Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mzee MS hii habari uliyoandika hapa ni nzito lakini kuna bwana mmoja anaitwa Gwalihenzi anapenda sana kukutukana mimi namshangaa halafu Nguruvi anampa likes nyingi mimi namshaa sana huyu jamaa sijawahi hata siku moja akielezea historia yoyote anayoijua dah mzee MS kazi uliyoifanya ni kubwa nakuomba upumzike waachie wao waliokuwa wanashindana badala ya kufundisha kama wewe.

Unasema apumzike we unauwezo wa kujibu mswali yaliyoelekezwa kwake?

Au baada ya kuona upper cut zimekuwa nyingi mdo mnarusha taulo katikati? hapa hatoki mtu

Akiingia Nguruvi tu mzee wako huyo fasta anakuja kutafuta nguo za kujisitiri.

Bila uwepo wa watu hawa Mzee Mwanakijiji , Mag3 , Jasusi , Nguruvi3 , Nyambala (mara moja moja akija kuweka mambo sawa) sweke 34 ,na wengine wengi wapenda amani huu mjadala haunogi hawa ndo watu muhimu na Watu hawa 100,000+ wanawasikiliza hawa.

Mzee wako akikimbia hapa ataadhirika.
 
Last edited by a moderator:
MWANAKIJIJI,
Umesoma tamko la Kanisa kuhusu kuchinja?

na hapa utawahukumu vipi Viongozi wenu?
Tangu kuumbwa kwa dunia, Mwenyezi Mungu ameweka, kuziondoa au kuzirudisha sheria mara kadhaa, kwa mfano, vyakula, hapo zamani kuleni vyote (Mwanzo 9:1-4).

Baadaye msile vyakula fulani (Walawi sura ya 11) sasa kuleni vyote (Luka 10:8). Kuchinja sadaka: Zamani chinjeni wanyama kwa toba (Wal. 5:6-13) sasa hakuna kuchinja, Yesu amechinjwa inatosha (Mathayo 26:28, Ebr. 10:4-9). Kutawadha: Zamani kutawadha (Kutoka 30:17-21) sasa hakuna haja (Ebr. 9:10). Kutahiri: Zamani hakuna kutahiri, baadaye kutahiri (Mw. 17:11-4) Sasa hakuna haja (Rumi 2:30).
 
Msafara ulipoingia Sikukuu na naKirk kuna shaka alinyoosha shingo yake kuangalia nyumba aliyoijua sana, nyumbani kwa Abdulwahid Sykes na mama yake Bi Mluguru.

Hapa jicho la Nyerere likagongana nia sura ya Bi Mluguru aliyekuwa amejipanga mstari pamoja nawananchi wengine kuangalia msafara wa Nyerere.

Alipotambua kuwa yule mamaaliyesimama alikuwa Bi Mluguru, Nyerere aliamrisha gari yake isimame na kwa ghafla dereva wake alisimamisha gari.

Nyerere alitoka nje ya gari akamwendea BiMluguru kumwamkia.

Mapikipiki yalisimama madereva wamepigwa na butwaa.

Wanaangalia nyuma wanamuona Nyerere anazungumza na mama mmoja mtu mzima.

Haraka walinzi wakawa wamemzunguka Nyerere na Bi Mluguru.

Kwa hakika kitendo kile kilikuwa cha kushangaza.

Nyerere alipoondoka na msafara wake nyuma aliacha gumzo kubwa.

Ilikuwa miaka michache baada ya kifo cha Abdulwahid.

