Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wewe ndie uliyeutangazia ulimwengu kuwa Tanzania niyamfumo kristu,

Sasa tukihoji kuwa mtu huyo wa kigeni alifikaje nchini kufanya kazi za uislamu? Wewe unatuambia tukahiji wizara????????? Inaingia akilini mkuu?

Sasa JF imehamia bungeni maswali ya papo kwa papo! Waziri Mkuu ni nani?
 
Nguruvi,
Swali lako umelielekeza sipo.Hayo ni ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Wanajamvi naomba msaada kidogo,kuna mahali nimesoma Mohamed anasema Tanzania haijiungi na taasisi za kiislam kama OIC na hata ''commonwelath'' kwasababu ya mfumokristo hautaki.

Sasa hili la World Muslim league kufanya kazi Tanzania liliwezekana vipi.
Tena mkuu wake alikuwa mtu wa Burundi ingawa kuna ''Utanzania'' kwa namna fulani.

Anyway,nifungueni macho kwa hili. Naona kuna kitu labda sielewi.
 

Kitanzi kinaanza kubana;
Ya Shelikh Ilunga Hassan Kapungu waulizwe wanazuoni wanaomzidi ilmu!
Ya Rukara (wa kwetu Kariakoo) na Muslim League waulizwe Mambo ya Ndani!
Mohamed Said atakimbia sana lakini hatapata pa kujificha na bado!
 

Mi nadhani kabla hujasaidiwa, ungetufahamisha kwanza World Muslim na OIC ni nini? na nini maana ya Mkuu wake ni Mburundi ingawa kuna UTZ kwa namna fulani?
 
JASUSI:
Wewe huwa unaamini na kukubali anayosema Dr. Slaa?

Mengi anayoyasema yana ukweli. Unakumbuka alipotangaza orodha ya mafisadi 11? Watu walimwita majina ya ajabu sana. Lakini baadaye imegundulika kuwa ni kweli CCM inatuibia hela zetu benki kuu kwa ajili ya uchaguzi. Wewe mtu kama huyo utampuuza kweli?
 
Mi nadhani kabla hujasaidiwa, ungetufahamisha kwanza World Muslim na OIC ni nini? na nini maana ya Mkuu wake ni Mburundi ingawa kuna UTZ kwa namna fulani?
Usilolijua ni kama usiku wa giza...kwa nini huwezi kukaa kimya ukisoma tu kama kitu hukijui? Tulia kijana mambo yanakuja, hii tabia ya kurukia hata usivyovielewa ni hatari kubwa...bila shaka huyo Rukara hata hukuwahi kumsikia!
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza...kwa nini huwezi kukaa kimya ukisoma tu kama kitu hukijui? Tulia kijana mambo yanakuja, hii tabia ya kurukia hata usivyovielewa ni hatari kubwa...bila shaka huyo Rukara hata hukuwahi kumsikia!

Mwanafunzi anauliza swali, akiambiwa afafanue swali ili apate jibu anakuwa mkali na povu kumtoka mdomoni! Mag, kaa chini kidogo, piga fundo moja la maji kabla ya jingine, kunywa mara tatu huku ukipumua taratibu kabla ya kuongea tena! nadhani hii itasaidia kushusha kama sio kumaliza hasira!
 
Mengi anayoyasema yana ukweli. Unakumbuka alipotangaza orodha ya mafisadi 11? Watu walimwita majina ya ajabu sana. Lakini baadaye imegundulika kuwa ni kweli CCM inatuibia hela zetu benki kuu kwa ajili ya uchaguzi. Wewe mtu kama huyo utampuuza kweli?

Katika hayo machache ya uongo miongoni mwa mengi yenye ukweli kama la kukamatwa kontena la kura bandia mpakani na Zambia na la yeye alishinda urais mwaka 2010 ni miongoni mwa uongo huo? au haya ni miongoni mwa ukweli wake au unaweza kututajia mfano mmoja tu wa machache ya uongo wake?
 

Nadhani WARSHA walikuwa wanatumia gazeti likiitwa MIZANI. Naikumbuka makala moja ilikuwa imekaa ki-Moh Moh mwaka 1992 ikilalamikia kuanzishwa kwa uchangiaji elimu ya juu, na kudai kuwa ilikuwa ni kufunga milango ya Elimu kwa waislam. Katika makala hiyo walilalamikia na tangazo la redioni, lile la " mimi maimuna, nasema mimi maimuna"
 
Kadogoo,
Kuhusu uchaguzi ngoja nikusimulie matokeo kwenye kituo nilichosimamia kama wakala. Tulikuwa na wapiga kura 390 waliojiandikisha. Na kati ya hayo ni 301 waliopiga kura. Na kati ya hizo Kikwete alipata kura 39 huku Slaa akipata kura 258. Hizo ni kura nilizosimamia mimi mwenyewe. Kuhusu contena, baadhi ya kura bandia, sijui kama zilitoka kwenye contena hilo au la, zilishikwa Musoma. Kuna vijana wanne wa CCM walikamatwa na masanduku ya kura. Polisi waliitwa wakaondoka na vijana hao lakini mpaka leo hakuna hata mmoja aliyefikishwa mahakamani. Hebu nikuulize kitu kuhusu contena. Hivi kweli wale vijana wa TRA pale Tunduma hawajui ni vitu gani vinavyoingizwa kilahali na ni vipi haviruhusiwi? Kwa nini walilazimika kuita polisi na polisi wakaondoka na hilo contena? Tafakari halafu urudi kwenye mnakasha.
 


