Nyambala,
Ungejiepusha na maneno kama ''ngano'' nk ningefurahi wacha wengine watumie hayo
mimi sijui vipi lakini nakuhisi nawe nikafanya majadiliano ya maana na wewe.
Sitoweza kufanya hivyo na mtu ambae ananikebehi.
Nakushukuru kwa bandiko hilo lakini ukweli ni kuwa hizo si habari mpya kwangu.
Deleted! duplication.
Haina shida mzee wangu naweka pembeni hilo neno!
I rest my case.
Kilichobaki nisikilize EGYPTIAN MUSICAL CLUB....''yatima''
"Definition" ya Mfumo Kristo ina mantiq
Katika Posti ya ndugu yetu Ami hapo juu (akinukuu mwingine) aanasema nnini maana ya Mfumo Kristo: Kwamba,
Sasa kwa haraka haraka mtu anaweza kukubali hili. Na ninaomba kwa sekunde chache tukubaliane na tafsiri hiyo kabla sijaionesha kuwa haina ukweli na haitafsiri Mfumo Kristo ninavyouelewa mimi. Ukisoma maana hiyo Mfumo Kristu ni:
1. Hali - Ni "condition" au tuseme siyo kitu ambacho ni 'concrete'.
2. Wakristo wa Tanzania - ina maana Mfumo Kristu hauwahusu Wakristu wa sehemu nyingine duniani na inapozungumzia Wakristu wa Tanzania inazungumzia "Wakristu" wote.
3. Wamehodhi Madaraka - kwa maneno mengine "Monopoly of power". Kwamba hao watu wa kundi hilo hapo juu wamehodhi madaraka bila kutoa nafasi kwa watu wa dini nyingine.
4. Madaraka ya ngazi zote muhimu za serikali na maamuzi - Hii ni sifa muhimu sana ambayo tutakapoiangalia tutaona inavunja kabisa dhana ya uwepo wa "mfumo huu". Ikumbukwe 'operative word' hapa ni "zote". Nitarudia hili hapa chini kidogo.
5. Kutumia nafasi hizo kuendeleza Wakristu wenzao na Ukristo na kuwabagua Waislamu.
Sifa hizi tano kutokana na maana ya mfumo kama kina Ami wanaamini au wanataka tuamini zinafanya mfumo kuwepo na kutenda kazi. Lakini katika hayo matano ni hilo la nne ndilo HASA linafanya mfumo huu kuwepo kwani bila kushika madaraka yote muhimu hauwezi kuwa na nguvu.
Niwarudishe kidogo kwenye falsafa na hususan kwenye somo la Mantic (Logic). Mantik ni somo ambalo linamsaidia mtu kujenga hoja vizuri, kuepuka makosa ya hoja (fallacies) na wakati huo huo kuhakikisha anagundua makosa hayo kwa wengine. Ukisikia mtu anasema "hii haina mantiki" manake nikuwa kilichosemwa hakijakubaliana na fikra zake - hata kama anaweza asijue maneno yote ya logic.
Kosa la Kwanza la tafsiri ya "Mfumo Kristu" kama alivyoweka Ami iko kwenye kutokuelewa Mantiki na walioandika hilo wenyewe wanaweza kufikiri wamesema cha maana kumbe ndani yake imejaa makosa ya hoja. Nitoe mfano.
Mtu anakuja na kusema "Mimi ni Mtanzania" halafu anasema "Watanzania WOTE ni waongo" halafu akasema "Mimi sisemi uongo".
Sasa mtu mwingine anaweza kuamini hilo lakini mara moja mtu mwenye uelewa mdogo wa mantiki ataonesha "inconsistency" katika madai hayo. Ataonesha hivi:
Kama Wewe ni Mtanzania, na Watanzania wote ni waongo basi wewe huwezi kuwa unasema kweli. Kwa hiyo na huyo anayesema hivyo ama ni mwongo au si Mtanzania. Kama Watanzania WOTE ni waongo basi hakuna Mtanzania anayeweza kuwa anasema kweli.
