Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed, hivi kwa mtazamo wako gazeti la Annur linakidhi viwango? hii ni by the way
 
Jasusi,unamsoma between the lines MS!!!!!!

"Sawa mie na wewe ni watu wa tamaduni tofauti sana.
Wewe unatoka Musoma mimi nimezaliwa Dar es Salaam.

Makuzi yetu ni tofauti sana."

Halafu unaona alivyokwepa hoja yangu ya yule mama wa Songea kiaina?
 
Mmh...we nawe bana; sijui ndio reasoning gani hiyo; basi Nyerere kutokujibu nako ni kujibu!

OO, Na hii sijui ndio reasoning gani jamani toka kwa Great thinker! hivi hujui kuwa unapomwambia Msichana Mwanamwali kuwa unataka kumposa halafu anyamaze bila kujibu hujui kuwa amekubali ombi lako? au wewe Mzee ungeendelea tu kumwambia hayo hayo?

Nyerere kutokujibu hoja za Mohamed, bila shaka amekiri kuwa hoja hizo ni sahihi! ndio maana alifuatwa na Profesa Haroub Othman ili kukanusha kitabu cha Mohamed lakini Mwalimu alikuwa binaadamu na lazima tukubali kunakutahayari pia!
 
Halafu unaona alivyokwepa hoja yangu ya yule mama wa Songea kiaina?

Jasusi,
Sijapata kumkwepa mtu.

Unakikumbuka kilio cha mke wangu Zena biti Farijala na suala la ''wazimu?''
Pasco alizungumza sana.

Mke wangu Biti Farijala akisema, ''Sasa mie ndiye ntakuwa mke wa kupeleka
vyakula jela wakati wenzangu wanastarehe na waume zao? Maana dalili naziona
huyu Mohamed kazoa ule wazimu wote wa babu yake.''

Sisi hatukimbii watu si asili yetu.
 
Nguruvi,
Warsha haipo hapo.
Ninasema hivi, makala zote za WARSHA zilikuwa zinarudiwa ndani ya Annur. In fact baadaye member wa WARSHA walikuwa na mkono mkubwa sana ndani ya gazeti hili. Na hadi leo kundi la iliyokuwa WARSHA linatumia sana Annur. Kuna mengi katika hili. Naomba ''tusimgeuze geuze nyoka sana tunaweza kuona miguu''

Turudi kwenye baibui
 
Mohamed hivi yule Sheikh akigutiwa Rukara wa Muslim agency ni seneta wa bunge kule kule Burundi, huyu akijulikana sana kama mzawa wa kariakoo.
 

Nguruvi,
Warsha tuwe tusiwemo katika Annuur si jambo la siri.

Nilikuwa nakupa taarifa tu.
Kuhusu baibui...

Kwangu hilo si muhimu.
Hutaki nikupe ''Reflections...?''
 
Mohamed hivi yule Sheikh akigutiwa Rukara wa Muslim agency ni seneta wa bunge kule kule Burundi, huyu akijulikana sana kama mzawa wa kariakoo.

Nguruvi,
Sheikh Rukara wala si mtu wa Dar es Salaam.

Alikuja Tanzania kama mfanyakazi wa World Muslim League.
 

Mimi nilishangaa mahali fulani alipokataa kwamba tiketi ya Shirika la Meryknol haina maana yeyote lakini
wakati huohuo akielezea hisani zoote alizofanyiwa Nyerere mpaka za kupikiwa chapati. Na nikamwambia
kuna mambo mengine kama hayo ni kawaida mwenyeji kumkirimu mgeni kwa taratibu za Jamii zetu za Ki-tanzania.

Na nikamwambia wazi Ni aibu tu inayomzuia angeweza hata kuelezea Nyerere alikuwa anakula kilo ngapi kwa
siku akiwa kwa Abdu. Na ukimsoma between the lines unaona dharau fulani hivi, sijui kama ingekuwa yeye
ndiye aliyekuwa anamkirimu Nyerere masimango yake yangekuwaje!

Nilipouliza tena vipi hisani alizowafanyia Wazee wako mbona yeye alikuwa kimya. MS anadai kwa taratibu
za Pwani Mgeni anakirimiwa siyo yeye kumkirimu mwenyeji, apparently anamaanisha Nyerere hajawafanyia
chochote wazee wake!
 

Nguruvi,
Hii na mapenzi yako katika kalamu yangu au kitu gani?

Unakijua kisa cha ''Bridge on the River Kwai?''

Kuna kitabu nadhani na movie yake hebu tafuta kuna mafunzo.
 

Platozoom,
Unataka kujadili ni mie habari ya ''chapati...''
 
 
Dr. Slaa alikwishatoa ufafanuzi juu ya MOU. Na nadhani uzi huo umo humu ndani ya mnakasha huu. Hakuna fedha za walipa kodi zilizochotwa ila naona wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kuwa uwongo ukirudiwa mara kwa mara watu wataamini kuwa ni ukweli.
 
Nguruvi,
Sheikh Rukara wala si mtu wa Dar es Salaam.Alikuja Tanzania kama mfanyakazi wa World Muslim League.
Kwahiyo baada ya mkataba wake kwisha alirudi Burundi. Kuna mahali anaunganishwa unganishwa sana na harakati za waasi. Anyway sijui. Sasa ilikuwaje huyu alikuwa anaratibu shughuli za ndani za misikiti kupanga mikakati akiwa mfanyakazi tu wa washirika la ''Kimataifa''.

Na hawa world muslim league waliwezaje kuingia na kufanya shughuli hapa nchini maana kwa maandiko yako Tanzania ikiwa chini ya mfumo hairuhusu kujiunga na mashirika ya kiislam.

Hawa World Muslim league walikuwa wanafanya shughuli gani kiasi kwamba mfumo ambao ahuruhusu Tanzania kuwa na mhausiano na mashirika ya dini ya kiislam ukawasahau. Na vipi huyu Rukara mfanyakazi wa kigeni aliweza kumiliki Nyumba na kujihusisha na shughuli za harakati za waislam nchini.

Mohamed, hili tuliweke sawa lisije likaleta utata kwa vizazi vijavyo kama la EAMWS.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…