Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Sikujibu kwa sababu sikuamini mtu mwenye chembe za Ubongo zinazofanya kazi vizuri hawezi kuuliza swali kama hilo. Kwani jibu lake liko dhahiri kwa mtu yeyote ambaye hana hofu ya kufikiri. Kwa vile hata hivyo umeuliza na licha ya kukuacha kwa muda ujifariji (nikitumaini utagundua fallacy ya swali lako) bado umeendelea nalo. Ili kutokukutafunia na kukumezea nitajibu swali lako kwa kutumia Socratic method...
Swali: Ukristo na Uislamu ni ipi dini iliyotangulia mwenzake?
Jibu: Ukijua nani alianza kufundisha kati ya Mohammed na Yesu utajua dini gani iliyotangulia mwenzake?*
NB*: Uislamu kama dini umekuja na kujulikana baada ya Mohammed kuanza mafundisho yake na ukakua na kueleweka zaidi baada ya kuenea kwake katika Bara Arabia na sehemu nyingine za dunia hadi leo hii; kabla yake hakukuwa na watu walioamini katika Uislamu kama tunavyouelewa sasa.
Uislamu umekuwepo kabla hata Yesu hajazaliwa.Uislamu ulianza na binadamu wa mwanzo duniani na unaendelea mpaka leo.Sikujibu kwa sababu sikuamini mtu mwenye chembe za Ubongo zinazofanya kazi vizuri hawezi kuuliza swali kama hilo. Kwani jibu lake liko dhahiri kwa mtu yeyote ambaye hana hofu ya kufikiri. Kwa vile hata hivyo umeuliza na licha ya kukuacha kwa muda ujifariji (nikitumaini utagundua fallacy ya swali lako) bado umeendelea nalo. Ili kutokukutafunia na kukumezea nitajibu swali lako kwa kutumia Socratic method...
Swali: Ukristo na Uislamu ni ipi dini iliyotangulia mwenzake?
Jibu: Ukijua nani alianza kufundisha kati ya Mohammed na Yesu utajua dini gani iliyotangulia mwenzake?*
NB*: Uislamu kama dini umekuja na kujulikana baada ya Mohammed kuanza mafundisho yake na ukakua na kueleweka zaidi baada ya kuenea kwake katika Bara Arabia na sehemu nyingine za dunia hadi leo hii; kabla yake hakukuwa na watu walioamini katika Uislamu kama tunavyouelewa sasa.
Qur'an 2:136 inaweka wazi hilo
قُولُواْ آمَنَّا بِاللَّهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَى إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwakeHapo utaona Mitume wote tangu baba yetu Adam A.S ni waislamu pamoja na Yesu (Issa a.s).
Socratic method... sijui kama inasemaje kuhusu kukua na kusambaa kwa dini lakini sisi tujuavyo ni kuwa Uislamu tangu binadamu wa mwanzo huwa unakuwa na kuenea halafu watu huasi hasa Mtume aliyetangulia anapokufa.Baadae Mwenyezi Mungu hutoa Mtume mwengine miongoni mwa watu na kuwazindua tena watu kuufuata uislamu.NB*: Uislamu kama dini umekuja na kujulikana baada ya Mohammed kuanza mafundisho yake na ukakua na kueleweka zaidi baada ya kuenea kwake katika Bara Arabia na sehemu nyingine za dunia hadi leo hii; kabla yake hakukuwa na watu walioamini katika Uislamu kama tunavyouelewa sasa.
Baada ya kuondoka kwa nabii Musa A.S ilipita miaka mingi watu wakarudi kwenye ukafiri na dini zao za kishirikina mpaka alipoletwa Yesu a.s na kuendeleza ujumbe wa uislamu kwa watu wake.Na hivyo hivyo alipoondoka Yeye watu wakazidi kukufuru mpaka alipoteremshwa Mtume Muhammmad s.a.w na kuahidiwa kuwa huyu atakuwa ndiye Mtume wa mwisho kabla ya kiyama.