Mtu akisema Viongozi "WOTE" wa ngazi za juu ni "Wakristu" basi ni lazima tuone kuwa ni Kweli viongozi wote ni "Wakristu". Ukifanikiwa kuonesha kuwa kiongozi mmoja tu ni Mpagani basi hoja kuwa "Viongozi WOTE" ni Wakristu inakufa pale pale.
Ami ametuletea bandiko ambalo tafsiri ya Mfumo Kristu inadai kuwa Wakristu wameshika "nafasi ZOTE MUHIMU". Sasa hii ni rahisi kuonesha; ukionesha Wakristu wameshika nafasi zote muhimu za serikali na "za Maamuzi" basi unathibitisha uwepo wa Mfumo Kristu at least kwa suala la idadi kabla hatujaangalia ile element ya mwisho (ya tano). Lakini ukifanikiwa kuonesha kuwa mojawapo ya nafasi muhimu zinashikiliwa na Muislamu au mtu asiye Mkristu basi hoja kuwa Wakristu wanashika nafasi zote muhimu inakufa. Ukiweza pia kuonesha kuwa zipo nafasi muhimu zinazoshikwa na Waislamu basi HOJA KUWA NAFASI ZOTE ZIMEHODHIWA NA WAKRISTU nayo inakufa.
Hapa inabidi nilete zile orodha alizozileta Ritz kwa fahari kubwa akiamini kuwa anasema kitu very profound:
Ametuwekea 'composition' ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:
Sasa, kitu cha kwanza kuangalia ni kuwa mawaziri wote na manaibu wao wameteuliwa na Rais Kikwete ambaye ni Muislamu. Nafasi kubwa kabisa nchini ya serikali na ya kimaamuzi nchini Tanzania inaongozwa na Muislamu. Ni Muislamu ndiye mtu mwenye nguzu zaidi ya maamuzi Tanzania. Hii ni KWELI (its a Fact). Kikwete akihutubia Bungeni miaka michache nyuma alitamba kuwa ana madaraka makubwa kiasikwamba akitaka Dr. Slaa akamatawe anaweza akakamatwa! HUYU NI MUISLAMU. Hakuna Mkristu yeyote anayempita au kumkaribia kwa madaraka.
Nafasi Muhimu:
Kina Ami wanasema nafasi "Muhimu" zimeshikiliwa na Wakristu hebu tuangalie:
Urais - Jakaya Mrisho Kikwete - Muislamu
Makamu wa Rais - Ghaibu Bilal - Muislamu
Waziri Mkuu - Mizengo PInda - ni Mkristu - aliyeteuliwa na Muislamu!
Waziri wa Mambo ya Nje - Bernard Membe - Mkristu - kateuliwa na Muislamu
Waziri wa Ulinzi - Vuai Nahodha - Muislamu
Waziri wa Viwanda na Biashara - Abdallah Kigoda - Muislamu
Waziri wa Maliasili na Utalii - Khamis Kagasheki - Muislamu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Shukuru Kawambwa - Muislamu (ikumbukwe wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kufeli waliingia kidato cha kwanza hadi cha nne chini ya uongozi wake- NECTA iko chini yake)
Waziri wa Maji - Jumanne Maghembe - Muislamu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii - Hussein Mwinyi - Muislamu
Waziri wa Nchi TAMISEMI - Hawa Ghasia - Muislamu
Sasa hizo ni nafasi "muhimu" za kutosha tu. Nafasi nyingine zote za Mawaziri Wakristu wote wameteuliwa na Rais Muislamu na yeye ndiye mwenye madaraka juu yao.
Je ni kweli "nafasi zote muhimu" zimehodhiwa na Wakristu? kina Ami na Ritz na vijana wengine humu wasiojua mantiki wanasema kwa haraka "ndio"!!
Mfumo Kristu - kwa maoni yao - ndio umewaweka Waislamu hawa kwenye madaraka makubwa hivyo!
