. Halafu soma hii hapa. Nyerere alikuwa katibu wa tawi la Tabora. Ukishasema HQ ina maana ilikuwa inajua nani anaongoza chama na eneo gani. Unless HQ ilikuwa ndio nchi nzima sentensi hii ina mashaka makubwa. Hata hivyo Nyerere alipokutana na Dosa hakuna shaka waliongelea kuhusu chama na hasa HQ. Kwa mantiki hiyo Dosa atakuwa amemweleza nani anafanya nini HQ na hapo jina la Abdul lazima litokeo. Sijui kama kuna ukweli kuwa Nyerere aliksikia habari za Sykes akiwa Uingereza kupitia Mwapachu.
Hapa anaonyesha jinsi Nyerere alivyokuwa dhalili mbele ya Abdul. Lakini anajichanganya kwasababu experience ya siasa alikuwa nayo kuanzia Tabora alipokuwa katibu wa Tawi, Makerere alipotaka kuanzisha TAWA na Uingereza alipokuwa exposed katika world politics. Kulinganisha watu hawa wawili ni kutafuta udhalili wa mmoja wapo. Tuwaheshimu kama historia ilivyo na si kutumbukiza chuki, fitna na husada katika historia iliyojikamilisha bila chumvi, hamira au magadisodaHapa tunaona uwepo wa Nyerere ndio uliozaa neno Nationalist na si Uislam. Hili ni jambo jema Ahaa kumbe hawa watu walikaa kama nationalist kwa ajili ya kumkomboa mwafrika. Jambo jema kwasababu inaonyesha hawakukaa kama waislam bali nationalist. ) Hapa Mohamed ameshabadili historia kwa utashi wake. Amesema Nyerere aliongea na kundi pekee la waislam. Ukweli ni kuwa aliongea na wazee wa Dar es Salaam kama alivyokuwa anaongea nao wakati akaitaka kulihutubia taifa. Hakuna mahali popote panapoonyesha Nyerere alifanya hivyo kwa ajili ya waislam. Mohamed ameondoa neon Nationalist kama tulivyoona hapo juu na kuja na kitu ambacho hakikuwepo katika historia au ukweli.
Hata leo JK anapoongea na wazee wa Dar es Salaam haongei nao kama waislam, ndivyo ilivyokuwa kwa Mkapa na Mwinyi. Ni chumvi na hamira ili ngano iumuke na wala si ukweli au historia. Nadhani hata Tabora ilikuwa ni hivyo na Nyerere aliweza kutia mguu na kuwa katibu wa tawi. Aliokwenda kuonana na Abdul Nyerere ahakufanya hivyo bila makusudio. Hata hivyo inaonekana wazi kuwa elimu yake ilikuwa msaada kwa TAA na hivyo bila kujali imani yake uwezo wa kuwa na political base ulikuwepo, lilikuwa suala la muda tu. . Si kweli, Nyerere alianza siasa kabla ya kuonana na Abdul Sykes. Mwaka 1947 alipokutana na Dosa hakukutana naye kama mwakilishi wa wanafunzi au wakulima. Alikuwa katibu wa tawi na hata Makerere alishakuwa na political ambition.Mtu aliyewahi kuhudhuria mkutano mkuu wa TAA haiwezekani awe ameanza siasa baada ya kukutana na Abdul. After Abdulwahid and Nyerere had gone out, voting began. Anajichanganya hapa.Kama matokeo yalishapangwa kwanini kuwe na utata huu. Kura zinaonyesha zilipigwa kwa mikono sasa ni kweli kuwa hakukuwa na ukweli kwa watu wengine ambao ulijulikana baada ya uchaguzi hadi watu wawili au watatu tu watuambie kilichotokea. Na matokeo ya kupangwa kwanini kura zirudiwe mara tatu.Then Mo anaweka historia yake mwenyewe kutoka chumbani