Na unategemea mimi ntakuja kujadiliana na wewe huo utumbo, wewe unatakiwa uwe mtulivu mjadala unapoendelea kwa sababu huna inputs zozote zaidi ya upambe kazi ambayo bado hujaimudu. Mimi najadiliana na mwalimu wako ebo!!!!!!!!!
Na unategemea mimi ntakuja kujadiliana na wewe huo utumbo, wewe unatakiwa uwe mtulivu mjadala unapoendelea kwa sababu huna inputs zozote zaidi ya upambe kazi ambayo bado hujaimudu. Mimi najadiliana na mwalimu wako ebo!!!!!!!!!
THE BIG SHOW.
Kuna watu huku kwa kutukana ni mabingwa hasa ikifika weekend nafikiri kuna kitu wakishakipata akili yao inaharibika, eti Mwanakijiji wanamuona anahoja za maana hivi wakiitwa waandishi na mwanakijiji ni mwandishi dah...nimekosa la kusema ngoja ninyamaze ninywe kwanza chai ndio nimetoka madrasa nasikia raha sana kwenda madrasa na najivunia kwenda madrasa tukaneni lakini madrasa siachi kwenda. Cc Mwanakijiji,Nguruvi3,Mag3,GWALIHENZI and Jasusi
Eti Ami,hata mi nashangaa,, mwanakijiji, mwanakijiji,hata angekuwa mwanatown, anadhan umaarufu alioupata hapa Jamii forum na kwingine eti basi anaweza kuja kufikia status ya Moh Said,Status hutafutwa,status haiuzwi mnadani au haigaiwi gurion..! Uandishi aujulie wapi? Nani anamjua yeye Tanzania hii sembuse duniani? Mwambie apandishe juu suruali yake..
wewe mwanakijiji unamuona wa maana sana? Labda kwako,sisi hatuoni la maana analojiua zaid ya kuvaa suruali chini ya kiuno..! Mnasema Moh Said anaoga na watoto na kumkejeli huku mnamuacha huyo limbuken anaetembea huku kalegeza mavazi yake? Tutaenda jino kwa jino hadi mtujuze uchochez wa Moh said hapa., mufilisi wakubwa nyie...
huyo anaejiita mzee mwanatown,
kama vile mnavomkejeli Mwalimu wetu moh said kuwa aache kuoga na watoto,sisi tunamshauri na yy mwanakijiji apandishe suruali yake juu,ni aibu kwa mzee kama yeye kuja hapa kwa hoja za kilamri lamri huku akisafiria nyota yake ya umaarufu,
asitegemee umaarufu wake utambeba mbele ya Nguri wa historia Moh Said,
hana alijualo katika haya yasemwayo hapa,
pia asidhan status huuzwa dukan au mnadani,
Moh Said hakuipata status hii kwa bahati nasibu ati..!
Bado hamjafanikiwa kutuonesha uchochez wa moh said...
Niwie radhi Mzee Mohamed Said, turudi kwenye mnakasha...Mzito Kabwela,
Mimi ni mtu mzima nadhani wewe hunipati mimi kwa umri.
Nadhani umepata kusoma humu mtu mmoja akinituniza kwa
kuniita ''zee.''
Hakika umri umekwenda.
Sasa Mzito Kabwela unapozungumza na mimi fanya staha.
Usitie kejeli kwangu wala usiniite muongo.
Mathalan jambo nimesema na wewe hulikubali.
Kataa tu kwa adabu ukasema, ''Hapana hili Mzee Mohamed
mimi napinga kabisa haiwezi kuwa hivyo nk. nk.
Tuheshimiane.
Usinitie unyonge.
Watu wa matusi nawajua na nimewaweka katika orodha yangu.
Wewe si mmojawao.
Isalia,
Huyo Yericko hana moja alijualo.
Mimi siwezi kuingia ubishi na yeye.
Maryknoll walitoa msaada safari ya pili ya UNO·
Safari ya kwanza iligharamiwa na TANU wenyewe na Al Jamiatul
Islamiyya fi Tanganyika.
Idd Faiz ndiye alikuwa mweka hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya
na ni yeye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere.
Itakuwa kichekesho mie kujibishana na Yericko kuhusu historia ya TANU.
Son...
Hakuna wa kunibana.
Hilo la kanisa kupinga TANU linajulikana sana.
Waliovunja ngome hiyo huko Jimbo la Kusini ni akina
Masoud Mnonji, Yusuf Chembera, Salum Mpunga,
Shariffa biti Mzee Sheikh Mohamed Yusuf Badi na
wengineo.
Hiki kisa maarufu kipo katika kitabu changu.
NItamsaidia; mafundisho na maandisho yako yamechochea chuki baina ya Wakristu na Waislamu na kwa kiasi kikubwa kumwagika kwa damu baina ya watu wa pande hizi mbili kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya ulaghai wa historia ulioufanya kwa miaka 15 na wenzako wengine walioufanya zaidi ya hapo. Lengo lako ni kufanya yale ya Muslim Brotherhood (ambayo una uhusiano nayo wa karibu - kama siyo mwanachama) yaani kulazimisha utawala wa sharia za Kiislamu dhidi ya Watanzania na kuondokana na mfumo wetu wa kisekula. Nothing less than that will make you content.
In my humble, unsolicited and somehow offensive opinion...
Acha kujimilikisha huu ukumbi,tusikilize kipya kipi na kuna viporo vya maswali kuhusu maandiko yako hujajibu hapa?
