Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sheikh Mohammed,
Bismi natakadam naishika kalamu,nazituma salaam ama leo mezizindua fahamu!ahahaa!! Nahisi utakuwa unapenda viburudisho japo kiduchu kama hivi!ahaha!!

I really admire your encyclopaedic memory,I mean your head is like a museum! I'm sure sure your brain is densely populated with loads of information and I'm glad that you are sharing it with us. Above all I envy your undisputed your historical connection.
The only people mad at you for speaking loud and clear are those living a lie. Keep speaking na sitie shaka maana tupo pamoja.

Facts do not cease to exists because they are ignored - A. Huxley

Salaam na Insha Allah ukae salama.

Gombesugu,
Ahsante ndugu yangu.

Yote haya ni hidaya kutoka kwa Allah kuwa nimezaliwa
na watu hawa na nikakua katika kipindi kile.

Yeyote yule angepita katika mikono ya watu hawa na yeye
angeliyajua haya kama niyajuavyo mie.

Umenifariji pakubwa.
Allah akulipe kheri.

Amin.
 
kAZI kwelikweli wewe umejiunga jana tu,leo ushakuwa authority humu-anyway sijui hizi multiple identities zitatupeleka wapi

Son of Alaska,
Mbona unanikaribisha kwa mbwembwe na kunitisha!? Authority ipi niloitoa humu,mimi nalifanya tu kutoa ushauri na jinsi hali nilivyoiona mimi binafsi. Na wala usiwe na paranoid na dhana zisizo na mwelekeo,mimi ni mgeni kweli hapa na wala hakuna multiple IDs kama unavyohisi!
Nakutakia weekend njema!
 
Hiyo hotuba ya maandishi siku ilipowekwa tu mimi nilisema kuna sehemu imechakachuliwa kilichoandikwa na tulichokisikia RTD ni vitu viwili tofauti.

Ritz, be reasonable even to the level of P/S pupil.
Hoja hujibiwa kwa hoja; lete hotuba halisi ambayo haijachakachuliwa badala ya maneno matupu.
 
HUU ukumbi ni "FREE FOR ALL" hii naona ni wimbo wa taifa na retreat mechanism ya Mohamed Said punde maji yakimfikia shingoni

Son...

Hapa ni maji ya kifundoni.
Nimepambana na watu wajuzi tena katika viwanja vyao.

Watu wanaochukia Uislam khasa na wamekuja pale
na hamaki.

Wazungu hao wanazungumza katika ndimi waliyozaliwanazo.
Mimi Mohamed Said Kiingereza si lugha yangu nimejifunza tu.

Niko katika uwanja wa ugenini.
Ukumbi mzima nikitazama wamejaa wao.

Waeshaambiwa huyo hapo mbele ni ''terrorist sypathiser...etc, etc.''

Ipo dua aliisoma Nabii Daud alipokuwa anakwenda kupambana na
Jalut (Goliath) kafiri mkubwa asjiyemjua Allah...

Basi mimi wakijipanga mimi dua hiyo inanitoka...

Kisha nasoma dua nyingine ya Mussa alipokuwa anakwenda kupambana na
Firauni kafiri mkubwa aliyesema yeye ndiye Mungu mwenyewe hii inalainisha
ulimi wangu...

Qur'an hiyo yote kaka sina langu hapo.

Mwisho wa siku wanapiga makofi wananisifia wanasema ''...we hear Mohamed
you went to a Catholic school and that is where yo picked up the language...''

Wanasimanga kistaarabu.

Nami nawajibu ''...Yes I did together with my elder brother he is a Ph D Genetics
but my wife did not attend these schools... she is an alumni of two American Universities..''

Hapo sasa ndiyo ukumbi mzima hauna mbavu.
Wanacheka na kutingisha vichwa.

Nakaa nasema Alhamdulilah Mola wangu nakushukuru kwa kunifunza kufikiri na kujibu
haraka na Allah walipe kheri walimu wangu wote walonisomesha kote nilikopita.

Son...
Toa hofu hapa JF kwangu ni maji ya kisigino.
Hayawezi kunizamisha.
 
Wapi nimekuambia Iliffe alimtumia Daisy Sykes kama rejea. Nimeandika kuwa John Iliffe aliweza kukusanya habari nyingi sana na muhimu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake. Unabisha bila kujua "The Townsman Kleist Sykes" ipo kwenye kitabu gani.