Nanren,
Mizani lilipoanzishwa Warsha ilikuwa haipo.

Hili si jambo kubwa nakupa taarifa tu upate kujua.
Mimi sikuwa naandika kwa staili hiyo uliyosema.

Kwa wakati ule nadhani hukuwa unanifahamu vyema
kiasi cha kujua staili yangu ya uandishi.

Ingelikuwa leo hakika ungelijua.
 

Nguruvi,

Jamaa yangu anasena nakimbia maswali ya Rukara na World Muslim League na OIC.
Afahamu tu ni katika ustaarabu mtu kusema lile unalolijua.

Usilolijua unasema kuwa hujui.

Wanaosajili mambo kama hayo ni Wizara ya Mambo ya Ndani na wao ndiyo walowapo
tasjila.

Vipi mimi nizungumzie kile nisichojua?
 
Jokakuu,

Hivi Wafanyabiashara huwa wanawezeshwa au kupewa ruzuku na Serikali? Hapa panazungumzwa hali ya Serikali kupendelea dini moja dhidi ya dini zingine usichanganye mambo!
Kadogoo,

..mimi sijui kwanini hali iko hivyo, kwamba tangu kabla ya uhuru na mpaka leo miaka 50+ biashara zote kubwa ni za Waasia tu?

..naomba umsome Prof.Maghembe hapa anazungumzia Waislamu na elimu dunia:

"Suala la elimu ya Dunia pia ni muhimu lakini mfano mzuri wa elimu kushuka ni katika mikoa ya pwani ambapo ndio ilipoanzia mwaka 1995 wanafunzi walioanza darasa la kwanza walikuwa 35,000 lakini walikuja kumaliza darasa la saba 9000 hapa inaonesha kua waislamu tunarudi nyuma badala kwenda mbele,"alisema Profesa Maghembe.

..Sasa hebu tafakari hayo maneno ya Prof.Jumanne Maghembe. Waislamu wa aina yako mnatumia muda mwingi kujenga fitina na chuki ktk jamii badala ya kushughulikia matatizo ya Waislamu.
 
Mohamed, hapa kuna vitu viwili.
1. Rukara na harakati akiwa mfanyakazi wa shirika la kimataifa na akiwa si Mtanzania
2. World Muslim League na shughuli zake na kama ni shirika la kliislam

Hilo la kwanza tuliache kwanza kwasababu muda ukiwadia tutalijadili

Hili la pili ndilo haswa tunataka tufahamu. Je, unakubali kuwa World Muslim League ni shirika linalojihusisha na mambo ya waislam na je, linafanya kazi Tanzania?
Hili halihitaji wizara ya mambo ya ndani, lipo katika uwezo wetu na ndilo tulijadili.
 
Kwaushahidi wako huu kuwa Wizara ilitoa kibali tena ni ushahidi wa kimaandishi bado unaamini Tanzania ni yamfumo kristu kama unavyoendelea kuhadhiri?
 

Nguruvi,
Tujadili mambo yetu.

WML hawapo tz na huyo Rukara halikadhalika.
 
Nguruvi,
Tujadili mambo yetu.WML hawapo tz na huyo Rukara halikadhalika.
Mhh, Mohamed huyu sheikh Rukara hakuwepo hapo kariakoo kweli na ofisi zake. Ni wewe umesema Rukara alikuwa na world muslim league na ninakubaliana nawe kabisa.
Ukasema mambo mengine iulizwe wizara ya mambo ya ndani! sasa kama hawapo Tanzania kwanini tuulize wizara mambo yasiyohusika.

Mohamed, huu mnakasha unachimbua kila jambo ili liangaliwe kwa undani wake.
Tumeona ya EAWMS na kutimuliwa kwa sheikh Amir. Mbona la Rukara linaonekana kama siri.

Wewe ni mwenyeji wa hapo kariakoo, tuthibitishie kuwa hawapo au hawakuwepo, I mean WML.
 
Wanajamvi kuna article alileta Mohamed ikisema kuwa wakristo wana fursa za kujiunga na mashirika kama vile world vision, world church council na mengine mengi tu. Waislam wamenyimwa fursa za kujiunga na IOC.
Ikasema katika kupendelea ukrsito hata commonwelath sisi ni wanachama.
Kama kuna mtu anakumbuka post anikumbushe(aivute hapa mapema kabisa tuongee tukiwa na bandiko lake)

Hili la World Muslim League halitaisha hivi hivi. Itabidi tuangalie shirika na wakuu wake maana lina uhusiano mkubwa sana na yale yaliyotokea EAMWS kwa ulinganifu na litatupa mwanga zaidi wa habari hii.

Just a tip, huyo mkuu wa WML hakuwa mtanzania lakini kwa namna zisizoeleweka alikuwa Mtanzania. Kuna jambo.
Taratibu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…