Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Nguruvi,
Siamini kuwa hadi leo baada ya kuwa nami kwa kipindi humu JF hujanijua.

Mimi huwa silazimishwi jambo na mtu yoyote.
Huo ''mfumokristo'' maana yake nimeacha wakujibu wengine.

Nini utakachopata kutoka kwangu?
Kuanzia jana nimekuwa nikiweka hapa vipi mfumokristo unavyofanya kazi.

Hiki ndicho utapata kutoka kwa Mohamed Said.
 

Winama,
Ndugu yangu basi mie kuchanganya Mbulu na Monduli ndiyo iwe mwao?

Haya si makosa ya kibinadamu tu ndugu yangu?
Nakushukuru kwa kunielimisha.
 


Kwa kumbukumbu zangu (kwa kuwa nilisoma somo la Siasa Msingi na Sekondari), Prof Malima alikuja kuwa Waziri enzi za Mzee Mwinyi akiwa Rais, wakati waSerikali ya Mwl Nyerere Prof Malima hakuwa Waziri na isitoshe Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa MAmbo ya Ndani wakati wa Serikali ya Mwalimu Nyerere.

Uzushi mwingine wa Mzee Mohammed na Elimu kwa Wajinga wanaomshabikia.
 
Mzee Mwanakijiji,

Unajidanganya sana kuhusu fikra zako dhidi ya Waislam na Uislam unawapanga makundi jinsi unavyopenda takuambia kitu kimoja tu hakuna kipindi Waislam wameshikamana kwenye kamba mmoja kama kipindi hiki. Unachekesha unavyompa vyeo Mohamed Said hivi unadhani Waislam ni watu wakushikiwa akili.

Uislam haufuati mtu Uislam una misingi yake Muislam ni yule anayefuata Qur'an na Sunna basi hakuna kingine Waislam wanajitambua Waislam wanaongozwa na mtu mwenye Ilm ya dini na muadilifu, Mohamed Said wala siyo Sheikh ni maamuma kama mimi tu wala hawezi kufutu masuala ya dini unachekesha unavyompa vyeo kuwa Waislam wanamfuata yeye unamuogopa sana Mohamed Said mpaka umeamua kuzusha kuwa kuna Waislam wanafuata yeye sijui hii umeitoa wapi.

Wewe endelea kujifariji na kujiliwaza hakuna Muislam ambaye anakubaliana na wewe Muislam hawezi kupewa darsa la dini na Mkristo, sijui umetoa wapi mamlaka ya kuwasemea Waislam eti kuna wengine wapo kimya, wengine hawataki fujo, Allah anatufundisha kuwa hakuna Uislam wa makundi makundi Uislam ni mmoja na wote ni ndugu anapodhulumia Muislam mmoja wote mnatakiwa mumsaidie Uislam umekataza mtu kudhulumiwa na umekataza mtu kudhulumu.

Waislam wanajua dhulma walizofanyiwa kabla hata Mohamed Said ajaandika kitabu chake, Mwanakijiji fanya utafiti wako tu na hivi haujulikani ingia kila Msikiti wowote unaoujua wewe halafu ongea maneno yako uliyoandika salamu utazipata.

Huna uadilifu wa kuwasemea Waislam na wewe kujua Muislam safi ni yupi wakati wewe siyo Muislam wewe endelea kuwaona Waislam kama watu wenye akili za kushikiwa hakuna Muislam anayemfuata Mtu kwanza unatakiwa ulitambue hilo hizo ni fikra zako katika kujiliwaza.

Mwanakijiji hujui tu Waislam wanapenda sana nyie muendele kuandika hizi habari kuwa hakuna Muislam ambaye amedhulumiwa, lakini Chadema ndiyo wanadhulimiwa wewe na wenzako mnasaidia sana kuwaamsha Waislam waliokuwa wamelala wakupitia huu uzi.
 
Last edited by a moderator:
Hizi nyundo mnazogongelea kichwani kwa Mohammed Said ni tosha kabisa kufuta hizo hisia za kiipuuzi alizowajaza wapambe wake kina Ritz, hongera sana Nguruvi , Mzee Mwanakijiji, Winama .... Kwa hoja murua, mnaufanya usiku wa leo niwe na furaha kwa ajili yenu.
 

Yoso,
Mnakasha ni mzuri ila nakuomba epuka maneno kama ''upuuzi''
hilo ni tusi.

Hizo ''nyundo'' nk. zinanogesha na kukoleza mnakasha hata mie
nikikusoma hufurai.
 

