Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Orodha ni kubwa sana MM. Nadhani Gombesugu kama ni ''mgeni'' basi hakuwahi kuwepo hapa 2010,2011,2012.
Hata alipojiunga April 4 mwezi huu hajapata nafasi ya kusoma nyuzi hii kwa utulivu.

Nimfahamishe kuwa kama kuna mtu kafanya research na kuandika thesis halafu siku ya ku-defend akashindwa huyo hapewi hata certificate of attendence.

Gombesugu baada ya kukusoma kwa ukaribu nimeona umeongozwa na nguvu ile ile aliyoiweka Mohamed.
Nguvu ya kuamini kumpinga ni kukana Uislam na ni kuunga mkono ukafir.

Ukishanasa hapo basi Mohamed atakwambia Kawawa alikuwa makamu wa rais 1988 na utakubali.
Mohamed atakwambia Warioba alikutwa machungani na Nyerere akaletwa Dar bila viatu na kuwa waziri mkuu, utakubali.

Mohamed atakuambia Nyerere alimkana Abdul bila ushahidi nawe utakubali.
Mohamed atakuambia kila anachotaka na utakuwa huna ujanja wa kufikiri zaidi kwasababu huyu ni mmoja wa watu walioletwa kuwakomboa waislam wa Tanzania.

Mohamed atakwambia huyu ni mwislam, huyu ni nusu mwislam, huyu ni kafir bora, huyu ni dhalim na hata kukuaminisha kuwa bila kumsikiliza ni moto unakusubiri.

Kwasababu amekufunga katika minyororo ya fikra kwa kamba maalum aanayoita dini ya uislam basi hapo huna ujanja, atakuambia Bila Wazulu, wanubi na Wamanyema ungekuwa chini ya minyororo ya mwingireza.

Atakuaminisha kuwa Nyerere alizaliwa Bulawayo na alikuja hapa akapewa hotuba na sheikh Chaurembo ndipo Utanganyika wake ulipoanza, utakubali! ufanyeje na wewe unaitafuta pepo!!

Sasa kama kweli tunahitaji kufanya utafiti na kuandika kitabu cha je kawawa alikuwa makamu wa rais mwaka 1988, sijui hilo tutaliita nini.

Na mwisho Gombesugu nimewahi kusema nikiweka tafiti ya mambo yangu Mohamed hawezi kuchagangia hata mstari mmoja. Hilo si kosa na wala halimzuii yeye kufanya hivyo. Kwabahati nzuri sisi wengine tumeweza kumweka kitako, kumfunua yeye na vitabu vyake na wala si lazima kila mmoja aandike kitabu.

Tunaweka rekodi vema ili wanadamu waliotoka katika ubavu wa Adam na Hawa wasiendelee kuumizwa kipuuzi.
Miaka 15 inatosha, kukaa kimya ni kukisaliti kizazi huku tukiwa na hazina vichwani mwetu. Hilo halitatokea
 

Nguruvi,
Hii historia imekubalika kwingi ndani na nje ya Tanzania.

Ni tabu kwa yeyote kujaribu kuikana.
Hapa tulipofika ni mbali mno.

Wala mimi sina hofu ya kuwa iko siku nitaitwa muongo.
 

Nguruvi,
Nimekusoma.

Majibu yapo lakini ya nini ndugu yangu.
Mimi hupenda kueleza yale yasiyojulikana.

Sipendi kumchosha msikizaji kwa ubishi.
Hii ndiyo staili yangu ya mnakasha.
 
Ndugu yangu pembuka pasi angalau hata kidogo,

Hivi ulitaka uwaone makasisi kwenye picha hiyo ndupo uamini kuwa kanisa lilifadhiri safari hiyo kwakukata tiketi ya kwenda na kurudi UNO?

Nimeeleza vema jinsi ilivyokuwa vigumu kwa kanisa kujiingiza katika siasa zamoja kwa moja mpaka ikawalazimu kutumia mashirika yake yaliyokuwa nje kama Maryknoll Sister kuratibu siasa za Tanganyika.

Kasisi Zelger alistaafishwa kwa lazima mwaka 1927 baada ya kugundulika kuwa anajihusisha na masuala ya siasa.

Ninarudia kukueleza tena kuwa uimara wa siasa za TANU ulikuwa na mkono wa KANISA.

Vivyo hivyo ulikuwa na mkono wa uislamu Chini ya Shehe Issa bin Amir.

Lakini ifahamike kuwa dini hizi hazikuwa msingi wa kuwepo kwa TANU wala turufu ya UHURU wa Tanganyika bali UTANGANYIKA wa watanganyika hai.
 
Nguruvi,
Nimekusoma.

Majibu yapo lakini ya nini ndugu yangu.
Mimi hupenda kueleza yale yasiyojulikana.

