Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Huu mjadala umemaliza. Wengi waliodandia behewa lako kwa juu wamedondoka njiani.
Tumefaidika kwa mengi lakini uchochezi hatujauona.
Sijui una maslahi gani kuendelea kutuzungusha papo kwa hapo na hoja zako muflis.
Kama hujui huyo Padre Maranta ni mmoja wa waasisi wa mfumokristo.
Kanisa tangu lini likamsaidia mtu katika kufikia wema.Kila linapoingia hutanguliza shari kwa faida yake.

 
Mfumo,
Na mimi nakufikishia ujumbe huu. Hakuna yeyote atakayekwenda kwa mola bila kupitia kwa Yesu Kristo.
 

Wewe na mwalimu wako ndo mnaoangalia historia ya Tanganyika kwa jicho la Udini

Leo hamuamini baada ya miaka kumi na tano watu wanakuja kufumbuliwa macho kitabu kinageuka Ngano,ukweli unajulikana sasa kwamba:
-Si kweli kwamba mnaowaita wazee wenu walisahaulika kwenye historia
-Jengo la TANU kuna watu walifisadi
-leo utafiti mufilisi wa WARSHA umejulikana kuwa ni kiini macho tu ulitaka kujenga chuki katika jamii.
-tunajua kwamba kuna tiketi ilitolewa na Kanisa ili Mwalimu aende UN
-Tumejua kwamba Mwalimu hakuandikiwa hotuba kama mwalimu wenu alivyotaka kutuaminisha
-tunajua kuwa si kweli kwamba Mwalimu alianza Siasa alipofika Dar,ila alianza muda mrefu tu huko nyuma
-leo tunajua kwamba Mwalimu ndio aliyeleta changamoto mpya kwenye TAA na Siasa za Tanganyika wakati ule na kuibadilisha toka Chama Cha Starehe mpaka chama cha Siasa hata mnaowaita wazee wenu hili walikiri.
-tunajua kwamba hakuwabagua watu kwa Dini zao
-uongo kuhusu NECTA na SENSA,EAMWAS(kama sijakosea)...nk nk nk nk nk nk
One moment.....
-tumejua pia kwanza Mfumo Kristo ni kitu cha kufikirika tu kwasababu hata nyinyi hamjui mfumo Kristo ni nini

Yapo mengi nitarudi baadae kuongeza...
Wait....
Usisahau kwamba mwalimu wako alitaka kumdhalilisha mwalimu eti alienda sokoni hana hata senti na akapewa mia tano njiani na Mzee Mshume Kiyate na ikumbukwe kuwa kule Butiama baada ya mwalimu kuacha kazi alikuwa akilipwa Sh 600 na Kasisi Art Willie wa Maryknoll kabla ya kurudi Dar?Mwalimu wako anasema kipindi kile sh500 unajenga nyumba ya vyumba sita Kariakoo leo mnasema mwalimu alikosa senti mfukoni?(think... think...think!!)

Kwa kweli shukrani kubwa ziende kwa hawa;
Yericko Nyerere Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Mag3 sweke 34 Jasusi Ngongo Nyambala Son of Alaska Wimana WC,Wickama,Gwelihenzi JokaKuu na wengine wengi wa aina yao nimewasoma nimefaidika sana

Hata wewe,big show,boko boko,kadogoo,mdokoaji,ami na wengine wa aina yako hamjapuuzwa saaana mmekuwa na mchango pia tumewasoma....

Nitarudi!
 
Last edited by a moderator:

gombesugu,

A.K.A The Great Thinker.

Thank you I really appreciate.

Cc.. Barubaru, THE BIG SHOW, Mohamed Said, Nguruvi3, JokaKuu, WildCard, Ami, Jasusi, Yericko Nyerere, Kadogoo, Mzee Mwanakijiji, Invisible, Ngongo, Nyambala, Spike Lee Boko haram, Mag3 Pasco, mfumo, zomba,
 
Last edited by a moderator:

Maswala ya Dini jadiliana la Ritz
 
Duh mfumo huu mnakasha umekuzidi kimo ni vyema ukaufualia bila kuchangia chochote.

 
Last edited by a moderator:

Rapheri,
Hakika umeandika kwa hamaki na ukiandika kwa hamaki unapoteza mengi.

