Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed, nimekushauri usioge na watoto mtoni hutatakata. Mohamed, katika uandishi kuna kitu unachokifahamu ambacho ni lazima uweze ku-define terminology unazotumia.

Hawa vijana wanaoimba nyuma yako si tatizo, tatizo ni wewe mtu ambaye kwa miaka 20 umekuwa unaelezea jambo ambalo huwezi kulielezea ni kitu gani. Soma vitabu vyote vya historia na tafiti utaona ni wajibu wa mwandishi kueleza kinagaubaga kile kinacholeta utata miongoni mwa wasomaji. 20 years huwezi ku-define mfumokristo ni nini! real halafu unaunga mkono hoja za kitoto za watoto! Mo acha kuoga mtoni na watoto.

Hili la definition au maelezo ''mfumokristo ni nini'' unawajibu kwa jamii kulieleza. Wewe ndiye muasisi sasa ulifikiria nini usichokijua maana yake. Umehadhiri Ulaya, Marekani, Yemeni n.k. Please come forward boldly and define the mfumokrsito, don't pick up simple justification from simple minded kid with ululation.

Nguruvi,
Siamini kuwa hadi leo baada ya kuwa nami kwa kipindi humu JF hujanijua.

Mimi huwa silazimishwi jambo na mtu yoyote.
Huo ''mfumokristo'' maana yake nimeacha wakujibu wengine.

Nini utakachopata kutoka kwangu?
Kuanzia jana nimekuwa nikiweka hapa vipi mfumokristo unavyofanya kazi.

Hiki ndicho utapata kutoka kwa Mohamed Said.
 
Nyundo nyingine hiyo Mwanakijiji, ndio maana Mzee Mo amefanikiwa kuwadanga Wamarekani na Waghaibu wengine ambao hawaijui historia yetu. Hata mimi wa juzi tu najua Philp Marmo alikuwa Mbunge wa Mbulu!
Huyu Mzee aendelee kuwa mwalimu wa kina Ritz na Big Show, wafunzi wa aina hiyo wakifeli wanazingizia Mfumo Kristo! Very shame!!

Winama,
Ndugu yangu basi mie kuchanganya Mbulu na Monduli ndiyo iwe mwao?

Haya si makosa ya kibinadamu tu ndugu yangu?
Nakushukuru kwa kunielimisha.
 
Ndio maana kama nilivyoonesha kwenye zile facts nyingine nasema hujaandika historia; Unafika mahali you start making up your own history na kutaka watu wengine waamini. Philip Marmo hajawahi kuwa MBunge wa Monduli!! Mzee Said una haki ya kuwa na maoni yako lakini hauna haki ya kuwa na ukweli wako. You have the right to your own opinion but not your own facts!

Jamani nimepitia shajara zangu zilizochakaa chakaa sikuona mahali ambapo Mwinyi na Kighoma Malima walifanya kazi katika nyadhifa alizosema Mohamed.
Lakini inawezekana pia kuwa kiingereza changu ambacho ni cha alam alam kinanipa tatizo kuelewa.

Bi idhin Llaah mwenye ufahamu wa hili jambo atusadie. Mohamed nisaidie kidogo hapa nimekwama.
Ni lini Mwinyi na Kighoma ''were both ministers in vice president's office''

Kwa kumbukumbu zangu (kwa kuwa nilisoma somo la Siasa Msingi na Sekondari), Prof Malima alikuja kuwa Waziri enzi za Mzee Mwinyi akiwa Rais, wakati waSerikali ya Mwl Nyerere Prof Malima hakuwa Waziri na isitoshe Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa MAmbo ya Ndani wakati wa Serikali ya Mwalimu Nyerere.

Uzushi mwingine wa Mzee Mohammed na Elimu kwa Wajinga wanaomshabikia.
 
Mzee Mwanakijiji,

Unajidanganya sana kuhusu fikra zako dhidi ya Waislam na Uislam unawapanga makundi jinsi unavyopenda takuambia kitu kimoja tu hakuna kipindi Waislam wameshikamana kwenye kamba mmoja kama kipindi hiki. Unachekesha unavyompa vyeo Mohamed Said hivi unadhani Waislam ni watu wakushikiwa akili.

Uislam haufuati mtu Uislam una misingi yake Muislam ni yule anayefuata Qur'an na Sunna basi hakuna kingine Waislam wanajitambua Waislam wanaongozwa na mtu mwenye Ilm ya dini na muadilifu, Mohamed Said wala siyo Sheikh ni maamuma kama mimi tu wala hawezi kufutu masuala ya dini unachekesha unavyompa vyeo kuwa Waislam wanamfuata yeye unamuogopa sana Mohamed Said mpaka umeamua kuzusha kuwa kuna Waislam wanafuata yeye sijui hii umeitoa wapi.

Wewe endelea kujifariji na kujiliwaza hakuna Muislam ambaye anakubaliana na wewe Muislam hawezi kupewa darsa la dini na Mkristo, sijui umetoa wapi mamlaka ya kuwasemea Waislam eti kuna wengine wapo kimya, wengine hawataki fujo, Allah anatufundisha kuwa hakuna Uislam wa makundi makundi Uislam ni mmoja na wote ni ndugu anapodhulumia Muislam mmoja wote mnatakiwa mumsaidie Uislam umekataza mtu kudhulumiwa na umekataza mtu kudhulumu.

Waislam wanajua dhulma walizofanyiwa kabla hata Mohamed Said ajaandika kitabu chake, Mwanakijiji fanya utafiti wako tu na hivi haujulikani ingia kila Msikiti wowote unaoujua wewe halafu ongea maneno yako uliyoandika salamu utazipata.

Huna uadilifu wa kuwasemea Waislam na wewe kujua Muislam safi ni yupi wakati wewe siyo Muislam wewe endelea kuwaona Waislam kama watu wenye akili za kushikiwa hakuna Muislam anayemfuata Mtu kwanza unatakiwa ulitambue hilo hizo ni fikra zako katika kujiliwaza.