Sipendi kumchosha msikizaji kwa ubishi.
Hii ndiyo staili yangu ya mnakasha.
Kwamba Warioba aliokotwa Ikizu akiwa na msafara wa ng'ombe kuelekea Kyabakari akapakizwa katika motorcade na kuja kuwa waziri mkuu! tafadhali Mohamed!
 
Mohamed Said tunaomba umwambie huyu jamaa yako,John Rupia alitoa % ngapi ya hii nauli ya Nyerere kwenda UNO.wewe atakuamini, au ni mwage mtama???
 
Last edited by a moderator:

Pole sana kaka yangu Jasusi,
Uongozi ni kupokezana vijiti - relay.

Yote niloandika umeguswa na hotuba ya Nyerere UNO peke yake.
Tusubiri kuna kitabu cha Nyerere kinaandikwa.

Sijazungumza mimi kuhusu ''plagiarise'' siwezi kumkosea Mwalimu
adabu kiasi hicho.

Mchango haukuwa wa Abdu peke yake.

Alikuwako Hamza Mwapachu, Dk. Kyaruzi, Steven Mhando, Earl Seaton
Sheikh Hassan bin Amir...

Ama mmepatikana.
Poleni sana ndugu zangu.

Pita Rhodes House, Oxford lipo jalada la wanasiasa wa Tanganyika ndani
utapata mengi sana.

Sasa hivi Waingereza wamefungua zile faili zao za Special Branch wanaita
Intelligence Gazette.

Mna mengi kuhusu Abdu Sykes, Steven Mhando, Hamza Mwapachu na jinsi
makachero walivyokuwa wakiwaandama hadi anonymous/nom de plume letters
katika Tanganyika Standard katika 1950s wakimshuku Abdu...wakafananisha
staili yake baada ya kumsoma katika faili za TAA...

Ndugu yangu ni suala la kuufungua ubongo tu mengi yatakudhihirikia.
Wazee wangu walianza shughuli hizo toka 1920s.
 
Kwamba Warioba aliokotwa Ikizu akiwa na msafara wa ng'ombe kuelekea Kyabakari akapakizwa katika motorcade na kuja kuwa waziri mkuu! tafadhali Mohamed!

Nguruvi,
Hivi ndugu yangu hadi leo hujanijua?

Waswahili sisi adab ni mbele kuliko
kitu chochote.

Nakusihi kwa hisani yako tujitulize na
tuchunge heshima za watu.

Kuna maneno ukiyatumia kwangu najisikia
simanzi.

Wala mimi sijui alikotoka Warioba najua ni
Musoma tu wala sijapadharau.
 


Pembeni ya Nyerere ni Sheikh Suleiman Takadir mwenyekiti wa kwanza wa baraza la wazee wa TANU.

Masikini Shekh Sulemani Takadir kumbu ndiye huyu! sifa zake zimo ktk kitabu cha Mohamed Said. Shekh kwa ujasiri wake alimnyooshea Nyerere bakora mbele ya wajumbe na kutamka kuwa atakuja kunufaisha Kanisa lake na kuwasahau Waislamu! Nyerere aliangua kilio ili apate huruma za wajumbe na kweli alipowauliza anayosema Shekh wanaunga mkono? kwa nguvu ya uchawi wa kilio chake wajumbe wakawa upande wa Nyerere miongoni mwao Mzee Bilali Waikela ambae bado yuko hai! Matokeo yake shekh Takadir alisusiwa mpaka akafariki kwa uhoro!

Leo nenda kamuulize Mzee Bilali Waikela kama bado yuko na Nyerere au na Shekh Takadiri!
 

Hivi Kasisi anafanyia kazi nyumba ya Mungu au Mkoloni?
 
Wimana,
Hapana haya nisemayo ni kweli tupu.

Ukweli hauwi ukweli kwa sababu umesema ni "kweli" au kwa sababu unaamini ni "kweli". Ukweli unakuwa ukweli kwa sababu unaweza kuoneshwa kuwa ni kweli. Ndio maana sifa moja ya ukweli ni 'self evident'. Ukweli haupingiki. Umesema Marmo alikuwa MBunge wa Monduli na bado unadai ni "kweli tupu". Hatuna namna ya kukusaidia kwa kweli, kwani umetengeneza (fabricate) ukweli wako, umeuamini, ukawaeleza na wengine nao wameamini na umekataa kabisa kuangalia ukweli ulivyokuwa isipokuwa ule uliouunda mwenyewe.
 

N,
Ulimi wako ni mwepesi...

Pima neno kabla hujalisema.
 

