"Definition" ya Mfumo Kristo ina mantiq
Katika Posti ya ndugu yetu Ami hapo juu (akinukuu mwingine) aanasema nnini maana ya Mfumo Kristo: Kwamba,
Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.
Sasa kwa haraka haraka mtu anaweza kukubali hili. Na ninaomba kwa sekunde chache tukubaliane na tafsiri hiyo kabla sijaionesha kuwa haina ukweli na haitafsiri Mfumo Kristo ninavyouelewa mimi. Ukisoma maana hiyo Mfumo Kristu ni:
1. Hali - Ni "condition" au tuseme siyo kitu ambacho ni 'concrete'.
2. Wakristo wa Tanzania - ina maana Mfumo Kristu hauwahusu Wakristu wa sehemu nyingine duniani na inapozungumzia Wakristu wa Tanzania inazungumzia "Wakristu" wote.
3. Wamehodhi Madaraka - kwa maneno mengine "Monopoly of power". Kwamba hao watu wa kundi hilo hapo juu wamehodhi madaraka bila kutoa nafasi kwa watu wa dini nyingine.
4. Madaraka ya ngazi zote muhimu za serikali na maamuzi - Hii ni sifa muhimu sana ambayo tutakapoiangalia tutaona inavunja kabisa dhana ya uwepo wa "mfumo huu". Ikumbukwe 'operative word' hapa ni "zote". Nitarudia hili hapa chini kidogo.
5. Kutumia nafasi hizo kuendeleza Wakristu wenzao na Ukristo na kuwabagua Waislamu.
Sifa hizi tano kutokana na maana ya mfumo kama kina Ami wanaamini au wanataka tuamini zinafanya mfumo kuwepo na kutenda kazi. Lakini katika hayo matano ni hilo la nne ndilo HASA linafanya mfumo huu kuwepo kwani bila kushika madaraka yote muhimu hauwezi kuwa na nguvu.
Niwarudishe kidogo kwenye falsafa na hususan kwenye somo la Mantic (Logic). Mantik ni somo ambalo linamsaidia mtu kujenga hoja vizuri, kuepuka makosa ya hoja (fallacies) na wakati huo huo kuhakikisha anagundua makosa hayo kwa wengine. Ukisikia mtu anasema "hii haina mantiki" manake nikuwa kilichosemwa hakijakubaliana na fikra zake - hata kama anaweza asijue maneno yote ya logic.
Kosa la Kwanza la tafsiri ya "Mfumo Kristu" kama alivyoweka Ami iko kwenye kutokuelewa Mantiki na walioandika hilo wenyewe wanaweza kufikiri wamesema cha maana kumbe ndani yake imejaa makosa ya hoja. Nitoe mfano.
Mtu anakuja na kusema "Mimi ni Mtanzania" halafu anasema "Watanzania WOTE ni waongo" halafu akasema "Mimi sisemi uongo".
Sasa mtu mwingine anaweza kuamini hilo lakini mara moja mtu mwenye uelewa mdogo wa mantiki ataonesha "inconsistency" katika madai hayo. Ataonesha hivi:
Kama Wewe ni Mtanzania, na Watanzania wote ni waongo basi wewe huwezi kuwa unasema kweli. Kwa hiyo na huyo anayesema hivyo ama ni mwongo au si Mtanzania. Kama Watanzania WOTE ni waongo basi hakuna Mtanzania anayeweza kuwa anasema kweli.
Mtu akisema Viongozi "WOTE" wa ngazi za juu ni "Wakristu" basi ni lazima tuone kuwa ni Kweli viongozi wote ni "Wakristu". Ukifanikiwa kuonesha kuwa kiongozi mmoja tu ni Mpagani basi hoja kuwa "Viongozi WOTE" ni Wakristu inakufa pale pale.
Ami ametuletea bandiko ambalo tafsiri ya Mfumo Kristu inadai kuwa Wakristu wameshika "nafasi ZOTE MUHIMU". Sasa hii ni rahisi kuonesha; ukionesha Wakristu wameshika nafasi zote muhimu za serikali na "za Maamuzi" basi unathibitisha uwepo wa Mfumo Kristu at least kwa suala la idadi kabla hatujaangalia ile element ya mwisho (ya tano). Lakini ukifanikiwa kuonesha kuwa mojawapo ya nafasi muhimu zinashikiliwa na Muislamu au mtu asiye Mkristu basi hoja kuwa Wakristu wanashika nafasi zote muhimu inakufa. Ukiweza pia kuonesha kuwa zipo nafasi muhimu zinazoshikwa na Waislamu basi HOJA KUWA NAFASI ZOTE ZIMEHODHIWA NA WAKRISTU nayo inakufa.
Hapa inabidi nilete zile orodha alizozileta Ritz kwa fahari kubwa akiamini kuwa anasema kitu very profound:
Ametuwekea 'composition' ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:
kazi ya Mfumo Kristo kwenye bold wote Wakirsto
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu , Stephen M. WasiraMb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
(Utawala Bora)
Ndugu
George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (
MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3.
OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (
Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu
Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4.
WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu
Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu
Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu
Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu
Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu
Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
NduguGaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5.
NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (
TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (
TAMISEMI)
Ndugu
Aggrey Mwanry,Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu
Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu
Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu
Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu
Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu
e,Gerson Lweng Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu
George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.
Angalieni "Ratio" hiyo Waislam wapo wa ngapi na Wakirsto wapo wangapi.
Sasa, kitu cha kwanza kuangalia ni kuwa mawaziri wote na manaibu wao wameteuliwa na Rais Kikwete ambaye ni Muislamu. Nafasi kubwa kabisa nchini ya serikali na ya kimaamuzi nchini Tanzania inaongozwa na Muislamu. Ni Muislamu ndiye mtu mwenye nguzu zaidi ya maamuzi Tanzania. Hii ni KWELI (its a Fact). Kikwete akihutubia Bungeni miaka michache nyuma alitamba kuwa ana madaraka makubwa kiasikwamba akitaka Dr. Slaa akamatawe anaweza akakamatwa! HUYU NI MUISLAMU. Hakuna Mkristu yeyote anayempita au kumkaribia kwa madaraka.
Nafasi Muhimu:
Kina Ami wanasema nafasi "Muhimu" zimeshikiliwa na Wakristu hebu tuangalie:
Urais - Jakaya Mrisho Kikwete - Muislamu
Makamu wa Rais - Ghaibu Bilal - Muislamu
Waziri Mkuu - Mizengo PInda - ni Mkristu - aliyeteuliwa na Muislamu!
Waziri wa Mambo ya Nje - Bernard Membe - Mkristu - kateuliwa na Muislamu
Waziri wa Ulinzi - Vuai Nahodha - Muislamu
Waziri wa Viwanda na Biashara - Abdallah Kigoda - Muislamu
Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki - Muislamu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Shukuru Kawambwa - Muislamu (ikumbukwe wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kufeli waliingia kidato cha kwanza hadi cha nne chini ya uongozi wake- NECTA iko chini yake)
Waziri wa Maji - Jumanne Maghembe - Muislamu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Hussein Mwinyi - Muislamu
Waziri wa Nchi TAMISEMI - Hawa Ghasia - Muislamu
Sasa hizo ni nafasi "muhimu" za kutosha tu. Nafasi nyingine zote za Mawaziri Wakristu wote wameteuliwa na Rais Muislamu na yeye ndiye mwenye madaraka juu yao.
Je ni kweli "nafasi zote muhimu" zimehodhiwa na Wakristu? kina Ami na Ritz na vijana wengine humu wasiojua mantiki wanasema kwa haraka "ndio"!!
Mfumo Kristu - kwa maoni yao - ndio umewaweka Waislamu hawa kwenye madaraka makubwa hivyo!
Tujiulize mahali pengeine ambapo pamewahi kuwa na mifumo ya kibaguzi:
Utawala wa Makuburu wa Afrika ya Kusini ulitukuza rangi nyeupe kwa muda wa karibu miaka mia nne. Je, ulitengeneza weusi wangapi kwenye nafasi muhimu? NI vipi mfumo wa kibaguzi ulifanya kuwepo Rais Mweusi, mawaziri weusi wakautumikia? NI mweusi gani aliyekuwa na nafasi ya juu kabisa katika serikali ya utawala wa makaburu?
Hili ni kweli hata Marekani wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi (segregation). Ni vipi mfumo ule uliwezesha kutoa nafasi kwa weusi kushika madaraka ya juu?
Kimsingi mfumo wa kibaguzi wa kundi hautoi nafasi kwa wanaobaguliwa kushika madaraka mazito. THIS HAS NEVER HAPPENED BEFORE ANYWHERE IN THE WORLD!
Hakuna mahali duniani ambapo mfumo wa kibaguzi (sifa ya tano ya tafsiri ya Mfumo Kristu kama alivyotuwekea ndugu yetu Ami) umewapa madaraka ya juu wanaobaguliwa. Ila wanatuambia Tanzania hili linawezekana. Kwamba Mfumo Kristu katika Tanzania unatupatia viongozi wa Kiislamu!!
Hii tunaweza kusema ni oxymoronic!!
Naomba nitoe changamoto kwa wale wanaoamini kwamba upo mfumo wa kibaguzi dhidi ya Waislamu Tanzania uitwao "mfumo Kristu".
NIONESHENI MAHALI POPOTE DUNIANI AMBAPO MFUMO WA KIBAGOZI (A DISCRIMINATORY SYSTEM) IMEWEZA KUTOA VIONGOZI WA WALE WANAOBAGULIWA NA KUWAPA NAFASI MBALIMBALI HADI ZA JUU KABISA WAKATI MFUMO HUO UNAFANYA KAZI!
Naomba mfano mmoja tu.