Nimeweka hapa katika siasa za wafanyakazi mambo yaliyojitokeza katika mgomo wa
makuli wa bandari ya Dar es Salaam 1947 na 1948.

Nimeeleza jinsi Abdu Sykes alivyoshiriki kama katibu wa Dockworkers Union na yote
yaliyotokea hadi kufika mapambano na mabomu kupigwa 1950 na chama cha makuli
kupigwa marufuku nana serikali ya kikoloni na baadhi ya makuli kufungwa.

Hii nililieta jamvini kwa makusudi maalum ili umuone Abdu anaingia katika
uongozi wa TAA 1950 kama katibu akiwa na turufu gani mkononi.

Ikiwa utakumbuka utafahamu kuwa uongozi wa wazee ulipinduliwa kwa juhudi za Hamza
Mwapachu, Abdu Sykes na Schneider Abdilllah Plantan na Abdu pamoja na Dk. Kyaruzi
wakachukua uongozi wa TAA Dk. Kyaruzi akiwa rais.

Uongozi huu ndiyo ulioandika ile memorandum ya Constitutional Development Committee
chini ya TAA Political Subcommittee waraka ambao uliwasilishwa kwa Gavana Edward
Francis Twining na huu waraka ukajadiliwa kwenye mkutano wa kuasisi TANU 1954 na ndiyo
uliotengeneza hotuba ya Nyerere aliyosoma UNO February 1955.

Hii kwa mukhtahsari ndiyo historia ya hotuba hiyo ya Nyerere ambayo aliisoma UNO 1955
lakini inaelekea wenzangu kuna kitu kinakuchomeni nyoyo zenu.

Hampendi historia iwe hivyo mnataka ibadilike iwe nyingine kabisa.
Si kitu.

Waliotangulia wao walifanya ujanja mmoja.

Historia ya hotuba hii hawakuigusa kabisa kwa hiyo watu walikuwa hawajui chanzo chake.
Kiasi ilisaidia maana hapakuwa na mabishano.

Sasa turudi nyuma kidogo.

Hata ilipofika 1953 katika ule uchaguzi wa 17 April kati ya Nyerere na Abdu Sykes ''track record''
ya Abdu katika TAA na katika siasa za Dar es Salaam ilikuwa ikifahamika na wengi.

Hakuna mtu aliyekuwa anamjua Nyerere ukiwatoa labda hao wenzake wa Makerere.

Kwa hakika Nyerere hakuwa na historia yoyote kuwa aliwahi kuwatia misukosuko wakoloni.
Hii ndiyo sababu katika uchaguzi ule Nyerere alishinda kwa kura chache.

Hili nalo linawachoma baadhi ya ndugu zangu.
Historia hii hawaipendi wangetaka iwe vinginevyo.

Waliotutangulia katika kuandika historia walikuwa watu ''makini.''
Uchaguzi huu haukutajwa kabisa wala jina la Abdu halikupewa uzito wowote.

Waandishi wale walikuwa wanasema Nyerere kachukua uongozi wa TAA 1953 hawataji
kauchukua kutoka mikononi kwa nani.

Mimi ndiye niliyekuja kuweka mambo sawa kwa kumrejesha Abdu Sykes katika historia
ya TANU.

Ndiyo maana unaona kadi ya TANU namba 1 Julius Nyerere, No. 2 Ally Sykes na No. 3
Abdu Sykes.

Idd Faiz aliyeratibu na kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO kadi yake No. 25.

Hii haikuja hivi hivi tu.
Haya hayakuja bure.

Yote hayo yana historia yake.

Rapheri,
Umeleta suala la dhulma alofanya Kleist Sykes kwa nyumba ya African Association.
Mimi ningependa kujua nini khasa alifanya.

Mimi nitatosheka na maelezo wala usitafute ushahidi kwani mie si mtu wa ubishi kauli
yako itanitosha.

Mengine nimeyaacha maana naona si muhimu sana kwangu kuyasemea.
 
Kinachonishangaza ni kuona jinsi Mzee Ms anavyoaminiwa kwa kila bandiko lake na jinsi ambavyo kuna wadau ambao wako tayari kumtetea hata pale alipopotosha!
Ujinga mtupu!