Tujiulize mahali pengeine ambapo pamewahi kuwa na mifumo ya kibaguzi:
Utawala wa Makuburu wa Afrika ya Kusini ulitukuza rangi nyeupe kwa muda wa karibu miaka mia nne. Je, ulitengeneza weusi wangapi kwenye nafasi muhimu? NI vipi mfumo wa kibaguzi ulifanya kuwepo Rais Mweusi, mawaziri weusi wakautumikia? NI mweusi gani aliyekuwa na nafasi ya juu kabisa katika serikali ya utawala wa makaburu?
Hili ni kweli hata Marekani wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi (segregation). Ni vipi mfumo ule uliwezesha kutoa nafasi kwa weusi kushika madaraka ya juu?
Kimsingi mfumo wa kibaguzi wa kundi hautoi nafasi kwa wanaobaguliwa kushika madaraka mazito. THIS HAS NEVER HAPPENED BEFORE ANYWHERE IN THE WORLD! Hakuna mahali duniani ambapo mfumo wa kibaguzi (sifa ya tano ya tafsiri ya Mfumo Kristu kama alivyotuwekea ndugu yetu Ami) umewapa madaraka ya juu wanaobaguliwa. Ila wanatuambia Tanzania hili linawezekana. Kwamba Mfumo Kristu katika Tanzania unatupatia viongozi wa Kiislamu!!
Hii tunaweza kusema ni oxymoronic!!
Naomba nitoe changamoto kwa wale wanaoamini kwamba upo mfumo wa kibaguzi dhidi ya Waislamu Tanzania uitwao "mfumo Kristu". NIONESHENI MAHALI POPOTE DUNIANI AMBAPO MFUMO WA KIBAGOZI (A DISCRIMINATORY SYSTEM) IMEWEZA KUTOA VIONGOZI WA WALE WANAOBAGULIWA NA KUWAPA NAFASI MBALIMBALI HADI ZA JUU KABISA WAKATI MFUMO HUO UNAFANYA KAZI!
Naomba mfano mmoja tu.
Nipo safarini ndugu zangu lakini naufutilia munakasha kwa karibu sana tayari nimefyonza Ilm tayari tarudi tena nimeku--copy post ya Wimbi Mbele.
Mzee Said, toka mtoni usioge na watoto watakutia matope! Katika maelezo ya huyo bwana kuna kitu kweli umeelewa wewe ukiwa muasisi wa neno hilo. Siku zote neno likiwa lina utata hutolewa tafsiri kulingana na mazingira. Wewe kama mtafiti huwezi kuacha umma utafute maana ya neno na kisha useme hiyo ndiyo tafsiri.Ami,
Ahsante ndugu yangu kwa kutuanikia mfumokristo.
Wangazija wana msemo maiti hafi ila kwa mzishi wake.
Tumesubiri hadi mzishi ulipowasili na sanda na vyote
vinavyomuhusu maiti.
Kazi kwake aliyekuwa anamkomalia Mohamed Said atoe
"definition."
Nguruvi,
Nikumbushe kwa hisani yako Warioba ni kipi tusichokubaliana au nilichokosea.
Mzee Saidi usikumbie, jibu hoja
1. Ni lini Philip Marmo alikuwa mbunge wa Monduli?
2. Ni lini Kighoma Malima na Mwinyi waliserve kwa pamoja in the vice president's office?
3. Ni kwa nini na kwa vipi Warioba alikwa ni unknown face with no credentials alipoteuliwa kuwa Waziri mkuu?
4. Je Malima alipokuwa akilalamika kuwa anahujumiwa na Kikwete kwa nini hakumtaja Nyerere?
5. Ni baraza lipi la mawaziri Malima na Mwinyi walisevu pamoja? Na Malima kiwa waziri wa nini na Mwinyi waziri wa nini?
Kama kawaida Mzee wetu eti sasa hivi ndiyo anakumbuka OIC.
Mzee Mwanakijiji,
Kwenye tamko la Maaskofu wanasema Kanisa Tanzania limo katika kipindi kigumu cha mateso ya kimfumo (systematic persecution)
Tupe "definition" ili tusonge mbele na huu mnakasha.