Wewe unabisha ili hujue au unabisha kubisha tu.
Kukusanya habari nyingi sana kutoka kwa mtu mmoja ndio tafsiri ya rejea kuu ndugu,

Ndiomana nimesema sio kweli uliyoyasema,
 
Kukusanya habari nyingi sana kutoka kwa mtu mmoja ndio tafsiri ya rejea kuu ndugu,

Ndiomana nimesema sio kweli uliyoyasema,

Hakuna haja ya kuminyana kwenye hilo kama unaona siyo kweli hakuna tatizo.
 
gombesugu,

..hapo kwenye RED naona kuna dharau kwa mbaaali.

..ndugu yangu, all of us, bila kujali ni wenyeji wa wapi, can learn from one another.

..kwamba fulani kazaliwa Tandahimba, Ngara,etc na anakula senene haimaanishi kwamba hana la maana analoweza kumfunza yule aliyezaliwa na kukulia Kariakoo, Mzizima.

cc: Mohamed Said, Jasusi, Ritz, Mag3, Nguruvi3

JokaKuu,
I didn't mean to harm anybody's feelings and I hope there's no need for apology. Well, I was only trying to be objective.

Nimekuelewa na haikuwa madhumuni yangu kuleta dharau. Najaribu tu kuonyesha kuwa zile dasturi na tamaduni zinazoonekana za ovyo,za kipuuzi na zisizo na maana mbona ziko pande zoote.
Kwa kuwa wewe umekua member wa hii JF kitambo na kuchangia sana kwenye hii thread,nina hakika umeshuhudia jinsi wengine walivyoitwa walowezi(japo vizazi vyao vina takriban karne hapo Tanganyika),wakaa vibarazani,wala kashata na wanywa gahwa,wavivu wa kusoma,wafia dini wa gerezani na mengineyo kadhaa!
Sikatai asilani kuwa kila mmoja wetu ana haki ya kujadili na kujifunza toka kwa mwenzie bila ya kujali social status,class,tribe and /or political affiliation,customs,cultures,skin colour or any other differences.
Kwa hiyo ilikua haina maana pale Mohammed Said anapoambiwa ati asilete hadithi zake za togwa na vinyozi wa kipata na gerezani!? Naona pale hata wewe hukuweka RED wala kukemea!?
Nakuheshimu na wala sitathubutu kukwita hypocritic(nafikiri kuna kabila hapo linasema ndumila kuwili!?)

Haina neno tuendelee kupendana soote na nakutakia weekend njema!
 
Son of Alaska,
Mbona unaniwekea maneno ya karaha!? Kama unahisi kuna pahala nimekosea au sijui ni vyema tu unambie nami nakuhakikishia nitajirekebisha. I find it shocking and disturbing when an Afrikan man/non white use them kind of absurd slogans/qoutes. Nakusihi hayo maneno waachie wenyewe kina BNP,KKK,Neo-Nazis na mababu zao akina Hitler,Mussolini Churchill na yule maluuni Leopold II na wengine kadhaa!

It doesn't make others hateful to speak the truth and honestly. They express what they know and how they feel. It is an undeniable fact that some section of our society are beneficiaries of inherited colonial white supremacy past that created systematic annihalation torwards others. to suggest otherwise,it is not only pathetic but social and historical illiterate!
Therefore,I would expect those who benefited from those dubious circumstances,out of gratitude,atleast to have decency,empathy and civil exchanges during this "mnakasha".
Hii nchi tunaipenda soote bila ya kujali dini zetu ,makabila,rangi,itikadi na matabaka tulonayo/tulorithi!
Ahsanta.
 
gombesugu,

Wapi hiyo Mukarram, Sharjah, Al Khaneej, karibu sana JF Kadogoo na Ami, wanakuandalia Basmat ya ndama wa ngamia na Mohamed Said atakupa zawaidi ya juice ya tende.

Ritz,
Acha matata yako watu tumo kwenye darsa hapa!ahahaah!! Wallahi nipa salaam jamaa woote hapo na pia nitolea shukran zangu za dhati kwa Mabwana Kadogoo na Ami. Sheikh Mohammed nae pia nina zawadi zake penye maajaliwa.

