Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Huyo bwana alishamtukana mara nyingi MS na kuvumiliwa! na imani ya MOhamed haifundishi ukizabwa kofi shavu la kulia geuza na la upande wa shoto! ila wewe GWALIHENZI umekuwa na tabia ya kumtukana kila mtu yaani huchagui wala kutazama! angalia hapa ulivyotudhalilisha!

1) Majitu mengine kwa kujifariji hamjambo! Nguruvi3 ahangaike na huu upumbavu wenu? ama kweli maajabu hayataisha! wewe umeona kunalolote la maana hapo? kama ni hivyo basi tunajadili na mazuzu humu!

2) Wewe huwa hutumii akili na huwa huna kumbukumbu. Kwa taarifa yako, ni Mwanakijiji huyo huyo aliyewashauri wapuuzi wenzako akina kadogoo, Boko na Ami wayapeleke maoni yao kuhusu Yesu kwenye jukwaa la...
Wewe kwa kuwa unamhara sana Mzee Mwanakijiji

3) Hivi Boko unaakili timamu kweli? sasa huyo mungu wako ananihusu nini mimi? na huo upumbavu wa Mohamed mnaouita ilm unamanufaa gani kwangu? Boko, ninaishi bila hayo matakataka yako naninaraha zangu..Taabu mnataka kuileta nyie wapuuzi na hilo zee lenu chochezi!..

4) Huna mpya mpuuzi wewe, hilo zee lako halifai kwa chochote katika nchi yetu. Kwa visa vya kipuuzi kama hivi wewe kwa ujinga wako unadhani ndio historia ya Tanzania! mpumbavu, hizo ni stori za wavuta unga mitaani tu.

5) Kwanini uchukue likizo? ondoka kabisa fatani mkubwa!

6) Wacha vilio vya kitoto hivyo, mtu mzima hovyooo!

7) Huna lolote mzee mchimvi wewe, baada ya kushindwa hoja unataka kujitoa kijanja! muoga mkubwa! dalili za kushindwa na kutaka kukimbia zilianza na makele yako ya kila siku... mara oh.. anzisheni uzi wa utumwa muone... oh mimi ndie mbabe hapa... mara oh... wenzetu wamehamaki.... matusi yameanza. Mohamedi wewe umeshindwa kabisa hoja, huna hata tafsiri sahihi ya "Concept" mfumo kristo uliyoiasisi katika kuendeleza chuki na fitna zako kwa watanzania. You are doomed embicile old man.

8) Ulivyo mpumbavu, unadhani watu wote ni wafuasi wa imani yako!

9)Mtauonaje na nyie mmeshalogwa akili? kwenu kila asemacho mzee wenu Mohamed Said mnaona ni sahihi kabisa, hata anapodanganya waziwazi kuwa Marmo alikuwa mbunge wa Monduli nyie mnashangilia kama mazuzu! poleni sana walevi wa falsafa za uwongo wa Mohamed.

10) Wewe mpumbavu ni kwambie mara ngapi kuwa mimi ni "adent atheist"? ebu niondolee hayo makonokono yako, kwangu mimi hayana nafasi na wala hayana umhimu wowote.

Gwalihenzi,
Kama kweli wewe ni msomi na mstaarabu utatuomba radhi kwa kutudhalilisha la sivyo wahudhuriaji wa mnakasha huu wanaozidi 130,000 wataamua nini hukumu yako!
 

Sheikh Mohammed,
Nimekufahamu haina neno hii ndo raha na buraha za humu JF! Ahsanta nimepata salaam kwa Bwana Ritz kuwa umeniwekea shake ya tende! Wallahi nimetamani pasipo kiasi,nami pia nna zawadi yako nzuri Insha Allah tuombe uhai.

Nina tamani saana ile darsa yako ya kisa cha vita ya majimaji,na ile safari yako mpaka kule Songea. Najua umeshikwa na hii darsa ya kujibu hizo shutuma za uchochezi,lakini tafadhali kipata wasaa tupe japo snap shot ya ile habari.

