[/LIST]
Hapa kwa vyovyote vile inaonekana vinara walioogopwa na Wakoloni ni wasomi
Dr. Vadasto Kyaruzi na
Hamza Mwapachu na madai kuwa kuwa TAA ilizorota kidogo hadi alipokamata uongozi Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1953 yakawa na ukweli. Pia yawezekana katika kipindi hicho Abdulwahid Sykes hakuwa tishio kwa serikali ya kikoloni kama Mohamed Said anavyotaka kuwaaminisha wasomaji. Lakini mshuhudieni hapa chini
Mohamed Said anavyoelezea harakati za mwana masumbi Abdulwahid aliyekuwa tayari kutumia ubabe na ngumi kutwaa madaraka ...kila kitu ni Abdul!
Mtu ukisoma hizo simulizi za
Mohamed Said bila shaka utajiuliza mambo kadhaa...Je ni nani alikuwa kiongozi mkuu wa TAA,
Raisi wake Dr Vedasto Kyaruzi au
katibu wake Abduwahid Sykes? Kwa nini vongozi watatu Abdul, Sheikh Hasan na Mwapachu wanatajwa na kuelezewa kwa dini zao? Hii ni moja katika tofauti kubwa kati ya Mohamed Said na waandishi wengine, yeye anatanguliza udini na ukabila mbele ya Utaifa,
Utanganyika hata kama mhusika hakuwa Mtanganyika
!. Sasa linganisheni na haya maandishi machache ya huyo
Seaton anayetajwa na Mohamed Said kuwa alikuwa karibu na TAA na alisaidia sana katika kutoa ushauri wa kisheria!
Kusema kweli
Mohamed Said namvulia kofia, ni mpiga stori mzuri tu na hasa katika kuelezea kwa njia ya mipasho ya mitaani...hapo wengine hatumwezi! Lakini tunapojadili mambo ya historia, upotoshaji anaoupamba kwa mipasho na hivyo kuwavutia na kuwapumbaza watu wasio makini, hapana, hapo tunampiga stop. Amb. Juma Mwapachu ameelezea historia ya baba yake bila ushabiki na bila kuwabagua wala kuwalisha maneno wapendwa waliokwisha kutangulia mbele za haki. Hakuna sehemu hata moja anapotaja dini wala kikundi cha kidini, no, anaongelea Watanganyika kama Watanganyika, period. Na ameeleza jinsi mzee wake alivyokuwa karibu na Mwalimu hadi mauti yalipomfika na Mwalimu hakumsahau! Lakini Mohamed Said anadai Mwalimu, baada ya uhuru, aliwasahau wazee wake wa Gerezani kwa sababu walikuwa Waislaam!