoja kwa kutumia vikabrasha vya familia moja, akatangaza Mwalimu kuwasahau watu kwa DINI zao wakati Mwalimu hakuwahi kuandika historia ya nchi hii wala yake mwenyewe!
Majina yote siwezi kuyakumbuka. Mwaka 1964 yalikuwa ni maasi ya kikosi kizima pale Colito, sasa Lugalo. Kiongozi wa maasi yale hakupata kujitokeza wazi. Jaribio lile likazimwa.
Mwaka 1969(72?) walikuwemo ndugu wa OK akina Michael Kamaliza, Colonel William Makori Chacha, Bibi Titi Mohamed,...
Mwaka 1982 walikuwa ni vijana wasomi jeshini akina Capt Roberts, Lt Maganga, Zacharia Hans Pope,..., wakiongozwa na tapeli mmoja wa Kihaya, Uncle Tom Lugangira, ndugu yake Cardinal Rugambwa!
Mkuu Remote, hilo mbona lipo wazi na ndio mkakati wa mahubibiri ya chuki na fitina yanayoenezwa na hawa viumbe wawili!Asante sana waislamu mumemtuma ahamasishe mauaji dhidi ya cardinal, maaskofu, mapadri na wachungaji wengine hakika matunda ya mlichomtuma tumeanza kukishuhudia huko Zanzibar.
cc Yericko Nyerere, Jasusi, Mag3, Pasco Gwalihenzi
nadhani mmemsoma mzee MS hapo juu
Naomba unitajie majina ya hao watu waliotaka kumpindua Nyerere kwenye ivyo vipindi vitatu. Ni kweli mahakama ziliwakuta na hatia.
Mohamed Said,
..mimi nadhani watu wanaona una "ill motives" pale unapojaribu kumdunisha Nyerere huku ukitumbukiza mambo ya udini-udini.
..zaidi unaposhindwa at least kuji-disassociate na kauli za watu kama Ustaadh Ilunga Kapungu, ndivyo unavyozidisha suspicions hizo.
..hivi umesikiliza ile video ya Ustaadh Ilunga? Umeridhika na jinsi anavyowaelimisha vijana wa Kiislamu kwamba kitendo cha Mwamwindi kumuua mkuu wa mkuu wa mkoa ni cha kishujaa? Hivi matendo yale ya kuweka maiti ktk buti la gari halafu kwenda polisi na kuwaambia, "nimewaletea "----" wenu," ni mambo ya kuelezwa kwa MAWAIDHA YA SWALA yoyote ile???
cc: Pasco, Nguruvi3, Ritz
Mkuu Jokakuu, ukiisikiliza ile video ilivyoandaliwa hakika ni seansational tupu. Ilipoongelewa mauaji ya Dr Kleruu utasikia sauti ''akampiga risasi.. ghruuuuuuuuu!'' kuonyesha kilichotokea kwa sauti za risasi. Hakuna uhakiki kuwa sauti za risasi zilirindima kwa namna video inavyoonyesha, kilichofanyika ni kuongeza hamasa na ''ushujaa wa mwamwindi''. Kwa kiongozi wa dini video ile asingeihusisha na mhadhara wake hata kidogo.Mohamed Said,
..mimi nadhani watu wanaona una "ill motives" pale unapojaribu kumdunisha Nyerere huku ukitumbukiza mambo ya udini-udini.
..zaidi unaposhindwa at least kuji-disassociate na kauli za watu kama Ustaadh Ilunga Kapungu, ndivyo unavyozidisha suspicions hizo.
..hivi umesikiliza ile video ya Ustaadh Ilunga? Umeridhika na jinsi anavyowaelimisha vijana wa Kiislamu kwamba kitendo cha Mwamwindi kumuua mkuu wa mkuu wa mkoa ni cha kishujaa? Hivi matendo yale ya kuweka maiti ktk buti la gari halafu kwenda polisi na kuwaambia, "nimewaletea "----" wenu," ni mambo ya kuelezwa kwa MAWAIDHA YA SWALA yoyote ile???cc: Pasco, Nguruvi3, Ritz
Ritz,WildCard,
Nashukuru tuendelee na darsa hawa wa 1969 alikuwemo Kambona ambaye alihukumiwa bila kuwepo mahamani na wengine Bibi Titi Mohamed, Michael Kamaliza, Gray Mattaka, Eliya Chipaka, Prisca Chiombolo, hawa walikataa rufaa wakashinda kesi. Vipi walilipwa fidia na serikali?
Mkuu Ngongo hao uliowataja hapo juu ukitoa Mzee Mohamed hawajawahi kuwa na mchango wa kuishughulisha hyo list hapo chini
Huwa wanajibiwa tu ili kupewa elimu lakini hakuna anayeweza kufanya mnakasha na hiyo orodha ya chini
Mwalimu wao hataki kabisa kuona post za Mzee Mwanakijiji anaona anamuharibia mission yake
Endeleeni kutupa elimu Watanzania 100,000+ wanakusikilizeni nyie hapa
Mkiwa hampo hapa zinabaki porojo tu.