Mimi nina contacts nzuri hapa Vienna,Minsk,LSE na pale Jarumani takribani Universities nyingi twaweza kutumia watu pale turejeshewe ile picha nafikiri ulisema ilichukuliwa na wazungu fulani ati kupelekwa Jarumani!?

Kipindi ulichopita pale Leipzig bado Proffesor Abdilatif Abdalla alikuwapo pale,najua ameshamaliza muda wake pale lakini bado tuna jamaa wengi tu. Maana nimekuona kwenye baadhi ya picha zao nilipopita pale

Nikikaribia kuja hapo Mzizima,takutumia ujumbe na contacts zangu hapo na nitafurahika mno kikutana.

Salaam jamaa woote huko na Isha Allah Mola tajaalia amani na utulivu kwenye nchi yetu na mapenzi baina yetu waTanganyika soote.
Ahsanta.
 
Kadogoo, naona unaota ndoto za mchana!majina yote niliyowaita humu ndani mnastahili, tena na shangaa sana kuona watu wabaya kama ninyi kuomba mpewe heshima! hamstahili heshima yeyote watu wabaya ninyi! hivi hamsikii aibu kuja na madai yenye nia ya kuwafarakanisha watanzania kwa tamaa zenu?Nyie ni mijitu mibaya sana kuliko hata shetani wa vitabuni mwenu. Wabaya kuliko wote ni wewe Kadogoo ambaye umeamua makusudi kutokutumia akili yako kuchambua mambo kisomi na kujificha kwenye kichaka cha imani yako kutetea uovu unaoenezwa na muovu Mohamed!
 

Mundungus Fletcher,

Kwanini mimi ninae amini Yesu si Mungu unifungie jela na kunitaka niamini tu bila kusema?(Kutenda) huku yule anae amini kuwa ni Mungu unamruhusu aamini moyoni na kuyatamka hadharani? hujui kuwa ktk Uislamu kuamini tu moyoni bila kutamka imani hiyo ni batili? haiwezekani kuamini Yesu si Mungu moyoni tu bali ni lazima nithibitishe na kwa ulimi ndipo Imani itakamilika!

Hiyo ndiyo maana ya Uvumilivu(RELIGIOUS TOLERANCE) kama mimi naweza kuvumilia wewe kutamka YESU ni Mungu kwanini wewe huwezi kuvumilia kama mimi? na kwanini tubishane kama wote tuna weza kutii kanuni hii?

Tatizo linakuja pale wenzetu mnaposhindwa kuwa wavumilivu kwa kutii kanuni hiyo, ndio maana mwaka 1998 Padre Lwambano aliitaka Serikali iwachukulie hatua za haraka Waislamu waliokuwa wakihubiri YESU sio Mungu! na Serikali bila kuchelewa 28.2.1998 ikachukua hatua kwa kuuwa Waislamu waliokuwa Msikitini Mwembechai!

Kwanini hakuna Shehe hata mmoja alieiomba Serikali iwachukulie hatua wahubiri wa Kikristo walioongozwa na Simbaulanga huku wakitumia vipaaza sauti kwa kumuita YESU ni Mungu na kashfa tele dhidi ya Uislamu?

Mundungus Fletcher,
Kati ya Waislamu na Wakristo nakuapia kwa jina la Allah muumba wa Mbingu na Ardhi nani anaetii kanuni ya Religious Tolerance? wakati mwingine tueke udini pembeni ili tuwe wakweli!
 
Mkuu Ngongo, hoja zako huwa zinaniburudisha sana, zinakuwa kama mzaha hivi lakini nzito sana... Kwenye fasihi huitwa "understatement".
 
gombesugu,

Wapi hiyo Mukarram, Sharjah, Al Khaneej, karibu sana JF Kadogoo na Ami, wanakuandalia Basmat ya ndama wa ngamia na Mohamed Said atakupa zawaidi ya juice ya tende.