Unapontajia hayo maanjumati basi roho huniruka,ndo hasara ya kuishi ughaibuni tunakosa mambo organic ya kinyumbani! Wallahi jana nalitamani saana vipopoo au mikate ya chila!ahaha!!
Kwaheri yakhe siniponze na mie kuanza tukanwa humu!ahahaah!!
 
Usijali humu sote ni ndugu tunaunganishwa na utanzania wetu.

Ukirudi lazima uanze na bokoboko la mbuzi na swamri au mandi ya kuku wa kienyeji...ha ha haaa.
 
Mjomba ni hapa ndipo wengi mlipotekwa kimawazo, na ndiyo maana Mzee Saidi bila kujua anaongea na hadhira ya namna gani alishawahi kuja hapa na tambo "Mtaniambia nini nyie, mimi vitabu vyangu vinasomwa mpaka library of congress". Hiyo ni tambo katika mijadala aliyoizoea ilikuwa tosha kufanya mtu asiyefikiri kabla ya kumeza kuamini kuwa basi haya aliyoandika Mzee Saidi ni ya kweli. Tatizo alileta hiyo hoja hapa JF, wrong place. Tukamweleza kuwa na kitabu library of congress sio ujuvi wa ujuzi na haaimaanishi chochote kuhusu ukweli wa kilichoandikwa ndani ya hicho kitabu. Tukamletea live catalog ya the library of congress na kumuonyesha kuwa si mtanzania pekee aliyekuwa na kitabu kule hata Shigongo, Hammie Rajab na Musiba wanavyo. (Hii ilikuwa ni baada ya kijana wake kusema, ingekuwaje kama kuna "mgala" angekuwa na kitabu ndani ya the library of congress).

Mzee Saidi akasema tunamlinganisha na waandishi wa riwaya. Tukamwambia hapana kule kwenye hiyo maktaba kuna vitabu vingi tu vya kipuuzi na ambavyo si riwaya na tukaviorodhesha. Mojawapo ni kile cha Dinesh Disouza anachodai mama yake Obama (a sitting presidaa) alikuwa lijimalaya (Yes size was mentioned) aliyependa ku-fantasize na wanaume wa third world na kwamba ana mpango wa kuiangamiza Marekani kama kulipiza kisasi dhidi ya wakoloni wa Kenya.

Toka wakati huo ukawa mwisho wa tambo hiyo humu JF.

Nyambala,
Nimekufahamu uzuri na ndio raha ya hapa JF! Madai yako kuwa Sheikh Mohammed Said ameniteka mawazo si kweli. Mimi nachambua tu baadhi ya yale nilokua siyajui. Itakua kinyume na field yangu mie kuchukua jambo na kulimeza ghafla bila ya kutumia standard methods/procedures and scientifically proven evidences.
Ahsanta kwa kujuana hapa na nakutakia weekend njema.
 
GombeSugu, nakushukuru kwa majibu,

Kuna mahali hujapembuka sawasawa,

Kwanza inaonyesha wazi kitabu cha mohamed Said tunachokinga hapa hujakisoma,

Pili historia ya uhuru huijui na hutaki kuruhusu akili yako iijue.

Jitulize kisha ruhusu fikra mpya kichwani na moyoni ndugu yangu

Yericko Nyerere,
Nashukuru sana kwa ustaarabu wako na nafurahi kwa kujuana hapa. Samahani mie kiswahili changu kibovu hivi kupembuka ndo nini!? Hii kwamba historia kuwa siijui yawezekana ni kweli maana siku hizi zimekua ni nyingi mno,na ndo najitahidi kusikiliza kila upande. Lakini ati sitaki hata kuruhusu hata akili yangu iijue hilo si kweli na niwie radhi ndugu yangu. Laiti ungelijua,lakini iko siku tutajuana kiukweli!
Usiwe kama wale ndugu zetu wa Roman Gypsies,maana wao ndo mashuhuri kwa mambo ya mind reading!ahaha!!
Haina neno,sisi soote ni wanaTanganyika,la muhimu tupendane na kuelimishana kwa ustaarabu tulorithi kwa mababu zetu!
 
Kadogoo,
Achana na huyo mtu.

Nipe habari za Cairo ndugu yangu.
Kila chakula lazima kitangulie na ''hums.''
Halafu salad zao...
Angalia usionngeze kilo...