Hili ni mojawapo ya masimulizi yako ambayo yanavutia kweli usomaji lakini ukiyasogelea kwa karibu yanavunja vunja kabisa dhana kuwa Nyerere alikuwa na chuki na Sykes, au Waislamu! Unasema mara nyingi kuwa ugomvi wake na Waislamu ulianza mwaka 1963; lakini hapa unasema hili lilitokea miaka kadhaa baada ya kifo cha Abdul. Nyerere huyu aliyekuwa na chuki na ugomvi na Sykes anapita kwenye mitaa akiangalia kukumbuka alikopita miaka mingi nyuma. Yuko ndani ya gari anaangalia angalia nje (sijui kama lilikuwa gari la wazi au la kawaida maana kama ni gari la kawaida watu waliojazana pembeni ya barabara sijui Nyerere aliweza vipi kuziona nyumba zile! - tuliache hilo.. lakini Nyerere mwenye chukina Waislamu na asiyetaka kuwaenzi wale alioshirikiana nao miaka mingi baada ya kifo cha Abdul; anawakumbuka, ana hamu ya kuona wanakoishi na kufikia mahali anasimamisha msafara wa Rais, kutoka nje, kwenda kuamkia..!!!

Kama hii ni chuki basi upendo hauna maana tena!!

Walioijua historia ya Nyerere na marehemu Abdulwahid Sykes kitendo kile cha kiungwana chaNyerere hakikuwashangaza.

Kuna masimulizi kama haya mengi sana kumhusu Nyerere; Nyerere alikuwa Muungwana kweli kweli. Hakuwa na chuki dhidi ya Waislamu au wale alioshirikiana nao wakati wa uhuru; wengine walikuwa na tofauti na tena tofauti kubwa tu lakini chuki ya kuwatakia mabaya, kuwasusa?

Tabu walipata wale waliokuwa hawaijui vyema historiaya Nyerere alipofika Dar es Salaam kutokea Musoma mwaka wa 1952 na kupokelewa na Abdulwahid Sykes akiwa Rais wa TAA

Kama kawaida unatengeneza historia mpya; Nyerere alipokuja Dar mwaka 1952 akitokea Musoma alipokelewa na Abdulwahid Sykes? Really? Wapi huko?
 
MWANAKIJIJI,
Umesoma tamko la Kanisa kuhusu kuchinja?

Hayo nawaachia watu wa kanisa na wanaohangaishwa na hilo; miye nakula kinachochinjwa na yeyote!! hata kinachojichinja chenyewe kinaliwa vile vile. Ufalme wa Mungu si katika kula na kunywa!!!
 
MM,
naona sasa umeamua kuhamishia huu uzi toka uchochezi hadi YESU ni Muislamu! labda kwa kuwa Leo YESU kafufuka soma kipande hiki:

Kadogoo, hili eneo wala silitaka nilifanya haya miaka ya themanini na kina Mwaipopo; nimemsoma Ahmed Deedat na vitabu vyake vyote na hoja zake zote. Nimeshafanya mihadhara hii na kuwakimbiza watu wale kwenye hili hunikaribii. Tunazungumzia historia iliyopotoshwa na Mohammed Said kuhusiana na harakati za Uhuru na tuhuma za dhulma dhidi ya Waislamu. Hii mihadhara ya jangwani na 'Nabii Yule" nimeachana nayo kwani nitavuruga imani yako bure. Tuendelee na haya mengine; ukitaka kujadiliana nao nenda kwenye dini kule kuna kina Ex Pastor na Max Shimba wanajadiliana sana kuhusu haya.

Pole kama nitakukwaza.
 
Ni lazima ujue kuwa watu hawa Njozi, Said na mfadhili wao wote wako pamoja. Ni wao ndio walioanzisha madai ya kudhulumiwa Waislau mwanzoni mwa miaka ya themanini wako sehemu ya kundi la vijana wa Warsha. Ukielewa hili utaona kuwa anachosema Njozi kimefichika katika lugha ya kisomi lakini nacho kinakabiliwa na changamoto zile zile anazokutana nazo Mzee Said hapa.

Mzee Mwanakijiji,

Sijui kama unahifadhi kumbukumbuku ya maandiko yako.

Kupitia huu uzi uliandika kuwa Mohamed Said na Prof Njozi wapo tofauti Prof Njozi yeye hana chuki na Nyerere chuki yake ni CCM.