Mohamed hajaeleza John Garang (Alumni wa UDSM) alipokelewa vipi uwanja wa ndege.Mohamed Said: Probably in response to this visit by Garang, theg overnment of Al Bashir sent its official delegation to try and explain to the people of Tanzania its own point of view to the conflict. The Sudan government delegation was coldly received at the University. Protocol was flouted shamelessly.While Garang was accorded all the honours fit for a head of state, the Vice Chancellor himself receiving him, the Sudanese government delegatio nwas received by one of the academic staff in the Department of Political Science
Hii ni kwa mujibu wa Mohamed na kwavile haku-balance habari yake kwa kuhoji watu wa chuo kwanini walifanya anavyosema bado inabaki kuwa ni maoni yake wala si maoni ya waislam.The University administration knows who can speak in the lecture theatre and who cannot speak in Nkrumah Hall. The University community made sure that the Sudan government delegation understands that it had walked into an alien territory,where Islam in whatever form was not tolerated
Hapa umekuja mdoogo kabisa,sio kama zile mbwembwe zako za kawaida unapokuja na uzi mrefu wa kujaribu kujibu nukta baada ya nukta.Mzee Said, toka mtoni usioge na watoto watakutia matope! Katika maelezo ya huyo bwana kuna kitu kweli umeelewa wewe ukiwa muasisi wa neno hilo. Siku zote neno likiwa lina utata hutolewa tafsiri kulingana na mazingira. Wewe kama mtafiti huwezi kuacha umma utafute maana ya neno na kisha useme hiyo ndiyo tafsiri.
In short, Mohamed Said huna definition ya neno mfumokristo. Kama ''mwandishi na mtafiti'' this is too low.
Sisi tumetoa definition ya mfumo kristu kulingana na mazingira yetu.Sasa unataka nini tena.?Siku zote neno likiwa lina utata hutolewa tafsiri kulingana na mazingira.
Mohamed hajaeleza John Garang (Alumni wa UDSM) alipokelewa vipi uwanja wa ndege.
Anasema Garang alipewa heshima zote zinazomstahiki mkuu wa nchi. Mohamed sijui amepata wapi hili kwasababu chuo kikuu kina taratibu zake za kupokea wageni wa madaraja tofauti.
Chuo kikuu hakina hakitoi mapokezi ya kitaifa isipokuwa mapokezi yanayolingana na protocol za chuo.
Mohamed anapaswa awaeleze wasomaji 117K je, mapokezi ya John Garang yanatokana na ukristo wake yanawezaje kufananishwa na serikali kuunga Mkono PLO na POLISARIO?
Ni zaidi au ni pungufu! Hii ni kwa mujibu wa Mohamed na kwavile haku-balance habari yake kwa kuhoji watu wa chuo kwanini walifanya anavyosema bado inabaki kuwa ni maoni yake wala si maoni ya waislam.
Hii inatumbusha pale aliposema 10% ya waislam hawakupewa nafasi ya kuuliza jambo.
Kwanza hatujui 10% ameitoa wapi kwasababu kwa mujibu wa maandishi yake waislam ni 20%.
Je, 10% ni wale waliohudhuria mkutano wa Garang au ni jumla ambayo imebadilika kutoka 20%.
Mohamed hakueleza utaratibu uliotumika kuwazuia waislam wasipewe nafasi ya kuuliza maswali.
Lakini kinachoshughulisha fikra za wanaotumia akili ni kuwa kwanini adhani waislam asifikiri wahindi,wapagani na wasioamini?
Huko nyuma Mohamed aliwahi kutuhumu chuo kikuu kwa kusema Lecturers wakristo walipiga marufuku kitabu chake kisitumiwe.
Tuliwahi kumuuliza kama alishawahi kuwasiliana na chuo kupata ufafanuzi, Hakuwa na jibu.
Tukamuuliza ana majina ya lecturers wanaopiga marukufu kitabu chake, hakuwa na jibu.
Sidhani hayo hapo juu atakuwa na jibu.