Mdondoaji
Sina ujuzi wa mengi uliyouliza. Na kwa hiyo siwezi kuyajibu. Ninachojua mimi ni kuwa Vatican ni nchi, solomon Islands, ni nchi, Vanuatu, ni nchi, Guam ni nchi, Western Samoa ni nchi. Nchi zote hizo ukiniambia nitaje majina ya wazawa na wageni wao, kwakweli sijui na siwezi. Ila haibadilishi ukweli kuwa hizo ni nchi.
Si lazima tukubaliane sote katika kila jambo. Hata ujio wa Xi Jinping, Rais wa China, sio wote wameuona ni wa manufaa. Lakini bado, serikali na wananchi wengine wameona ni wa manufaa. Kumbuka Tanzania tunasema Sahara Magharibi ni nchi, lakini Morocco wanasema ni sehemu ya nchi yao. Tofauti zitaendelea kuwepo tu. Kwa hiyo, wewe unaweza ukaendelea tu kuumia kwa mawazo kuwa Vatican sio nchi- utaumia kwa vile ulitaka ndio ujengee hoja ya OIC. Sisi wengine tunasema ni nchi. And life goes on....Tunakubaliana kutokukubaliana. By the way, usije ukafikiri mimi ni mkatoliki, sio. Lakini najitahidi tu kuwa objective.
Mkuu Ritz mapinduzi ya mwaka 1982 washiriki ni
(1) Lt Eugene Maganga kama sikosei huyu kashatangulia mbele ya haki.
(2) Seleman Kamando
(3) Zakaria jina la pili nimelisahau unajua muda mrefu umepita
(4) Vitalis Mapunda
(5) Mbogoro
(6) Kajaji Badru
(7) Hatty MacGhee (jina halisi Hatibu Hassan Ghandi) Huyu alikuwa ni Pilot
(8) Capt Christopher Kadego
(9) Mohamed Tamimu aliuwawa katika harakati za kukamatwa
(10) Rugangira huyu alikuwa ni mfadhili wa mapinduzi.
Nguruvi, Nitakuwekea hapa ile barua ya Ivor Bayldon ili usome nimesema nini katika kitabu changu. Kuandika yale mlokuwa hamyajui si kudhalilisha mtu. Naelewa mnatabika na historia hii kwa kuwa hamkutegemea kuwa kulikuwa na historia nyingine. Wewe si wa kwanza kupata mshtuko kwa yale ulosoma kutoka kwangu. Wengi tu wamekipenda kitabu changu kwa ajili ya kuleta yaliyokuwa hayajulikani. Ingekuwa naandika maneno ya kudhalilisha kitabu kisingepita. Kingeishia kwenye fikra zangu.Mkuu Jokakuu, ukiisikiliza ile video ilivyoandaliwa hakika ni seansational tupu. Ilipoongelewa mauaji ya Dr Kleruu utasikia sauti ''akampiga risasi.. ghruuuuuuuuu!'' kuonyesha kilichotokea kwa sauti za risasi. Hakuna uhakiki kuwa sauti za risasi zilirindima kwa namna video inavyoonyesha, kilichofanyika ni kuongeza hamasa na ''ushujaa wa mwamwindi''. Kwa kiongozi wa dini video ile asingeihusisha na mhadhara wake hata kidogo. Hata kama Dr Kleruu alikosea(assumption) je Ilunga anataka kusema ile ndio njia sahihi waislam wanatakiwa kuifuata? Labda nikukumbushe kuwa katika maelezo ya kuundwa kwa UTP, Mohamed ameorodhesha majina ya watu waliopelekewa barua za kujiunga ambao wengi ni wazee wake. Hilo halina tatizo! Mstari wa mwisho akasema ''Nyerere hakupelekewa barua''. Maana yake ni kujenga mazingira ya kumweka Nyerere katika hatia ya ima hakupelekewa kwasababu alikuwa tayari ana uhusiano na kiongozi wa UTP au hakuwa muhimu sana kupelekewa barua kama Abdul Sykes. Katika watu wote kwanini Mohamed amem ''single out'' Nyerere peke yake na wala si Dr Kyaruzi au Mwingine! Jibu ni rahisi, Nyerere ni target na jitihada zote ni kumdunisha ili kuwapandisha wengine. Hapo nyuma kuna post Mohamed kasema ''Nyerere alipewa uongozi na Sykes''. Tunafahamu kuwa kulikuwa na uchaguzi na Nyerere alimshinda Sykes, sasa alipewa uongozi kwa maana ipi? Mimi nadhani role ya kila mmoja inasimama yenyewe bila kumdhalilisha mtu mwingine. Uzuri wa historia ya kweli ni kujidhihiri na haihitaji nakshi au utuli. Pamoja na dunia na vyombo vya habari wakiwemo waandishi na wasomi kuandika kwa nguvu zote mabaya ya Idd Amin na Hitler bado historia inawatetea kwa kila walillofanya kwa nchi zao baya au zuri. Historia inawatetea na si mtu kwasababu historia inasimama yenyewe haiumbwi au kunyumbuliwa.
Mohamed Said,Joka Kuu,
Hilo la dini ndiyo maisha yangu.
Hayo ya Sheikh Ilunga na Kleruu kwa hakika mimi naingiaje humo?
Mimi ninayoandika si nyote mnayajua?
Hayo hayatoshi hadi nizungumze hata yale yalosemwa na wengine?