Leo tena unatuambia Mohamed Said na Prof Njozi wapo pamoja na mfadhili wao ndiyo walioanzisha madai ya Waislam kudhulumiwa. Unajidanganya sana unapenda sana kutumia fikra zako kwenye masuala ya Waislam bila kufanya utafiti.

Narudia tena kukwambia Mohamed Said, Prof Njozi, ndani ya Misikiti ni maamuma tu kama mimi kuna Masheikh wakubwa ndiyo viongozi unawaogopa sana hawa jamaa aisee!

Dhulma dhidi ya Uislam zipo wazi toka miaka ya 1962 siyo leo kama unavyofikiri wewe kuna Masheikh wengi wamefungwa jela wewe ili unaweza kuliona dogo sababu alikuhusu na ukaona siyo dhulma.

Kuna Masheikh wamepelekwa jela hata siasa hawazifahamu.

Hawa hapa Sheikh Al Amin Maftah, Sheikh Suleiman Masudi Manoji, Sheikh Jumanne Bias, Sheikh Nurdin Hussein, Sheikh Shariff Hussein Badawiy, Sheikh Ali Migeyo, Sheikh Adulkarim Adulwahid, Sheikh Matar, Sheikh Shariff Adnan.
 
Unasema apumzike we unauwezo wa kujibu mswali yaliyoelekezwa kwake?

Au baada ya kuona upper cut zimekuwa nyingi mdo mnarusha taulo katikati? hapa hatoki mtu

Akiingia Nguruvi tu mzee wako huyo fasta anakuja kutafuta nguo za kujisitiri.

Bila uwepo wa watu hawa Mzee Mwanakijiji , Mag3 , Jasusi , Nguruvi3 , Nyambala (mara moja moja akija kuweka mambo sawa) sweke 34 ,na wengine wengi wapenda amani huu mjadala haunogi hawa ndo watu muhimu na Watu hawa 100,000+ wanawasikiliza hawa.Mzee wako akikimbia hapa ataadhirika.
Mzee Mohamed anatafuta mlango sasa anataka kuchomoka, wapambe wanamshauri mahali aliposasa hapafai. Kama hana kumbu kumbu za mwaka 1983 basi zingine zina uwalakini mkubwa.
Kama hafahamu Garang ni alumni wa UDSM anamfahamu kama mkristo kwasababu ya jina John lazima aangalie pa kutokea.
Viporo vingi hajui aguse wapi aache wapi.

Kingine kasukumiwa dakika chache, Nyerere alikuja Dar na kukutana na Sykes 1952!

Hebu ngoja niangalie shajara zangu ili akitokea mlango wa uani akutane na stats huko aliko na afahamu kuwa akioga na watoto kama Ami mtoni hatataka.

Nitarudi.
 
Boko Haram,
Nachukua likizo.

Ahsante kwa ushauri mwema.
Ushauri na uamuzi mzuri.Somo la historia limeeleweka.Umefanya kazi bila kupumzika kwa miezi kadhaa ni zamu yako kuchukua likizo.Sisi tutabaki hapa kwa uwezo wa Allah kuendelea na chapter nyengine kuhusu utumwa na uislamu na ukristo.
Soma Qur'an suratul Baqara kuanzia aya ya 1-18.Aya ya 18 imemalizia kwa kusema
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لاَ يَرْجِعُونَ
Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.

Tahadhari hiyo imetolewa kwenye Qur'an kuhusiana na tabia ya makafiri.Wao wanaharibu huku wanasema wanatengeneza.Ukweli wakipewa husema ni uongo.
Ushahidi wote uliotolewa kuhusu dhulma za Nyerere wanasema si lolote si chochote.Ikifika hapo anayejuwa jinsi ya kuwafahamisha na wakafahamu sio si sisi ni Allah s.w mwenyewe.
 