Ndugu zetu wanashindwa kuuona ukweli hata kidogo,kuna vitu hata kwa elimu ndogo tu unaweza kuona kwamba haviko sawa ila hawataki kuona wao ni mfumo kristo...tunaonewa...sisi tupo wengi kuliko wao...watoto wetu wanafelishwa..vitu ambavyo havina ushahidi kwasababu kama ni hali ngumu ya maisha sote inatuhusu bila kuangaliana dini ya mtu
 


Mzushi na mnafiki.
Huyu mtu kasoma shule ya wakatoliki.
Juzi hapa amemshukuru Allah kwa kumpa walimu wazuri waliomuandaa kuwa na uwezo wa kujibu hoja (Nafikiri walimu hao ni pamoja na mapadre waliomfundisha huko St.Joseph). Amefaidi huduma za kanisa katoliki.
Huyu huyu, kwenye machapisho yake fulani yaliyoko kwenye mtandao, amekitaja chama cha mapinduzi kama "Catholic Church Movement"-CCM

Huyu huyu, kwenye chaguzi za majuzi akaanza kuwatuma vijana wake wachague wagombea wa CCM (Catholic Church Movement) kuwapigia campaign misikitini, na wasichague wagombea wa Chadema, eti Chadema kinaongozwa na padre wa Catholic. Anakataa nini na anataka nini? Huo sio unafiki?

Najua dini yenu inalaani UNAFIKI.
Najua kuwa huwezi ukampinga Mohamed Said (ukimpinga utaonekana wewe sio muislam swafi) na kwa hiyo huwezi ukamwita ni MNAFIKI. Najua kuwa unaelewa kuwa kuna mambo anazusha katika simulizi zake (Probably uzushi is not forbidden by his faith). Lakini huwezi ukakubali hapa kuwa Moh Said ni mzushi...
Well, huna haja ya kukubali haya niliyosema. Lakini I hope the message has hit home.
 
Kumbuka wazi kuwa TANU imezaliwa 1954, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Julius Nyerere akutane kwa faragha na kasisi Maranta,

Na mwaka uliofuata kanisa likaisaidia TANU kumsafirisha Mwalimu Nyerere kwenda UNO akipitia Londan,

Lakini Mohamed kadiri tulivyombana amebadili maneno yake na kusema kuwa kanisa liligharimia safari ya pili ya Mwalimu kwenda UNO,

Yericko Nyerere acha kupotosha safari ya kwanza ya kwenda UNO waliochanga pesa ni Wazee wetu wanywa gahawa nakupa picha ya safari yao



Hii picha Wazee wa Dar es Salaam wanamsindikiza Nyerere uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Kulia kwa Nyerere alievaa kanzu na kofia ya "tarabushi" ni mweka hazina wa TANU Idd Mafongo ambaye alipewa jukumu la kukusanya michango ya safari alisafiri sehemu mbalimbali kukusanya michango.

Wanajamvi huu ni ushahidi wa historia ya Tanganiyka ambao ulikuwa umefichwa.
 
Nanren
Kwanza kabisa nionyeshe kunamaandiko gani yanamkataza muislamu kusoma shule za kikiristo maadamu hulazimishwi kufuata mila zao,pili wapi imekatazwa kumsifu mkiristo akifanya vizuri nje ya mambo ya kiimani?tatu hapo kwenye red niletee ushahidi wapi kaandika hayo, kuhusu dini yetu kukataa mambo ya unafiki ni kweli na vile vile dini yetu haituruhusu kuamini kila habari sasa na wewe ukishindwa kunithibitishia haya utakuwa ni fasiki kama hii aya hapa chini inavyosema.
Sahih International
O you who have believed, if there comes to you a disobedient one with information, investigate, lest you harm a people out of ignorance and become, over what you have done, regretful.
 