Mwanakijiji hujui tu Waislam wanapenda sana nyie muendele kuandika hizi habari kuwa hakuna Muislam ambaye amedhulumiwa, lakini Chadema ndiyo wanadhulimiwa wewe na wenzako mnasaidia sana kuwaamsha Waislam waliokuwa wamelala wakupitia huu uzi.
 
Last edited by a moderator:
Hizi nyundo mnazogongelea kichwani kwa Mohammed Said ni tosha kabisa kufuta hizo hisia za kiipuuzi alizowajaza wapambe wake kina Ritz, hongera sana Nguruvi , Mzee Mwanakijiji, Winama .... Kwa hoja murua, mnaufanya usiku wa leo niwe na furaha kwa ajili yenu.
 
Yoso,
Mnakasha ni mzuri ila nakuomba epuka maneno kama ''upuuzi''
hilo ni tusi.

Hizo ''nyundo'' nk. zinanogesha na kukoleza mnakasha hata mie
nikikusoma hufurai.
 
Ndio maana kama nilivyoonesha kwenye zile facts nyingine nasema hujaandika historia; Unafika mahali you start making up your own history na kutaka watu wengine waamini. Philip Marmo hajawahi kuwa MBunge wa Monduli!! Mzee Said una haki ya kuwa na maoni yako lakini hauna haki ya kuwa na ukweli wako. You have the right to your own opinion but not your own facts!

Mwanakijiji, kwa kuwa Mzee Mohammed amesema kuwa Marmo alikuwa Mbunge wa Monduli Ritz lazima akubali tu, ni mwanafunzi asiye na maarifa na si mtafiti, anameza kila anachopewa hata pumba anamezeshwa na anakula!

Ritz nakusaidia na wenzako wanaomezeshwa kila kitu. Sokoine alikuwa Mbunge wa Monduli miaka hiyo na akafuatiwa na Ole Moloimet na Lowassa. Philip Marmo ambaye ni Balozi kule China alikuwa Mbunge wa Mbulu hadi uchaguzi wa 2010 aliposhindwa na Akonaay wa CDM.

Inashangaza sana watu wanataka kuwasemea Waislam matatizo yao na wengine wanasema hakuna dhulma yeyote waliofanyiwa Waislam wala wanayofanyiwa.

Watu wanapinga hakuna mfumo kirsto.

Lakini hawa hawa wanakubaliana na tamko la Maaskofu kuhusu mfumo.

Kwenye tamko la Maaskofu wanasema Kanisa Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (Systematic Persecution).

Huu mfumo ni upi tunaomba kufahamishwa difinition ya Systematic Persecution.

Hapa umeshindwa kabisa kuunganisha kauli ya Maaskofu kuhusu Sytematic Persecution na hili la uzushi kuhusu Mfumo Kristo. Maaskofu hawaainisha kuwa hiyo hiyo Systematic Persecution wanayodai ni Mfumo upi hasa zaidi ya kuonyesha wasiwasi kuwa ni Mfumo maalumu wa kuwadhulu Viongozi wa Dini yao na Ukristo wao.
 
Nyambala,
Ulipotea kidogo.

Utafiti wa kisomi utatoka kwangu?
Wala hujakosea ndiyo hivyo tena tunajifunza kwenu.

Mzee Saidi bana unajua hii ni tabia sasa inakuwa ya kitoto, ukishindwa hoja lazima utafute symphathy mimi nilichofanya ni kukritiki maoni yako lakini wewe tayari umekurupuka kwenye upuuzi wa sisi na nyie. Hii utaiacha lini? Nilishakwambia huko nyuma mimi nakuja hapa kama mimi kwa nini utake kuhusisha maoni yangu na the so called "nyie"? Man up bro!!!!!!!!
 
Mungu ni mwema sana mzee wangu bila shaka tutaenda vizuri tu

Pia tunaomba ujibu viporo vya maswali yalioelekezwa kwako.

Rapheri,
Mimi huwa sisemi kila kitu wala sijibu kila swali.

Kubwa ni kuwa siko hapa katika kutafuta ubishi
au ushindi katika hoja zangu.

La hasha.

Mimi niko hapa JF kueleza yale ambayo wengi
hamkuwa mnayajua.

Katika hili nadhani nimefanikiwa sana.

Tuko hapa mwezi wa tatu sasa na watazamaji
wamefika 117, 000 plus.
 
Mzee Saidi bana unajua hii ni tabia sasa inakuwa ya kitoto, ukishindwa hoja lazima utafute symphathy mimi nilichofanya ni kukritiki maoni yako lakini wewe tayari umekurupuka kwenye upuuzi wa sisi na nyie. Hii utaiacha lini? Nilishakwambia huko nyuma mimi nakuja hapa kama mimi kwa nini utake kuhusisha maoni yangu na the so called "nyie"? Man up bro!!!!!!!!

Nyambala,
Ndugu yangu usiwe mkali na kutoa lugha za ''upuuzi.''

Hakika nimesema ''nyie.''
Na hii nadhani lipo katika fikra zangu uniwie radhi sana.

Nitajitahidi kukumbuka hiki kila tunapowasiliana.
Hakuna aliyemkamilifu ila Allah.

Kukosea ndiyo ubinadamu.
To err is human.

Samahani sana Mkuu.
 
Rapheri,
Mimi huwa sisemi kila kitu wala sijibu kila swali.

Kubwa ni kuwa siko hapa katika kutafuta ubishi
au ushindi katika hoja zangu.

La hasha.

Mimi niko hapa JF kueleza yale ambayo wengi
hamkuwa mnayajua.

Katika hili nadhani nimefanikiwa sana.

