Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hahaha hapa hachomoki mtu mpaka ukweli ubaki huru, hawa wachochezi na wazushi kama Mohame tuwaambi

Yericko,

Sie tuchomoke twende wapi ndugu yangu?
Pokea hii hapo chini ni makhsusi kwako:

Bi Mluguru ni kati ya wanawake watu wazima wa mwanzo kumkaribisha Nyerere katika nyumba zao.
Kuna kisa mashuhuri kati ya Nyerere na Bi Mluguru.

Baada ya uhuru kupatikanamengi yakapita na waliokuwa karibu na Nyerere ghafla wakajikuta wako nje ya ulingo lakini maisha hayakusimama yaliendelea kama ilivyo ada.

Siku moja Nyerere akiwa ndani ya msafara wake wa mapikipiki akienda Gerezani kufungua mradi wa viwanda vidogo vidogo, msafara wake uliingia Mtaa wa Sikukuu ukawa unaelekea mitaa ya Kiungani.

Nyerere akiwa ndani ya benzi lake alikuwa akitupa macho huku na huku akiangalia mitaa yake aliyokuwa akiikanyanga kwa miguu enzi za kudai uhuru.

Bila shaka msafara ulipopita Kipata na Sikukuu Nyerere aliiangalia nyumba ya Mzee Mtamila.
Katika nyumba hii ndipo Nyerere alipowasilisha barua alitoandikiwa na waajiri wake achague mawili siasa au ualimu.

Uamuzi ulitolewa pale wa kumwambia kuwa aache kazi.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu wa TANU wakati ule alikwa Mzee Clement Mtamila na mmoja wa wajumbe waliohudhuria mkutano ule muhimu alikuwa Bi. Tatu biti Mzee.

Msafara ulipoingia Sikukuu na naKirk kuna shaka alinyoosha shingo yake kuangalia nyumba aliyoijua sana, nyumbani kwa Abdulwahid Sykes na mama yake Bi Mluguru.

Hapa jicho la Nyerere likagongana nia sura ya Bi Mluguru aliyekuwa amejipanga mstari pamoja nawananchi wengine kuangalia msafara wa Nyerere.

Alipotambua kuwa yule mamaaliyesimama alikuwa Bi Mluguru, Nyerere aliamrisha gari yake isimame na kwa ghafla dereva wake alisimamisha gari.

Nyerere alitoka nje ya gari akamwendea BiMluguru kumwamkia.

Mapikipiki yalisimama madereva wamepigwa na butwaa.

Wanaangalia nyuma wanamuona Nyerere anazungumza na mama mmoja mtu mzima.

Haraka walinzi wakawa wamemzunguka Nyerere na Bi Mluguru.

Kwa hakika kitendo kile kilikuwa cha kushangaza.

Nyerere alipoondoka na msafara wake nyuma aliacha gumzo kubwa.

Ilikuwa miaka michache baada ya kifo cha Abdulwahid.

Walioijua historia ya Nyerere na marehemu Abdulwahid Sykes kitendo kile cha kiungwana chaNyerere hakikuwashangaza.

Tabu walipata wale waliokuwa hawaijui vyema historiaya Nyerere alipofika Dar es Salaam kutokea Musoma mwaka wa 1952 na kupokelewa na Abdulwahid Sykes akiwa Rais wa TAA
.
 

Maneno ya busara sana haya Mkuu.
 
Ritz,
Maalim wangu Sheikh Haruna alikuwa anasema ukiona sasa mtu anatoa matusi
jua ushamshinda.

Mwenye hoja hana muda wa kutukana.
Atapambana na wewe kwa hoja siyo matusi.

MS,
Wataelewa tu, twende nao taratibu! Kumbuka hata Mtume ilimchukua miaka 23 kufafanua Kalima Tawhiid! Hata Abuu Sufiyani aliyekuwa hataki kusikia hata jina la Mtume na kumfanyia vitimbi vya kila aina, mwishoni alimkubali Mwenye enzi Mungu na Mtume wake! seuze wewe MS? halafu nakuomba uendelee na ule ukarimu wako wa kumkaribisha Sahib wako barazani na sharbati, kahawa tende na Lozi bila kusahau sahani hii ya halua ya karoti! kama RITZ ameshindwa kulipa naomba nitumie bili mi talipa tu!
 