Nikikuletea utakubali kuwa huyu mzee Muddy ni mnafiki?
Infact unanishangaza. Mbona yapo tu kwenye mtandao with all the hallmarks of Moh Said?
kwa sasa hivi natumia simu.
Ngoja kesho niingie kwenye laptop, nitakuwekea.
 

Kadogoo,

Usiseme hayo maneno jamaa zetu wanasema Nyerere kaanza kupingwa na WARSHA.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Kasisi anafanyia kazi nyumba ya Mungu au Mkoloni?

Ningependa nikujibu, lakini nahisi mjadala huu umekuzudi kimo,

Laiti ungesoma makala yote hapo juu ungeendelea kupembuka kimang'amuzi zaidi ndugu yangu.

Kwa sasa jisomee tu hakuna utakachopoteza kisha njoo tujadiliane!
 
Umeamua kurudia rudia vitu vidogo visivyoepukika katika uandishi ukidhani kwa kufanya hivyo unaweza ukabadili ukweli ulioganda kwenye vichwa vya waislamu baada ya kushuhudia kwa macho yao na wengi wao wakiwa hawajawahi hata kukiona hicho kitabu mnachojaribu kumpelekea Kikwete akitaje kwenye hotuba yake ya mwezi fulani ujao kabla hamjakifanyia maandamano.Aibu tupu kwenu!.
Kumbuka waislamu tuko wengi mno kuliko nakala zilizochapishwa za kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika.
Nani asiyeona miongoni mwa waislamu kuwa:
1.Baraza la mitihani NECTA ni kama jimbo la kanisa na hakuna wa kulifumua hata likifanya dhulma za wazi kwa waislamu.Waziri na raisi wake wanawaogopa wakristo kuliko wanavyoheshimu waislamu wenzao na manung'uniko yao.
2.Serikali inatoa ruzuku kwa taasisi kama za mahospitali ya kanisa na kuzifanya hospitali za serikali ambako raia wote wakiwamo waislamu wangetibiwa bila kushinikizwa na kejeli za kikristo?
3.Ajira zote muhimu serikalini kuanzia ngazi za juu mpaka kata zimehodhiwa na wakristo na baadhi yao ni vihiyo kabisa?
4.Serikali imeacha kujiunga na OIC na kuanzisha mahakama ya kadhi na si kwa sababu nyengine yoyote ile bali matakwa ya makanisa tu.
5.Serikali imekaa kimya huku makanisa yakisambaza takwimu za bandia za idadi ya waislamu na wakristo Tanzania na hata waislamu walipolalamika sana hatimae serikali imetoa takwimu nyengine za bandia na kufanya visasi na waislamu?.
6.Serikali imewakalia kimya wachungaji wanaovunja kanuni juu ya uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya biashara huku ikiwashughulikia waislamu wanaokataa kulishwa vibudu?.
Orodha ni ndefu juu ya dhulma zinazofanywa na serikali ambazo baadhi wala hazimo kwenye kitabu cha Mohammed Said,ni mpya kabisa.Kwa mfano ikiwa neno mfumokristo limewatia kiwewe basi kizazi kipya kwa kuona dhulma wanaweza kutumia neno tofauti na mpambano kati ya haki na batili ukabaki pale pale.Itaondoka kutoka christian lobby kuwa mfumokristo na kwenda neno jengine litakalowaudhi zaidi madhali tatizo lipo bado.


 

Kanisa hutanguliza shari eeh?
Lakini ndio lililompa elimu ya awali mwalimu wako Sheikh Moh. Au ndio maana ana shari?
 
Wanajamvi: Hapa kuna Tathmini ya kitabu cha Mzee Mohammed Said, sijahangaika kuweka link kwa vile ku-access hiyo article yabidi uanachama katika maktaba na majarida husika. Italics za ndani ya review ni zangu. Kwa waliokwishaisoma popote itakuwa marudio.

BOOK REVIEWS:

MUSLIM NATIONALISTS IN TANGANYIKA: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika. By MOHAMEDSA ID. London: Minerva Press, 1998. Pp. 358. ? 1.99, paperback (ISBN 0-754IO- 223-8). KEY WORDS: Tanzania, colonialism, nationalism, Islam.

REVIEWER: JONATHON GLASSMAN (Northwestern University): SOURCE: The Journal of African History, Vol. 42, No. 1 (2001), pp. 164-166

In recent years historians of nationalism, like historians of science, have been turning to the stories of the losers. In studies of South Asia as well as Africa, authors such as Allman, Geiger and Mbembe have sought to escape the triumphalist trap of assuming that nationalist politics were shaped solely by the men who eventually took power.