Tuko hapa mwezi wa tatu sasa na watazamaji
wamefika 117, 000 plus.

hakuna mjadala uliowahi kufatiliwa na watu wengi kama huu hapa Tanzania sasa naamini mijadala ya Udini ina nguvu sana!
soon kutakuwa na wafuatliaji 120,000!!!!!!
 
Mwanakijiji, kwa kuwa Mzee Mohammed amesema kuwa Marmo alikuwa Mbunge wa Monduli Ritz lazima akubali tu, ni mwanafunzi asiye na maarifa na si mtafiti, anameza kila anachopewa hata pumba anamezeshwa na anakula!

Ritz nakusaidia na wenzako wanaomezeshwa kila kitu. Sokoine alikuwa Mbunge wa Monduli miaka hiyo na akafuatiwa na Ole Moloimet na Lowassa. Philip Marmo ambaye ni Balozi kule China alikuwa Mbunge wa Mbulu hadi uchaguzi wa 2010 aliposhindwa na Akonaay wa CDM.

Hapa umeshindwa kabisa kuunganisha kauli ya Maaskofu kuhusu Sytematic Persecution na hili la uzushi kuhusu Mfumo Kristo. Maaskofu hawaainisha kuwa hiyo hiyo Systematic Persecution wanayodai ni Mfumo upi hasa zaidi ya kuonyesha wasiwasi kuwa ni Mfumo maalumu wa kuwadhulu Viongozi wa Dini yao na Ukristo wao.

Wewe na Maaskofu tumuamini nani sijui Maakofu wanasema Kanisa Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (Systematic Persecution) kuliko kipindi chochote.

Mfumo ni nini nipe darsa mkuu mimi sichagua darsa.
 
Mohamed, nimekushauri usioge na watoto mtoni hutatakata. Mohamed, katika uandishi kuna kitu unachokifahamu ambacho ni lazima uweze ku-define terminology unazotumia.

Hawa vijana wanaoimba nyuma yako si tatizo, tatizo ni wewe mtu ambaye kwa miaka 20 umekuwa unaelezea jambo ambalo huwezi kulielezea ni kitu gani. Soma vitabu vyote vya historia na tafiti utaona ni wajibu wa mwandishi kueleza kinagaubaga kile kinacholeta utata miongoni mwa wasomaji. 20 years huwezi ku-define mfumokristo ni nini! real halafu unaunga mkono hoja za kitoto za watoto! Mo acha kuoga mtoni na watoto.

Hili la definition au maelezo ''mfumokristo ni nini'' unawajibu kwa jamii kulieleza. Wewe ndiye muasisi sasa ulifikiria nini usichokijua maana yake. Umehadhiri Ulaya, Marekani, Yemeni n.k. Please come forward boldly and define the mfumokrsito, don't pick up simple justification from simple minded kid with ululation.
Usomi wako Nguruvi una walakini.Kwamba jawabu huitaki mpaka itoke kwa mtu fulani.Au tuseme ndio una kisasi na Mohammed kwa kukufedhehesha huko nyuma?.
Mimi nimejaribu kukupa definition fupi ninayoielewa ya mfumokristo,hujaridhika.Basi soma na hii ya mwenzangu Wimbi la Mbele katika uzi huu huu halafu eleza iwapo umetosheka au tukuongezee.Na ukimaliza kusoma onesha utoto wetu unaomsisitiza Mohammed asioge nasi.Soma.
Issue hapa inatokana na Dhana ya Serikali kutokuwa na Dini au Serikali ya Kisekula Dhana hiyo ni maarufu Tanzania. Mara nyingi katika masuala yahusuyo dini, viongozi wa serikali husikika wakisema «serikali haina dini, ila wananchi wake wana dini zao ».Hoja ya usekula wa serikali ni ya kihistoria. Ilijengwa kiasi cha miaka miambili iliyopita ikitaka serikali ijiepushe na shughuli za kidini hususan katika masuala ya elimu, mafundisho ya maadili na na ibada.Japokuwa Tanzania imekuwa ikidai kwamba serikali yake ni ya kisekula, hali halisi haioneshi hivyo. Pamoja na madai hayo, serikali ya Tanzania imewahi kuingia katika msuguano na Waislamu na baadhi ya wasiokuwa waislamu pale Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipotaka kuanzisha somo la dini au maadili ya nchi. Kadhia hii ni maarufu kwa jina la "dini mseto". serikali ya kisekula haiwezi ikaja na mipango ya kusomesha dini kwa jina lolote lile liwe la maadili au vyovyote vile.

Mifano mingine inayotia wasiwasi usekula wa serikali ya Tanzania ni hii ifuatayo:

1. Wimbo wa Taifa – unaomba mungu aibariki nchi

2. Dua ya Bungeni – ina muomba mungu

3. Kuapishwa kwa wanaochukua nafasi za uongozi.
Japo wanaoapa huapa kwa dini zao, aneapishasi kiongozi wa dini husika bali wa serikali au wabunge.

Utaratibu huo hauendani na madai kuwa nchi au serikali ya Tanzania haina dini, bali wananchi wake ndiyo wenye dini. Swali ni je, tunapomtaja Mungu katika wimbo wa taifa au katika dua ya bungeni, na kadhalika, tunamkusudia mungu yupi? Mungu wa Waislamu? Wa Wakristo? Wa dini za asili? Je, kuna mungu wa kitaifa? Mungu huyo wa kitaifa ni yupi na ni wa dini gani?Je, katika hali hiyo, ni kweli serikali haina dini? Katika mazingira ya Waislamu kuandamwa na kukandamizwa na mila ya Mfumokristo, mfumo ambao unajidhihirisha zaidi katika vitendo vya kibaguzi vinavyofanyiwa Waislamu na sehemu kubwa ya watendaji serikalini na katika taasisi mbalimbali, kwa nini mwananchi Muislamu asiamini kuwa serikali hii si ya kisekula bali ni ya kidini; na dini yenyewe ni Mfumokristo.

