Nguruvi,
Hapana neno.
Tusibaki hapa hapa tuendelee na mnakasha.
Ila jisemee nafsi yako.
Unaetatanishwa ni maandishi yangu ni wewe na
wengine watatu au wanne.
Wengi wanaelewa.
Angalia uwanja unavyofurika.
Hawaji kusoma maswali kwani maswali siku zote
huwa kitu cha mwisho.
Wanakuja kusikiliza darsa langu.
Wanakuja kusoma hoja.
Wanasoma kuwa Warioba alikuwa na credential na wao walijua hivyo.
Aliyekuwa hajui kuwa Warioba alikuwa waziri wa sheria kabla ya uteuzi na mwinyi ni wewe peke yao.
Haya wanayaona kama walivyoona lile la Kawawa kuwa makamu wa Rais mwaka 1988, Marmo kuwa mbunge wa Monduli, Nyerere kuja Dar mwaka 1950, na msomi wa master kubeba hotuba ya bila kuisoma hadi New York. n.k.
Kinachowavuta sana ni pale wanapotambua kuwa takwimu zako ni za kupika na wala hazifuati kanuni achilia mbali weledi wa somo la stats. Wameona jinsi miaka takribani 15 walivyolishwa feki, kwamba mto takwimu hawezi kuzielezea!
Wanakuja kusoma na kushangaa iweje muasisi wa mfumokristo hajui maana yake ni nini.
Na wengine wanashangaa imekuwaje mzee wa US na EU anababaika
Mohamed, kukuuliza maswali ni njia ya majadiliano ambayo kwa mtu anayekimbia hoja kama wewe inamvuta kwenye kona halafu inamwacha kama alivyozaliwa. Hili unalijua.Ulitegemea watu wakae kitako wakisema hewala! wrong palce.
Mtu mwenye ufahamu na kitu anapokuuliza sikwamba hajui ni kwamba anajua na anataka kujua ima unajua kiasi gani au unasimamia wapi. Kama hujui utauliza nini?
Lakini pia hao wasomaji wanaona jinsi hoja zako zinavyobomolewa kama nyumba ya barafu na ndicho kinawashtua.
Wengine hawakujua kuwa hii ni tamthilia mwanana katika umbile la ngano.
Hao watatu wanne wasiokuelewa unaosema ni wale wasiokuelewa ni wale usiowapenda kwasababu wananyong'onyeza hoja zako na kutibua mission yako ya kuasambaza chuki, fitna ,farki kwa mgongo wa dini. No! dini haisemi hivyo.
Kuna hoja nzito zinakusubiri hebu tuwape hao wasomaji raha, zirejee
Mnyambala nadhani atakuwa mtabiri!