Mohamed,
Najua umeshasema mara khamsa ishreen kuwa hotuba aliyoisoma Nyerere UN iliandikwa na akina Sykes. Kaisome tena hiyo hotuba kwenye kitabu cha Nyerere "Freedom and Unity" halafu uje hapa utuambie ama a/ Nyerere aliplagiarize maandiko ya Abdulwahid au b/ ni maudhui gani yalikuwa mchango wa akina Sykes ni ni kiasi gani ni mchango wake mwenyewe. Kwa sababu haiingii akilini eti Nyerere aweke kwenye kitabu cha hotuba zake hotuba iliyoandikwa na wengine. Hiyo memorandum ya constitutional development committee huenda ilikuwa na points ambazo Nyerere alizizingatia lakini ukisoma ile hotuba ni "typical" Julius Nyerere katika lugha na presentation.
 

Mzee mjanja sana; angalau umeanza kuconcede some facts. Umedai kwa muda mrefu kuwa kabla ya Nyerere kuja tena Dar mwaka 1952 alikuwa hajulikani na mtu yeyote makao makuu ya TAA. Na umedai kuwa siasa alizianza baada ya kuingizwa katika siasa na Abdul Sykes. Sasa hivi baada ya kukuonesha kwa ushahidi kuwa Nyerere alikuwa anajulikana na alikuwa ameshaanza siasa kabla ya kukutana na Abdul umeanza kukubali.

Kwamba wenzake wa Makerere walikuwa wanamjua kabla ya kuja tena Dar in 1952 ni concession kubwa kwako maana kwa miaka 15 umewaaminisha wasiojua kuhoji kuwa kweli Nyerere alikuwa hajulikani kabla ya 1952. Mwendo mzuri.
 

Wrong; kitabu cha Mohammed Said siyo kitabu cha Kitaaluma kama unavyodhani. Hakijafanyiwa utafiti wa kitalaamu na kimetumia madai ya 'historia' kuficha udhaifu wa kitabu chenyewe. Hiki ni kitabu cha maoni ya kiharakati; hakina msingi wa utaalamu wa historia. NI kwa sababu hiyo kupingwa kwake wala hakuhitaji sana kazi ya kitaaluma. Nikiamua kuandika kitabu kukosoa (kwa sasa sina muda sana) nitakikosoa siyo kwa vile nakiona ni kitabu cha kitaalum bali kwa sababu kimesingiziwa kuwa ni cha kitaaluma na matokeo yake watu wamekiamini.

Inanishangaza zaidi kuwa wewe kama Mwanasheria unaweza hata kukipa credibility kitabu hiki kwa ushahidi wa hisia ambao unatolewa. Sijui kama umekisoma au unasoma tu vipande vipande vinavyotolewa hapa. Hakuna lolote lililomo kwenye kitabu hiki ambalo linaweza kutumiwa mahali popote kwenye an impartial jury kuthibitisha dhulma dhidi ya Waislamu wa Tanzania. NONE.
 
Thank you MM. Ameonyeshwa na amekubali.

Hapa ndipo tunasema hakuna utafiti na wala haihitaji mtu kuwa mtafiti au kufanya utafiti kujua kuwa hakukuwa na utafiti. Makala zake mwenyewe zimemuumbua.
Tumemuonyesha kuwa Dosa Aziz alikuwa anamjua kabla ya 1952! Kwa kutumia maandiko yake mwenyewe.

Dosa alikuwa inner circle wa TAA na HQ na wala hakuwahi kukanyaga Makerere.
Anaposema eti wenzake wa Makerere automatic ameshamuondoa Dosa katika inner circle.

Katika jitihada za kumdhalilisha Nyerere na kumkweza Abdul Sykes, Mohamed anajikuta anadhalilisha sana wazee wetu.
Keshamdhalilisha Dosa kuwa hakumjua Nyerere na hakuwa Makererian.
Keshamdhalilisha sana K.Sykes kwa kushindwa kutetea Ufisadi wa Nyumba kama ulivyobainishwa na Mag3
Kamdhalilisha Hamza Aziz kwa kumpa ushujaa leo tunajua alikuwa mhalifu na aliokolewa na Nyerere
n.k n.k

Kwa wale wanaodhani huwa tunachambua mistari ya Mohamed moja baada ya mwingine ili kumkomoa huu aliousema ni ushahidi kuwa Mohamed hana ground to stand. Leo amekiri, narudia baada ya kukana miaka nenda Ulaya na Marekani leo ndani ya free for all JF amekiri kuwa Nyerere alijulikana TAA. Case dismissed.
 

Karibu sana Gombesugu...

