MM,
naona sasa umeamua kuhamishia huu uzi toka uchochezi hadi YESU ni Muislamu! labda kwa kuwa Leo YESU kafufuka soma kipande hiki:
Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea (Matt. 18:11)."
Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"
Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:
"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""
Mbona unasoma maandiko out of context yaani una chop mistari na kuiunga kwa kupindisha maana kamili. Neno la Mungu ni moja Mungu hajikanganyi hata siku moja ndio maana tunaliita "Neno" la Mungu na sio "maneno ya Mungu" hivyo ungekuwa umetufanyia fadhila kutupa contextual meaning of those verses.
Zaidi, Yesu mara zote aliongea kwa namna tofauti na watu tofauti tofauti. makundi ni pamoja na wanafunzi, thenashara, makutano na mitume. hawa walimfuata ila pia walikua waliompinga mafarisayo, waandishi na walimu wa sheria na alijulikana kutumia mifano alipokua na makutano na kuongea wazi alipokua na wanafunzi na kutumia vitendawili alipokua na group la mafarisayo na wenzao. Sababu hasa ilikua kumpa kila mtu stahiki na stahili yake. Kumbuka Yesu alikua na uwezo wa kusoma mawazo ya mioyo ya watu. Kwa mantik hiyo kuchambua maneno ya Yesu juu juu hivyo na kusema Yesu hakuja kwaajili ya mataifa si sahahi.
Nitakupa mfano
Mie nikinukuu Mathew 21:
MT. 21:28-46
Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini. Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki. Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
------------------
Hapa katika mfano wa kwanza tunaona Yesu anaonesha utii wa wana wawili na ya kwamba utii wa kutenda maagizo au ndio hasa utii sio tu kukubali. Wana wa Israel walikua wanakiri maagizo na maandiko bila kutenda ambapo mfano wa pili unaonesha wazi ufalme wa Mungu utaondolewa kwao na kupewa wengine wenye utii wa kweli kwa kuwa Mungu hana upendeleo hata watoza ushuru wakitii husamehewa.
---
Again, sio vema kuanzisha mjadala wa kidini hapa kwa ku attack dini ya mwenzio tukifanya hivyo itakua ni kuchepuka katika mada. Ila pale kunapotukia upotoshaji tutaweka rekodi sawa tukiwa hapa.