Mjomba ni hapa ndipo wengi mlipotekwa kimawazo, na ndiyo maana Mzee Saidi bila kujua anaongea na hadhira ya namna gani alishawahi kuja hapa na tambo "Mtaniambia nini nyie, mimi vitabu vyangu vinasomwa mpaka library of congress". Hiyo ni tambo katika mijadala aliyoizoea ilikuwa tosha kufanya mtu asiyefikiri kabla ya kumeza kuamini kuwa basi haya aliyoandika Mzee Saidi ni ya kweli. Tatizo alileta hiyo hoja hapa JF, wrong place. Tukamweleza kuwa na kitabu library of congress sio ujuvi wa ujuzi na haaimaanishi chochote kuhusu ukweli wa kilichoandikwa ndani ya hicho kitabu. Tukamletea live catalog ya the library of congress na kumuonyesha kuwa si mtanzania pekee aliyekuwa na kitabu kule hata Shigongo, Hammie Rajab na Musiba wanavyo. (Hii ilikuwa ni baada ya kijana wake kusema, ingekuwaje kama kuna "mgala" angekuwa na kitabu ndani ya the library of congress).
Mzee Saidi akasema tunamlinganisha na waandishi wa riwaya. Tukamwambia hapana kule kwenye hiyo maktaba kuna vitabu vingi tu vya kipuuzi na ambavyo si riwaya na tukaviorodhesha. Mojawapo ni kile cha Dinesh Disouza anachodai mama yake Obama (a sitting presidaa) alikuwa lijimalaya (Yes size was mentioned) aliyependa ku-fantasize na wanaume wa third world na kwamba ana mpango wa kuiangamiza Marekani kama kulipiza kisasi dhidi ya wakoloni wa Kenya.
Toka wakati huo ukawa mwisho wa tambo hiyo humu JF.
Nyambala,
Kama umechukulia hiyo ni kutamba basi si mwisho wa kutamba.
Nifahamishe kama kitabu cha kaka yangu Hammie Rajab, Shigongo nk. kama
vimepata review katika majarida ya kisomi.
Kitabu changu kina review mbili ndani ya Cambridge Journal of African History.
Moja ya John Iliffe na nyingine ya Jonathan Glassman.
Nadhani unawatambua mabingwa hawa wa historia ya Afrika.
Zipo nyingine...
Kutokana na kitabu hicho nimealikwa Chuo Kikuu cha Ohio na Chuo Kikuu Cha
Northwestern, Chicago ambako kote nimefanya mihadhara.
Au unataka nikuwekea hapa chini na vyuo vingine hapa Afrika ambavyo nimepata
kualikwa na kuzungumza?
Nilipata kuwa member wa Library of Congress zaidi ya miaka 25 iliyopita na katika
nchi nzima hatukuzidi watu watano.
Walimu walionisomesha hawakupata kupewa heshima hiyo.
Aliyekuwa akitoa hiyo alikuwa Mkurugenzi wa USIS.
Alipata kunisoma na ndiyo akanitunuku uanachama huo.
Bado unataka ''tambo'' zaidi au niishie hapa?
Ati mimi sijui hadhira ya JF...
Hivi wewe Nyambala kutia timu yako katika kiwanja hiki unaona ndiyo umefika?
Hapa si mdadi wako tu unaandika?
Uwanja huu si ''free for all?''
Hii si Hyde Park?
Wewe unajua timu yangu ishacheza viwanja gani duniani?
Fanya staha lau kidogo hata kama jina langu ni Mohamed.