Inaonekana na wewe unasoma maandishi haya kwa mwanga ule ule - wa dini. Umejaribu kuwa 'balanced' mwanzoni lakini kwa kadiri muda unavyokwenda unajionesha kuwa hujali academic integrity and honesty ya mwandishi. Na badala yake umeingia kumtetea Mohammed Said solely kwa sababu ya Uislamu wake na siyo kwa kazi yake. Hili sina tatizo kwani wakati mwingine damu ni nzito kuliko maji.

Ndugu Gombesugu, hatubishani kuhusu maoni ya mtu; kwani maoni ya mtu ni maoni yake. Tunabishana kuhusu some facts. Inasikitisha kuwa unaamini kazi ya Mohammed Said imefanyiwa "thoroughly researched" na "closely scrutinized". Kama kweli unaamini haya basi na wewe umeingia kwenye mtego ule ule wa kuamini hisia za mtu kuhusu historia kuwa ni facts za historia! Tunabishana na Mohammed SAid kuhusu facts sir, siyo hisia zake kuhusu hizo facts.

1. Mohammed Said anadai kuwa Nyerere aliingia siasa mwaka 1952 na kuwa aliingia siasa na uongozi wa TAA baada ya kuingizwa na Abdulwahid Sykes - hapa hadai maoni anadai facts. Tumeonesha kuwa Nyerere alianza siasa miaka karibu 10 nyuma na wakati anakuja Dar tayari alishapata kuwa kiongozi wa TAA huko Tabora na alishaanzisha chama cha kutetea maslahi ya Watanganyika akiwa Makerere (kabla ya kukutana na Abdulwahid Sykes karibu miaka saba nyuma. Hili ni suala la facts Gombesugu siyo opinion! Mohammed Said was/is factually wrong.

2. Mohammed Said anadai kuwa Philip Marmo alikuwa ni mbunge wa Monduli wakati wa sakata la OIC mwanzoni mwa miaka ya tisini; tumeonesha kuwa Marmo hajawahi kuwa Mbunge wa Monduli; hili siyo suala la maoni Gombesugu ni suala la facts. Mohammed Said was/is factually wrong!

3. Mohammed Said amekuwa akidai kuwa Kanisa halikuhusika katika harakati za Uhuru na kuwa halikutoa mchango wowote kwani Wakristu walikuwa wanafaidika na Ukoloni. Imeoneshwa humu kuwa Wakristu wengi tu walishiriki harakati za Ukoloni na waliupinga sehemu mbalimbali nchini na hata wao pia kutoa misaada kuchangia TANU. HIli siyo suala la maoni ndugu Gombesugu, ni suala la facts; Mohammed Said was/is factually wrong!

4. Mohammed Said amekuwa akidai kwua Nyerere alikuwa na chuki na Waislamu na Uislamu; hadi leo hii hakuna mahalipo popote ambapo ameonesha ushahidi wa jambo lolote Nyerere alilolisema au kulifanya lenye kuonesha chuki ya Nyerere dhidi ya Waislamu. Lakini amejaza ushahidi lukuki wa mahusiano ya karibu ya Nyerere na Waislamu kabla na baada ya Uhuru. Mohammed Said was/is factually wrong!

5. Mohammed Said amedai kuwa kile alichokiita 'Christian Lobby" ndio kinaendesha nchi na kuwa ndio leo kinaitwa "Mfumo KRistu" ambao unawabagua Waislamu. Mohammed Said ameshindwa vibaya kuonesha jinsi gani mfumo wa kibaguzi unatoa nafasi kwa wale wanaobaguliwa kushika madaraka na nafasi mbalimbali. Hili halijawahi kutokea mahali popote duniani ambapo mfumo wa kIbaguzi ulitengeneza na kuwapa nafasi wale wanaobaguliwa huku mfumo huo ukifanya kazi! Mohammed Said is/was factually wrong.

Gombesugu, tunaweza kuendelea na kuangalia 'facts' ambazo Mohammed Said amekuwa akizidai na kuonesha ni kwanini hazina ukweli wa kihistoria. Kwa wewe kuamini kuwa maandisshi yake yamefanyiwa "thoroughly" research inashangaza; labda neno thoroughly researched limepoteza maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…