Gwalihenzi;
Hapana, sisi sote ni Wa TZ! ila siwezi kubadilisha kauli ya Mwenye enzi Mungu kuwa, Sema: Enyi makafiri! mimi siabudu mnachokiabudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu, Wala sitaabudu mnacho abudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu, Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. (Qur:113)
Tanzania katuumbia Bwana Mungu tuishi humu humu hata kama tunaimani tofauti! la muhimu ni kila mtu aheshimu dini ya mwenzake na muhimu zaidi ni kuvumiliana! mfano: Wewe unaamini kuwa Yesu ni Mungu na ukiimba na kutangaza kila mahali hivyo sina budi nivumilie lakini na wewe pia huna budi kuvumilia pale mimi ninapotangaza kuwa Yesu si Mungu! hayo ndio mafundisho ya dini yangu! Gwalihenzi unakubaliana na mimi?