Mzee Mohamed amatafuta malango sasa anataka kuchomoka, wapambe wanamshauri mahali aliposasa hapafai. Kama hana kumbu kumbu za mwaka 1983 basi zingine zina uwalakini mkubwa.
Kama hafahamu Garang ni alumni wa UDSM anamfahamu kama mkristo kwasababu ya jina John lazima aangalie pa kutokea.
Viporo vingi hajui aguse wapi aache wapi.

Kingine kasukumiwa dakika chache, Nyerere alikuja Dar na kukutana na Sykes 1952!

Hebu ngoja niangalie shajara zangu ili akitokea mlango wa uani akutane na stats huko aliko na afahamu kuwa akioga na watoto kama Ami mtoni hatataka.

Nitarudi.

Mkuu nakusubiri sana.
Hayo na mengine mengi ameshindwa kuyatetea.Eti wanafunzi wake wanasema waachiwe ukumbi yeye apumzike!kituko ni kwamba sioni kati yao anayeweza kusimama kwa hoja na kufanya mnakasha na wewe.

Wape tu elimu bure Mungu atakulipa wala usijibu matusi yao.

Ila maswali mpelekee Mzee Mo mwenyewe ajibu hao hawawezi kukujibu

Tumeambiwa kuna Mfumo Kristo ila tukiuliza ni nini tunajibiwa na wanafunzi!Mwalimu hana jibu.HAJUI!

Mwanakijiji alichambua tafsiri moja hapa ya Mfumo Kristo iliyoletwa na Mwanafunzi mmoja wa Mzee Mohamed wote wakakaa kimya

Mzee Mo Alileta habari kuhusu Sokoine watu wakampa ukweli!KIMYA
nk nk nk nk

Ni mengi mengi mengi hayajapatiwa majibu

Nashangaa Mwafrika anashabikia mijadala ya UTUMWA eti nani alifanya dhambi kumzidi mwenzake kati ya Waislamu na Wakristo?

Nguruvi wewe ndo Star hapa bila wewe watu wanakula ngano nzima nzima bila kukobolewa
 
Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea (Matt. 18:11)."

Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"

Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:

"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""
Kadogoo,
Kuna mtu amekushauri kuwa haya masuala ya dini yaweke kule kwenye uzi wa dini. Na mimi naongezea tu kwamba kitu usichokifahamu ni kama usiku wa kiza. Hii ya kuchukua mstari mmoja mmoja wa kauli za Yesu na kututupia usoni kwamba Yesu alikuja kwa ajili ya waisraeli peke yao unahitaji kuanzisha uzi ukumbane na akina Max Shimba huko, wanaojua injili katika muktadha wake wote. Paulo hakuwa Myahudi. Huyu naye alikuwa na uwezo wa kuponyesha na alifanya hivyo baada ya Yesu kupaa mbinguni. Fungua uzi wake.
 
Ni lazima ujue kuwa watu hawa Njozi, Said na mfadhili wao wote wako pamoja. Ni wao ndio walioanzisha madai ya kudhulumiwa Waislau mwanzoni mwa miaka ya themanini wako sehemu ya kundi la vijana wa Warsha. Ukielewa hili utaona kuwa anachosema Njozi kimefichika katika lugha ya kisomi lakini nacho kinakabiliwa na changamoto zile zile anazokutana nazo Mzee Said hapa.
Na kabla ya uzi huu watu wengi waliamini kuwa WARSHA ni kitu kilichofanywa na watu wengine kabisa.

Sasa hivi tunajua WARSHA ni kundi hili analoongelea MM ambalo lilifanya utafiti likiwa na majibu na kisha kuzama katika kuusherehesha utafiti huo kwa kuandika vitabu na kusubiri matukio ili kuandika paper.

Kinachosumbua zaidi ni kuona kuwa utafiti huo wa WARSHA ulisimamiwa na Sheikh Malik kutoka Pakistan ambaye baada ya kugundulika hila zake serikali ikampiga PNG(Persona non grata).