According to TRA / HAZINA....

https://www.jamiiforums.com/attachmen...p;d=1356427583

https://www.jamiiforums.com/attachmen...p;d=1356427126

https://www.jamiiforums.com/attachmen...p;d=1356427583

https://www.jamiiforums.com/attachmen...p;d=1356427583

https://www.jamiiforums.com/attachmen...p;d=1356427673

Mbinu zinazotumiwa na Mfumokristo katika Kujihakikishia Fursa Tanzania

Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

1. Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni.
Wakoloni wa kijerumani ndio walioanzisha mfumo wa kuwabagua Waislamu katika elimu baada ya kushinikizwa na makanisa. Ushahidi wa mashinikizo hayo unaweza kupatikana katika rejea zifuatazo: Cameroon and Dodd 1970:56, Kurtz1972:19, Smith 1963:16. Hatimaye kutokana na mashinikizo hayo serikali ilikubali kufaya yafuatayo:-

i. Kuwafukuza kazi Waislamu waliokuwa serikalini na kuwaingiza Wakristo (Tazama Cameroon and Dodd1970: 25, 56, pia Roland 1970:205)

ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50)

iii. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114.

iv. Kujenga hoja kwamba Waislamu kwa asili yao si watu wa kuendelea na kuwa ni wavivu. Tazama E.B Castle 1966:37 ambaye anasema, " Islam hinders progressive attitude to change in society and a community that accepts Islam is less likely to advance in social welfare and education", yaani Uislamu ni kikwazo cha fikra za maendeleo na mabadiliko katika jamii, na kwamba jamii ikiukubali Uislamu haiwezi kamwe kupiga hatua za katika ustawi wa na elimu. Pia Abel Ishumi 1980:208 anasema, "From the beginning Muslims were opposed to western type formal education", Kwamba Waislamu walipinga elimu. Pia Abel Ishumi 1981:43, "Muslims believe highly in fatalism" Kwamba Waislamu wanabweteka na kuamini kwao kuwa mambo yameshakadiriwa.

2. Kuhujumu taasisi za Waislamu na kuweka viongozi mamluki.

Baada ya uhuru Serikali ya Tanzania imekuwa na muelekeo wa kuziandama taasisi zinazoonekana kuwa na mipango madhubuti ya kuwakomboa Waislamu kuondokana na ujinga na umaskini. Rejea Bergan 1981:26 na Sivalon 1992:3 kuhusu kuvunjwa kwa EAMWS na kuanzishwa kwa BAKWATA. Pia soma Anuur na. 13 la Agosti 1992 juu ya taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya kuitaka Serikali kuifuta EAMWS. Pia tazama Njozi 2000:31. "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusu kadhia ya kuvamiwa kwa Msikiti wa Mwembechai na hatimaye kuuliwa kwa Waislamu.

3. Kuhodhi mfumo wote wa elimu nchini.

Tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo.

Huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, "udini".

Aidha katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi zawakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara.

Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.

Mfumokristo ni hali ambayo Wakristo wa Tanzania wamehodhi madaraka ya ngazi zote muhimu katika serikali na katika vyombo vya maamuzi, na kuzitumia nafasi hizo kuwaendeleza Wakristo na Ukristo na kuwabagua Waislamu na dini yao.

1. Kuendeleza mfumo wa kibaguzi katika elimu kama ulivyoachwa na wakoloni. Wakoloni wa kijerumani ndio walioanzisha mfumo wa kuwabagua Waislamu katika elimu baada ya kushinikizwa na makanisa. Ushahidi wa mashinikizo hayo unaweza kupatikana katika rejea zifuatazo: Cameroon and Dodd 1970:56, Kurtz1972:19, Smith 1963:16. Hatimaye kutokana na mashinikizo hayo serikali ilikubali kufaya yafuatayo:-

i. Kuwafukuza kazi Waislamu waliokuwa serikalini na kuwaingiza Wakristo (Tazama Cameroon and Dodd1970: 25, 56, pia Roland 1970:205)

ii. Kuzipa shule za wamisheni msaada wa kifedha kutoka kodi za wananchi huku wakizibagua zile za Waislamu (Tazama Roland: 1970: 205,na Cameroon and Dodd 1970:50)

iii. Kuweka mpango mkakati wa kuwabagua na kuwahujumu Waislamu na Uislamu wao. Tazama Roland 1970:205, Kurtz 1972:29. Cameroon and Dodd 1970:114

iv. Kujenga hoja kwamba Waislamu kwa asili yao si watu wa kuendelea na kuwa ni wavivu. Tazama E.B Castle 1966:37 ambaye anasema, " Islam hinders progressive attitude to change in society and a community that accepts Islam is less likely to advance in social welfare and education", Yaani Uislamu ni kikwazo cha fikra za maendeleo na mabadiliko katika jamii, na kwamba jamii ikiukubali Uislamu haiwezi kamwe kupiga hatua za katika ustawi wa na elimu. Pia Abel Ishumi 1980:208 anasema, "From the beginning Muslims were opposed to western type formal education", Kwamba Waislamu walipinga elimu. Pia Abel Ishumi 1981:43, "Muslims believe highly in fatalism" Kwamba Waislamu wanabweteka na kuamini kwao kuwa mambo yameshakadiriwa.

2. Kuhujumu taasisi za Waislamu na kuweka viongozi mamluki. Baada ya uhuru Serikali ya Tanzania imekuwa na muelekeo wa kuziandama taasisi zinazoonekana kuwa na mipango madhubuti ya kuwakomboa Waislamu kuondokana na ujinga na umaskini. Rejea Bergan 1981:26 na Sivalon 1992:3 kuhusu kuvunjwa kwa EAMWS na kuanzishwa kwa BAKWATA. Pia soma Anuur na. 13 la Agosti 1992 juu ya taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ya kuitaka Serikali kuifuta EAMWS. Pia tazama Njozi 2000:31. "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania kuhusu kadhia ya kuvamiwa kwa Msikiti wa Mwembechai na hatimaye kuuliwa kwa Waislamu.