Gwalihenzi karibu na wewe vitu kama hivi huwezi kuvipata huko uliko njoo pande hizi
 

Nguruvi, Nguruvi, Nguruvi,
Kaka...
 
Nguruvi, Nguruvi, Nguruvi,
Kaka...
Nikumbushe kwa hisani yako Warioba ni kipi tusichokubaliana au nilichokosea.
........
 
Tunakuomba sana usithubutu kuondoka utatuacha wakiwa tufyonza wapi Ilm.

Spike,
Habari za safari nakukaribisha na hii ndugu yangu:

Ukivuka Nyamwezi Street sasa mkono huo huo wa kushoto unafika nyumbani kwa Mashado Ramadhani Plantan, mwanachama shupavu wa African Association, TAA, TANU na AllMuslim National Union of Tanganyika (AMNUT).

Mashado Plantan alizaliwa Mozambique mwaka 1900 na alikuja Tanganyika mwaka wa 1905 akiwa mtoto mdogo wa miaka mitano.

Mashado Plantan ni miongoni mwa wanachama mwanzo wa TANU naMwafrika wa pili katika Tanganyika kuwa na gazeti lake mwenye - Zuhra.

Mwafrikawa kwanza kuwa na gazeti alikuwa Erika Fiah, Mwafrika kutoka Uganda aliyelowea Tanganyika.

Gazeti lake likiitwa "Kwetu" Mashado Plantan ndiyo alikuwa mzalendo wa kwanza kuifanyia propaganda TANU na kumjulisha Nyerere kwa wananchi wa Tanganyika kupitia gazeti lake la Zuhra.

Mashado Plantan, Kleist Sykes na Mdachi Sharifu ni miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa jengo la AfricanAssociation, New Street mwaka wa 1933 jengo ambalo lilifunguliwa na Gavana Donald Cameroon.

Baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu na ugomvi uliotokea baina ya Mwenyekti wa Baraza la wazee wa TANU Dar es Salaam na Julius Nyerere mwaka wa 1958 Mashado alitoka TANU yeye na wanachachama wengine kuunda AMNUT na nyumba yake ikawa ndiyo ofisi ya kwanza ya chama hicho.

Mashado aliondoka duniani akiwa na kinyongo na TANU jinsi ilivyovunja ndoto za wengi walioweka matumaini makubwa katika uhuru waTanganyika.

Alimaliza siku zake akitumia muda wake mwingi katika msikiti waSheikh Juma Tego Mtaa wa Lindi.
 
Nguruvi, Nguruvi, Nguruvi,
Kaka...

Nikwambie kitu mz MS hebu kuanzia kesho pumzika halafu tuwaache wajadiliane wenyewe Nguruvi3,Mag3,Mwanakijiji,Nyambala etc..... kuna mambo mengi ya kufanya kama kuhifadhi Quran kupitia Hadith za mtume haya kesho allah atakulipa huku kuna watu hawamtambui mungu nimeweka aya za mwenyezimungu matusi niliyo yapata mungu ndio anajua.
 

Boko Haram,
Nachukua likizo.

Ahsante kwa ushauri mwema.
 

Kadogoo,

Hapo lazima upate na gahawa kidogo au chai ya mdalisini ni mjarabu...talipa hiyo bili.
 
Last edited by a moderator:

Mzee MS hii habari uliyoandika hapa ni nzito lakini kuna bwana mmoja anaitwa Gwalihenzi anapenda sana kukutukana mimi namshangaa halafu Nguruvi anampa likes nyingi mimi namshaa sana huyu jamaa sijawahi hata siku moja akielezea historia yoyote anayoijua dah mzee MS kazi uliyoifanya ni kubwa nakuomba upumzike waachie wao waliokuwa wanashindana badala ya kufundisha kama wewe.
 

Nafyonza Ilm kisha nakwenda zangu vitu kama hivi tavipata wapi tayari nimecopy kwenye laptop yangu.
 
Nafyonza Ilm kisha nakwenda zangu vitu kama hivi tavipata wapi tayari nimecopy kwenye laptop yangu.

Spike Lee bora hata weweunapata ilm kunawatu humu jamvini kazi yao ni kutukana tu lakini si makosa yao ni imani yao ni dhaifu mwenyezi mungu anasema vifua vyao amevipiga kufuli.Cc Gwalihenzi
 
Rapheri,
Kama unabisha tupinge.