Duh,
RITZ, utafikiri ulipata habari yangu juzi nilinunua ndama wa ngamia kilo 1 kwa Paundi 50 za KiMisri na jana Ijumaa nikajichana na nyama hiyo kwa iliyokaangwa barabara kwa Arabic Spices na Wali wa aina ya Basmati!

Mwambie Gombesugu tayari nimeshamuandalia nayeye chakula hicho TAFADHWALU hapa Misri maana ake ni karibu!
 
Kadogoo,
Nakuonea wivu sana.

Ule wivu mzuri wa kutamani nami nipate kama upatayo wewe
bila ya neema hiyo wewe kukuondoka.

Insha Allah shuwei shuwei lugha itapanda.

Salahudin Ayubi...
Ahsante sana.

Sawa kabisa Mohamed, huu ndio wivu stahili na sahihi sio Mwenzako ana University moja wewe unazo mia halafu bado unachukia mwenzako kuwa na hiyo 1 huku ukilalamika ati mwenzako ni mdini sababu chuo chake kimejaa Watu wa dini moja tu!

Allah akujaze kila la Kheri Mohamed kazi ya Uandishi hasa Historia iliyosahaulika si ndogo ila unachotakiwa kuwa nacho ni subra!
 
Mohamed Said,

..darsa lako kuhusu Prof.Kighoma Malima mimi nilishalipata zamani sana.

..lakini nilikuwa na masuala ya ziada, kuna mambo sikuyaelewa kidogo.

..kwanza naomba ufafanuzi kuhusu waraka wa Prof.Malima kwenda kwa Mwalimu Nyerere. Inasemekana ktk waraka huo Malima aliwatoa tuhuma kwamba kuna wasaliti ktk chama na serikali. Je, unaweza kutupatia waraka huo??

..pili kuna ule waraka wa Prof.Malima kwenda kwa Raisi Mwinyi kuhusu masuala ya elimu. Hapa ingependeza kama ungetuwekea waraka huo kwa faida ya darsa lako.

..tatu, naomba utoe verdict yako kuhusu ubishi uliotokea kati yangu na Kadogoo. Naomba unasaidie kumthibitishia mwanachama mwenzangu kwamba Prof.Malima alikuwa waziri wa mwisho wa fedha wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..MWISHO, kuna yale maswali yangu kuhusu Balozi Abas Sykes. Aliyepata kuwa Balozi wetu kwa muda mrefu. Je, yeye alipewa nishani na Mwalimu Nyerere. Mwingine, ni IGP mstaafu Hamza Aziz, je yeye alipewa nishani mwaka 1985 wakati Nyerere anastaafu??
 
Last edited by a moderator:

Gwalihenzi,

Naona umekasirika! basi tusameheane yaishe! Tufuate nyayo za Mzee Madiba hata baada ya kudhalilishwa na Makaburu miaka nenda miaka rudi waliamua kupatana! angalia Arafat na Mayahudi, Sadat na Mayahudi na sasa Marekani anataka kupatana na Talibani! itakuja kuwa sisi sote wa Tanganyika?
 
tatu, naomba utoe verdict yako kuhusu ubishi uliotokea kati yangu na [/COLOR]Kadogoo. Naomba unasaidie kumthibitishia mwanachama mwenzangu kwamba Prof.Malima alikuwa waziri wa mwisho wa fedha wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

Jokakuu, hakuna haja MS aingilie kati! hakuna haja ya kubishana wewe umeshathibitisha basi kwanini tuvutane? Kwa hiyo rudi kule ulikosema kwa kuwa Malima alikuwa Waziri wa Fedha ndio maana Mwinyi alipoingia madarakani kakuta hazina tupu sio?
 

Joka Kuu kama ushapata darsa la Prof. Malima basi wewe hulihitaji.
Insha Allah nitatoa kwa wengine ambao hawajapata kusikia habari zake.