3. Kuhodhi mfumo wote wa elimu nchini. Tangu kuondoka kwa Mkoloni Wakristo wamekuwa kama mabaki ya wakoloni na ukoloni. Ukiondoa shule za msingi na sekondari za Kata, huko katika shule za sekondari za Serikali, vyuo vya kati na vyuo vikuu wanafunzi na wafanyakazi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80. Siku hizi katika shule za Kata wanafunzi Waislamu wameanza kuonekana. Katika taasisi za elimu mfano T.I.E, TEA, NECTA, Bodi ya Mikopo, I.A.E na vyuo vyote nchini, uongozi umekuwa ni mali ya Wakristo. Huko mwanzo walidai kwamba hamna Muislamu mwenye elimu ya kutosha kuongoza. Kwa siku za hivi karibuni madai yao kwa wale Waislamu wachache waliofanikiwa kupata elimu ni kuwa hawafai kwa vile wana, "udini". Aidha katika Wizara ya Elimu (MOEVT) tangu Wizara hiyo kuundwa uongozi umekuwa mali ya Wakristo kwa zaidi ya asilimia 90. Nafasi kama ya Kamishina wa Elimu haijawahi hata kuwa na Kaimu Muislamu na wala haitarajiwi chini ya Mfumochristo. Nafasi za wakurugenzi nazo zimemilikiwa na Wakristo. Mfumokristo umejikita barabara. Uongozi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu nao umemilikiwa vilivyo. Nafasi za Maafisa elimu Wilaya na Mikoa na wakaguzi wakuu wa elimu wa Kanda kwa zaidi ya asilimia 85 zinaendelea kuwa miliki ya hawa Wakristo.

4. Kukataa kutunga sera za kuondoa upendeleo wa Wakristo katika elimu na kuendeleza ulaghai dhidi ya wananchi wasiokuwa Wakristo. Mara baada ya uhuru ilielezwa na viongozi wetu akiwemo Mwl. Nyerere kuwa serikali itachukua hatua kuondoa mpango ulioasisiwa na Wakoloni wa kuwabagua Waislamu. (tazama A. Jumbe 1994:123, Court 1976 na Nyerere in Hansard Desemba 10, 1962). Badala yake hatua zilizochukuliwa hazikulenga kuondoa tatizo la ubaguzi wa kidini katika elimu nchini na kuwaondoa pia katika ajira na madaraka.Mfano wa hatua hizo ni pamoja na:

i. Kufuta ada shule za msingi na sekondari miaka ya 1960/70.

ii. Kuweka kikomo cha elimu ya msingi kuwa miaka 7 bila kusita.

iii. Kuondoa mitihani ya darasa la 4 na 5. iv. Kuanzishwa kwa mpango wa UPE.

v. Kujenga shule za msingi za bweni kwa watoto wa wafugaji na wavuvi wanaoishi kwa kuhamahama

vi. Kutaifisha shule za binafsi zilizokuwa chini ya mashirika ya dini na watu binafsi. Mpango huu haukuhusisha seminari za Wakristo.

vii. Kupeleka wanafunzi sekondari kwa kigezo cha KUCHAGULIWA badala ya KUFAULU kulikoendana na kuyafanya matokeo ya mtihani wa darasa la saba kuwa ni siri.

viii. Kuanzishwa utaratibu wa "quota system" ambapo kila mkoa ulipangiwa idadi ya wanafunzi watakaochaguliwa kwenda sekondari.

ix. Kuweka utaratibu mgumu wa kuanzisha na kuendesha shule binafsi chini ya sheria ya elimu ya mwaka 1978, hivyo watu wote kulazimika kusoma katika shule chache za sekondari za Serikali

x. Kuanzishwa kwa shule maalum za vipaji katika miaka ya tisini mfano: Kibaha, Kilakala, Ilboru, n.k.

xi. Kutoa upendeleo maalum (Affirmative Action) kwa watoto wa kike kuingia sekondari na vyuo. Aidha kuwepo pia kwa mipango ya kuwasomesha watoto wa kike kutoka familia maskini.

xii. Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata. Sera hizi zote pamoja na nyinginezo hazikusaidia kuondoa uwiano mbaya au ubaguzi wa elimu kwa Waislamu. Tuangalie mfano michache ifuatayo: Ni ukweli usiopingika kwamba UPE awamu ya kwanza iliyosukumwa na UNESCO na awamu ya pili iliyosukumwa na Malengo ya Milenia (MDGs) na Mpango wa Elimu kwa wote (EFA) zimesaidia kuwahakikishia watoto wengi wa Kiislamu elimu hiyo ya msingi. Lakini sera hii ilikuja katika kipindi ambacho elimu ya msingi haikuwezi tena kumpatia mtu ajira katika sekta rasmi na hata ile ya binafsi.

Ikumbukwe kwamba katika kipindi hicho cha miaka ya 60 hadi 2000 nafasi za masomo ya sekondari ziliendelea kuwa haba. Wakati wote huu watoto wa Kikristo ndiyo walioendelea kufaidika na elimu ya sekondari. Masomo hayo ya sekondari hatimaye yaliwapatia fursa za kuingia vyuo vikuu na hivyo kuwa katika nafasi za kuajiriwa serikalini, kuteuliwa katika vyeo na nyadhifa mbalimbali huku Waislamu waliowaacha shule za msingi wakiambulia ajira za usafi na utarishi.