Unataka kutulisha tu kama ulivyozoea?Watu wanakushangaa wewe unasema wanakusikiliza!?
Unasema Mzee Mwanakijiji anaropoka!?sasa kama hayo ya Mwanakijiji ni kuropoka sijui wewe na maandiko yako tukuitaje?
INAKUUMA KUONA MWANDISHI MWENZAKO ANAKUKOSOA sasa umebaki kusema unampuuza!
Uwezo wa Mzee Mwanakijiji ni mkubwa sana kulinganisha na wewe,waropokaji hujawaona humu wanakuja na ID mbili mbili
Unashindwa kutetea maandishi yako unaleta chuki,Ni aibu kubwa!
Huu uzi bila Nguruvi3 et al ningekuwa nishaachana nao siku nyingi sana.
Kuandika aandike wapi huyo? Labda kama kuandika humu JAMII FORUM.. Zaid ya hapo,ajivunie ufia DINI WAKE tuh..Hivi vitabu vilivyoandikwa na Mzee Mwanakijiji vinapatikana ktk maktaba ipi vile au duka gani maana sikujua kama na yeye kaandika vitabu naomba mnijulishe vinauzwa au ni bure? ningefurahi sana kusoma vitabu ya mwandishi asiyejulikana hata kwa sura!
Hivi vitabu vilivyoandikwa na Mzee Mwanakijiji vinapatikana ktk maktaba ipi vile au duka gani maana sikujua kama na yeye kaandika vitabu naomba mnijulishe vinauzwa au ni bure? ningefurahi sana kusoma vitabu ya mwandishi asiyejulikana hata kwa sura!
Mohamed,
Usiwafiche bana waeleze waziwazi kuwa Kanisa ililipia safari ya pili ya Nyerere baada ya kugundua kuwa Tanu inapata nguvu kila uchao sasa kumlipia Nyerere nauli ni aina ya kutahayari au uhakika wa mtu wao kuja kushika madaraka ya nchi! hembu jiulize swali hili; kama Abdulwahid Sykes ndio yeye anakwenda UNO kweli Kanisa lingemlipia nauli?
Afanalekii..! Sasa anatambia kitu gani? Mwanakijiji,,very very ridiculous.. Kumbe ni mtunzi wa maandiko wa sampuli ya sani na lete raha?.. Vioja kweli hivi...Kuna kitabu chake kimoja cha mapenzi kipo kinauzwa pale Mlimani City jina nimesahau kinafanana na kitabu cha Shigongo.
Son of Alaska,Eti,Inspector General wa police, Hamza Aziz amekataa kutii amri ya Rais Nyerere ya kumkamata Sheikh Hassan bin Amir.
Nyerere huyu tunaemjua au mwingine?? Hizi porojo nyingine!!!! ndio maana nilikuuliza nana hasa mlengwa wa vitabu vyako???
JokaKuu,tunapokuwa tunafanya analysis ya maandishi yake ni kujaribu kuuonyesha umma kile kilichofichika kama ulivyodadavua hapa. Hili la conclusion nadhani ndilo tatizo lake kubwa.Son of Alaska,
..IGP Hamza Aziz alikumbwa na kashfa ya kukanyaga raia kwa gari. Raia huyo alifariki dunia.
..kesi yake ilikwenda mahakamani, lakini ikamalizwa ktk namna ambayo imeacha maswali mengi kuliko majibu.
..baada ya hapo Mwalimu Nyerere akampa uhamisho kwenda kufanya kazi ubalozi wa Tz marekani.
..sasa kuna kipindi Mohamed Said alikuwa anapiga kelele kwelikweli kwamba Dossa Aziz, ndugu yake Hamza Aziz, alinyimwa nishani kwasababu ya Nyerere kutothamini mchango na hisani ya Waislamu kwake. Dossa alipewa nishani nadhani a week later. Sasa mimi nikajiuliza hivi Nyerere alipomhamishia Hamza Aziz ubalozini baada ya kashfa kubwa namna ile, haikuwa kulipa hisani?
..vilevile, Mohamed Said, anasema Nyerere hakuthamini mchango wa familia ya akina Sykes. Wakati huohuo tunaelewa kwamba kuna Abas Sykes, nduguye Abdulwahid Sykes, alikuwa balozi wetu kwa muda mrefu. Sasa kama Abas Sykes aliteuliwa kuwa balozi, what prevented Abdulwahid kuteuliwa ktk nafasi yeyote ile? Mimi kwa mtizamo wangu nadhani Abdulwahid aliamua mwenyewe kutojihusisha na mambo ya siasa na serikali. Lakini mwenzetu Mohamed Said yeye anaona hapo kuna udini.
..Pia nimemuuuliza Mohamed Said, kama Hamza Aziz na Abas Sykes walipewa nishani na Mwalimu Nyerere. Mimi nilitegemea Mohamed atakuwa na majibu on his finger tips lakini inaelekea labda hakufanya utafiti huo, au kuna kitu anaficha.
..Maoni yangu ni kwamba, Mohamed Said ana conclusions zake tayari kuhusu Mwalimu na historia ya Tanganyika, sasa yeye hukusanya data ambazo zita-prove conclusions zake tu. Jambo lolote lile ambalo linaweza kumpeleka nje ya conclusions zake hajishughulishi kulitafiti.CC: gombesugu, Wimana, Nguruvi3, THE BIG SHOW, Ritz, Kadogoo