Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hahaha hapa hachomoki mtu mpaka ukweli ubaki huru, hawa wachochezi na wazushi kama Mohame tuwaambi
Yericko,
Sie tuchomoke twende wapi ndugu yangu?
Pokea hii hapo chini ni makhsusi kwako:
Bi Mluguru ni kati ya wanawake watu wazima wa mwanzo kumkaribisha Nyerere katika nyumba zao.
Kuna kisa mashuhuri kati ya Nyerere na Bi Mluguru.
Baada ya uhuru kupatikanamengi yakapita na waliokuwa karibu na Nyerere ghafla wakajikuta wako nje ya ulingo lakini maisha hayakusimama yaliendelea kama ilivyo ada.
Siku moja Nyerere akiwa ndani ya msafara wake wa mapikipiki akienda Gerezani kufungua mradi wa viwanda vidogo vidogo, msafara wake uliingia Mtaa wa Sikukuu ukawa unaelekea mitaa ya Kiungani.
Nyerere akiwa ndani ya benzi lake alikuwa akitupa macho huku na huku akiangalia mitaa yake aliyokuwa akiikanyanga kwa miguu enzi za kudai uhuru.
Bila shaka msafara ulipopita Kipata na Sikukuu Nyerere aliiangalia nyumba ya Mzee Mtamila.
Katika nyumba hii ndipo Nyerere alipowasilisha barua alitoandikiwa na waajiri wake achague mawili siasa au ualimu.
Uamuzi ulitolewa pale wa kumwambia kuwa aache kazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu wa TANU wakati ule alikwa Mzee Clement Mtamila na mmoja wa wajumbe waliohudhuria mkutano ule muhimu alikuwa Bi. Tatu biti Mzee.
Msafara ulipoingia Sikukuu na naKirk kuna shaka alinyoosha shingo yake kuangalia nyumba aliyoijua sana, nyumbani kwa Abdulwahid Sykes na mama yake Bi Mluguru.
Hapa jicho la Nyerere likagongana nia sura ya Bi Mluguru aliyekuwa amejipanga mstari pamoja nawananchi wengine kuangalia msafara wa Nyerere.
Alipotambua kuwa yule mamaaliyesimama alikuwa Bi Mluguru, Nyerere aliamrisha gari yake isimame na kwa ghafla dereva wake alisimamisha gari.
Nyerere alitoka nje ya gari akamwendea BiMluguru kumwamkia.
Mapikipiki yalisimama madereva wamepigwa na butwaa.
Wanaangalia nyuma wanamuona Nyerere anazungumza na mama mmoja mtu mzima.
Haraka walinzi wakawa wamemzunguka Nyerere na Bi Mluguru.
Kwa hakika kitendo kile kilikuwa cha kushangaza.
Nyerere alipoondoka na msafara wake nyuma aliacha gumzo kubwa.
Ilikuwa miaka michache baada ya kifo cha Abdulwahid.
Walioijua historia ya Nyerere na marehemu Abdulwahid Sykes kitendo kile cha kiungwana chaNyerere hakikuwashangaza.
Tabu walipata wale waliokuwa hawaijui vyema historiaya Nyerere alipofika Dar es Salaam kutokea Musoma mwaka wa 1952 na kupokelewa na Abdulwahid Sykes akiwa Rais wa TAA.