Naam, Mfumokristo umefanikiwa kuwafanya Wakristo kuwa warithi wa wazungu wakoloni na kuwaacha Waislamu katika hadhi lie ile waliokuwa nayo wakati wa ukoloni. Aidha kutaifishwa kwa shule hakujasaidia Waislamu kupata elimu ya sekondari kama inavyodaiwa kuwa Nyerere alitaifisha shule ili Waislamu wasome.

Kama tulivyoona awali kuwa tangu wakati wa Mjerumani serikali ya kikoloni ilikuwa ikitoa pesa kusaidia ujenzi na uendeshaji wa shule za Wakristo ni dhahiri kuwa shule hizi zilikuwa zimeshalemazwa na pesa za serikali kwa kipindi cha miaka 55, tangu mwaka 1914 hadi mwaka 1969 zilipotaifishwa. Tazama maandiko ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki (TEC) Fr Robinson, D.W 1965:14 kwamba, "The Church is now totally dependent on State aid for the administration of these schools. If this aid were withdrawn the church will be forced to close its schools"

Yaani, Kwa sasa Kanisa limekuwa tegemezi kabisa kwa serikali katika kutoa pesa za kuendesha shule zake na ikiwa serikali itasita kutoa fedha kwa shule hizi basi Kanisa litalazimika kuzifunga. Ni dhahiri basi kwamba hatua aliyochukua Julius Nyerere ilikuwa na malengo makuu ya kuziokoa shule za Kanisa kufungwa kwa sababu ingekuwa jambo la kiroja kwa serikali ya Tanzania kuendelea kutoa pesa za kuendesha shule za Kanisa kwa wakati ule, na pili kuhakikisha kwamba malengo ya shule zile ya kuwasomesha Wakristo yanaendelea kutekelezwa kwa kutumia pesa za umma.

Kimsingi kilichobadilika ni jina la mmiliki tu uongozi na malengo ya shule yalibaki vile vile. Ndiyo maana hakuna mtu yoyote aliyethubutu au atakayethubutu kudai eti kwamba ukienda katika shule zilizotaifishwa mfano, Pugu, Minaki, Tambaza, Zanaki, Jangwani, Kibasila, Ilboru, Weruweru, Tosamaganga, Msalato, Umbwe, Ndanda n.k, utakuta idadi ya kuridhisha ya wanafunzi Waislamu wanaosoma huko. Lakini hata katika shule za sekondari chache mpya ambazo serikali ilijenga au kujengewa mwishoni mwa miaka ya 70, kama vile: Kibiti, Ruvu, Karatu, Bagamoyo n.k , kote walimu, wafanyakazi na wanafunzi ni Wakristo kwa zaidi ya asilimia 80.

Watoto wachache wa Kiislamu wanaosoma huko huonekana kama wakimbizi wanaosaidiwa katika nchi ya ughaibuni. Kuhusu kuingia sekondari kwa kigezo cha kuchaguliwa na mpango wa quota system, watendaji Wakristo waliojazana katika mfumo wa elimu nchini wamekuwa wakihakikisha kwamba Waislamu hawasomi kutokana mbinu zifuatazo:-

i. Kufanya matokeo ya darasa la saba kuwa ni siri hivyo kuweza kuibadili nafasi walizoshinda Waislamu na kuwapa wengine. Tazama ushahidi mzito uliotolewa na Njozi mwaka 2000; katika kitabu cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania uk. wa 62 -70. Hapa vijana wa Kiislamu waliofaulu darasa la saba walinyimwa nafasi kuingia sekondari na wale waliofaulu kidato cha nne walinyimwa kuingia kidato cha tano. Kazi hii ya kuwakwamisha vijana wa Kiislamu ilifanywa vyema na mawakala wa Mfumokristo waliojazana katika mfumo wote wa elimu nchini.

ii. Kuhamisha wanafunzi Wakristo kutoka maeneo yenye ushindani mkubwa kwenda Mikoa iliyokuwa na alama ndogo za kuchaguliwa kama Pwani, Dar, Lindi, Mtwara na Tanga ambayo pia ni maeneo ya Waislamu . Tazama Malekela 1983 in"Access to secondary education in Sub- Sahara Africa"

iii. Huko nyuma kabla ya wanafunzi kupangiwa shule za sekondari namba zao za mtihani ziliambatanishwa na majina ili kujua nani Mkristo apendelewe na nani siyo awachwe iv. Kuhakikisha kwamba viongozi na watendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) wote ni Wakristo. Aidha kwa asilimia kubwa kabisa watungaji wa mitihani na wasahihishaji pia ni dini hiyo hiyo. Tazama kitabu cha Miaka Thelathini ya NECTA, 2004 au www.necta.ca.tz.
 
WanaJF,

Lolote mnalobishania hapa nadhani ni kwa vile mnaipenda nchi yetu.

Naweka angalizo tu kuwa dini zililetwa na merikebu na zililetwa na wazungu kwa upande wa wakristo na waarabu kwa upande wa waislamu WAKARITHISHWA BABU ZETU.

Tupendane!

Sawa tupendane lakini wapendanao ni lazima wawe na mapenzi ya dhati na ya kutoka moyoni si mdomoni! huwezi kusema unampenda mwanao halafu unamwacha alale na njaa na kutembea bila viatu! kama huko ndiko kupendana afadhali tuishi kama mbingu na ardhi!
 
Unadhani hajui basi; anajua ila ni hofu ya kivuli tu. Wanafikiria sisi tunatetea Wakristu au Ukristu! Wenzie tunagombania historia isipotoshwe. Mzee Mohammed amefanikiwa sana kupotoshahistoria na kaipotosha hadi unaweza kuiamini - kama huijui vizuri. Na ameipotosha kwa kuingiza dini tu katika historia.