A focus on historical dead-ends can illuminate the contingencies that shaped nationalism, and can also help explain many post-colonial political conflicts. Mohamed Said's book is one such study. Its title is misleading: relatively little is about Abdulwahid Sykes, a member of a prominent Dar es Salaam family, and the book fails to substantiate Said's claim that his hero 'founded a political party [TANU] and made a President [Julius Nyerere]'.[/I] Yet the title points to the author's general approach. Using a collection of documents preserved by the Sykes family, as well as the memories of informants drawn from the author's extensive network of personal contacts, Said tells the story of Tanganyika nationalism from the Sykes family's point of view. In doing so, he creates a valuable resource for the study of colonial Dar es Salaam (a place that has received surprisingly little scholarly attention), and makes a strong case that the prevailing literature on Tanganyika nationalism, much of which is centred on the figure of Nyerere, has underestimated the contribution of Muslim townsmen and needs to be reassessed. Private sources such as Said's are often available only to interested parties rather than disinterested professional historians.

To his credit, Said opens with a forthright statement of his connection to the Sykes family (this statement itself tells the reader much about the ties of neighbourhood that sustained nationalist politics in Dar es Salaam), and he makes his polemical agenda clear throughout.

Briefly, his argument is as follows. TANU was created by Muslim townsmen, led by the Sykes brothers, who envisioned the party in 1945 while serving in the Burma Infantry. The Sykeses recruited Nyerere late in the game and made him president of the new organization in a self-sacrificing ploy to encourage Christians to join the nationalist cause. The latter were essential to success because, having been favoured by the colonial regime, they dominated the ranks of the educated elite. But the Christians were unreliable nationalists because of their indoctrination by 'the Church' (Said often assumes that all Christians were Catholic), portrayed here as a highly effective tool of colonialism. After uhuru, TANU's new Christian leaders reneged on promises they had made to keep religion and politics separate, and together with the Church plotted to rid TANU of Islamic influence. By 1970, this conspiracy was complete: TANU had been effectively wrested from the hands of the people who had created it, and had become a tool of Christian power.

Needless to add, Said is a tendentious writer. Yet remarkably little of his argument is directly contradicted by standard accounts, and, although it is impossible to evaluate his sources (footnotes are few and not always useful), he presents some fascinating new material. He is most persuasive in the two-thirds of the book that discuss the period before independence. Said surely has a point when he chastises historians for having failed to note the Islamic factor in the nationalist politics of Dar and other towns. Also valuable is his focus on Muslim-Christian tensions within TANU and its predecessor, the Tanganyika African Association (TAA): indeed, such tension was noted by observers at the time but has since failed to capture the attention of historians who perhaps have been too accepting of official myths of nationalist unity. Yet these strengths are often vitiated by the book's combative tone.

Two over argued themes, in particular, come in conflict. On the one hand, Said wishes to convince his readers that the Sykes circle created the nationalist movement virtually single-handedly and, in its early phases, totally dominated it. In this regard, he presents Nyerere in the early 1950os as an utter neophyte, a cipher who was shrewdly manipulated by Sykes and his allies. (This depiction of Nyerere as 'a complete stranger' to nationalist politics is partly a function of Said's Dar-centred perspective.) On the other hand, he perceives the history of Tanganyika nationalism as a grand struggle in which the Muslim townsmen who created the movement fought each step of the way against the wiles of their Christian enemies. These opposing themes catch Said in some absurd contradictions, such as in his narrative of the 1953 contest in which Nyerere assumed leadership of the TAA, immediately before it was transformed into TANU. That narrative portrays Nyerere simultaneously both as Sykes's tool and as his arch nemesis.

But the most troubling aspect of Said's tendentiousness consists of his portrayal of a Manichean conflict between Muslims, depicted as uniformly dedicated nationalists since the days of Maji Maji, and Christians, depicted as unsteady collaborators. That such images are often contradicted by his own rich data is all the more cause for disappointment.

Said is at his most contentious in the book's closing section, entitled 'Conspiracy against Islam'. It would be difficult to refute the core of his indictment there: TANU's misguided efforts in the late I960s to quash autonomous Islamic institutions. (This sordid tale has been told with more convincing detail, albeit on a strictly local level, by Abdin Chande.) Yet in his determination to reveal TANU's plots to impose 'Christian hegemony', Said ignores the fact that these efforts were part of a broader move to control all institutions of civil society. Still, as a statement of perceptions that are widely shared by Tanzanian Muslims, perceptions grounded in two generations of historical memory, this discussion, and Said's entire argument, should not be ignored by anyone who cares about Tanzania's future.

NAWAKILISHA
 

Yericko Nyerere,

Naona unataka kulazimisha kuziba shimo la panya kwa mkate wa nyama.

Hiyo safari ya kwanza Nyerere kwenda UNO tarehe 17 februari 1955 Kanisa hawahusiki kabisa safari ya pili ndiyo Kanisa wametoa tiketi.

Hizo ngano zako na mambo ya kupembuka walishe wenzako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…