Wanakuja kusoma hoja.
Wanasoma kuwa Warioba alikuwa na credential na wao walijua hivyo.
Aliyekuwa hajui kuwa Warioba alikuwa waziri wa sheria kabla ya uteuzi na mwinyi ni wewe peke yao.
Haya wanayaona kama walivyoona lile la Kawawa kuwa makamu wa Rais mwaka 1988, Marmo kuwa mbunge wa Monduli, Nyerere kuja Dar mwaka 1950, na msomi wa master kubeba hotuba ya bila kuisoma hadi New York. n.k.
Kinachowavuta sana ni pale wanapotambua kuwa takwimu zako ni za kupika na wala hazifuati kanuni achilia mbali weledi wa somo la stats. Wameona jinsi miaka takribani 15 walivyolishwa feki, kwamba mto takwimu hawezi kuzielezea!
Wanakuja kusoma na kushangaa iweje muasisi wa mfumokristo hajui maana yake ni nini.
Na wengine wanashangaa imekuwaje mzee wa US na EU anababaika
Mohamed, kukuuliza maswali ni njia ya majadiliano ambayo kwa mtu anayekimbia hoja kama wewe inamvuta kwenye kona halafu inamwacha kama alivyozaliwa. Hili unalijua.Ulitegemea watu wakae kitako wakisema hewala! wrong palce.
Mtu mwenye ufahamu na kitu anapokuuliza sikwamba hajui ni kwamba anajua na anataka kujua ima unajua kiasi gani au unasimamia wapi. Kama hujui utauliza nini?
Lakini pia hao wasomaji wanaona jinsi hoja zako zinavyobomolewa kama nyumba ya barafu na ndicho kinawashtua.
Wengine hawakujua kuwa hii ni tamthilia mwanana katika umbile la ngano.
Hao watatu wanne wasiokuelewa unaosema ni wale wasiokuelewa ni wale usiowapenda kwasababu wananyong'onyeza hoja zako na kutibua mission yako ya kuasambaza chuki, fitna ,farki kwa mgongo wa dini. No! dini haisemi hivyo.
Kuna hoja nzito zinakusubiri hebu tuwape hao wasomaji raha, zirejee
Mnyambala nadhani atakuwa mtabiri!
Unajua Mzee MS aliposema wawili watatu ndiyo hawamwelewi nilibaki kucheka tu, hiyo
wawili watatu ujue ina maana kubwa sana...Imemvua nguo. Nguruvi ukiona mtu
anayejinasibu kwamba hapa anatoa darsa tena akirudia rudia ujue ni pigo kubwa amepata.
Alikuwa amezoea kulisha watu pumba huku anawachanganyia maziwa kidogoo. Hapa watu wanapata
mchanganyiko maalum. Kwa ambao walikuwa wanameza tu sasa wataelewa MS anposema 20% au
10% ya utafiti fulani huwa ana malengo yake kichwani.
Sasa wanajua hila zake katika uandishi. Watu wanajua Garang alipokuja UDSM alikuwa ni alumni
kama yeye alivyo alumni wa ST Joseph, na kwa kweli Kardinal Pengo akiita Alumni wa St Joseph
Mzee MS atapewa kiti cha mbele kama ambavyo Garang alipewa.
Sasa sote tunajua 10% ya Waislam UDSM (source Daily news?) ambao hawakumuuliza maswali Garang ni takwimu zisizokuwana mtetezi (iko siku ataita vijana wake walielezee kwa sababu yeye hana ujuzi nalo!).
Sasa Watu wanajua wazi Warioba alikuwa anajulikana vizuri tu wakati wa uteuzi wake kuwa Waziri mkuu.
Sasa watu wanajua Muasisi wa dhana ya Mfumo Kristo ameshindwa kutupa maana yake ila anajua "unavyo
fanya kazi! Yaani kwa maneno mengine anaijua vizuri mitaa ya Gerezani na Kipata lakini hajui iko mkoa gani!!
Sasa wengine tunamjua ni mtu mwenye misheni zake na hila. Ukiona ameandika kitu kwa makosa ujue ana hila
zake. Ukiona anasema magazeti ya Africa Events yalikusanywa na kuchomwa moto msikilize vizuri sana, halafu
muulize ya kweli hayo? (atajua kuna kitu unajua) halafu atakwambia yaliondolewa kwenye News stand!!
Soma vizuri "News stand"!!
Kuna mengi yamenifanya nimjue huyu mtu. Na kwa kweli huu uzi umemwacha uchi. Na dalili zake ni hizi....
"Mimi ndiyo nayetoa darsa hapa" kuna watu 10K+ wanaonisoma mimi sio nyie"...Hah ha ha .