Harakati za Uhuru kageuza kuwa harakati za Uhuru wa Waislamu
Uongozi wa TANU kageuza kuwa ni uongozi wa TANU ya Waislamu
Wapigania Uhuru kawageuza - wapigania Uhuru wa Waislamu
Migongano ya kiuongozi baada ya uhuru - imekuwa ni dhidi ya Waislamu
Matukio ya uhalifu anayaangalia kama ni Waislamu Vs. Wakristu
Umaskini nchini kaugeuza kuwa ni "Umaskini wa Waislamu"
Utawala mbovu wa CCM kageuza kuwa ni tatizo la Wakristu

Lakini huyu huyu na wenzie ndio wale wale ambao waliipigia debe CCM irudi madarakani; ni hawa hawa hutawasikia wakimlalamikia Kikwete ambaye kwa maoni yao ni mtumishi wa Mfumo Kristu (angalia mifano ya Ritz hapo). LEo hii Muislamu asiyekubaliana na narrative yao hii mpya ya histohisia anaonekana siyo Muislamu mzuri. Muislamu wa kweli (ukimsoma Mohammed Said) ni yule ambaye anakubaliana na simulizi la kudhulumiwa Waislamu na uadui dhidi ya Wakristu na hujuma dhidi ya makanisa. Muislamu asiyefanya hivyo haitwi hata MUislamu anaitwa "Kibaraka'.

Hawa kwao Uislamu siyo Imani tena ya Mungu Mmoja na Utume wa Mohammed; Uislamu kwao ni vipi mtu anakubaliana masimulizi ya Mohammed Said. Kama Muislamu anaamini katika Mungu mmoja, Unabii na Sunna ya Mtume na anatekeleza nguzo zote tano za dini na sunna si Muislamu mzuri na si Muislamu wa kweli hadi awe anaamini katika mafundisho potofu ya Mohammed Said. Utaona kumbe Mohammed Said ameingiza katika dini kitu kisichokuwepo - historia potofu. Ametengeneza 'litmus test' kwa tu kuwa Muislamu. Ukimsoma utaona kuwa:

a. Asiyekubali simulizi la MS hawezi kuwa Muislamu mzuri
b. Ambaye anakubali BAKWATA kama chombo cha Waislamu - si Muislamu
c. Aneyeshirikiana vizuri na Wakristu na haoni mfumo Kristu - si Muislamu (Waislamu wanatakiwa waone Mfumo Kristu)
d. Asiyechukia Kanisa na kuona lina nguvu sana - si Muislamu (Muislamu lazima achukie Kanisa)
e. Shehe ambaye anahubiri amani na umoja na haki na upendo baina ya Watanzania (si Shehe Mzuri, shehe mzuri ni dizaini ya Ilunga)

Kwangu mimi hii ndio tragedy kubwa kabisa ya mafundisho potofu ya Mohammed Said ambaye tunapambana nayo. Siyo tu yamewagawa Waislamu na Wakristu kama alivyotaka bali yanalenga kuwagawa Waislamu wenyewe. Na bahati mbaya sana wapo Waislamu walioingia katika mtego huu ukamatao na sasa wanawaangalia Waislamu wenzao ambao hawakubaliani na histohisia hii kuwa si Waislamu wazuri au wa kweli.

Na cha kusikitisha zaidi ni kuwa wapo Waislamu ambao kutokana na kutotaka kujiletea matatizo na wenzao wameamua kukaa kimya kwa sababu wanajua wakisimama kumpinga Mohammed Said na kukataa mafundisho yake au kumhoji ukweli wa madai yake wataiwa "vibaraka wa mfumo Kristu"!

Mada hii tumetoa somo zuri ambalo limewafungua wengi kuweza kuona na kutambua jinsi gani masimulizi ya Mohammed Said hayana msingi katika ukweli, hoja dhake ni dhaifu na yamejaa hisia ya kutukuza. Nina bahati ya kujifunza kidogo kinachoitwa "Elimu ya Nafsi" na "Elimu ya Roho". Kuna roho fulani inatenda kazi hapa ambayo haiwezi kuondolewa kwa kukaa kimya bali kwa kupingwa waziwazi bila kuionea haya. Ndio maana nimesema huko nyuma utawala wa ulaghai wa histohisia ya Mohammed Said umefikia kikomo baada ya kutamalaki kwa karibu miaka 20 sasa. Wakati wa kuwavunjia minyororo wale wote waliofungwa minyororo ya porojo na Bw. Said umefika na minyororo hiyo kama iliyotiwa mafuta na kugongwa na nyundo ya ukweli inaanza kuachia - pingili baada ya pingili.

Mzee Said amebaki kurudia rudia yale yale ambayo yameshaoneshwa kuwa si ya kweli; haamini kuwa minyororo yake aliyoidhania kuwa ni ya chuma kumbe ya ukoka! Ukweli hata ukicheleweshwa bado unabakia kuwa ukweli; uongo unaweza kukaa kwenye kiti cha enzi kwa miongo lakini ukweli ukija uongo unavuliwa taji!

Teh, teh, baada ya kuomba upewe ushahidi wa ubaguzi wa elimu TZ na RITZ kukupa sasa umekasirika na kuendeleza shutuma na Hisopropaganda zako! si neno tunamuomba Mungu akuoneshe njia huenda haya uyafanyayo huna elimu nayo!
 
Kwa kumbukumbu zangu (kwa kuwa nilisoma somo la Siasa Msingi na Sekondari), Prof Malima alikuja kuwa Waziri enzi za Mzee Mwinyi akiwa Rais, wakati waSerikali ya Mwl Nyerere Prof Malima hakuwa Waziri na isitoshe Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa MAmbo ya Ndani wakati wa Serikali ya Mwalimu Nyerere.

Uzushi mwingine wa Mzee Mohammed na Elimu kwa Wajinga wanaomshabikia.