MS,
Huyu bwana tuendenae polepole huenda akaelewa!
Cairo mambo poa kabisa! jana nilienda ktk makumbusho ya Salah Diin kamanda maarufu wa jeshi la kiislamu alieikomboa Quds na Misri lakini kumbe wanafunga saa 10 jioni nami nilienda baada ya saa10 jioni! ntajaribu tena inshaallah!

Jana sala ya Magharibi Masjid Bilali kuna bwana mmoja kidogo nimsalimie nikidhani ni wewe Mohamed Said! yaani mmefanana ile mbaya! kavaa kofia ya Kizanzibari, kanzu safi nyeupe na miwani yaani kopi kabisa na wewe! nilimsogelea na kumwangalia usoni mara mbili mbli na yeye kuingiwa na shaka lakini nilimwahi na salamu na kumwomba radhi kuwa nimemfananisha!

Kuhusu kuongeza uzito naogopa ndo maana nimelipa paundi 150 za Gym kila jioni mara 3 kwa wiki! napata shida sana na lugha mpaka nimeamua kusoma Lugha miezi 3!
 
Mkuu wangu gombesugu karibu jamvini ingawa nina kila sababu wewe si mgeni JF kila nikitazama mtiririko wa maandishi yako na hoja zako dhaifu nakufanananisha ........ ha ha ha ha ha ha hizi multiple ID za nini kwanini haujiamini yamkini unajua unachotetea hakina mashiko.

Ngongo,
Vipi tena mbona unaleta mambo ya kitoto na sie soote tupo hapa kubadilishana mawazo na kupta habari kwa wale wajuao!? Acha dhana zisizo maana,ni kipi hicho kinachokufanza ati uwe na hakika kuwa nimo humu kitambo!? Hakuna multiple ID hapa acha kujitisha na kivuli!ahaha!!
Umesema ninachotetea hakina mashiko,hivi mashiko ndo nini au una maanisha matiti!? Samahani mie kiswahili changu ni cha kuungaunga,kipata wasaa naomba nifafanulie!
Nafurahi kujuana hapa japo mwenzangu yaelekea ati unanujua zaidi!ahaha!!
Nakutakia weekend njema!
 
Yericko Nyerere,
Nashukuru sana kwa ustaarabu wako na nafurahi kwa kujuana hapa. Samahani mie kiswahili changu kibovu hivi kupembuka ndo nini!? Hii kwamba historia kuwa siijui yawezekana ni kweli maana siku hizi zimekua ni nyingi mno,na ndo najitahidi kusikiliza kila upande. Lakini ati sitaki hata kuruhusu hata akili yangu iijue hilo si kweli na niwie radhi ndugu yangu. Laiti ungelijua,lakini iko siku tutajuana kiukweli!
Usiwe kama wale ndugu zetu wa Roman Gypsies,maana wao ndo mashuhuri kwa mambo ya mind reading!ahaha!!
Haina neno,sisi soote ni wanaTanganyika,la muhimu tupendane na kuelimishana kwa ustaarabu tulorithi kwa mababu zetu!

Gombesugu,
Huyo ndiyo Yericko Nyerere.

Anasema lile limjialo kiasi siku moja sikuweza kustahamili.

Yeye alimkejeli Abdu Sykes nikamwambua wewe hujui ihsani
ya Abdu lakini uliza kwa binamu zako watoto wa shangazi yako
marehemu Bi. Sophia.

Hao nduguzo walikuwa wadogo lakini watakuwa na kumbukumbu.

Umenifurahisha kumueleza Yericko kuwa ipo siku mtajuana.
Umenikumbusha kisa cha Muhammad Ali na Bertrand Russel.

Ali juu ya vurugu zake siku alipokutana na Russel Ali alimtaka radhi
akasema, "Sikuwa nakujua niwie radhi sana."
 
Ritz, be reasonable even to the level of P/S pupil.
Hoja hujibiwa kwa hoja; lete hotuba halisi ambayo haijachakachuliwa badala ya maneno matupu.

Wimana,

Ili la hotuba ya Nyerere bahati nzuri Yericko Nyerere alijitolea kuwa atakwenda TBC na ataileta humu jamvini.

Alivyokwenda akaja kutufahamisha kuwa amekwenda TBC bahati mbaya wamesema hiyo hotuba ya Nyerere inauzwa basi waungwana wa JF wakajitolea kuinunua. Mpaka leo mwezi wa 4 bado ajasema kiasi gani inauzwa waungwana watoe pesa.
 