Mwanakijiji, kwa kuwa Mzee Mohammed amesema kuwa Marmo alikuwa Mbunge wa Monduli Ritz lazima akubali tu, ni mwanafunzi asiye na maarifa na si mtafiti, anameza kila anachopewa hata pumba anamezeshwa na anakula!

Ritz nakusaidia na wenzako wanaomezeshwa kila kitu. Sokoine alikuwa Mbunge wa Monduli miaka hiyo na akafuatiwa na Ole Moloimet na Lowassa. Philip Marmo ambaye ni Balozi kule China alikuwa Mbunge wa Mbulu hadi uchaguzi wa 2010 aliposhindwa na Akonaay wa CDM.


Hapa umeshindwa kabisa kuunganisha kauli ya Maaskofu kuhusu Sytematic Persecution na hili la uzushi kuhusu Mfumo Kristo. Maaskofu hawaainisha kuwa hiyo hiyo Systematic Persecution wanayodai ni Mfumo upi hasa zaidi ya kuonyesha wasiwasi kuwa ni Mfumo maalumu wa kuwadhulu Viongozi wa Dini yao na Ukristo wao.
 
Nyambala,
Ulipotea kidogo.

Utafiti wa kisomi utatoka kwangu?
Wala hujakosea ndiyo hivyo tena tunajifunza kwenu.

Mzee Saidi bana unajua hii ni tabia sasa inakuwa ya kitoto, ukishindwa hoja lazima utafute symphathy mimi nilichofanya ni kukritiki maoni yako lakini wewe tayari umekurupuka kwenye upuuzi wa sisi na nyie. Hii utaiacha lini? Nilishakwambia huko nyuma mimi nakuja hapa kama mimi kwa nini utake kuhusisha maoni yangu na the so called "nyie"? Man up bro!!!!!!!!
 
 

Nyambala,
Ndugu yangu usiwe mkali na kutoa lugha za ''upuuzi.''

Hakika nimesema ''nyie.''
Na hii nadhani lipo katika fikra zangu uniwie radhi sana.

Nitajitahidi kukumbuka hiki kila tunapowasiliana.
Hakuna aliyemkamilifu ila Allah.

Kukosea ndiyo ubinadamu.
To err is human.

Samahani sana Mkuu.
 
 

Wewe na Maaskofu tumuamini nani sijui Maakofu wanasema Kanisa Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (Systematic Persecution) kuliko kipindi chochote.

Mfumo ni nini nipe darsa mkuu mimi sichagua darsa.
 
Usomi wako Nguruvi una walakini.Kwamba jawabu huitaki mpaka itoke kwa mtu fulani.Au tuseme ndio una kisasi na Mohammed kwa kukufedhehesha huko nyuma?.
Mimi nimejaribu kukupa definition fupi ninayoielewa ya mfumokristo,hujaridhika.Basi soma na hii ya mwenzangu Wimbi la Mbele katika uzi huu huu halafu eleza iwapo umetosheka au tukuongezee.Na ukimaliza kusoma onesha utoto wetu unaomsisitiza Mohammed asioge nasi.Soma.
 
WanaJF,

Lolote mnalobishania hapa nadhani ni kwa vile mnaipenda nchi yetu.

Naweka angalizo tu kuwa dini zililetwa na merikebu na zililetwa na wazungu kwa upande wa wakristo na waarabu kwa upande wa waislamu WAKARITHISHWA BABU ZETU.

Tupendane!

Sawa tupendane lakini wapendanao ni lazima wawe na mapenzi ya dhati na ya kutoka moyoni si mdomoni! huwezi kusema unampenda mwanao halafu unamwacha alale na njaa na kutembea bila viatu! kama huko ndiko kupendana afadhali tuishi kama mbingu na ardhi!
 

Teh, teh, baada ya kuomba upewe ushahidi wa ubaguzi wa elimu TZ na RITZ kukupa sasa umekasirika na kuendeleza shutuma na Hisopropaganda zako! si neno tunamuomba Mungu akuoneshe njia huenda haya uyafanyayo huna elimu nayo!
 

Bila shaka somo la siasa hukua ukihudhuria barabara kwani Profesa Kighoma Ali Malima alipata kuwa Waziri wa mipango ya uchumi kipindi cha Mwalimu! Bajeti ya Serikali ikianza kusomwa anaanza Waziri wa Fedha halafu Profesa anafuatia kuelezea vipi mipango ya uchumi kwa nchi itakavyokuwa!
 

Sahih International
And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it]. wacha uongo Mwanakijiji usichanganye haki na batili baba
 
Reactions: Ami
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…