Kuhusu medali kwa Abbas Sykes najua aliwahi kupewa medali ila sikumbuki lini.
Hamza Aziz sina taarifa zake za medali.
 

Kadogoo,
Amin. Amin. Amin.
 

Kadogoo,
Kuwa na huruma kaka...

Yaani unanitamanisha kiasi hiki nasikia ubao.
Duuuu nyama lainiiiii.

Hiyo ni baun siyo pound Waarabu kwa kuwa hawana ''p''
''b'' inawacheza kweli kweli.

Ila siku moja nimepanda Gulf nasikia wale wasichana
wahudumu wanazungumza Kiingereza na accent ya London
tena kwetu Finsbury Park...

Nkawauliza kulikoni?
Wakanambia wamesoma huko kwa Malkia Elizabeth.
 
Ritz, andika kwa kiswahili, kiingereza hukimudu ndugu yangu.

Nilijua tu lazima watu wataingia kichwa kichwa baada ya kuona neno "gentlemany" tatizo unaleta mazoea ulitegemea nitaandika "gentleman".

Nakushauri tafuta dictionary au google gentlemanly-definition.

Wewe huwezi kunifundisha mimi lugha ya kiingereza kijana labda nifundishe lugha ya kichagga ndiyo sikifahamu tafurahi kama utafanya ivyo.
 

Gombesugu,
Furaha yangu haisemeki.

Nilikuwa Berlin (ZMO) na Abdilatif alikuja kunisikiza katika mada yangu
''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania''
akanialika kwake Humburg nikenda.

Nilifika katika safari hiyo hadi Switzerland sijui kama visa yangu ya Shengeen
(sijui kama spelling nimepatia) ingenifikisha kwako Vienna.

Mimi ni mgonjwa kidogo wa mawaltz ya kina Mozart, Bach...
Ahsante ndugu yangu.

Insha Allah tutakutana.
 

Mohamed Said,

Mashaa Allaah.,. Huu uzi umevuta watu wengi sana mimi binafsi nimepata marafiki wengi sana kupitia huu uzi.

Mie napenda kumuita The Great Thinkers gombesugu,

Ha haa haaa hii ndiyo raha ya JF.
 
Last edited by a moderator:
Ritz, mapovu ya nini? kiingereza hakisomwi kwa Dictionary bwana mdogo! angalia mazigira (context) ya ulivyolitumia neno hilo! "gentlemanly" is an adjective, wewe ukaamua kulitumia kama "noun" ebu rudia kuusoma upuuzi wako kabla ya kuja na mapovu yako hapa.
 
Jokakuu, hakuna haja MS aingilie kati! hakuna haja ya kubishana wewe umeshathibitisha basi kwanini tuvutane? Kwa hiyo rudi kule ulikosema kwa kuwa Malima alikuwa Waziri wa Fedha ndio maana Mwinyi alipoingia madarakani kakuta hazina tupu sio?
Kadogoo,

..wakati mwingine umekuwa huamini yale ninayokwambia. unataka mpaka niandike kitabu wakati mimi uandishi siyo fani yangu, ndiyo maana nikaomba msaada toka Mohamed Said.

..sasa kuna lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa Mwalimu Nyerere binafsi, au serikali yake, kutokana na hali mbaya ya kifedha pale hazina wakati anaondoka madarakani. sasa katika minajili hiyo, huoni kwamba kuna ulazima tukamjua waziri wake aliyekuwa na dhamana na wizara ya fedha??

..pia kuna waraka ambao inasemekana Prof.Malima aliandika kwa Mwalimu Nyerere akiwatuhumu kwa usaliti wale waliokuwa na maoni tofauti kuhusu muelekeo wa uchumi wa Tanzania kwa kipindi kile. kwasababu Mohamed Said amesema atatoa "darsa" kuhusu Prof basi ingependeza akatuletea waraka huo.
 
Last edited by a moderator:

Mimi na wewe nani anatokwa na povu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…