Kwavyovyote tunachosema hapa ni kuwa ngano hii imeundwa kujenga chuki kwa kutumia matukio halisi na watu wa kweli kwa kupotosha ukweli
Usitoke nje ya mada.Suali ilikuwa Ukristu na uislamu ni dini ipi iliyoitangulia mwenzake?.Sikujibu kwa sababu sikuamini mtu mwenye chembe za Ubongo zinazofanya kazi vizuri hawezi kuuliza swali kama hilo. Kwani jibu lake liko dhahiri kwa mtu yeyote ambaye hana hofu ya kufikiri. Kwa vile hata hivyo umeuliza na licha ya kukuacha kwa muda ujifariji (nikitumaini utagundua fallacy ya swali lako) bado umeendelea nalo. Ili kutokukutafunia na kukumezea nitajibu swali lako kwa kutumia Socratic method...
Swali: Ukristo na Uislamu ni ipi dini iliyotangulia mwenzake?
Jibu: Ukijua nani alianza kufundisha kati ya Mohammed na Yesu utajua dini gani iliyotangulia mwenzake?*
NB*: Uislamu kama dini umekuja na kujulikana baada ya Mohammed kuanza mafundisho yake na ukakua na kueleweka zaidi baada ya kuenea kwake katika Bara Arabia na sehemu nyingine za dunia hadi leo hii; kabla yake hakukuwa na watu walioamini katika Uislamu kama tunavyouelewa sasa.
Muhimu ni kuwaonyesha wasomaji wapi wamepotoshwa.Huwezi kuandika habari za John Garang akiwa UDSM ukaacha kusema huyo ni alumni.Nguruvi,
Kadri utakavyojenga maswali na kutaka ushahidi...Nilichotaka wasikilizaji wakijue ni nini kiliyokea katika
ziara ya Garang.Kwangu mimi hilo ndiyo muhimu.Hayo mengine kwangu si muhimu.
Hapa umekuja mdoogo kabisa,sio kama zile mbwembwe zako za kawaida unapokuja na uzi mrefu wa kujaribu kujibu nukta baada ya nukta.
Mimi nabang kwenye meza kama Abdulrahman Mwalongo.Nakwabia Nguruvi Toka zako hapa huna JIBU!
Sisi tumetoa definition ya mfumo kristu kulingana na mazingira yetu.Sasa unataka nini tena.?
Muhimu ni kuwaonyesha wasomaji wapi wamepotoshwa.Huwezi kuandika habari za John Garang akiwa UDSM ukaacha kusema huyo ni alumni.
Hapa ulificha kitu ili kuteka akili za watu! Kwa maneno mengine unaelezea mtu usiyejua background yake.
Unamfaham John kama mkristo tu, mengine si muhimu.
Huwezi kutoa madai mazito ya waislam kunyimwa nafasi ukiwa huna proof ya utaratibu uliotumika.
Huwezi kutupa takwimu nyingine(10%) tukameza tena kama zile walizomeza wananchi kwa miaka 15, tukae kimya.
Huwezi kutuambia unaeleza kile tusichokijua na ni ukweli wakati tukijua kuna upotoshaji.
Hayo ambayo si muhimu ni yale usio na majibu nayo, kwa wasomaji ni muhimu.
Kitu ulichosema ambacho si kweli ni hikiNukuu hii ndugu yangu ingemfaa sana Mwalimu wenu humu; ni yeye aliyeandika historia akichanganya ukweli, uongo, porojo na hisia zake na kuziita "ukweli"! Ni kipi nilichokisema mimi ambacho si cha kweli? NONE.
Nyerere mwenyewe hakujuwa udugunization bali alichagua watu kwa imani zao.Angalia uongo wako hapaKuna kitu kimoja ambacho wanaolia "dhulma" wanadhani Watanzania hawakijui sana. Wakati wa Nyerere kama kuna kitu kilikuwa kinapigwa vita sana ni kile alichokiita "undugunization" yaani kwa neno la kimombo "nepotism". Tafsiri moja ya nepotism inasema ni "patronage bestowed or favoritism shown on the basis of family relationship, as in business and politics".