Bila shaka somo la siasa hukua ukihudhuria barabara kwani Profesa Kighoma Ali Malima alipata kuwa Waziri wa mipango ya uchumi kipindi cha Mwalimu! Bajeti ya Serikali ikianza kusomwa anaanza Waziri wa Fedha halafu Profesa anafuatia kuelezea vipi mipango ya uchumi kwa nchi itakavyokuwa!
 
Unadhani hajui basi; anajua ila ni hofu ya kivuli tu. Wanafikiria sisi tunatetea Wakristu au Ukristu! Wenzie tunagombania historia isipotoshwe. Mzee Mohammed amefanikiwa sana kupotoshahistoria na kaipotosha hadi unaweza kuiamini - kama huijui vizuri. Na ameipotosha kwa kuingiza dini tu katika historia.

Harakati za Uhuru kageuza kuwa harakati za Uhuru wa Waislamu
Uongozi wa TANU kageuza kuwa ni uongozi wa TANU ya Waislamu
Wapigania Uhuru kawageuza - wapigania Uhuru wa Waislamu
Migongano ya kiuongozi baada ya uhuru - imekuwa ni dhidi ya Waislamu
Matukio ya uhalifu anayaangalia kama ni Waislamu Vs. Wakristu
Umaskini nchini kaugeuza kuwa ni "Umaskini wa Waislamu"
Utawala mbovu wa CCM kageuza kuwa ni tatizo la Wakristu

Lakini huyu huyu na wenzie ndio wale wale ambao waliipigia debe CCM irudi madarakani; ni hawa hawa hutawasikia wakimlalamikia Kikwete ambaye kwa maoni yao ni mtumishi wa Mfumo Kristu (angalia mifano ya Ritz hapo). LEo hii Muislamu asiyekubaliana na narrative yao hii mpya ya histohisia anaonekana siyo Muislamu mzuri. Muislamu wa kweli (ukimsoma Mohammed Said) ni yule ambaye anakubaliana na simulizi la kudhulumiwa Waislamu na uadui dhidi ya Wakristu na hujuma dhidi ya makanisa. Muislamu asiyefanya hivyo haitwi hata MUislamu anaitwa "Kibaraka'.

Hawa kwao Uislamu siyo Imani tena ya Mungu Mmoja na Utume wa Mohammed; Uislamu kwao ni vipi mtu anakubaliana masimulizi ya Mohammed Said. Kama Muislamu anaamini katika Mungu mmoja, Unabii na Sunna ya Mtume na anatekeleza nguzo zote tano za dini na sunna si Muislamu mzuri na si Muislamu wa kweli hadi awe anaamini katika mafundisho potofu ya Mohammed Said. Utaona kumbe Mohammed Said ameingiza katika dini kitu kisichokuwepo - historia potofu. Ametengeneza 'litmus test' kwa tu kuwa Muislamu. Ukimsoma utaona kuwa:

a. Asiyekubali simulizi la MS hawezi kuwa Muislamu mzuri
b. Ambaye anakubali BAKWATA kama chombo cha Waislamu - si Muislamu
c. Aneyeshirikiana vizuri na Wakristu na haoni mfumo Kristu - si Muislamu (Waislamu wanatakiwa waone Mfumo Kristu)
d. Asiyechukia Kanisa na kuona lina nguvu sana - si Muislamu (Muislamu lazima achukie Kanisa)
e. Shehe ambaye anahubiri amani na umoja na haki na upendo baina ya Watanzania (si Shehe Mzuri, shehe mzuri ni dizaini ya Ilunga)

Kwangu mimi hii ndio tragedy kubwa kabisa ya mafundisho potofu ya Mohammed Said ambaye tunapambana nayo. Siyo tu yamewagawa Waislamu na Wakristu kama alivyotaka bali yanalenga kuwagawa Waislamu wenyewe. Na bahati mbaya sana wapo Waislamu walioingia katika mtego huu ukamatao na sasa wanawaangalia Waislamu wenzao ambao hawakubaliani na histohisia hii kuwa si Waislamu wazuri au wa kweli.

Na cha kusikitisha zaidi ni kuwa wapo Waislamu ambao kutokana na kutotaka kujiletea matatizo na wenzao wameamua kukaa kimya kwa sababu wanajua wakisimama kumpinga Mohammed Said na kukataa mafundisho yake au kumhoji ukweli wa madai yake wataiwa "vibaraka wa mfumo Kristu"!

Mada hii tumetoa somo zuri ambalo limewafungua wengi kuweza kuona na kutambua jinsi gani masimulizi ya Mohammed Said hayana msingi katika ukweli, hoja dhake ni dhaifu na yamejaa hisia ya kutukuza. Nina bahati ya kujifunza kidogo kinachoitwa "Elimu ya Nafsi" na "Elimu ya Roho". Kuna roho fulani inatenda kazi hapa ambayo haiwezi kuondolewa kwa kukaa kimya bali kwa kupingwa waziwazi bila kuionea haya. Ndio maana nimesema huko nyuma utawala wa ulaghai wa histohisia ya Mohammed Said umefikia kikomo baada ya kutamalaki kwa karibu miaka 20 sasa. Wakati wa kuwavunjia minyororo wale wote waliofungwa minyororo ya porojo na Bw. Said umefika na minyororo hiyo kama iliyotiwa mafuta na kugongwa na nyundo ya ukweli inaanza kuachia - pingili baada ya pingili.

Mzee Said amebaki kurudia rudia yale yale ambayo yameshaoneshwa kuwa si ya kweli; haamini kuwa minyororo yake aliyoidhania kuwa ni ya chuma kumbe ya ukoka! Ukweli hata ukicheleweshwa bado unabakia kuwa ukweli; uongo unaweza kukaa kwenye kiti cha enzi kwa miongo lakini ukweli ukija uongo unavuliwa taji!

2_42.png
Sahih International
And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it]. wacha uongo Mwanakijiji usichanganye haki na batili baba
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Back
Top Bottom