MS,
Huyu bwana tuendenae polepole huenda akaelewa!
Cairo mambo poa kabisa! jana nilienda ktk makumbusho ya Salah Diin kamanda maarufu wa jeshi la kiislamu alieikomboa Quds na Misri lakini kumbe wanafunga saa 10 jioni nami nilienda baada ya saa10 jioni! ntajaribu tena inshaallah!

Jana sala ya Magharibi Masjid Bilali kuna bwana mmoja kidogo nimsalimie nikidhani ni wewe Mohamed Said! yaani mmefanana ile mbaya! kavaa kofia ya Kizanzibari, kanzu safi nyeupe na miwani yaani kopi kabisa na wewe! nilimsogelea na kumwangalia usoni mara mbili mbli na yeye kuingiwa na shaka lakini nilimwahi na salamu na kumwomba radhi kuwa nimemfananisha!

Kuhusu kuongeza uzito naogopa ndo maana nimelipa paundi 150 za Gym kila jioni mara 3 kwa wiki! napata shida sana na lugha mpaka nimeamua kusoma Lugha miezi 3!

Kadogoo,
Nakuonea wivu sana.

Ule wivu mzuri wa kutamani nami nipate kama upatayo wewe
bila ya neema hiyo wewe kukuondoka.

Insha Allah shuwei shuwei lugha itapanda.

Salahudin Ayubi...
Ahsante sana.
 
@Kadogoo,

..nimekuwekea bandiko toka gazeti la serikali Daily News kukuthibitishia kuwa Prof.Malima ndiye waziri wa mwisho wa fedha wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..kama hujaridhika na ushahidi huu, nieleze kwasababu ninao mwingine.

The first Minister to hold the finance portfolio was Sir Ernest Vaasey and the first indigenous minister was Paul M. Bomani who held the post from 1962 to 1965. Mr Amir H. Jamal held the post three times; from 1966 to 1972 and came back from 1976 to 1977 and was appointed to the post again in 1982.
Mr Cleopa D. Msuya held the portfolio twice, between 1974 and 1975 and from 1986 to 1989. Next came Mr Edwin Mtei who was appointed Minister for Finance from 1978 to 1981. Another minister who had held the post more than once was Prof. Kighoma A. Malima. He held he post between 1983 and 1985 and again from 1993 to 1994.

Mr Steven A. Kibona headed the ministry between 1990 and 1993 and was replaced by Mr Jakaya M. Kikwete (the current President of the United Republic of Tanzania) who headed the ministry from 1994 to 1995.

Prof. Simon M. Mbilinyi took over from Kikwete from 1995 to 1996. Mr Daniel N. Yona was appointed Minister for Finance from 1997 to 2000 and was replaced by Basil P. Mramba who headed the ministry between 2001 and 2005, handing the portfolio over to Ms Zakia H. Meghji (the only woman to head the ministry so far) between 2005 and 2007.

The incumbent, Mr Mustafa H. Mkulo, was appointed to the post in 2008 and has the privilege to be heading and nursing the heartbeat of the government when the nation is celebrating 50 years of independence.

Daily News | Weathering economic storm in 50 years

Yericko Nyerere,
Nashukuru sana kwa ustaarabu wako na nafurahi kwa kujuana hapa. Samahani mie kiswahili changu kibovu hivi kupembuka ndo nini!? Hii kwamba historia kuwa siijui yawezekana ni kweli maana siku hizi zimekua ni nyingi mno,na ndo najitahidi kusikiliza kila upande. Lakini ati sitaki hata kuruhusu hata akili yangu iijue hilo si kweli na niwie radhi ndugu yangu. Laiti ungelijua,lakini iko siku tutajuana kiukweli!
Usiwe kama wale ndugu zetu wa Roman Gypsies,maana wao ndo mashuhuri kwa mambo ya mind reading!ahaha!!
Haina neno,sisi soote ni wanaTanganyika,la muhimu tupendane na kuelimishana kwa ustaarabu tulorithi kwa mababu zetu!
Nikuwie radhi kwa hilo.
Nadharia yangu inasimama kwenye uchaguzi wa pembuzi zako, natoa shilingi katika hilo
 
Back
Top Bottom