Sasa undugunization ulianza kwa kasi baada ya kuanza kuwa na kada ya watumishi wa umma wasomi ambao wameanza kushika nafasi. Kwa kiasi wale waliopata nafasi kidogo walianza kuwaingiza wana familia wao kwenye hizo ajira. Kama Baba alikuwa meneja wa Benki basi mtoto wake akigraduate naye anatafutiwa kazi benki; hii ilikuwa kweli kwenye polisi, na ilikuwa kweli kwenye ajira nyingi sana. Na kwa kadiri watu walivyozidi kupata nafasi za juu ndivyo nao walivyozidi kuwaingiza ndugu zao kwenye ajira na hawakufungwa na ofisi zao kwani waliweza kuwaunganisha na marafiki zao kwenye kada nyingine. Hivyo, mtu anaweza kuwa yuko Ikulu lakini mtoto au jamaa yake akaunganishwa kupata kazi Benki Kuu, au taasisi nyingine.
Jibu la ngano ya Mwanakijiji lipo kwenye paragraph chache alizozinakili Mohammed Said katika kitabu chake kama hivi
Kwenye kitabu cha Developement and religion in Tanzaia cha Bergen uk365 alimnukuu mwalimu Nyerere akisema
" I am a layman but I try to do what I can and will not go against my own church.I want to give the church a better chance here.Tell the bishops that I have established in TANU a department of political education and have put a Lutheran minister in charge;he was not a greater politician. I selected him because of his strong faith"
Sokoine alifanya kazi na Nyerere kama waziri wake.Mohamed Said;6026296] Sokoine had all the necessary qualifications as per CCM's standards to lead the government and later when the time was appropriate, the Party. Nyerere advised Sokoine to resign his post as Prime Minister on medical grounds to go to Yugoslavia for studies. Sokoine came back...... Nyerere wasted no time and appointed him Prime Minister for the second time. Sokoine did not waste time either; he enrolled at the Dar es Salaam University as a post-graduate student. This is how powerful and influential the Christian lobby is.
.Sokoine did not obtain his masters degree as he was killed in a freak road accident in 1984 while travelling from Dodoma to Dar es Salaam.
Na hadi leo Sokoine anabaki kuwa kiongozi maarufu katika historia ya nchi yetu. Wengi walimlilia sana hadharani na hadi sasa wanamkumbuka. Kwa mtu aliyefanya kazi kwa ukaribu na Nyerere katika nyakati ngumu sana sioni kwanini Nyerere akililia hadharani ionekane kama jambo linalohusu wadhaifa na wala si urafiki na ubinadamu.Nyerere shed tears openly for all and sundry to see. His succession plan had crumbled.
Salim Ahmed yupo leo na ingewezekana angetupa ushahidi.Nyerere had to look for another candidate to groom fast to succeed him.
If he had a choice he could have by pass Salim Ahmed Salim but the political scenario as at was at that time, there was no way he could have passed Salim.
Kwa maneno mengine unakubali kuwa Salim alikuwa na uwezo. Sasa kipi kibaya kama Nyerere aliona mtu mwenye uwezo zaidi ya Mwinyi.Short of options and the elections being around the corner, Nyerere backed Salim Ahmed Salim against Mwinyi who was at that time the President of Zanzibar.Salim was the most able than any other person in the whole cabinet. He settled for Salim as the person to succeed him after his retirement.
Angalia hapo Nguruvi anaanza kuja na habari tofauti badala kukiri kuwa definition ya mfumo kristo ndiyo yenyewe na yeye kaikubali na kushindwa kuijibu.Ami,
Serikali tumewaeleza tatizo la mfumokristo.
Sheikh Ilunga katembea nchi nzima kuwaeleza Waislam
kuhusu mfumokristo.
Kipi kitushughulishe kwa Nguruvi?
Wanakuja kusoma hoja.Nguruvi,
Hapana neno.
Tusibaki hapa hapa tuendelee na mnakasha.
Ila jisemee nafsi yako.
Unaetatanishwa ni maandishi yangu ni wewe na
wengine watatu au wanne.
Wengi wanaelewa.
Angalia uwanja unavyofurika.
Hawaji kusoma maswali kwani maswali siku zote
huwa kitu cha mwisho.
Wanakuja kusikiliza darsa langu.