Wanachama wa WARSHA ndio hao wanaoandika magazeti ambayo kila siku ni kuleta tension badala ya kutafuta chimbuko na matatizo ya jamii si ya kiislam tu bali ya nchi kwa ujumla.

Haiwezekani magazeti hayo yasione ukweli kuwa wizi uliofanywa na kundi dogo la watu wa imani zote linaigharimu serikali dollar 150 kwa siku achilia mbali mabilioni yatokanyo na kesi mahakamani.

Haiwezekani kundi hilo lisione bilioni 30 za Radar na jinsi zinavyotafunwa sana na kukaa kimya bila kuona kama ni tatizo kwa jamii.
 
MM,
naona sasa umeamua kuhamishia huu uzi toka uchochezi hadi YESU ni Muislamu! labda kwa kuwa Leo YESU kafufuka soma kipande hiki:

Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea (Matt. 18:11)."

Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"

Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:

"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""

Mbona unasoma maandiko out of context yaani una chop mistari na kuiunga kwa kupindisha maana kamili. Neno la Mungu ni moja Mungu hajikanganyi hata siku moja ndio maana tunaliita "Neno" la Mungu na sio "maneno ya Mungu" hivyo ungekuwa umetufanyia fadhila kutupa contextual meaning of those verses.

Zaidi, Yesu mara zote aliongea kwa namna tofauti na watu tofauti tofauti. makundi ni pamoja na wanafunzi, thenashara, makutano na mitume. hawa walimfuata ila pia walikua waliompinga mafarisayo, waandishi na walimu wa sheria na alijulikana kutumia mifano alipokua na makutano na kuongea wazi alipokua na wanafunzi na kutumia vitendawili alipokua na group la mafarisayo na wenzao. Sababu hasa ilikua kumpa kila mtu stahiki na stahili yake. Kumbuka Yesu alikua na uwezo wa kusoma mawazo ya mioyo ya watu. Kwa mantik hiyo kuchambua maneno ya Yesu juu juu hivyo na kusema Yesu hakuja kwaajili ya mataifa si sahahi.

Nitakupa mfano

Mie nikinukuu Mathew 21:

MT. 21:28-46

Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini. Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki. Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.

------------------
Hapa katika mfano wa kwanza tunaona Yesu anaonesha utii wa wana wawili na ya kwamba utii wa kutenda maagizo au ndio hasa utii sio tu kukubali. Wana wa Israel walikua wanakiri maagizo na maandiko bila kutenda ambapo mfano wa pili unaonesha wazi ufalme wa Mungu utaondolewa kwao na kupewa wengine wenye utii wa kweli kwa kuwa Mungu hana upendeleo hata watoza ushuru wakitii husamehewa.

---
Again, sio vema kuanzisha mjadala wa kidini hapa kwa ku attack dini ya mwenzio tukifanya hivyo itakua ni kuchepuka katika mada. Ila pale kunapotukia upotoshaji tutaweka rekodi sawa tukiwa hapa.
 
Mzee Mwanakijiji,

Sijui kama unahifadhi kumbukumbuku ya maandiko yako.

Kupitia huu uzi uliandika kuwa Mohamed Said na Prof Njozi wapo tofauti Prof Njozi yeye hana chuki na Nyerere chuki yake ni CCM.

Ni miongoni mwa watu wenye kumbukumbu nzito sana rafiki yangu; rudi kasome nilichoandika halafu uje kujisahihisha mwenyewe.
 
View attachment 88720
Kwa wale waliokuwa wanazungumzia census ya 1967 nawawekea hapa summary yake

safi sana; na miye nimeagiza kitabu cha sensa ya mwaka huo kutoka MSU; sasa ndugu zetu hawa ambao wamekuwa wakirudia matokeo ya sensa hiyo wana nafasi ya kuonesha kuwa matokeo haya si ya kweli kwa kuweka matokeo ya sensa hiyo kama ilivyo hapa tuone tofauti iko wapi...
 
Back
Top Bottom