Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Hakuna cha ubishi ni hoja tu. Hilo la EAMWS tuliache maana huna hoja ya maana ya kujibu unafahamu kuwa ni uzushi tu kama ule wa Warioba na Kawawa. Tuliache lisije likawa la Warioba.Mohamed, umesema mara nyingi sana kuwa maandiko yako yapo katika utafiti kwa maana yametafitiwa. Unajua wazi kuwa EAMWS ilianzia Mombasa na ilianzishwa na Wapakistan.Kisa cha kuvunjika EAMWS ni kirefu sana kwa hapa sitokitendea haki
Lakini kwenye kitabu changu nimekieleza chote pamoja na wahusika
wakuu nimewataja kwa majina yao.
Kuwa kwa nini huko kwengine nako chama kikafa sababu sijui.
Ila sababu ya hapa kupigwa marufuku ni kuwa EAMWS ilikuwa
inataka kujenga chuo kikuu.
Hii ikatia hofu Kanisa Katoliki na Nyerere ikabidi afanye kila juhudi
EAMWS ipigwe marufuku.
Source ya hiyo info. ya sensa ni Islam and Politics cha August Nimitz
unaweza kupata thesis yake Maktaba ya Chuo Kikuu.
Nitajaribu Insha Allah kuangalia kitabu nikupe na ukurasa ninacho katika
''archives'' yangu.
Unafahamu habari zake zote.Kama unadai kuwa hujui kwanini ilikufa Uganda na Kenya basi utafiti wako haukuwa sahihi au kamili.Huwezi kuandika utafiti wa kifo bila kuzaliwa kukua na kuenea kwa EAMWS!!! kwamba ni dude lilianguka kutoka angani!!
Nadhani hapa kuwa mkweli kwa Namren, unajua sababu zitaondoa maana halisi iliyokusudiwa katika kisa kizima vinginevyo ungemueleza alichohitaji.
Ama kuhusu kifo cha EAMWS kama njama za kuzuia kujenga chuo kikuu naona unaturudisha nyuma ambako tulikubaliana kabisa kuwa mabaki ya AMNUT ndiyo yalijificha katika kivuli cha EAMWS.
Kama ni fihi na husuda mbona taasisi za Agakhan aiyekuwa mlezi hazikuondoka na zinajenga chuo kikuu?
Hofu imewaondoka lini?
Kuhusu Sena ya mwaka 1957 kwanza nikupongeze kwasababu kwa mara ya kwanza unakubali kuwa historia yako si masimulizi ni pamoja na nukuu za kazi za wengine jambo ambalo ni kawaida katika uandishi na utafiti.
Nadhani somo zuri ulilojifunza ni lile la kujivika kazi usizo na ushahidi nazo ukashadidia kuwa huo ndio ukweli.
Na pengine ni mwanzo mzuri wa kuitambua Tanganyika na si Mtedeni kama Tanganyika.
Sasa nenda mbali na kuacha kukata vipande vya kitabu chako ukasema huo ni ukweli, kwasababu kuna ukweli kwingine.
Kazi ya kujua ukweli aachiwe msomaji bila kumtisha kiimani, usafiri wa nje, majina ya vyuo n.k.
Hata hivyo bado swali linabaki kuwa ni kweli Tanganyika ilifanya sensa mwaka 1957 ni taasisi gani ilipewa jukumu hilo hata kama tulikuwa chini ya Mwingereza. Kuanzia hapo tutaendelea.Nguruvi,
Sipo hapa kwa ajili ya ubishi.
Hili la Sensa ya Mwaka 1957 unawajibika. Umeleta namba na umeonyesha kuwa Tanganyika ilikuwa ya pili kwa waislam wengi chini ya Sahara na baada ya Nigeria.
Haya ni madai mazito hivyo unapaswa kutueleza kama mwaka 1957 ilifanyika sensa na taasisi gani ilifanya kazi hiyo licha ya ukweli tulikuwa na Mkoloni. Hili huwezi kulikwepwa na wala halihitaji ubishi!
**Kumbu kumbu zinaonyesha Mohamed alishawahi kudai Nigeria ina waislam wengi Afrika