Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed, hivi kwa mtazamo wako gazeti la Annur linakidhi viwango? hii ni by the way
 
Jasusi,unamsoma between the lines MS!!!!!!

"Sawa mie na wewe ni watu wa tamaduni tofauti sana.
Wewe unatoka Musoma mimi nimezaliwa Dar es Salaam.

Makuzi yetu ni tofauti sana."

Halafu unaona alivyokwepa hoja yangu ya yule mama wa Songea kiaina?
 
Mmh...we nawe bana; sijui ndio reasoning gani hiyo; basi Nyerere kutokujibu nako ni kujibu!

OO, Na hii sijui ndio reasoning gani jamani toka kwa Great thinker! hivi hujui kuwa unapomwambia Msichana Mwanamwali kuwa unataka kumposa halafu anyamaze bila kujibu hujui kuwa amekubali ombi lako? au wewe Mzee ungeendelea tu kumwambia hayo hayo?

Nyerere kutokujibu hoja za Mohamed, bila shaka amekiri kuwa hoja hizo ni sahihi! ndio maana alifuatwa na Profesa Haroub Othman ili kukanusha kitabu cha Mohamed lakini Mwalimu alikuwa binaadamu na lazima tukubali kunakutahayari pia!
 
Halafu unaona alivyokwepa hoja yangu ya yule mama wa Songea kiaina?

Jasusi,
Sijapata kumkwepa mtu.

Unakikumbuka kilio cha mke wangu Zena biti Farijala na suala la ''wazimu?''
Pasco alizungumza sana.

Mke wangu Biti Farijala akisema, ''Sasa mie ndiye ntakuwa mke wa kupeleka
vyakula jela wakati wenzangu wanastarehe na waume zao? Maana dalili naziona
huyu Mohamed kazoa ule wazimu wote wa babu yake.''

Sisi hatukimbii watu si asili yetu.
 
Nguruvi,
Warsha haipo hapo.
Ninasema hivi, makala zote za WARSHA zilikuwa zinarudiwa ndani ya Annur. In fact baadaye member wa WARSHA walikuwa na mkono mkubwa sana ndani ya gazeti hili. Na hadi leo kundi la iliyokuwa WARSHA linatumia sana Annur. Kuna mengi katika hili. Naomba ''tusimgeuze geuze nyoka sana tunaweza kuona miguu''

Turudi kwenye baibui
 
Mohamed hivi yule Sheikh akigutiwa Rukara wa Muslim agency ni seneta wa bunge kule kule Burundi, huyu akijulikana sana kama mzawa wa kariakoo.
 
Warsha tuwe tusiwemo katika Annuur si jambo la siri.

Nilikuwa nakupa taarifa tu.
Kuhusu baibui...

Kwangu hilo si muhimu.
Hutaki nikupe ''Reflections...?''
 
Mohamed hivi yule Sheikh akigutiwa Rukara wa Muslim agency ni seneta wa bunge kule kule Burundi, huyu akijulikana sana kama mzawa wa kariakoo.

Nguruvi,
Sheikh Rukara wala si mtu wa Dar es Salaam.

Alikuja Tanzania kama mfanyakazi wa World Muslim League.
 
Mohamed,Hivi si wewe ulienza uzi huu kwa kuonyesha Nyerere alivyopewa pesa na Mshume Kiyate wakati anaelekea kuomba mboga Kariakoo.

Tena ukasema pesa aliyompa wakati huyo ilikuwa inatosha kujenga nyumba.
Mohamed, si wewe uliyeeleza jinsi Nyerere akiwa kwa Bi Mluguru alivyougua tumbo la kuhara.
Leo la baibui unaona halina tija, kwamba hayo uliyoyaeleza kuhusu Nyerere yalikuwa na tija ipi.

Tadhali Mohamed, mbona unatufanya sisi wasahaulifu kiasi hicho. Au ni wewe unayesahau ulichosema!
Jasusi ukiona anatoa kona ujue kipo kitu nyuma yake. Ilikuwa hivi hivi kwa ticket ya Maryknoll, Cecil Matola, mjengo wa Cameron, Ali Ramdhani,Hamza Aziz n.k.

Mimi nilishangaa mahali fulani alipokataa kwamba tiketi ya Shirika la Meryknol haina maana yeyote lakini
wakati huohuo akielezea hisani zoote alizofanyiwa Nyerere mpaka za kupikiwa chapati. Na nikamwambia
kuna mambo mengine kama hayo ni kawaida mwenyeji kumkirimu mgeni kwa taratibu za Jamii zetu za Ki-tanzania.

Na nikamwambia wazi Ni aibu tu inayomzuia angeweza hata kuelezea Nyerere alikuwa anakula kilo ngapi kwa
siku akiwa kwa Abdu. Na ukimsoma between the lines unaona dharau fulani hivi, sijui kama ingekuwa yeye
ndiye aliyekuwa anamkirimu Nyerere masimango yake yangekuwaje!

Nilipouliza tena vipi hisani alizowafanyia Wazee wako mbona yeye alikuwa kimya. MS anadai kwa taratibu
za Pwani Mgeni anakirimiwa siyo yeye kumkirimu mwenyeji, apparently anamaanisha Nyerere hajawafanyia
chochote wazee wake!
 
Hii na mapenzi yako katika kalamu yangu au kitu gani?

Unakijua kisa cha ''Bridge on the River Kwai?''