Mimi naondoka hapa jamvini kwa siku saba
tuone wasikilizaji kama watafungua stesheni
hii.

Sema su nitangaze likizo nikuache na Nguruvi
tuone.

Hapana Mkuu wangu usiondoke tafadhali mbona hapa kwa Nguruvi et al unatosha sana.

Hapa nasoma paper zako nyingi(nashukuru kwa hili),nakusoma mawazo yako japo yametawaliwa na chuki za kidini ila yapo mengi najifunza kutoka kwako

Ila sasa katika yale yanayoleta uchochezi na mifarakano na zile Fallacy ndo wanaingia MAGWIJI kama Nguruvi3,Mag3,Jasusi,Nyambala,WC,Mzee Mwanakijiji,Sweke34 na wengine wengi wanaingia wanakupinga kwa hoja na kuonyesha kwamba kitu fulani si kweli na ukweli ni huu na Ofcourse kwa mtu mwenye kufikiria anaona mapungufu kwenye maandiko yako

Sasa ni muhimu wewe kuwa hapa ili ku-set the record straight

Pia naomba kukukumbusha ujibu maswali yaliyoelekezwa kwako ni ya muhimu sana katika kutetea maandiko yako Mzee wangu.

Mnakasha unakolea sana wanapokuwepo watu kama Nguruvi wanawafanya watu kuyasoma maandiko yako kwa umakini sana na kugundua hila iliyo nyuma ya maandishi yako

Naomba kusema tena Nguruvi ni LULU si tu kwenye huu mjadala ni FJ yote...nani kamsoma Nguruvi hapa jf na hakujifunza kitu?HAKUNA! ata kama utakataa hadharani najua moyoni utakubali

Nguruvi ni mtu MUHIMU kwenye huu Mjadala.
 


Kweli unafikiri umetoa ushahidi wa kuwa Yesu alikuwa ni Muislamu au umethibitisha ninayosema mimi? Nje ya Qurani hakuna ushahidi wowote kuwa Yesu au mtu mwingine yeyote kabla ya ujio wa Uislamu alijitambua, alijua au alikuwa Muislamu. Yesu alizaliwa Myahudi na alikufa na kukufuka kama Myahudi. Ukristu haikuwa dini ya Yesu; Yesu kwa dini alikuwa ni Myahudi. Ukristu unaitwa hivyo baada ya watu kuanza kuamini ujumbe wa Yesu Kristu na kuufuata na hivyo kutofautisha na watu wengine walijitambulisha kama "Wa-Kristu" kwa maana ya kuwa wafuasi na waamini wa mafundisho ya Kristu.

Wakati wote wa Yesu na baada ya ufufuko waliomwamini Yesu walijulikana tu kama "Waamini" au "Wanafunzi (wafuasi)". Biblia inasema kuwa wanafunzi wa Yesu walianza kuitwa "Wakristu" huko Antiokia (Matendo 11:26).
 

Ni lazima ujue kuwa watu hawa Njozi, Said na mfadhili wao wote wako pamoja. Ni wao ndio walioanzisha madai ya kudhulumiwa Waislau mwanzoni mwa miaka ya themanini wako sehemu ya kundi la vijana wa Warsha. Ukielewa hili utaona kuwa anachosema Njozi kimefichika katika lugha ya kisomi lakini nacho kinakabiliwa na changamoto zile zile anazokutana nazo Mzee Said hapa.
 


Hakukuwa na ugomvi wowote ule; kulikuwa na chuki ya kidini dhidi ya Nyerere kwa kuwa ni Mkristu. Chuki hii iliongozwa na hao kina Plantain na ndio sababu ya kwenda kuanzisha chama chao cha kidini.

Mashado na wenzie ndio walikuwa watu wa kwanza kuanzisha chuki dhidi ya Nyerere kwa sababu ya dini yake; walitarajia kuwa wangepewa upendeleo wa pekee kuliko Watanganyika wengine wa vijijini na mbali na Dar. Nyerere kama kiongozi alitambua mara moja kuwa anaongoza Taifa siyo kikundi cha watu wachache.
 

MM,
naona sasa umeamua kuhamishia huu uzi toka uchochezi hadi YESU ni Muislamu! labda kwa kuwa Leo YESU kafufuka soma kipande hiki:

Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea (Matt. 18:11)."

Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"


Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:


"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…