Kuna kitabu nadhani na movie yake hebu tafuta kuna mafunzo.
 
Mimi nilishangaa mahali fulani alipokataa kwamba tiketi ya Shirika la Meryknol haina maana yeyote lakini
wakati huohuo akielezea hisani zoote alizofanyiwa Nyerere mpaka za kupikiwa chapati. Na nikamwambia
kuna mambo mengine kama hayo ni kawaida mwenyeji kumkirimu mgeni kwa taratibu za Jamii zetu za Ki-tanzania.

Na nikamwambia wazi Ni aibu tu inayomzuia angeweza hata kuelezea Nyerere alikuwa anakula kilo ngapi kwa
siku akiwa kwa Abdu. Na ukimsoma between the lines unaona dharau fulani hivi, sijui kama ingekuwa yeye
ndiye aliyekuwa anamkirimu Nyerere masimango yake yangekuwaje!

Nilipouliza tena vipi hisani alizowafanyia Wazee wako mbona yeye alikuwa kimya. MS anadai kwa taratibu
za Pwani Mgeni anakirimiwa siyo yeye kumkirimu mwenyeji, apparently anamaanisha Nyerere hajawafanyia
chochote wazee wake!

Platozoom,
Unataka kujadili ni mie habari ya ''chapati...''
 
Nguruvi,
Warsha tuwe tusiwemo katika Annuur si jambo la siri.

Nilikuwa nakupa taarifa tu.
Kuhusu baibui...

Kwangu hilo si muhimu.
Hutaki nikupe ''Reflections...?'

"modus operandi" ya Nyerere ilikuwa na kujua what is happening-intelligence walikuwa everywhere-huyo Sykes kama alikuwa shadowed-he was one of the many,kwa hiyo hakuna cha ajabu hapa
 
Lowassa ndie aliesaini mkataba wa MOU mwaka 1992 na kubariki kuchota fedha za walipa kodi wa nchi hii ili Kanisa linufaike! Leo anatoa sh. Milioni 5 kwa Misikiti! anatoa fedha hizo ili kuweka uwiano sawa kati ya Kanisa wanaochotewa mabilioni kila mwaka au ni takrima kwa uchaguzi wa 2015?

Ushauri wangu kwa Waswahili wenzetu walakashata na gahwa pokeeni hizo fedha za vigogo ama wawe CCM, Chadema au CUF lakini wa kumpa kura maelekezo tunangoja toka kwa Amiri wetu wa Shura ya Maimamu TZ! Hakuna kulala na kudanganywa tena mpaka kieleweke!
Dr. Slaa alikwishatoa ufafanuzi juu ya MOU. Na nadhani uzi huo umo humu ndani ya mnakasha huu. Hakuna fedha za walipa kodi zilizochotwa ila naona wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kuwa uwongo ukirudiwa mara kwa mara watu wataamini kuwa ni ukweli.
 
Nguruvi,
Sheikh Rukara wala si mtu wa Dar es Salaam.Alikuja Tanzania kama mfanyakazi wa World Muslim League.
Kwahiyo baada ya mkataba wake kwisha alirudi Burundi. Kuna mahali anaunganishwa unganishwa sana na harakati za waasi. Anyway sijui. Sasa ilikuwaje huyu alikuwa anaratibu shughuli za ndani za misikiti kupanga mikakati akiwa mfanyakazi tu wa washirika la ''Kimataifa''.

Na hawa world muslim league waliwezaje kuingia na kufanya shughuli hapa nchini maana kwa maandiko yako Tanzania ikiwa chini ya mfumo hairuhusu kujiunga na mashirika ya kiislam.

Hawa World Muslim league walikuwa wanafanya shughuli gani kiasi kwamba mfumo ambao ahuruhusu Tanzania kuwa na mhausiano na mashirika ya dini ya kiislam ukawasahau. Na vipi huyu Rukara mfanyakazi wa kigeni aliweza kumiliki Nyumba na kujihusisha na shughuli za harakati za waislam nchini.

Mohamed, hili tuliweke sawa lisije likaleta utata kwa vizazi vijavyo kama la EAMWS.
 
Nguruvi,
Warsha tuwe tusiwemo katika Annuur si jambo la siri.

Nilikuwa nakupa taarifa tu.
Kuhusu baibui...

Kwangu hilo si muhimu.
Hutaki nikupe ''Reflections...?'

"modus operandi" ya Nyerere ilikuwa na kujua what is happening-intelligence walikuwa everywhere-huyo Sykes kama alikuwa shadowed-he was one of the many,kwa hiyo hakuna cha ajabu hapa

Son...
Kwa Nyerere Abdu hakuwa ''huyo Sykes...''
Wala Abdu si '' one among many...''

Kisa cha Abdu na Nyerere ni kisa kingine.
Ni kisa cha udugu...mama zao wakaja kuwa mashoga.

Wakikesha pamoja Stanley Street nyumbani kwaa Abdu
wakisuka mbinu za kuisukuma TANU mbele...

Wake zao wakaja kuwa mashoga wakiongozana madukani
kununua khanga na vitambaa vya kushona sare za taarab za TANU...

Son...
Unajipunja...
Nami nakuacha hivyo ulivyo ya nini nikupe faida?

Baki hivyo hivyo.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ina mengi, mengi, mengi mno.

Lakini huenda vilevile unatishika unaogopa kuniisikiliza.
 
Back
Top Bottom